Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Raza awanyooshea kidole viongozi CCM
na Mkolo Kimenya
MFANYABIASHARA Mohamed Raza, amewataka viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakweli katika mambo yao kabla ya kukimbilia kutoa taarifa kwa wananchi.
Huku akionyesha kuwalenga baadhi ya wabunge, Raza alisema viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanapaswa kujiondoa katika Halmashauri na Kamati Kuu ya (CCM) ili kukipa heshima chama.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam, Raza alionyesha wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa mambo yanayojitokeza katika siku za karibuni yanayoonyesha baadhi ya viongozi kujali zaidi maslahi binafsi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaiathiri jamii.
Alisema ubabe unaofanywa na baadhi ya watendaji, ndio chanzo cha hali zinazojitokeza za malumbano ambayo kamwe hayawezi kujenga nchi.
Alitoa mfano kuwa mtu akivaa shati, nje likiwa safi na fulana ya ndani ikawa inatoa harufu maana yake ni mchafu, hivyo haiwezekani kutoa ukweli kwa watu wengine huku yeye hasemi ukweli unaomuhusu.
Lazima tuwe wakweli na tukiacha haya mambo yaendelee yawezekana uhuru wa Tanzania na Mapinduzi Zanzibar kutoweka kwa ajili ya matajiri wachache.
Hali ya nchi inatisha, tukiendelea kuyatazama haya yanayotokea sijui nchi tunaipeleka wapi, tunapaswa kulitazama hili ili kuinusuru nchi, alisema Raza.
Raza alisema sheria inapaswa kuchukua mkondo wake kwani kuna mabilioni ya fedha yamechukuliwa na matajiri huku karibu asilimia 90 ya Watanzania wakilia njaa.
Watu wanajulikana, hii subiri subiri inatoka wapi? Wachukuliwe hatua ili kujenga uaminifu kwa wananchi, Rais hawezi kufanya mambo yote peke yake lazima awe na wasaidizi, hivyo wamsaidie kwa kumtaarifu mabaya yanayotendeka na si kumueleza mazuri yaliyopo.
Nina hofu ndani ya chama changu na kama tungepata upinzani wenye nguvu, tungepata shida sana bungeni, kwani kinachoniumiza ni kuwa bado tunatakiwa kurudi kwa wananchi, tutawaambia nini? alihoji Raza.
Alisema kitendo cha watu kuingiza masuala binafsi na kuchafuana katika masuala yanayogusa jamii ni kutaka kuzima hoja zizilizopo.
Aliwalaumu watu wanaohuburi ukabila na udini kwa kutaka kuficha ukweli na kuwataka Watanzania kutokaa kimya wakiangalia uovu huu ukiendelea kutendaka.
upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM; mwalimu alisema