Wadau,
Baada ya kuukataa muswada wa sheria ya uundwaji wa tume maalum itakayoshughulika na kukusanya maoni ya wananchi ili kuleta katiba mpya, Serikali imeandaa muswada mwingine ambao ndio utawasilishwa bungeni hivi karibuni.
Muswada huu mpya umeingiza mambo kadhaa ambayo wadau waliyalalamikia kama vile:
1. Ushiriki sawa wa rais wa Zanzibar katika uteuzi kama ilivyo kwa rais wa muungano.
2. Muswada kuwa katika lugha za kiswahili na Kiingereza.
3. Kuwepo kwa bunge la katiba(japo wamelichanganya na wabunge wa sasa na wajumbe wa baraza la wawakilishi wa sasa).
4. Time frame zinazoeleweka kidogo n.k
Tatizo kubwa ambalo tunalikataa na bado serikali imelirudisha ni madaraka ya rais katika uundaji wa katiba mpya. u-Rais wa Tanzania ni cheo kinacholalamikiwa kuwa na madaraka makubwa mno, na sasa katika uandikaji wa katiba ya watanzania wote bado rais anapewa kusimamia kila kazi inayohusiana na katiba hii.
Tume ya taifa ya uchaguzi NEC na tume ya taifa ya uchaguzi ya Zaznibar ZEC bado zinapewa mamlaka yaleyale ya kusimamia masuala ya kura za maoni za wananchi wakati wa kupitisha katiba.
Serikali ya CCM ina kichwa kigumu sana, haisikii wala kusikiliza. Yaani tume ile ile inayochakachua matokeo ya uchaguzi kila kukicha ndiyo inapewa kazi ya kusimamia suala muhimu la katiba. Tume ya rais, katiba ya rais,nchi ya rais.
Ati mkuu wa wilaya, mtendaji wa kata,mtendaji wa kijiji na mtendaji wa mtaa ndio wanapewa kazi ya kusimamia taratibu za ukusanyaji wa maoni ngazi ya chini, ARE WE SERIOUS?
Kwani mpaka watu wabebe bunduki ndiyo serikali ione wananchi wanahitaji katiba mpya ya wananchi na siyo ya rais, DC,WEO,VEO,NEC,ZEC n.k?
Hivi ikulu ina hofu gani ikitengeneza utaratibu wa uhakika na wa haki wa kuleta katiba mpya? Kwa nini kila jambo katika kuleta katiba anapewa rais, kwa nini tusiunde tume maalum itakayoteuliwa kwa utaratibu maalum ikiwa na watu maalum ambao hata upatikanaji wao utatokana na uadilifu wao na watu hao watahojiwa kikamilifu live mbele ya watanzania wote katika televisheni n.k?
Kuna biashara gani katika ku-complicate hivi suala la katiba? Kwani serikali haijui ma-WEO, VEO, NEC, ZEC, DC, RAIS na kadhalika ni watu ambao wamelaumiwa sana kwa udhaifu mkubwa ambao wamekuwa wakiuonesha katika chaguzi mbalimbali na katika utendaji wao kwa ujumla kwa maana ya kuisaidia CCM?
Hivi sasa nchi inayumba sana kiuchumi, mfumuko wa bei, matatizo ya umeme na mauchafu kedekede, kwa nini rais wetu asishughulikie haya suala la katiba likawekwa katika mikono ya watu safi wanaoaminiwa na jamii ya watanzania?
Wasiwasi wangu ni kwamba, CCM wana hofu kuwa tukipata katiba ya haki ya ukweli ya maadili ya dira safi - wanajua wataondoka madarakani immediately. Lakini njia ya mwongo ni fupi sana, hii katiba ya RAIS na IKULU yake na chama CHAKE, tutaipinga kwa nguvu zote.
Kwa bahati mbaya hapa duniani, tangu ulimwengu uumbwe, haijawahi kutokea SERIKALI na MAJESHI yaliyowashinda wananchi wenye kiu ya haki na mabadiliko ambavyo ni haki yao.
TEMBELEENI TOVUTI YA BUNGE ,SOMENI KWA MAKINI - SOTE TUCHUKUE HATUA KWANI KATIBA HII SIYO YA MTU MMOJA NA FAMILIA YAKE NA MARAFIKI ZAKE, NI KATIBA YETU SOTE, WATANZANIA!
Julius Mtatiro,
26 Oktoba 2011.
Wanasiasa bwana! Kwanza CCM haikuwa na wazo la katiba mpya kwenye ilani yake,bali hili wamelikubali kutokana na joto kali ili waendelee kuaminika. Hivyo CCM na serikali yake wamekubali lakini wameweka limitations ili kujilinda,kamwe hawawezi kupeana talaka na NEC au ZEC. Mbali na CCM ukweli ulio wazi ni kuwa wapinzani wakubwa CHADEMA, CUF na NCCR ambao ni wapiga debe wa katiba mpya, hawa wote hawana jipya zaidi ya uchaguzi ili kuingia ikulu tu!
Kila wakati utasikia tume huru ya uchaguzi na kwa hili naomba kusema wapinzani wamerogwa na uchaguzi, kwani kila wakilala wanawaza na kuota uchaguzi. Slaa na Mtatiro hebu tuambieni juu ya rasilimali zetu na sio mauchaguzi. Hakuna kati ya ccm, chadema wala cuf wanaosema katiba mpya rasilimali zetu tuzilindeje na tuzitumieje au vipaji vya wazalendo juu ya ugunduzi na sayansi tuvitumieje na tuvihifadhije ili tusiendelee kutegemea wazungu na teknolojia zao, badala yake wanalia na uchaguzi.
Kama itakuwa hivi hata katiba mpya ikipatikana maisha ya mtazania wa kawaida hana chake. Jamani tuwaangalie sana wanasiasa!kwan katiba sio yao bali ni yetu wananchi.
]Ngoja nirekebishe miwani nisome vizuri[/B]
Kama watu wanaona kuwa mambo muhimu hayamo kwenye mswada huu ni wa kuukataa tu. Ni bora watu wasubiri chama ambacho kitakuja kuandika katiba mpya kwa misingi ya uwazi, usawa, demokrasia na utu wa Watanzania kuliko kuburuzwa kwa sababu watu wanataka Katiba Mpya. Tusiburuzwe kwani tutakachoandika ndio urithi wetu kwa kizazi kijacho.
Huwezi kwepa umuhim wa uchaguzi katika katiba mpya ati kisa rasilimali. Hao wanaopitisha na kusaini mikataba wanapatikana kwa uchaguzi huo huo. Au hulioni hilo?Wanasiasa bwana! Kwanza CCM haikuwa na wazo la katiba mpya kwenye ilani yake,bali hili wamelikubali kutokana na joto kali ili waendelee kuaminika.Hivyo CCM na serikali yake wamekubali lakini wameweka limitations ili kujilinda,kamwe hawawezi kupeana talaka na NEC au ZEC.
Mbali na CCM ukweli ulio wazi ni kuwa wapinzani wakubwa CHADEMA,CUF na NCCR ambao ni wapiga debe wa katiba mpya, hawa wote hawana jipya zaidi ya uchaguzi ili kuingia ikulu tu! Kila wakati utasikia tume huru ya uchaguzi na kwa hili naomba kusema wapinzani wamerogwa na uchaguzi, kwani kila wakilala wanawaza na kuota uchaguzi.
Slaa na Mtatiro hebu tuambieni juu ya rasilimali zetu na sio mauchaguzi.Hakuna kati ya ccm,chadema wala cuf wanaosema katiba mpya rasilimali zetu tuzilindeje na tuzitumieje au vipaji vya wazalendo juu ya ugunduzi na sayansi tuvitumieje na tuvihifadhije ili tusiendelee kutegemea wazungu na teknolojia zao,badala yake wanalia na uchaguzi.
Kama itakuwa hivi hata katiba mpya ikipatikana maisha ya mtazania wa kawaida hana chake. Jamani tuwaangalie sana wanasiasa!kwan katiba sio yao bali ni yetu wananchi.
Slaa na Mtatiro hebu tuambieni juu ya rasilimali zetu na sio mauchaguzi.Hakuna kati ya ccm,chadema wala cuf wanaosema katiba mpya rasilimali zetu tuzilindeje na tuzitumieje au vipaji vya wazalendo juu ya ugunduzi na sayansi tuvitumieje na tuvihifadhije ili tusiendelee kutegemea wazungu na teknolojia zao,badala yake wanalia na uchaguzi.
Wanasiasa bwana! Kwanza CCM haikuwa na wazo la katiba mpya kwenye ilani yake,bali hili wamelikubali kutokana na joto kali ili waendelee kuaminika.Hivyo CCM na serikali yake wamekubali lakini wameweka limitations ili kujilinda,kamwe hawawezi kupeana talaka na NEC au ZEC.