Rasimu ya "katiba mpya ya mapenzi"

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wanajamii;

Baadhi ya mahusiano ya Kimapenzi yamekuwa ya mafanikio makubwa sana lakini baadhi yamekuwa na matatizo ya hapa na pale na mengine yamekuwa mabaya kiasi cha kuvunjika. Ni nini hasa kilichopo ndani ya mapenzi? Msingi wake, madhumuni yake, nini kifanyike ili yadumu, kunapokuwa na matatizo nini kifanyike, wahusika wachukuliane vipi nk nk.

Kwa mara ya kwanza, JF inakuletea Rasimu ya Katiba ya Mapenzi itakayohusisha mambo mablimbali yahusuyo mapenzi.

Tafadhali pitia rasimu hii na wote tusaidiane kuiboresha hadi pale itakapokuwa imekamilika. Kwa wale wapendao, wanaweza kuitumia kama Katiba ya Mmapenzi.

KATIBA YA MAHUSIANO YA MAPENZI

Utangulizi

Ibara ya Kwanza

Jina

Jina la Uhusiano wetu utakuwa: Wanandoa au Mahawara au . . . .
Ibara ya Pili

Madhumuni

Sehemu 1 Madhumuni ya Mahusiano ya Mapenzi yatakuwa . . . ..

Sehemu 2 Mahusiano ya Mapenzi ni ya hiari na hayatakiwi yaingiliwe na mtu mwingine zaidi ya sisi wawili isipokuwa kwa makubaliano maalumu kwa mujibu wa Katiba hii. Katika Mahusiano haya hakutakuwa na Mwenye Cheo zaidi ya Mwingine.

Sehemu 3 Mahusiano haya ni ya Kimapenzi tu na yasihusishe siasa, dini, rangi au ubaguzi wa namna yoyote wala si ruhusa kuwa na mpenzi mwingine . . .

Sehemu 4 Mahusiano haya ni for non-profit. Si ruhusa kwa yeyote kati yetu kujinufaisha kwa faida binafsi hasa kwa maana ya kipesa au kimali. Mali au pesa zote zitakazopatikana zitatumika kwa mujibu wa makubaliano au kwa mujibu ya mmiliki atakavyo.

Ibara ya Tatu

UANACHAMA

Sehemu 1 Wanachamani lazima wawe na umri wa miaka 18 na kuendelea, wenye akili timamu nakupendana kwa dhati

(a) Nimarufuku wanachama kupishana zaidi ya miaka 15.hii itawafanya kuishi kwa kufurahianavizuri
(b) Wanachama lazima wawe na productive organszilizokamilika
(c) Kwawale wanachama wenye umri mkubwa(wanaume) lazima wahakikishe wanao uwezo wakuwatoshelezana kimwili wenzi wao.kabla ya kuingia kwenye mahusiano kuwepo navyeti vya daktari kuthibitisha ilo

Sehemu 2 Maombiya Uanachama yatakuwa kwa Kutongozana
(a) Ni marufuku wakati wa kutongozana mwanachama kutaja /kulazimishwa kutajamali anazomiliki/kiasi cha fedha alichonacho

Sehemu 3 Maombi ya Uanachama wa kuwa Wapenzi yatakuwa ya moja kwa moja kwa mdomo au SMS, Email, Barua, fax au kutumia mtu au watu.

Sehemu 4 Uanachama unaweza kusitishwa wakati wowote na kuvunja mapenzi kwa ukosefu wa Uaminifu, dharau, uzinzi, kifo nk nk. n Legion.

Sehemu 5 Mwanachama akipatikana na hatia uhusiano unaweza kusitishwa kwa muda Fulani mpaka hapo mwafaka baina ya wawili.

Sehemu 6 Kama kutakuwa na kuachana basi hakutakuwa na kurudiana labda baada ya mwaka moja kupita nah ii itahusisha kuanza kutongozana upya kwa mujibu wa Sehemu 2.

Ibara ya Nne

Maofisa

Sehemu ya l Wanakamati Wakuu wa Mahusiano haya watakuwa Mke na Mume (Wanandoa) au Wapenzi (GF na BF ) au Nyumba Ndogo (Vimada)

Sehemu 2 Hakutakuwa na Ofisa Mkuu wala Msaidizi. Wote watakuwa sawa . . .

Sehemu 3 Mkutano Mkuu wa Mambo ya Kimsingi ya mahusiano utafanyika walau mara moja kila baada ya miezi 3

Sehemu 4 Maofisa au wapenzi hawa hawatapigiwa kura bali watachaguana kwa kutongozana na kukubaliana.

Sehemu ya 5 Mwanachama yeyote ambaye makubaliano ya msingi yamefanyika anweza kuwa katika Kiongozi wa Mwenzake kwa kadiri Wapenzi wanavyotaka.

Sehemu ya 6 Kazi za kila mpenzi zitaainishwa kwa kadiri wapenzi watakavyokubaliana

Sehemu ya 7 Baadhi ya mambo ya kimsingi yanayopaswa kufanywa na Wapenzi wote ni:
Kutimiziana haja za Kimapenzi

1. Kutunzana
2. Kuheshimiana
3.
(tusaidiane kufafanua na kuongezea)

Sehemu ya 8 Pale ambapo Mapenzi yamevunjika kwa sababu yoyote, ifanywe jitihada ya kuziba pengo
Ibara ya tano

Pesa na Mahari

Sehemu 1 Mapato yatakayotumika katika mahusiano haya yatatokana na pesa itokanayo na Wapenzi hawa wawili au sehemu nyingine yoyote inayokubalika.

Sehemu 2) Kabla ya mahusiano ya ndoa Jinsia ya Kiume Itatoa Mahari kwa Wazazi wa Jinsia ya Kike . . Kiasi hich kitakuwa ni . . .

Sehemu 3 Utaratibu wa kutoa mahali utafuata Mila na dersturi na utahisisha barua ya posa nk. Ndoa ifanyike ndani ya miezi 6 toka barua ya posa itolewe.

Sehemy 4 Kama mahusiano ni ya BF na GF au Wachumba au Vimada nk, basi suala la mahari alihusiki.

Ibara Sita

Mali

Sehemu 1 Mali ya kila Mwanachama itabaki kuwa yake binafsi labda pale tu ambapo wote wameitolea jasho.

Sehemu 2 Kama mojawapo anahitaji kupata mali binafsi kutoka katika ile iliyochumwa pamoja, atafanya maombi kwa mwenzake.

Ibara ya Saba

Nyumba Ndogo

Sehemu 1 Kutakuwa na Nyumba Ndogo, au Vimada nk ambao hawataruhisiwa katika mahusano yetu maana ni tishio kwa mapenzi yetu isipokuwa pale tu ambapo kuna maafikiano maalumu.
Ibara ya Nane

Ndugu katika mahusiano

Sehemu 1 Katiba hii inatambua ndugu halali wa upande wa Kiume na Kike

Sehemu ya 2 Wajomba na mashangazi, wapwa, binamu nk ambao hawajadhibitishwa au wanaotiliwa mashaka, uhakikisho ufanyike haraka

Ibara ya Tisa

Watoto Watokanao na Mahusiano

Sehemu 1 katiba hii inatambua haki zote za Watoto halali watakaozaliwa katika mahusiano. Hawa watajulikana kama Watoto au Mtoto wetu.

Sehemu 2 Pale ambap Mpenzi moja anasita juu ya uhalali wa motto kuwa ni wao/wake basi DNA Test ifanyike

Sehemu 3 Watoto/Mtoto atalelewa kwa misingi ya makubaliano na masharti baina ya wapenzi wawili

Ibara ya Kumi

Kudumisha Mahusiano

Sehemu 1 Ili kudumisha mahusiano. Yafuatayo yazingatiwe

  1. Uaminifu katika ndoa/mahusiano
  2. Wahusika wawe wakweli (wasipotezeane muda wala kudanganyana)
  3. Kuwe na dhamira ya dhati ya mahusiano
  4. wahusika wasisikilize majungu wala kushawishiwa na marafiki/ndugu
  5. Wasinyimane ispokuwa wamepatana kwa muda, shetani asije kuwajaribu kwa kutokuwa na kiasi!

Sehemu 2 Kuepuka mahusiano mabaya, yafuatayo yasifanyike . . . .

1. . . . . .
2. . . . . .
NB: Tusaidiane kuyaweka yoe hapa

Ibara ya Kumi Na Moja

Kusitisha Mahusiano

Sehemu 1 mahusiano yanaweza kusitishwa endapo moja kati ya haya yametokea:

  1. Kutaka kufanya mapenzi kinyume na maumbile
  2. mmoja atagunduluka ni mwathirika
  3. mmoja atagundulika ana maslahi binafsi
  4. udanganyifu wa aina yeyote utakapogunduluka

Sehemu 2
Utaratibu ufuatao ufuatwe katika kusitisha mahusiano . . . .

1. . . . .
2. . . . .
NB: Tusaidiane kuyaweka yoe hapa

Ibara ya Kumi na Mbili

Nyumba Ndogo

Sehemu ya 1 Ama kuwe na makubaliano au la, kutakuwa na uhusiano unaojulikana kama Nyumba Ndogo ambao ni wa moja kati ya Wapenzi atakao uanzisha nje ya mahusiano halali.

Sehemu 2 Idadi ya Nyumba ndogi inatakiwa iwe moja lakini itategemea matakwa ya yule mhusika.

Sehemu 3 Mahusiano na Nyumba Ndogo yatakuwa na masharti yake. Baadhi ya masharti hayo ni:

1. ….
2. …..
NB: Tusaidiane kuyaweka yoe hapa

Sehemu 4 Kazi ya Nyumba Ndogo itakuwa ni . . . ..

Ibara ya Kumi na tatu

Mabadiliko

Sehemu 1 Katiba hii inaweza kufanyiwa mabadiliko kwa maafikiano ya Wanaohusika ili mradi tu mabadiliko hayo yasipingane na makubaliano ya msingi.

Sehemu 2 pale ambapo maafikiano ya kubadilisha katiba hii hayajafikiwa na uhusiano umekuwa mbaya, upatanishi kwa mujibu wa taratibu mlizojiwekea au mila na desturi.
 
superman leo jumatatu bwana huu msiredi wa ukweli unahitaji critical thinking
dah ngoja nitarudi
bravo boy
like like like
:bathbaby::bathbaby:
kwa kuchangia
Ibara ya Tatu

UANACHAMA

Sehemu 1 Wanachamani lazima wawe na umri wa miaka 18 na kuendelea, wenye akili timamu nakupendana kwa dhati
(a) Nimarufuku wanachama kupishana zaidi ya miaka 15.hii itawafanya kuishi kwa kufurahianavizuri
(b) Wanachama lazima wawe na productive organszilizokamilika
(c) Kwawale wanachama wenye umri mkubwa(wanaume) lazima wahakikishe wanao uwezo wakuwatoshelezana kimwili wenzi wao.kabla ya kuingia kwenye mahusiano kuwepo navyeti vya daktari kuthibitisha ilo
Sehemu 2 Maombiya Uanachama yatakuwa kwa Kutongozana
(a) Ni marufuku wakati wa kutongozana mwanachama kutaja /kulazimishwa kutajamali anazomiliki/kiasi cha fedha alichonacho
 
Mkuu ni bora useme wewe ndio unaleta Katiba hii na sio JF...maana unasema "Kwa mara ya kwanza JF inakuletea Katiba"
 
Mkuu ni bora useme wewe ndio unaleta Katiba hii na sio JF...maana unasema "Kwa mara ya kwanza JF inakuletea Katiba"

Hujasoma bado. Ni draft. Michango ya Wana JF ndo italeta katiba mpya! lol Easy. . .
 
superman leo jumatatu bwana huu msiredi wa ukweli unahitaji critical thinking
dah ngoja nitarudi
bravo boy
like like like
:bathbaby::bathbaby:

Umeona eeeh . . .

Ila slowly hatuna haraka nayo . . . Ni mchakato wa Katiba ya mapenzi huu . . .
 
Mkuu ni bora useme wewe ndio unaleta Katiba hii na sio JF...maana unasema "Kwa mara ya kwanza JF inakuletea Katiba"
mkuu mambo ya kukosoa topic bila sababu sio issue wewe weka mapendekezo yako.besides sioni alipotaja jf .sory kama nimekuudhi hangover hizi
 
Naomba nichangie Ibara ya Kumi, Kudumisha Mahusiano-Mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa
  • Uaminifu katika ndoa/mahusiano
  • Wahusika wawe wakweli (wasipotezeane muda wala kudanganyana)
  • Kuwe na dhamira ya dhati ya mahusiano
  • wahusika wasisikilize majungu wala kushawishiwa na marafiki/ndugu
  • Wasinyimane ispokuwa wamepatana kwa muda, shetani asije kuwajaribu kwa kutokuwa na kiasi!

Nitakurushia mchnago wangu mwingine baadaye.
 
mkuu mambo ya kukosoa topic bila sababu sio issue wewe weka mapendekezo yako.besides sioni alipotaja jf .sory kama nimekuudhi hangover hizi

Kwa mara ya kwanza, JF inakuletea Rasimu ya Katiba ya Mapenzi itakayohusisha mambo mablimbali yahusuyo mapenzi.

Next time uwe unasoma kitu vizuri kilivyoandikwa kabla haujaanza kubisha
 
Mmh . . . Interesting . . . will be back to update the Katiba . . .
 
Naomba nichangie Ibara ya Kumi, Kudumisha Mahusiano-Mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa
  • Uaminifu katika ndoa/mahusiano
  • Wahusika wawe wakweli (wasipotezeane muda wala kudanganyana)
  • Kuwe na dhamira ya dhati ya mahusiano
  • wahusika wasisikilize majungu wala kushawishiwa na marafiki/ndugu
  • Wasinyimane ispokuwa wamepatana kwa muda, shetani asije kuwajaribu kwa kutokuwa na kiasi!

Nitakurushia mchnago wangu mwingine baadaye.

Asante Mkuu kwa Mchango makini.

Nimesha update rasimu yetu.
 
superman leo jumatatu bwana huu msiredi wa ukweli unahitaji critical thinking
dah ngoja nitarudi
bravo boy
like like like
:bathbaby::bathbaby:
kwa kuchangia
Ibara ya Tatu

UANACHAMA

Sehemu 1 Wanachamani lazima wawe na umri wa miaka 18 na kuendelea, wenye akili timamu nakupendana kwa dhati
(a) Nimarufuku wanachama kupishana zaidi ya miaka 15.hii itawafanya kuishi kwa kufurahianavizuri
(b) Wanachama lazima wawe na productive organszilizokamilika
(c) Kwawale wanachama wenye umri mkubwa(wanaume) lazima wahakikishe wanao uwezo wakuwatoshelezana kimwili wenzi wao.kabla ya kuingia kwenye mahusiano kuwepo navyeti vya daktari kuthibitisha ilo
Sehemu 2 Maombiya Uanachama yatakuwa kwa Kutongozana
(a) Ni marufuku wakati wa kutongozana mwanachama kutaja /kulazimishwa kutajamali anazomiliki/kiasi cha fedha alichonacho

Smile, imetulia hii. Ngoja tuwasikie na Wadau wengine.

Nimesha update.
 
[

Ibara ya Kumi Na Moja

Kusitisha Mahusiano

Sehemu 1 mahusiano yanaweza kusitishwa endapo moja kati ya haya yametokea:

1. . . . .Kutaka kufanya mapenzi kinyume na maumbile

2. . . . .
3. . . . .
 
mahusiano yanaweza kusitishwa endapo
  • mmoja atagunduluka ni mwathirika
  • mmoja atagundulika ana maslahi binafsi
  • udanganyifu wa aina yeyote utakapogunduluka
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom