Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu!

Status
Not open for further replies.
Napinga sana Chenge kuachiwa aendelee kama business as usual minister, yaani frankly nashindwa kuona ni vipi Chenge anaweza kukaa nyumbani kusubiri gari ya ofisi, kisha aende kazini kufanya kazi bila kuzongwazongwa na tuhuma hizi. It will be best if steps down for our nation's sake!

Hata hivyo nasita kuungana na wito wa hapa kutaka RO ajiuzulu,kwa sababu unlike Hosea na AG Mwanyika, wengi humu wapo ignorant kujua mipaka ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa.

Kwa hakika tunakosea sana kutaka RO ajiuzulu kwa kulinganisha utedaji wake wa kazi na wale wa zamani, huyu ni mkurugenzi wa alama mpya za nyakati, hivi nani hajui kuwa moja ya mbinu za idara ya usalama ni kunearth maovu, who knows kama haya tunayoyasikia ni as a result ya kazi yao, problem kubwa ni kuwa unlike other state departments hii ya Intelligence haina PR officer, watu wanashindwa kujua iwapo kazi inafanyika au la, Hata wale wanaosema ''Jiuzulu Yes I said it'' nina hakika hawajui kazi rasmi za usalama wa Taifa ni zipi,

The little I know ni kuwa hawa jamaa ni washauri tu full stop na at times huwa wanaact on permission! na kazi zao ni undercover hivyo pale mahali kama wametia mkono au la ni beyond public knowldedge, how can you blame someone bila kujua kazi zake?!

Issue ya Chenge inaarifiwa kuwa SFO walikuja Tanzania, na other circles reports that walideal kwanza na upande na Intelligence....

Times have changed, zamani haya yakitokea ilikuwa ni rahisi kumwambia editor wa Dailynews and other handful papers kuwa stop this! sasa hivi ni magazeti lukuki and it helps kujulikana maovu, hivi ni vita ambavyo ukiangalia single issues utaona hata JK hawajibiki but if you look at the bigger picture corruption scandal's coverage ni healthy kwa nchi guys! Hii ni dalili ya wazi kuwa mafisadi sasa hawawezi kujinatanfasi katika bongo yetu.

Usalama sasa wana kazi ngumu ya kujaribu kupambana na mafisadi waliomzunguka JK ambao for some reason ni friends, but they have managed to do it if you look at the fallback position alonayo Rostam na Lowassa...The intelligence today has to collaborate with the media na what we are seeing is somehow the result of tip off from reliable sources huwa inakuwa ni usalama, inapohojiwa kuwa walikuwa wapi, inakuwa ni meaningless...

Now I think is the right moment kwa Chenge kuresign kwanza, we should stop beating around the bush katika hili!Na huu ''reliable sources'' zinaarifu kuwa ameaombwa aresign au atamuacha rais with no option but to sack him....There is no way... He has to go frankly....

The first thing ni watu kama wewe kuwekwa ndani kwa ufisadi kisha Chenge afuatie
 
Kashfa inayomhusu Waziri CHENGE kwamba ameficha fedha zaidi ya bilioni moja kisiwani Jersey (Uingereza) ni shutuma nzito ambayo inatakiwa ifanyiwe kazi na serikali. Hivyo, ni wajibu wa serikali kuchunguza kashfa hiyo kwa lengo la kubaini kama fedha hizo amezipata kwa njia halali. Na endapo ikibainika vinginevyo ni vyema Waziri huyo akaondolewa katika nafasi yake na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Aidha, sikubaliani na maoni ya Mzee Mwanakijiji kwamba kutokana na kashfa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, RASHID OTHMAN ameshindwa kazi na ajiuzulu. Sikubaliani na maoni hayo kwa sababu R. OTHMAN hajahusika moja kwa moja na kashfa hiyo. Anayepaswa kujiuzulu ni CHENGE mwenyewe ambaye kashfa hiyo inamkabili moja kwa moja.

Ni vizuri pia tutambue kuwa hakuna nchi duniani isiyo kuwa na kashfa zinazohusisha viongozi wake na kama Wakurugenzi wakuu wa Usalama wa Taifa wangetakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa hizo basi pasingekuwa na Mkurugenzi Mkuu ambaye angekaa madarakani kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa maoni yangu, R. OTHMAN atatakiwa kuwajibika (kujiuzulu) pale ambapo kashfa itakayojitokeza itaonekana imetokana moja kwa moja na uzembe (kutowajibika) kwa chombo anachokiongoza.

Anachotakiwa kufanya sasa Mkurugenzi huyo pamoja na vyombo vingine vya dola ni kuhakikisha kwamba kashfa dhidi ya CHENGE inafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mhusika zitekelezwe ipasavyo.
 
Hivi kuna mtu ana ushahidi kuwa Othman Rashid hakupeleka taarifa husika kwa wakubwa zake? Hapa naona anashambuliwa sana, na kwa kawaida yeye hawezi kujibu. Nataka kumtetea ktk hili
 
Maneno yako kwenye red ndiyo sababu kubwa ya kufanya RO atoke hapo na kujiuzulu haraka sana maana ameshindwa kuwajibika kwa chombo anachoongoza - kulinda usalama wa taifa la watanzania na mali zao! grrrrrrrrrrr
 
Hivi kuna mtu ana ushahidi kuwa Othman Rashid hakupeleka taarifa husika kwa wakubwa zake? Hapa naona anashambuliwa sana, na kwa kawaida yeye hawezi kujibu. Nataka kumtetea ktk hili

Kazi yake sio kupeleka taarifa tu, Kazi yake ni kuzuia mambo kama haya kutokea - hii ndiyo kazi ya usalama wa taifa --- kituo kilichojaa (full stop).
 
Hivi kuna mtu ana ushahidi kuwa Othman Rashid hakupeleka taarifa husika kwa wakubwa zake? Hapa naona anashambuliwa sana, na kwa kawaida yeye hawezi kujibu. Nataka kumtetea ktk hili

tatizo siyo yeye kupeleka taarifa; tatizo ni kuwa taasisi yake imeshindwa kukusanya taarifa za kijasusi ambazo zingeweza kuzuia sabotage of our country and plunder of our resources. Taarifa baada ya wizi zinasaidia vipi kuzuia wizi!?

Kwanini atoe taarifa kwa SFO na vyombo vingine vya nje vinavyofanya uchunguzi wakati vya kwetu "vinasubiri uchunguzi ukamilike". Kwa vile umeamua kuwa mtetezi wake naomba ujibu maswali yafuatayo:

a. Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 na sheria iliyounda TISS ya 1996 neno "Usalama" lina maana gani?

b. Sheria inapozungumzia "maslahi mengine ya Jamhuri" ina maana gani kama mojawapo ya maslahi hayo ni ulinzi wa fedha yetu na raslimali zetu nyingine?

c. Kwanini hadi hivi sasa siyo yeye au msemaji wa Taasisi hiyo ambaye amekanusha kuhusika kwa wafanyakazi wake au taasisi nzima katika BoT, au katika kumwagiwa "chemicals" kwa Kubenea. Kwanini RO yuko kimya wakati sheria haimkatazi hata kidogo kutoa taarifa kwa walipa kodi wa taifa letu?

d. TISS wamepata wapi majukumu ya kushiriki katika ulinzi wa viongozi au kutoa habari kwa viongozi kuhusu mambo ya kisiasa ambayo yanweza kutumiwa kisiasa?

Hapo ndiyo tunaanzia.
 
Kazi ya Usalam wa Taifa ni kukusanya taarifa, kuzichambua na KUSHAURI kwa vyombo husika kuchkua hatua zinazostahili. Wao kama Taasisi hawana nguvu ya kukamata, siku watakayofanya hivyo wataambiwa wameingilia kazi ambazo sio zao. vi kwa mfano, Othman amepata taarifa za ufisadi na akazipeleka ktk vyombo husika kwa hatua za kisheria, na kule alikopeleka wakaamua kuwalinda mafisadi, tena kwa vifungu vya sheria, unadhani Othman afanje nini? Mimi nadhani hapa sio Othman tu, tatizo ni mfumo mzima wa kushughulikia masuala ya Usalama wa Nchi. Sheria zetu bado zinampa nafasi kubwa mharifu kuendelea kutanua. Badala ya kumlaumu Othman, nashauri tuangalie mfumo mzima na mapungufu yake. Leo hii hata Othman akitoka, bila kubadilisha mfumo, mambo yatakuwa ni yale yale tu. Punguzeni madongo kwa Othman jamani
 
Wewe wenzako wanajaribu kumuepushia Kikwete balaa kwa kujaribu kumtwisha Othman mzigo (kama vile Kichaka alivyomtwisha lawama yule mzee wa siaiei) naona wewe unataka kurudisha mpira kwa JK.

yangu macho hapa ......
 
ukweli ni kuwa hawa jamaa dhana ya kujiuzuru bila kushinikizwa haipo akilini mwao.
yaani ile aibu ya kibinadamu hawana.

kuna mtu anaitwa hosea wa takukuru alitajwa wazi kuwa anahusika kwa kuficha ukweli katika lile skendo la richmond, lakini leo hii na cheo kingine kaongezewa.

kuna huyu mwanasheria mwanyika ambaye amehusishwa katika skendo la richmond still yupo anakula nchi na shuzi lake limeshapoa.

so huyo othman rashid akiangalia msululu uliomtangulia then ataufuatisha tu ule msemo wa wazungu " i learn from the best" kisha atanyamaza kimyaaa na ndio itakuwa imetoka hiyo...so watanzania tuamke
 
Kazi ya Usalam wa Taifa ni kukusanya taarifa, kuzichambua na KUSHAURI kwa vyombo husika kuchkua hatua zinazostahili. Wao kama Taasisi hawana nguvu ya kukamata, siku watakayofanya hivyo wataambiwa wameingilia kazi ambazo sio zao. vi kwa mfano, Othman amepata taarifa za ufisadi na akazipeleka ktk vyombo husika kwa hatua za kisheria, na kule alikopeleka wakaamua kuwalinda mafisadi, tena kwa vifungu vya sheria, unadhani Othman afanje nini? Mimi nadhani hapa sio Othman tu, tatizo ni mfumo mzima wa kushughulikia masuala ya Usalama wa Nchi. Sheria zetu bado zinampa nafasi kubwa mharifu kuendelea kutanua. Badala ya kumlaumu Othman, nashauri tuangalie mfumo mzima na mapungufu yake. Leo hii hata Othman akitoka, bila kubadilisha mfumo, mambo yatakuwa ni yale yale tu. Punguzeni madongo kwa Othman jamani

Lol I thought wana power ya kuarrest kama walivyo PCCB? I'm 100% wanayo hiyo power(baada ya reform wakati wa kipindi cha Mkapa wakapewa na vitambulisho vipya-gamba jekundu-)

Kama walishindwa kung'amua kuhusu Richmond nini kazi ya maagent wao ubalozini? sidhani Police force yetu na PCCB nao wana watu wao ubalozini.

Hivi alivyo wapeleka wana njeje kwenye harusi ya mwanaye zilikuwa ni hela zake za mfukoni au jamhuri?
 
Power of Arrest HAWANA. Nina imani kama wangukuwa nayo, wangeweza kujitoa ktk aibu. Kujieleza ktk JF hawawezi, kwani maadili HAYAWARUHUSU, basi wanabaki kubamizwa tu. Let's do justice to Othman, kazi yake ni ngumu sana kwani anaweza kutamani kufanya vitu furani lakini mfumo unambana. Punguzeni kumtupia madongo namna hiyo.
 
Mbona wanajieleza tayari kupitia kwako?
 
Kinvaba, ni lini TISS walifanya shughuli za ujasusi ambazo zimesababisha vyombo husika kufanya kazi yake ya kukamata?

a. Kama RO alijua kuhusu Richmond, Benki Kuu, na Chenge na akatoa ushauri akakataliwa na alijua yuko sahihi, alipaswa kujiuzulu wakati huo.

b. Kama hakuwa na taarifa za mambo hayo na baadaya akazipata taarifa hizo na akatoa ushauri ambao ungeweza kuzuia uhalifu wa EPA na taarifa hizo hazikufanyiwa kazi au alipuuzwa kwa sababu ya mfumo, alitakiwa kujiuzulu au kumshauri Rais kuhakikisha sheria mpya ya kuwapa nguvu ya kukamata, kupekua na kubamba. Ameshindwa kufanya hivyo hana budi kujiuzulu.

c. Kama anaona kazi yake ni ngumu kwa sababu ya mfumo, na ameamua kuendelea kufanya kazi katika mfumo mbovu kama huu ambao kazi yao ya kukusanya na kutoa ushauri ingeweza kufanywa na wanafunzi au idara ya kulipwa basi hiyo pia ni sababu ya kutosha kwa yeye kujiuzulu.

Ameshindwa kumshauri Rais kuhusu EPA
Ameshindwa kumshauri Rais kuhusu Deep Green, Mwananchi, Tangold, na Meremeta

Ameshindwa kumshauri Rais na Waziri Mkuu kuhusu Richmond kampuni feki

Ameshindwa kuanzia a => x na kama alifanya jambo lolote na hakusikilizwa au kutiliwa maanani basi hiyo ni SABABU TOSHA YA YEYE KUJIUZULU!
 
Nadhani wakati umefika wabunge wetu wamtolee uvivu. Hivi mnakumbuka jinsi gani wakurugenzi wa CIA na FBI walivyokuwa grilled kuhusu "the failure of intelligence". Kosa moja liliigharimu marekani maisha ya karibu watu 3000, sisi wakurugenzi wetu wamefanya mangapi? na matokeo yake yakoje.

..wabunge wataanzia wapi?

..kila siku wanazidi kufungwa midomo!
 
Mwanakijiji,

Asante kwa kuleta tena hii issue.Tulishazungumza sana hapo awali hapa hapa JF kuwa Usalama wa Taifa si Usalama tena wa Taifa letu bali ni Usalama wa Mafisadi! Hawa jamaa wakiongozwa na Rashid Othman wameshindwa kazi yao! Hawa jamaa inaelekea nao wanakula pamoja na mafisadi au wamelala usingizi wa pono kiasi kwamba hawasikii wala kuona nchi yetu inakwenda wapi! Wao kazi ni pale Mrema au CUF au wapinzani wanapofanya maandamano au wanafunzi wa chuo kikuu wanapogoma hapo ndio utawaona vinara hawa wakihaha huku na kule lakini inapofikia suala la maslahi ya Taifa hawako tena kazini wapo gesti na vimwana wakila raha...
Sasa kama Usalama wa Taifa unashindwa kupenetrate na kufichua hizi deal za mabilioni ya fedha jee hawa watu wataweza kutuletea habari za uvamizi wa Taifa letu pindi linapotaka kuvamiwa! Wananchi wa mikoa ya Kagera na Kigoma wamekuwa wakilia karibu kila siku kuhusu kuvamiwa kwa ardhi zao na warundi na watusi lakini si polisi au Usalama wa Taifa wamesikiliza.

Sasa mkuu naona umefika wakati wa kuanzisha petition ya kumwondoa Rashid Othman katika kazi yake na kuwapa vijana hodari,wenye machungu na Taifa lao.
Inavyoelekea Rashid Othmani anafanya kazi zake kiushikaji tu bila ya kutanguliza maslahi ya Taifa letu.Tanzania kuna zaidi ya watu milion 30 najua wapo watu wenye ujuzi,elimu,machungu,na usongo wa kuliendeleza Taifa letu na sio watu kama Rashid Othmani ambao wako hapo kula maraha na kutanua tu huku nchi ikifilisiwa namna hiyo!

Tunaomba wanaJF tuanzishe Petition ya kumwondoa Rashid Othmani mara moja katika nafasi yake ili apewe mtu mwingine mwenye uzalendo,usongo,maadili,ujuzi,elimu, na uchungu uliotukuka kwa Taifa letu ili aongoze chombo hiki muhimu kwa Taifa letu.

-Wembe Mkali.
 
Kujiuzuru ktk jambo hili hakutaleta mabadiliko yeyote zaidi ya kufurahisha umma tu. Ni afadhali aendelee kubakia na kushauri mabadiliko yafanywe kadiri atakavyoweza.

Kuanzia mwanzo nilisema wazi kuwa nitajaribu kumtetea Othman kwa kulazimishwa kujiuzuru eti kwa kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Kuna mambo mengine yamefanyika wakati Othman sio Mkurugenzi. Lakini jambo jingine ni lazima ulijue, kama Othman atamshauri KIONGOZI wa juu yake, na kiongozi huyo akaamua kupuuza ushauri wake, yeye afanye nini? Lets be realistic here. One will say 'ajiuzuru' but kujiuzuru kwake kutaleta ufumbuzi wa tatizo?

Tutumie akili zaidi kuliko jazba ktk kumhukumu Othman jamani.
 
Mojawapo ya credibilty ya kiongozi ni kujiuzuru kama unaona ushauri wako hautekelezwi, kwanini hakujiuzuru kama aliona ushauri wake unaonekana hovyo, Lakini mnaomtetea mkumbuke kuwa akiagizwa kuwafuatilia JF anafanikiwa lakini hafanikiwi kuwafutilia magaidi walioteka nchi yetu.
Huyu anaongoza taasisi mojawapo ya kulinda masirahi ya mafisadi na ndo maana hawezi kujiuzuru hata kama hasikilizwi.
 
Kujiuzuru ktk jambo hili hakutaleta mabadiliko yeyote zaidi ya kufurahisha umma tu. Ni afadhali aendelee kubakia na kushauri mabadiliko yafanywe kadiri atakavyoweza.

Nadhani akiuzulu ili aufurahishe umma nadhani siyo jambo baya kama unavyotaka lionekane. Sijui kama kinyume chako ni jambo zuri.

Kuanzia mwanzo nilisema wazi kuwa nitajaribu kumtetea Othman kwa kulazimishwa kujiuzuru eti kwa kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Kwa kushindwa kutimiza wajibu wake na kiapo alichokula.

Kuna mambo mengine yamefanyika wakati Othman sio Mkurugenzi. Lakini jambo jingine ni lazima ulijue, kama Othman atamshauri KIONGOZI wa juu yake, na kiongozi huyo akaamua kupuuza ushauri wake, yeye afanye nini? Lets be realistic here. One will say 'ajiuzuru' but kujiuzuru kwake kutaleta ufumbuzi wa tatizo?

Kutatuonesha kuwa viongozi wanapotoa ushauri wenye maslahi kwa Taifa lazima wasikilizwe na kama angefanya hivyo basi tungemtetea kuwa "alijaribu". Sijui kama unakumbuka yule afisa kilimo wa Arusha aliyeamua kujiuzulu nafasi yake kama miaka minne iliyopita baada ya onyo lake la ujio wa nzige kupuuzwa. Aliamua kuachia ngazi kwa sababu maafisa wa ngazi za juu wa kilimo hawakumsikiliza. Hujalisikia jina lake mahali popote kwa sababu hatukumuunga mkono na kusema alifanya kitu muhimu na cha kuwajibika. Kama RO alishauri kuhusu Richmond, EPA n.k na hakusikilizwa anaendelea nini kutoa ushauri usiosikilizwa? Aidha hawamuheshimu au hawajali ushauri wake au yote mawili!

Tutumie akili zaidi kuliko jazba ktk kumhukumu Othman jamani.

Bahati nzuri akili ni nywele...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom