Rashid Othman ndiye Boss wa Usalama

Status
Not open for further replies.
Kingwele please . I have got no beef na waislam na hakuna mahala mimi Mugishagwe nimehoji waislam kupewa madaraka . Naomba copy kipengele unipe tafadhali .Sina muda na malumbano ya kidini na kama alivyosema Mkwawa jamaa kesha pewa piga ua yeye ni DG hakuna la zaidi .

Nashauri swala la Mahiga Mzee Es liache tu maana linatu derail toka kwenye mada ya maana maelezo yake yanatosha we need more info about Mr. Mahiga . I personally have no beef na DG mpya lakini sasa ni mwaka 2006 we need to know him .Maana ni mkuu wa Usalama wa Taifa la Tanzania ambako ndiyo sisi Watanzania .Kuna maelezo mepesi yanatolewa kama yale ya Serikali na mapanki lakini kwa kina RO hajulikani sasa tunaomba CV . Kama huyu jamaa CV haitapatikana nitamuoma Mzeeshughuli Bwana afunge mjadala maana maelezo na mabishano bado hayajajibu maswali yale . Tukiri kwamba hatujui CV yake japokuwa yeye mwenyewe mwaweza kumjua .

Swala kuja mtu akawekwa kwa TZ is very much possible . Juzi Makamba kapewa Ubunge then kapewa UCC mkuu , Meghji hana hata jimbo kapewa na kupewa Upesa , wako wengi kwenye Serikali ya JK wamepewa pewa tu kwa sababu moja ama nyingine siwezi kushangaa kama DG atakuwa kwenye mkumbo huo ama hapana .

Kasema majambazi kwa uwazi na wizi wa kura na kuwabana wapinzani mbona hajasema ?
 
Mzee Muggy,

Una point, sasa ninaona ni mazungumzo tu baada ya habari na Chakubanga! Nimenawa mikono na kuwaachia wananchi waamue ukweli uko wapi.

Es -

Sindano Ya Motto!
 
tafiti,

Unajua mara nyingi huwa sipendi kuwaingiza watoto wa JK kwenye mijadala yetu. There are very nice ukimuondoa mmoja ambaye ni tapeli wa kutupwa nadhani hata baba yake anajua hilo ndiyo maana sehemu yoyote ile hatajwi kama ni mtoto wa JK hata wakati wa uchaguzi waandishi wa habari walikuwa wanaandika JK ana mtoto mvulana mkubwa mmoja ambaye ndiyo huyo anayefanya masters yake UK. Mpaka leo huwa tunajiuliza hivi ni kivipi JK alimuacha mtoto wake asote jela US kwa kushindwa kumlipia kiasi kidogo cha hela, Je alikuwa amechoka au alikuwa hana hela? Leo hii mnapotuambia ana hela za kuwasomesha lazima tujiulize.

Halafu hii issue ya Mahiga sijui mnaipeleka wapi, mtu akisema Mahiga anafaa haimaanishi kuwa rais amuondoe RO na amuweke Mahiga. Kama mimi naamini JK siyo kiongozi bora kuliko wanachama wote wa CCM lakini hey ni rais, huwezi kunilazimisha nisema haya tumuondoeni JK tumuweke Salim. Mtu mbovu ni mbovu tu, kuanzia hapo tunaanza kufikiria tufanye nini. Hapa tunapiga kelele we kwa JK, itakapofika 2010 pengine tutakaa na kuangalia huyu ni JK na hawa ni wagombea wengine na vyama vyao tutaishia kumpa yeye. Hivi watu hamjiulizi ni kivipi Bush alishinda wakati approval rate ilikuwa below 40%.

Kwa nyie mnaotaka kuingiza mambo ya dini naomba tu muache kwa maana nimechoka post zangu kuwa deleted kila mara ninapotoa michango ya kidini.
 
Tafiti,

Asante, Jina lako sio baya, ila naamini kuwa acha watu waseme una fikira muruwa, wewe jione ni duni tu. Jasusi acha nibakie FD. Hata Yesu alisema: ukienda kwenye harusi kaa kiti cha nyuma, inakuwa fahari pale bwana harusi akija kukunyanyua na kukupeleka viti vya mbele!!. kuliko ikiwa vice versa.

Back to the mjadala, Kwanza nimegundua tafiti hujatumwa, point nzuri. Mzee Es naomba kutofautiana na wewe kuhusu hilo, laiti kama angetumwa... angeshaleta CV ya RO, au anayo lakini kwasababu ni mbaya hataki kuianika??!!. Ila hoja za ES nyingi hazijajibiwa. Bado Tafiti kuna mengi unatakiwa ufanye utafiti, especially swali alilouliza ES na baadaye akauliza Seleman. Fanya Utafiti utupe vyeo vipo vipi huko UWT, kisha jibu swali.

Kingwele, Tulia kwanza kaka ufikiri kisha andika. Acha kuvamia.

Nimeshamaliza kupeta na kuchambua mchele na pumba.

FD
 
Nilidhamiria kuufunga mjadala maana ulisha poteza mwelekeo lakini rai mzee FD inanifanya niache maswali yajibiwe ili tuone nini hasa kimo ndani ya nyumba hii . Ok tuvute muda kidogo na sasa msisitizo ni kwa RO na maswali yajibiwe sasa tujenge hoja hata angalau vyeo tuuuuuuuuuu tupewe tujuwe ama ni siri kubwa ?
 
MzeeShughuli,

Ahahaha umenikumbusha mamaaShughuli Amina Chifupa Mpakanjia, au wewe ni mzee Mpakanjia??! (natania)

Yap! Utafiti unahitaji MUDA nami nimeonelea tumpe tafiti muda, yeye huwa anafanya utafiti wa kina.
 
Salaamz wanaforum,

Mimi mpya humu, inaonyesha kuna watu makini na wenye uchungu na nchi, ila ni wazi kuwa kuna ambao wako biased against rais JK and every move he makes. JK kama binadamu atakuwa na matatizo yake, lakini isiwe hata mazuri yake pia yakageuzwa kuwa ni mabaya.

Nimeshangaa kwa mfano mtu anatoa hoja kuwa uteuzi wa Saidi Mwema kuwa IGP ulikuwa based merely on ushemeji! ..C'mon, the guy was a heading Interpol SRB (Sub Regional Bureau) in Nairobi, ambayo ina-cover the whole of east Africa and beyond. I am of the view kuwa he was the man for the job.. sasa asipewe kwa kuwa tu, if at all it is true, ana ushemeji na rais?

Mzee ES, nnaenjoy data zako, kama ni za kweli zinatupa mambo ambayo mengine hatuyaoni katika vyombo vya habari... you must be well placed. Hata hivyo, nimeona mara nyingine unaexagerate, kwa makusudi au kwa kutojua. Kwa mfano, in what someone called a million dollar question unadai eti RO amepanda kutoka agent wa kawaida na kuwa Mkurugenzi katika kipindi cha miezi kumi tu, na kuwa eti Oktoba mwaka jana alikuwa bado yuko London. Hii si kweli! Si kweli kuwa alikuwa 'agent wa kawaida' tu pale London. Na pia Oktoba mwaka jana alikuwa ameshaondoka. RO aliteuliwa na Mkapa kuwa mkurugenzi wa utawala (Chief of Staff) usalama mwezi Desemba 2004. In that capacity, amekuwa akikaimu mara kwa mara nafasi ya ukurugenzi inapokuwa Mzee Apson hayupo, sasa unless iwe alifanya blunder katika kazi yake .. promotion to the post was a natural thing to do. Siku hiyo hiyo ya uteuzi wa RO, aliteuliwa pia Mr. Anthony Itatiro kuwa State House Controller ambayo kabla ya hapo alikuwa ni deputy Controller to Mr. Fanuel Kuzilwa aliestaafu.. see what I mean, a natural promotion.

Wanaodai CV ya RO nawatakia kila la heri, maana kwa mtazamo wangu mimi si rahisi CV ya mtu aliekuwa usalama full time kwa zaidi ya miaka 25 kuwekwa hadharani with all the details. You could get stuff like his education .. bachelors degree mlimani na masters in sheffiel UK; vitu kama 'special training', assignments na post nyingi ni za siri. Hata Dr. Mahiga, with all my respect to his accomplishements, CV yake niliyoiona netini haikutaja kwa uwazi kuwa alikuwa usalama na alishika cheo/vyuo gani (miaka hiyooooo ya zamani). Na hata yeye kuitwa shahidi X katika kesi ya uhaini ni dalili kuwa si rahisi kazi hizo kuwekwa hadharani. Pia kama lengo la kuipata CV ya RO ni ili ilinganishwe na ya Dr. Mahiga naona ni kupoteza muda. Dr. Mahiga hakuwa shortlisted for the job, ni vyombo fulani tu vya habari vilivyoamua kuzua hilo kwa msukumo/sababu wanazozijua wenyewe. Yaani ni sawa na kulalamika kuwa timu fulani haikuwa bingwa wakati haikuwemo kabisaaa katika ligi.

Kuna watu wamejenga fikra kuwa eti teuzi za JK zinazingatia dini, na wamekaa tayari tayari kusubiri nani atakuwa mkuu wa majeshi. Hii inaonyesha, by any chances, akiteuliwa mwenye jina like Abdallah Omari itakuwa kelele nyingi sana kabla hata ya kuangalia qualifications zake.

Nawasilisha.
 
Kulikoni,
Karibu sana Mzee. Hebu tupe orodha ya watu waliokuwa shortlisted.

Naona hii forum imekuwa Homepage ya watu wa usalama na serikali which is good.
 
Mzee ES
Hawa watu siku hizi wanaingia wana post mara moja halafu wanakimbia, ninachoshukuru hii forum imekuwa homepage yao.
 
Kulikoni,
karibu sana. Kwa taarifa yako Saidi Mwema alipokuwa RPC Mbeya kulitokea vifo vya mahabusu 20 katika rumande ya Polisi. IGP Mwema, wakati huo RPC, alipaswa kujiuzulu, au kustaafishwa kwa uzembe.
 
Yule mpumbavu wa kwanza sina hata haja ya kumuongelea.

Sam, you are becoming too soft.

Joka kuu, point, point bro.

Kulikoni, point point umesema ukweli kuhusu RO, natural promotion. At least wewe umetoa mwanga kidogo.
Lakini pia ukweli unabakia pale pale kuwa ni shemeji wa JK au??!? awe mchapa kazi hodari au mvivu mpaka mahabusu wanakufa kwa kurundikwa bado anabakia shemeji mzee.
 
Kulikoni,

Sorry, nilelezee na sifa ya Rajabu Adadi?? unafahamu ana uhusiano gani na JK??!!??, Je alistahili ubalozi wakati kavurunda kwenye U DCI?

Msitetee kulindana, na kusaidiana ki undugu na udini, jamaa woote waliojaa pale foreign bado unamteua mtu aliyeshindwa kazi hii akajaribu nyingine???????
 
Itatiro, kabla ya kuchaguliwa Ikulu alikuwa Acting Balozi Zaire, kabla ya kwenda Zaire alikuwa Protocol, na anakaa kule Segerea acha uongo wa mchana,

Mzee JM alipokwenda US mwaka jana kabla ya uchaguzi, ilikuwa ni wiki ya mwaisho ya mwezi wa TISA, SEPTEMBER, OTHMAN alikuwa pale London akajificha kabisaaa, mpakak mzee alipooondoka ndipo akajitokeza tena,

Ninakuomba umtaje kiongozi wa juuu Mkristo aliyechaguliwa in the last TWO MONTHS, JK anapofanya mazuri tunasema lakini samahani kumnunulia ndege ya shillingi BILLIONI 45, halafu akasafiri na ndege zingine wakati hiyo imekaaa tu sio political plus! Kusafiri na kundi la wajumbe 50, kwa wakati huu mgumu kwa nchi yetu kipesa sio political plus! Kumfukuza Mahalu kuwa ni mwizi bila ya kumfunga jela au kumpeleka mahakamani sio plus! Kuwaonea polisi wadogo 15, wakakti anashinda na mijambazi kina BM, Kigoda, Sumaye, EL, RO, sio plus! Kuipa mikoa shillingi BILLIONI MOJA kwa ajali ya ajira badala ya kuanzisha ajira kupitia serikali kuuu ni kuanzisha ulaji! Mzee EL kitendo cha kupita pita kwa wahindi anachofanya sasa hivi kwa kumtuma agenti wake sio plus, na tunajua usifikiri tumelala!, kumpeleka Private Advocate kuwa balozi wetu kituo muhimu kama London ni upungufu wa uwezo wa kufikiri, kumfukuza Mhandisi wa wilaya baada ya jengo kuuungua ni utoto!

I could careless kama una-enjoy my posting or not, ninaweka ukweli and let the chips fall where they may, and I am proud of it kuwa this time nimegusa panapotakiwa na huu ni mwanzo tu, mambo yenyewe bado kabisaaa, mpaka hawa viongozi watakapoelewa kuwa sisi wabongo sio wapumbavu kama wanavyofikiri, haya nenda ukawaambie waliokutuma kuwa huku kuna motto ,

Yaani hapa ni "KUMKOMA NYANI GILADI" manake hapa tunampiga nyani usoni bila huruma! Next time waambie wakupe data za kweli bro! hizo za kina Itatiro ni fake!
 
About Itatiro's previous being deputy prior to his promotion, I read it from Daily news (It is here: http://www.dailynews-tsn.com/news.php?id=2932) Kama mwandishi kadanganya, I admit to be misled.

RO kuwepo London Sept mwaka jana, labda iwe alikuwa safarini mara moja.. but he was already Chief of Staff in Dar since Dec 2004. Go and recheck.

We don't need to go two months back, two other appointees were sworn in the same day RO was sworn in by JK, they were both Christians.

Prof. Chachage kabla ya kufariki aliulizwa maoni yake nini baada ya JK kuteuamabalozi watano na wote waislamu, alijibu kuwa kabla ya kutoa maoni itabidi tupate list ya mabalozi wetu wote kisha tuhesabu kabla ya kutoa maoni.

Baada ya uteuzi wa wakuu wa wilaya, Askofu Sylvester Gamanywa aliandika katika gazeti la Msemakweli kuwa takwimu zinaonyesha idadi ya wakristo ni kubwa mno kulinganisha na wa dini nyingine. Akahoji kuwa kama idadi hiyo ingekuwa ni ya waislamu hali ingekuwaje... na kusema 'bila shaka yangetokea maandamano kupinga uteuzi huu'.

Tusiwe na prejudice.

Ikiwa kusafiri na presidential jet kunagharimu pesa nyingi sana, (I hear it cost no less than Tshs. 100M just to fly from Dar to London!), I would consider it a plus kusafiri kwa ndege nyingine ya gharama nafuu.

I am not sure if it is the president who is supposed to send Mahalu to prison or bring him to court. Kuna vyombo husika .. and for all I know they are working on it.

Yes, I am equally puzzled by some of the appointments and decisions. Like I didn't see Makamba being katibu mkuu wa CCM, or private advocate kuwa balozi sehemu nyeti kama London. Yeah .. kufukuzwa engineer on the spot was also a bit of show off.

Uhusiano wa JK na Adadi Rajabu siufahamu, enlighten if you wish.

Yes kukosoa ni muhimu pale sirikali inapoenda kombo but let's give credit when it's due.

Naungana na wengine kuwa hatuna haja ya kutumia matusi.
 
Kwa sasa MR kulikoni umeanza kuongea angalau vizuri.

Maana uliingia kwa mkwara mpaka nikasema la! huyu jamaa vipi!


Mimi hilo la idadi ya wateuliwa kutoka DINI FULANI huwa sipendi kuliongelea sana. Ila ninachosema ikitokea JK akawa anateua watu kwa kufuata Dini basi atajimaliza haraka SANA NA ANWEZA KUTAWALA NCHI HII KWA MIAKA 5 TU!!

PIA IKUMBUKWE KUWA IDADI YA WAISLAMU NI NDOGO KULIKO WAKRISTU KWA HIYO KINACHOTAKIWA NI PROPORTIONAL NA SIYO NUSU KWA NUSU. ILA HATA HIVYO KATIBA YETU HAIRUSHUS MTU KUPEWA NAFASI KUTOKANA NA DINI YAKE!

Mpaka sasa sidhani kama ana hayo mawazo ingawaje siwezi kuamani kwa asilimia mia!

Ila kuhusu uteuzi wa Rajabu, Mapuri ulinifanya nijiulize mara mia mia kuwa hivi kweli JK yuko serious??!
Nikasema hii siyo recycling aliyoikataa alipohojiwa na BBC??

MAMBO KAMA HAYA JK AKIYAKWEPA ITASAIDI WATU KUONDOKANA NA PRECONCEPT!

Nikaanza kuwa na MAWAZO KUWA HIVI NI KWELI RAIS AKIINGIA IKULU HUWA ANAUNGUA UGONJWA WA KUZIBA MACHO NA MASIKIO?

ANYWAY TO BE HONEST BADO NINA IMANI NAYE KUBWA TUMPE MUDA.
AKILIKOROGA ATALINYWA TU!!!

Mr Kulikoni humu kuna wakongwe kama akina Mzee ES, SAM mugy, FD, Ogah etc, ulikosea sana kusema hatuna point, ila kama ulivysema tuyaache hayo.

ninamuunga mkono mzee ES kwamba kuna wakati mwingine watu wanapigwa nyundo kichwani hapa hapa!!

ALUTA continua!


Everything is possible under the sun!, though people tend to forget!!!
 
tafiti
Nakupongeza kwa kujaribu kuonyesha njia mimi bado nasema naomba kila mwenye info aje hapa aseme ili tujue ni udini ama kazi kweli .Najua kuna wenye info hapa .Kusema Msc mzee mbona ziko kibao sisi tunaulizia kazi kweli kweli shule yake.

nakupinga kwa kasi zote juu ya kuanza kwa kishindo kwamba ndiyo kuonyesha kwa nini aliteuliwa mzee . JK aliungruma Dodoma nilimsikiliza na kumuon LIVE sikutegmea kwama akiwa huko huko semina Endelezi angeaza ku back off from his remarks kwamba Zenji na Muungano kuna utata . Sasa ma speech ama hata masomo ya aina ya RO mzee huandaliwa na anaweza kuelezea bila ya uoga lakini kazi inakuja kwenye kazi .

Mimi bado nasema tunaka kujua kama kapata kikazi na je alikuwa achukue yeye baada a Apson kwa maana ya kwamba alimfuatia ama ni udini .Ili kuwa watanzania hatutaki udini ndiyo maana swali langu linabakia tuwasikie wengine . Hongera RO kwa kutema Cheche Arusha lakini kazi ifanyike kwa speed ya Cheche zako. Uwe usalama wa Nchi na si Usalama wa CCM na rais na wapinzani wasiishi kaa wakimbizi na ukate Usalama kutumiwa kuiba kura kwa ajili y Boss wako next time .
 
Tafiti then jadili

Hebu tupe mwaka aliosoma hizo shule za Iliboru na St. Mary's na mwaka aliojiunga Chuo Kikuu kwani maelezo yako hayawiani na yaliyokuwepo wakati huo.

Huyu RO alipopandishwa cheo mwishoni mwa utawala wa Mkapa, watu wengi hawakufurahishwa na kitendo hiki siyo kwa sababu haiwezi kazi bali alikuwa karibu mmo na walioshika mipini ya Serikali. Nakumbuka kwenye sherehe ya kumpongeza pale Ikulu watu wengi walilalamika wakiwepo wazee wakongwe kwenye Usalama na JWTZ - Usalama.
Mpaka leo hii watu wanajiuliza ni procedure gani zilitumika lakini hatujapata jibu.

Mimi sina shida na yeye kuwa DG wa UWT, lakini hii nafasi inatakiwa apewe mtu ambaye anakubalika kwa wenzake hasa wale wanaofanya kazi yenyewe. Kumbuka wachapakazi wa UWT ndio uti wa mgongo na kama uti wa mgongo hauungani na kichwa basi hamna kitakachotoea.

Kuendana na uzoefu wangu na kuujua UWT, nadhani tutajionea wenyewe, tutakuwa na wanasiasa kwenye hiki kitengo muhimu kuliko kuwa na Usalama wa kweli. Tutarudi kwenye ile enzi ya Mahita na Jeshi la Polisi.

Kile kiapo cha kazi ya Usalama siku hizi hakina nguvu tena, siku za nyuma kidogo UWT ulikuwa unafanya kazi za kweli lakini siku hizi ni kusaidia wanasiasa tu.

BTW CV ya huyu Bwana haimo, ofisi ya Utumishi Serikalini,labda ipo Ikulu tu, tunaendela kuitafuta.
 
Tafiti hongera kwa tafiti zako,nimetosheka na wasifu wa huyu mheshimiwa bosi mpya wa usalama. Kumbe anashule ya kutisha kiasi hiki sio mchezo.Lakini kunamtu alitaka kujua walu elimu yake nk kitu ambacho kingetoa rough idea ya RO ni mtu wa namna gani,kwa maelezo ya wasifuhuu tumeshapata jibu.Kuna aliehoji kama mbona hizo Masters za MS zinatoka tu,nadhani anataka kutoa hoja kama jamaa atakuwa ameokota.Kumbuka amechukua UK recognized Uni na sio degree za web za marekani.Lakini pia mkumbuke kama ana fisrt class hivyo hii inazidi kutupa jibu kama jamaa sio Kilaza kama alivyochangia mtu mmoja humu.
Mimi sioni kama kuna mjadala tena na tumeoiona picha halisi ya Es kama licha ya kujikweza kama ana madata kibao na access to the information ameshindwa kulibani hat hili. Namimi nilimuona anajikweza pale alipodai kama ile habari ile kadhia ya Balozi na mpishi ameitoa Salva na anasema kama eti anawatu pale ubalozini London ina maan hao watu wamemdanganya au alikuwa ana bipu?tumekushtukia mzee.Hivyo experiance ya mire than 30 yrs on the same field na elimu aliyokuwa nayo sidhani kama kuna upendeleo umepita hapa.
Tafiti usisite kutupa mapya kama uko nayo..nimepanda sana tafiti zako na flow yako ya maelezo hii inaweza ikasaidia siku za usoni tukaepuka kuwaachia watu kuabdika wanayotaka hasa kwenye huu ulimwengu wa utandawazi.
 
Duh, Bw tafiti naona unajitahidi ku-live up to your name. Pamoja na hizo juhudi za kutafiti na kuleta wasifu/CV (pretty much all that can be made public) ambayo kumbe ni quite heavy, usishangae walio na misimamo yao sugu wakaikataa na kuipinga bila ushahidi. Wengine wameshaanza kuiwekea doubts bila kufafanua.

By the way, kuna jamaa nimemuuliza kiuchukozi kuwa eti naskia huyo RO hata English haipandi vizuri? akacheka sana na kusema kuwa lugha ana kipaji, wachilia mbali kiingereza, the guy speaks french, kihaya na kimasai .. while ni mtu wa tanga. Hatoshangaa ikiwa kiswedish na kibulgaria (if there is such a language) ikawa pia vinapanda to some extent.

Again, keep it healthy and clean.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom