Rare Pictures From My Personal Album!

tutafutie picha ya DC wa igunga alivyokuwa anaapishwa na mkuu wa mkoa alishika kitabu gani biblia au quran itatusaidia leo kumaliza mzozo imani ya DC huyu ipo wapi?
Una hoja,je kama alibadili katikati ya njia?
 
wakuu mwenye picha za kikosi cha yanga kilichotwaa kombe la cecafa mwaka 1993 pale Uganda atuwekee humu tuzione
 
mazee hizi picha ulizinunua pale k'koo sokoni nini? maana nakumbukua zilikuwa zinatandazwa pale na kuuzwa sokoni kwa nje..otherwise utakua kamati ya ufundi wewe ukisafiri na timu huku na huko!
 
Najua nitawakuna wengi sana kwa hii picha. Hii ndiyo Yanga iliyobatizwa jina la 'Umoja wa Mataifa'. Wazee hawa wangekuwa na marupurupu wanayopata wachezaji wa siku hizi wangefanya maajabu.

Kuanzia kulia kwenda kushoto ni:
Aboubakar Salum 'Sure Boy', John Alex, Thomas Kipese, Justine Mtekere, Said Sued 'Scud', nadhani ni mtoto wa Marehemu Abbas Gulamali, Said Zimbwe, Sanifu Lazaro, Salum Kabunda, Joseph Machela, Godwin Aswile, Athuman China, Issa Athumani, kipa msaidizi Sahau Kambi, kipa Steven Nemes na captain Keneth Mkapa.


33007955.jpg
sio zamani sana lakini kwa hakika mabadiliko ni makubwa mpaka sasa!

Inanikumbusha miaka zaidi ya 20 hivi ililopita, baadhi ya picha nyingi ninazo pia kwenye hard copies na by then zilikuwa zikiuzwa pale shule ya uhuru hasa studio moja inaitwa 'Snapy Snaps', sijui kama bado ipo.

Enzi hizo ukienda 'taifa' unawakuta manjagu wanakusanya za kwao na 'makomandoo' wakiwa wamekomaa haswa. Nadhani kilichofuatia hapo ni kuibuka kwa mtu mmoja aliyekuwa na vision lakini akakumbana na mawazo mgando ya tulio wengi, 'Mzee' Castro, George Mpondela na baadae akaingilia Mzee Reginald Mengi. Pamoja na wengine, hao walikuwa miongoni mwa watu wa mwanzoni walioamini kuwa klabu ingeweza kujiendesha bila watu waonajiita "wafadhili" wakati "wanafadhiliwa".

Cha kusikitisha miaka hii yote, bado somo halijakubalika. Mzee Akilimali na kijana Bakili katika mwaka 2012 hawaamini bado kama timu inaweza kuunda utaratibu wa kujiendesha bila kupata mtu wa 'kuigawia' pesa. Na hata akitaka uenyekiti ni lazima afikiriwe kwanza kabla ya wengine!

 
Back
Top Bottom