Hivi hawa wote wanaokufa ni wapinanaji wa CHADEMA? watanzania mbona sasa tunayumbishwa? mara waandishi mara wapiganaji wa CDMWakuu, mashujaa waliotoa uhai wao waenziwe, mfano, wale wa zamani, kina Mkwawa, wapiganaji wa majimaji,Mtemi Isike, Mirambo na wengi wengine. Hawa wamesahauliwa, tunasema eti tumepata uhuru bila kumwaga damu! Dhana hii si kweli hata kidogo.
Rangi nyekundu iongezwe katika bendera yetu ili kutambua na kuendelea kukumbuka michango yao na kutoa ujumbe kuwa tuko tayari kutetea haki yetu hata ikibidi kwa kumwaga damu. Bendera yetu inapotosha sana, wakati mwingine tunashindwa kutoa majibu tunapoulizwa ilikuwaje mkapata UHURU bila kumwaga damu!
Wale mashujaa wa zamani na hawa wanaoendelea kumwaga damu zao kupigania heshima na haki ya Nchi yetu, mfano mashujaa wa vita vya Kagera, na hawa wa hivi sasa wapewe heshima na kumbukumbu ya kudumu. Hili tutalisemea pia wakati wa kutoa maoni ya Katiba.
Sababu ya kuwapo kwa fikra ya kutomwaga damu ni kuwa tunaangalia kipindi kifupi cha enzi za TAA, TANU na hadithi za magamba. Kufanya watu wajinga na kudhani eti haki haipatikani kwa mapambano! Tulianza kudanganywa muda mrefu sana. Ukweli ni kwamba mapambano ya kudai haki na uhuru, heshima ya ubinadamu yalianza kipindi kirefu na sasa yanaendelea.
Kwa kuwa magamba hayakubali fikra mpya, CDM mlikumbuke hili mwaka 2015.
Lingine, CDM, anzisheni mara moja kitengo cha habari na documentation. Tunzeni matukio haya ya uonevu ya Morogoro, Iringa, Mbeya, Arusha na kwingineko. Tunzeni hard na soft copies, from time to time, wananchi wawe wanakumbushwa unyama huu na hasa mwaka 2015. Itawasaidia sana cz naamini kufikia kipindi hicho mtakuwa tayari mmeanzisha media zenu.
Mkifanya hivi, mtasaidia wengi na hata wale wanaodhani eti Watanzania wanasahau sana. Kama ni kweli, tuwasaidie Watanzania hawa kwa kuwakumbusha, waone, wasikie na kuchukua hatua.