Rangi Nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA ina maana gani?

I know what you are aiming at.But let me tell you frankly,it is too little,too late.
Napenda kusikia maoni yenu juu ya rangi nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA inayotumiwa kuandika signature ya Chadema huku ikiwa bolded na jina la chama hicho likiwa na muendelezo wa "aaaaaa" mwishoni.

Kuna lolote la ziada au ni ushabiki umekolea?

Naomba kujua kwa sababu maandishi na alama mara nyingi huashiria jambo hasa katika majukwaa ya kidini au siasa.
 
nchi za kiafrika zenye bendera zenye rangi nyekundu ni kiashirio kuwa kuupata uhuru damu ilimwagika.
 
kwa akili zao hawa jamaa na marangi ya hatari hatari kwenye mabendera yao tusijekushangaa mambo mabaya yakijakututokea
 
Nyeupe-maadili usafi
black-uafrika wetu
blue-mali asili (mito maziwa nk)
Nyekundu-UPENDO
 
Kipaumbele cha kwanza ni ELIMU
Kipaumbele cha pili ni ELIMU
Kipaumbele cha tatu ni ELIMU...
Mnaona umuhimu wa elimu watanzania. Kikanuni, katiba za almost vyama vyote vya siasa hufafanua maana ya rangi na alama zote zilizomo ndani ya bendera zao. Mtoa post una access na internet lakini hakutaka kutumia japo dakika 4 ku-google na kuisoma katiba ya CHADEMA aone imefafanuaje kuhusu rangi na alama zilizomo kwenye bendera yake. Hii imetokana na umakusudi wa CCM kuwafanya watanzania tusome na kufaulu mitihani na hawapendi tuwe wadadisi wa mambo na kupenda kusaka maarifa. Ukiwa mwanaCCM sio dhambi kusoma katiba za vyama vingine vya kisiasa na ukiwa huipendi CCM sio dhambi kuisoma katiba ya CCM. Kwa kukusaidia kidooogo, tafuta katiba ya CHADEMA then nenda kule mwishonimwishoni kwenye KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI CHAMA, sura ya kwanza. Utapata jibu lako. PIPOOOOOOZZZ!!!!
 
Napenda kusikia maoni yenu juu ya rangi nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA inayotumiwa kuandika signature ya Chadema huku ikiwa bolded na jina la chama hicho likiwa na muendelezo wa "aaaaaa" mwishoni.

Kuna lolote la ziada au ni ushabiki umekolea?

Naomba kujua kwa sababu maandishi na alama mara nyingi huashiria jambo hasa katika majukwaa ya kidini au siasa.

Naamini bendera nyingi zenye red maana yake zilijikwamua kwa kumwaga damu ss hawa jamaa sijui wana maana gani maana hata bendera ya nchi yao haina upuuzi huo nadhani ni sababu inayo wafanya kuwa na fujo zisizo na kichwa wala miguu muda mwingine
 
soma katiba ya CHADEMA"KANUNI NA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA"Rangi nyekundu ni ishara kuwa:Kama taifa tumevushwa na mashujaa kuelekea katika jamii yenye haki,na CHADEMA...Inaendelea
 
Rangi nyekundu ni kukumbuka maisha yaliyopotezwa na mashujaa wetu katika vita vilivyopigwana na mamangi,machifu na watemi WA Tanganyika kujikomboa na waarabu na wajerumani.
 
Napenda kusikia maoni yenu juu ya rangi nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA inayotumiwa kuandika signature ya Chadema huku ikiwa bolded na jina la chama hicho likiwa na muendelezo wa "aaaaaa" mwishoni.

Kuna lolote la ziada au ni ushabiki umekolea?

Naomba kujua kwa sababu maandishi na alama mara nyingi huashiria jambo hasa katika majukwaa ya kidini au siasa.

Mkuu nimefuatilia baada ya hizi story kuzungumzwa sana
Nimegundua habari ya rangi za bendera ni propaganda amabazo hazisadii
lolote kwenye uchumi wa nchi.

Nasema hilo kwa sababu,bendera ya nchi yetu haina rangi nyekundu
na watanzania tumejivunia hili kwa muda mrefu,lakini tujiulize
vipi bendera za nchi tunazoziita wadau wetu wa maendeleo
Angalia karibu wote bandera zao zina rangi nyekundu
nataja kwa uchache: USA,UK,Canada,Japan,Norway,China
na wengine wengi

Maelezo yanayotolewa ni kwamba nchi yetu ilipata uhuru bila kumwaga damu,
tujiulize kama hatukumwaga damu kwetu,vipi damu za wanajeshi wetu zilizomwagika
wakati wa kukomboa nchi za wenzetu chini ya misemo maarufu
TANZANIA HAIWEZI KUWA HURU WAKATI WENZETU WAKO CHINI YA UTAWALA WA KIBAGUZI je hizo hazikuwa damu?

Binafsi naamini rangi za bendera siyo issue ya kutugawa,
mbona hatujawahi hojI rangi ya bendera ya simba?
na simba sports club ina wafuasi wengi na hawajaleta madhara.

Naamini hata kama chama kina bendera nyeupe
lakini kina sera mbovu hakitufai,siasa za rangi za bendera
zimepitwa na wakati,tujari sera ndo zitatuletea maendeleo
na wala si rangi za bendera.
 
Back
Top Bottom