Rangi Nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA ina maana gani?

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Napenda kusikia maoni yenu juu ya rangi nyekundu kwenye bendera ya CHADEMA inayotumiwa kuandika signature ya Chadema huku ikiwa bolded na jina la chama hicho likiwa na muendelezo wa "aaaaaa" mwishoni.

Kuna lolote la ziada au ni ushabiki umekolea?

Naomba kujua kwa sababu maandishi na alama mara nyingi huashiria jambo hasa katika majukwaa ya kidini au siasa.
 
hiyo ni kuvuta attention za watu...hata wewe mwenyewe ukiona mahali palipoandikwa na rangi nyekundu utataka kujua pameandikwa nini...si sawa na kuandika kwa njano au kijani....:mmph:
 
Mbona Rangi za bendera ya chadema maana ya rangi zake inajulikana sana, vitu vingine jipe muda mwa kuvitafuta mwenyewe. kwa kukusadia wewe na hao wengine wanaoshabikia kuwa Rangi nyekundu ni hatari, fungua hiyo link hapo utaona maana ya rangi zote za chadema na kwanini walichagua hizo rangi.

Makala -Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Rangi ikishakubaliwa na taasisi yoyote kwamba ndio official color inaweza kutumiwa wa namna yoyote kufikisha ujumbe kwa walengwa, ama kwa maandishi au picha.

Uwe na amani tu hakuna ubaya wa hayo ulioyaona.
 
Rangi nyekundu inatukumbusha mababu zetu walimwaga damu wakati wa mkoloni nadhani CCM walizoea kutudanya kwamba Tanzania haikumwaga damu wakati wa kudai uhuru walisahau vita vya majimaji,walisahau Mtemi Mkwawa alijiua iliasikamatwe na wajerumani,walisahau Mangi Sina alinyongwa na wakoloni na nk.
 
RANGI NYEKUNDU NI RANGI YA KUASHIRIA DAMU INAYOENDELEA KUMWAGIKA TANZANIA, hasa kule migodini, damu inayomwagika kwa matukio ya majambazi kwa kushirikiana na Police, rejea sakata la Zombe.

Damu inayomwagika kwa watu kukosa huduma kutokana na Kina Rostam kuiibia Hazina ya Taifa, Damu inamwagika kutokana na KIna Lowasa kuliibia Taifa kupitia Richmond, Damu ya Kolimba, Imran Kombe, damu ya kila Mtanzania alieuwawa kwa makusudi ya watawala kwa Utashi wao huwakilishwa kwenye Bendera ya chama na nembo za CHADEMA.

CHAGUA CHADEMA ILI UWEZE KUSIMAMISHA DAMU INAYOTIRIRIKA TANZANIA.
 
Jamani, mbona mnajisahaulisha maana halisi ya rangi nyekundu?

ina maana wote mmesahau zawadi mnazonunuliana tarehe 14-02 (mnasema valentine day) zina rangi gani?

the answer is simple,,,, NYEKUNDU==UPENDO

Thats the meaning anaebisha abishe kama hatumia'gi rangi nyekundu kwa kuashiria upendo wake kwa naniliop
 
Jamani, mbona mnajisahaulisha maana halisi ya rangi nyekundu?

ina maana wote mmesahau zawadi mnazonunuliana tarehe 14-02 (mnasema valentine day) zina rangi gani?

the answer is simple,,,, NYEKUNDU==UPENDO

Thats the meaning anaebisha abishe kama hatumia'gi rangi nyekundu kwa kuashiria upendo wake kwa naniliop
hili neno!
 
kwa roho safi tu naomba mbadilishe bendera yenu kwa 7bu zfuatazo
1.haivutii
2.haimshawishi mtu(mgeni kutoka nch za nje) kuwa na hai ya kutaka kukifuatilia chama chenu na kukijua
3.rangi zake hazina uwiano
4.alama ya vidole viwili ni alama inayoashilia amani kwa kuwa nyie co watu wa aman..ndo mliowashawishi raia wa arusha kujifanya ma 'van damme' kwenda kuokoa watu waliokamatwa polisi na kuvamia polisi..
Ndio nyie nyie(sugu) mnaoambia wafuas wenu wapge mawe gari la jk
ndo nyie nyie(lema) mliosema 'fungen milango tupgane'..
Daaah bac inatosha
 
ukirusha jiwe jizani ukisikia mguno ujue limefika.

ccm wana bendera nzuri,sera nzuri,viongozi wenye sura nzuri baki hukohuko na wageni wako.
pipooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooozz........................................................................................................................................................................
 
Tunataka viongozi makini ndani ya chama siyo bendera ,sasa umejuaje wakibadilisha bendera watakuwa na wafuasi wengi? siongozwi na mvuto wa bendera bali viongozi waliomakini ndani ya chama.
 
Mmmh hata ikiwa kama kaniki
ama ing'are kama theluji ya kilimanjaro
haisaidii sera nzuri tu ziyayukomboa
nashauri waweke nyeusi kuliko kaniki
usihadaike na rangi tamu ya chai ni sukari
 
Kwa mawazo hayo naogopa kusema nakuonaje coz hutofurahi.anyway fahamu kwamba watu wanafuata sera na umakini wa chama na sio bendera.Ama kweli msafara wa mamba na kenge hawakosekani.
 
Back
Top Bottom