Rangi mbili

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
Wapendwa wana JF, rangi mbili ni jina linatotumika sehemu nyingi hasa vijijini kuita dawa aina ya tetracycline na jamii yake. Lakini rangi mbili nayotaka kuzungumzia hapa si vidonge bali ni binaadamu ambaye nimekutane naye leo asubuhi maeneo ya kariakoo.

Asubuhi ya leo nikiwa nimekwenda Kariakoo kununua mhogo wa ajili ya futari, nimemuona binti mmoja ambaye kwa kumuangalia usoni sikuweza kubaini utaifa wake au asili yake. Huyu binti amejichubua usoni mpaka damu inaonekana inavyotembea kwenye mishipa. Kutaka kumtafiti zaidi huyu "mzungu", nilishusha macho kidogo hadi shingoni. Ala haula, nilikutana na ngozi nyeusi kama mkaa!!! Kushusha zaidi macho kwenye miguu, mamaaaaaa!!! Sijawahi kuona kiumbe cheusi kama hiki.

Nilichokuja kugundua ni kwamba yule binti hakuwa mchina, mhindi wala mzungu bali ni mswahili ambaye alipata bajeti kidogo ya kuchubua usoni tu na ikawa imeishia hapo. Nataka niwaulize mabinti kwamba kufanya hivyo maana yake nini? Je ni kuchukia uafrika wao au ni kupenda uzungu wa wenyewe?
 
Kutaka kuwaridhisha wanaume wanaodai kwamba weupe ndio UZURI!!
Kukubalika kwenye jamii inayoamini weupe ndio UZURI!
Na yote hayo yanayokana na kutokujiamini bila kusahau ulimbukeni.
 
Kutaka kuwaridhisha wanaume wanaodai kwamba weupe ndio UZURI!! <br />
Kukubalika kwenye jamii inayoamini weupe ndio UZURI!<br />
Na yote hayo yanayokana na kutokujiamini bila kusahau ulimbukeni.
<br />
<br />
haswaa.. Mi nashangaa wanawake tunahangaika nini kujitafutia macancer bure kwa cream na madawa ya ajabu kwa sababu za kijinga! Halafu weupe wa kujichubua unajulikana tu hata ufanyeje!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom