Ramani ya Mji Mkuu Dodoma ilichorwa na huyu

Rebo Tz

Senior Member
Sep 26, 2016
169
124
Tujifunze au kujikumbusha kwa hili kidogo kwa tusiojua kuhusu Dodoma....

ANZA...

1475334304652.jpg


Wazo la kuhamia Dodoma liliasisiwa na Mwalimu Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 1970. Mwalimu alitaka kuona Dodoma ikistawi na serikali kuweza kuhamia huko ili kutekeleza kwa vitendo dhana ya mji mkuu. Baadhi ya sababu zilizomsukuma Mwalimu Nyerere kuichagua Dodoma ni pamoja na mji huo kuwa katikati ya miji yote Tanzania. Hii ingesaidia kurahisisha huduma miongoni mwa watu waliopo maeneo ya pembezoni. Lakini pia zilikuwepo sababu za kiuchumi na za kiusalama.
Ili kutekeleza mpango huo Mwalimu Nyerere alifanya mambo matatu makubwa. Kwanza kutafuta rasilimali (fedha) za kuijenga Dodoma na kuifanya kuwa mji mkuu wenye hadhi, ambapo alifanikiwa kupata ufadhili Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Pili alimtafuta mtaalamu wa mipango miji aliyechora ramani ya mji wa Dodoma Prof. James Stephan Rossaunt, (1928-2009), Mhandisi wa Kimarekani mwenye asili ya Kiyahudi. Prof. Rossaunt alifanya kazi yake na kukabidhi kwa Mwalimu Nyerere ramani ya Dodoma kama makao makuu ya nchi.

1475334339061.png


Baada ya kupokea ramani hiyo Mwalimu Nyerere alianzisha mamlaka ya ustawishaji wa makao makuu (CDA) mwaka 1973 na kuipa jukumu la kustawisha Dodoma kuwa mji mkuu kwa kufuata mpango ulioandaliwa na Prof. Rossaunt.

CDA ikaanza kutekeleza mpango huo lakini kwa kusuasua. Haikuweza kujenga hata jengo moja la wizara au idara kubwa ya serikali, haikuweza kuratibu ujenzi wa miundombinu, haikuweza kujenga vituo vya huduma za kijamii kuweza kukidhi mahitaji ya mji mkuu. Kwa kifupi CDA haikuweza kukidhi matarajio ya kuifanya Dodoma kuwa mji mkuu.
 
Squatters zipo sehemu kama chadulu,chang'ombe,kizota barabarani,maili mbili.lakini CDA wamefanya kazi nzuri ila walipoanza kuuza maeneo ya hovyohovyo ndipo lawama zimewapata lakini wako vizuri
 
Rockefeller Family Naskia walitaka waujenge mji wa dodoma kuwa city of Tanzania kwa masharti ya majengo hayo kuwa na majina ya rockefeller Mwl kakataa! Magufuli akakae nao meza moja warudi tena
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom