Ramadhani & Zarina Madabida na ARVs FEKI (Miradi ya CCM...?)

hakuna uhusiano wa madabida na ccm. Ingekuwa hivyo basi na slaa kwa kuwa ana masuala mazito ya ishu ya mke wake kuwa ni wa mushumbusi basi tuseme ni chama.tutofautishe taasisi na mtu binafsi

Hivi wizara ya Afya imeundwa na serikali ya CDM. Huwezi kumsafisha huyu kobe aitwaye CCM
 
Sijui kama unaloliongea unalifahamu au just a feeling, ila kama ulikuwa hujui ni kwamba Makongoro Mahanga na Didas Masabauri ni kambi ya Lowasa na wote wamepigwa mweleka kwenye uchaguzi wa Nec kwahiyo nguvu zao zote waliamishia kwa Janeth Masaburi na ndio maana akaweza kushinda otherwise mtandao wa kina Madabida Dar unatisha.

Hata kesi ya Makongoro Mahanga ya Ubunge wa Segerea ameshinda kwa mkono wa Lowasa, hii ni fact na ni Inside story.
Ninavyofahamu mimi hawa akina Madabida hawana mtandao unaoeleweka. Wanagombea nafasi hizi kulinda ufisadi wao na kutengeneza pa kutokea wanapokumbwa na tatizo. Wale Wajaluo, Mahanga na Masaburi, ni wanamtandao "orijino". Hilo halina ubishi. Wanafanana sana kwenye kutafuta utajiri kwa njia yoyote ile. Tutapona kweli?
 
hakuna uhusiano wa madabida na ccm. Ingekuwa hivyo basi na slaa kwa kuwa ana masuala mazito ya ishu ya mke wake kuwa ni wa mushumbusi basi tuseme ni chama.tutofautishe taasisi na mtu binafsi
Kama umetumwa kutoka Lumumba haya ni maji mazito huyawezi kuogelea utakumbwa na dhoruba tu, mwenzio Nape amekimbia hapa.
 
Ninavyofahamu mimi hawa akina Madabida hawana mtandao unaoeleweka. Wanagombea nafasi hizi kulinda ufisadi wao na kutengeneza pa kutokea wanapokumbwa na tatizo. Wale Wajaluo, Mahanga na Masaburi, ni wanamtandao "orijino". Hilo halina ubishi. Wanafanana sana kwenye kutafuta utajiri kwa njia yoyote ile. Tutapona kweli?
Madabida yupo kwenye mtandao wa udini na Uzawa yaani Upwani, mtandao ambao huwa haufanyi kazi muda wote ndio maana Abuu Jumaa aliangushwa Umeya wa Ilala na mtoto mdogo kwa sababu ya kutegemea mtandao huu wa kizawa na kidini.
 
Ukukikubari kutumiwa jiandae kudharilika huyu jamaa katumiwa leo hii wananmdharilisha hadharani bila hata aibu kweli ccm sikio la kufa
 
Mtu tayari kinga yake ina shida, unampa dawa feki. Tuone kama serikali dhaifu itawachukulia hatua hawa wahuni. Mpaka kufikia siku ya kuing'oa CCM madarakani, tutakuwa tumekiona cha moto aisee.
 
Ramadhani Madabida mwenyewe ndiye huyo hapo (kulia)
91AIDS%20Drugs1.JPG

Zarina Madabida naye huyu hapa,

Source: HII HAPA

DSC_0692.JPG
Hii familia kama haya ni kweli wameyafanya wana roho mbaya sana kwa watanzania,inasikitisha sana unauwa watu kwa ajili ya madaraka hii mbaya sana,mwisho wa haya yote ni aibu
 
Hii familia kama haya ni kweli wameyafanya wana roho mbaya sana kwa watanzania,inasikitisha sana unauwa watu kwa ajili ya madaraka hii mbaya sana,mwisho wa haya yote ni aibu

Mkuu habari ndo hiyo,

Baba ni mjumbe wa NEC ya CCM na nasikia anagombea uenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar...

Mama huyo ni Mbunge, mjumbe wa kamati ya kudumu ya huduma za jamii na kada wa ndani wa CCM (mwenyekiti wa UWT aliyemaliza muda wake)...

Kwa ushiriki wao katika kashfa hii na nafasi yao katika chama, nitashangaa kama Nape hataingia public na kukisafisha chama....Vinginevyo, wale wenye akili fupi tunaweza kuhisi kwamba huo ulikuwa mpango wa kukuza kipato cha chama kwa kuwaua maelfu ya waadhirika wa VVU/UKIMWI ambao hawana hatia!!
 
Kuwafukuza kazi ama kuwasimamisha kazi watu wa MSD kwa skendo ya ARV feki ni kuwaonea, walistahili kuwajibishwa kwa skendo ya kununua dawa zilizo expiry si hili la ARV feki.

Katika skendo hii walitakiwa kukamatwa na kushitakiwa Madabida mke na mume, TFDA na TBS. Kwa uelewa wangu sidhani kama MSD wanauwezo wa kutambua dawa feki ndio maana serikali ikaanzisha TFDA na TBS.
 
Gamba wewe kafie Uyole, unataka kujifanya hujui CCM wanavyogawana hizi tenda? kila mtu ukimuuliza nchi hii kiwanda cha madawa atakutajia ni Shellys Phamaceutical, sasa hawa kina Madabida walishindaje hii tenda?

Tena kama tungekuwa tunajali uhai wa watu hii kazi wangepewa Smith Klein ya Kenya, ndio wenye kiwango na madawa yao yanaaminika.

ulivonikejeli mm yakurudie na ww pia lakini hoja ya pili umeongea vzr kwamba kuwe na ushindani huru wa tenda.pia mm nasimamia hoja yangu kwamba madabida sio ccm
 
Hiki Chama Cha Mauaji imefika wakati sasa kiondoke!! Yaani kuua kila njia kwenye misitu ya pande, mabomu ya kumwaga miili vipande, dawa za ARV ambazo zitaua millions kabisa in Tanzania, maisha magumu kwa umaskini ambao sasa umeongeza Child and Maternal Mortalities, Unemployment, high rate of crimes, illigal activities, you name all vices associated to extreme poverty. Mabadiliko yanatakiwa haraka sana.
 
Kuna baadhi ya mambo ukiwaza sanaaa unajikuta unakitukana matusi ya nguoni kuanzia mwenyekiti mbaka mjumbe wa shina wa chama tawala ...Mpssxxyyyyyyyyyyyyy

kuna muhuri wa ccm umetumika? Acha hisia ww,hapa tunamlaani madabida
 
Mkulu umeamua kutuua watanzania hivi hivi in cold blood? ili iweje haswa? Hawa UWT ndio kazi zao hizi za kujua usalama wa taifa unakuwaje badala yake wanatumwa kufanya kazi za aibu wanaumbuka sasa.
 
Wana JF,

Mengi sana yameongelewa humu na wachangiaji mbali mbali mimi naomba niweke kitu kimoja tu wazi, hizi habari zimekuja zimechelewa sana na ni baada ya uchunguzi wa siri kufanyika kabla ya kutolewa kwenye vyombo vya habari. "JUST CACHE" NI NANI ALIYEGUNDUA KWAMBA KUNA ARV'S FEKI KUTOKA KIWANDA CHA TPI? Kuna mtu yeyote anyeweza kutoa jibu au kukisia ni nani aliyetoa taarifa kuwa kuna ARV'S.

Ngoja nitafute Email niliyotumiwa mwezi wa 6 ikieleza ni nani halafu nitai-upload jinsi ilivyo muweze kubaini ukweli. Familia ya MADABIDA wanaonewa.
 
Hii familia kama haya ni kweli wameyafanya wana roho mbaya sana kwa watanzania,inasikitisha sana unauwa watu kwa ajili ya madaraka hii mbaya sana,mwisho wa haya yote ni aibu

Naona serikali impe ulinzi mara moja, waliyoyafanya ni makubwa mno.
 
Wana JF,

Mengi sana yameongelewa humu na wachangiaji mbali mbali mimi naomba niweke kitu kimoja tu wazi, hizi habari zimekuja zimechelewa sana na ni baada ya uchunguzi wa siri kufanyika kabla ya kutolewa kwenye vyombo vya habari. "JUST CACHE" NI NANI ALIYEGUNDUA KWAMBA KUNA ARV'S FEKI KUTOKA KIWANDA CHA TPI? Kuna mtu yeyote anyeweza kutoa jibu au kukisia ni nani aliyetoa taarifa kuwa kuna ARV'S.

Ngoja nitafute Email niliyotumiwa mwezi wa 6 ikieleza ni nani halafu nitai-upload jinsi ilivyo muweze kubaini ukweli. Familia ya MADABIDA wanaonewa.

Weka basi hiyo Barua yako!
 
Back
Top Bottom