Rakesh wa KULEANA – HAKI ELIMU na sasa TWAWEZA ni KIVULI cha nani?

Naogopa kuwazungumzia DANIDA kwa sasa sina data yoyote

Mkuu huo nimekupa mfano ambao ni fact unaojieleza na unaokaribiana na hoja unayoizungumzia kuhusu Rakesh Rajan. Sasa unaposema huna data ni mifano ipi ambayo una data ili tukiitoa utoe maelezo na si kukwepa hoja????
 
Udhaifu wa Haki Elimu

Fedha nyingi sana ilitumiak kutengeneza machapisho na kugharamia matangazo katika vyombo vya ahabari endapo kama ingeelekezwa katika kusaidia jamii moja kwa moja leo tungekuwa walau kwa kiwango fulani mikoa miwili mitatu ya mradi wananafuu katika matatizo haya ambayo Haki Elimu waliamua kutuaminisha kuwa ni Jukumu la Serikali tu na wananchi tunapaswa kulishwa kwa ncha ya Kijiko.

Kazi ya haki elimu nadhani ni kuweka awareness kwenye jamii ili jamii yenyewe idai mabadiliko. Haki elimu sio mtekelezaji. Labda tungeshauri Serikali kama pilot project ichukue mkoa au wilaya moja iliyo chini kielimu then managemet ya elimu ya wilaya hiyo iwe leased kwa Hakielimu kwa miaka mitatu............. Si kama walivyo binafsiaha managemenet ya TANESCO.... wasione aibu.

So haki elimu hawana kosa kutumia pesa kwenye kuwahamasisha watu na matangazo.

Serikali yenyewe ambayo ni mtekelezaji nenda pale wizara ya elimu anagalia miradi iliyopo alafu uliza ni mingapi inatoa product kwa mwanafunzi. Miradi iliypo ni ya adminsitration na management na pesa zainaishia dar. haina direct input kwa mwanafunzi au shule

Serikali haiwezi kukwepa jukumu lake
 
Rajesh is my role model kwa sababu lengo lake kwa kiasi kikubwa lilikuwa zuri sana. Hata kama anapata hela ni halali yake kabisa kwani anastahili kabisa kwa juhudi na ubunifu wake mwingi.

Katika kila initiative kuna advantages na disadvantages na ndiyo maana inahitaji kuwa risk taker unapooamua kufanya jambo jipya la sivyo hutafanya. Tatizo letu tulio wengi tunaogopa kuanzisha kitu kwa kuhofia zaidi risk kuliko mafanikio yake na matokeo yake we remain idle kuanza kukosoa initiative za wengine. Utamsikia mtu akisema" mimi nilijua tu hii itakwama ndio maana sikuanzisha au nilijua haitafanikiwa ndio maana sikufanya" Hapa naona bora aliyeanza akfanya makosa akasonga mbele kuliko aliyekaa kibarazani na kuanza kukosoa.

Rajani siyo Mungu kwani alijitahidi kwa kadiri alivyoweza kufanya alichofikiri ni kizuri na kwa kukuwa hafanyii neutral environment bali duniani penye watu basi kuna eneo alilo excel na kuna eneo dogo dosari imetokea kama human being. hebu tuyachukue yale ya maana aliyofanya na yale mabaya ambayo obvious najua hakuyakusudia tuyatupe pembeni. Sijaelewa lengo la mtoa mada ni kumprove wrong completely au amekuja na Counteractive program iliyofanya kazi vizuri zaidi kuliko KULEANA, na HAKI ELIMU.
 
Kuna tatizo dogo lipo upande wa pili wa sarafu na hii nathubutu kulilinganisha na namna ambavyo tumekuwa tukitumiwa vibaya na wajanja wachache kwa kudai ati wanasaidia maboresho ya sera na maendeleo Nchini.

Kumbuka zilitoka fedha ujerumani kusaidia kuzuia hoja ya mfuko wa Jimbo isipite. walikuwa na masilahi gani mpaka leo mimi na wewe hatujui.

Sasa hii ya CDF hata mm sikubaliani nayo. Kwana inaondoa uhuru wa mbunge. wabuge wanatakiwa wawe watu wa kuhoji sio watendaji. Sasa ni wabunge wangapi umeona hata wametoa quarter report ya matumizi ya mifuko yako. Wabunge wangapi wanajua sheria na kaununi za finacial reporting.

Binafsi naona hili la CDF ilikuwa ni mtego kwa wabunge na wamenasa. With CDF wabunge hawana meno 32 tena.......... Na tusubiri CAG atakpoanza kukagua hayo matumizi hope haitakuwa 2015. Au na CDF ina kinga teh teh teh

kwa hiyo hizo Pesa za ujerumani nana hazikuw ana nia mbaya.
 
Gaijin soma hapa tafadhali.
Tatizo kubwa ni husky reading kwa watanzania. Imeua mpaka ubora wa elimu vyuo vikuu, watu wanajaa maktaba siku za assignment na wakati wa mitahani tu

GR.
Vyovyote iwavyo, wewe umekuja na accusations ambazo umezitoa kama umezifanyia utafiti kuwa kuondosha adhabu ya bakora kumesababisha watoto kupata mimba na mengineyo.

Ungelikuja na suala kuuliza iwapo ni kweli kuna correlation hiyo nafikiri ungepata mchango mwengine tofauti. Mimi suala langu lilikuwa umefikiaje correlation hiyo wakati huna data?

Nadhani na suala la mwanafunzi kufikia 'conclusion' kwa kufuata intuition zake tu kunaporomosha elimu Tanzania
 
Matokeo ya Utafiti wa G.R
Baada ya KULEANA ya Rajani kufanikisha Kam[peni hii ambayo pia ilipata Baraka za Bunge baada ya kulob kwa kutumia mashirika ya utetezi wa Hai za Mtoto kitaifa na Kimataifa, Hoja yao ya msingi ikapenya, matokeo yake sasa:
  • Tazama ongezeko la Mimba kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, sitaki kusema sekondari wanavyoziporomoa kila kukicha maana wao ni mazao ya awali ya azimio hili.
  • Leo ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi kufanya mapenzi na Mwalimu baada ya kuondoa ombwe la kinidhamu lililokuwepo kati ya Kada hizi mbili.
  • Maadili na Nidhamu kwa wanafunzi imeporomoka kupita maelezo ya kawaida.
  • Mbaya zaidi kutoakana na kushuka kwa Nidhamu na Maadili kiwango cha Elimu kimepromoka kwa karibu asilimia 60%
  • Knowledge is no longer a power

Nimejaribu kusoma mara kadhaa 'matokeo' ya huu utafiti wako lakini bado naona unapwaya sana kuweza kusupport thesis yako kuhusu Rakesh. Kwa mfano unasema 'knowledge is no longer a power'......hii maana yake nini hasa (au unakusudia kusema nini hasa)?

Kuhusu maadili, wala haihitaji kufanya utafiti (casual observation is enough) kujua kuwa maadili katika jamii kwa ujumla wake yameporomoka sana na si kwa waliokuwa wanafunzi miaka ya 1992 na kuendelea bali hata wa kabla ya hapo....na kimsingi sioni ni vipi suala hili unaweza kulihusisha na Rakesh. Wakati mimi nipo shule (sekondari) nakumbuka kuna mwalimu alikuwa anatumia viboko kama vitisho ili kupata 'rushwa' ya ngono kutoka kwa wanafunzi wa kike (na huyo mwalimu ameshatangulia mbele ya haki kwa Ukimwi!). Kwenye suala la maadili unaweza pia kuangalia viongozi wetu (ambao wengi ni waliosoma kabla ya hiyo 1992, and some are even older than Rakesh).
 
Tafiti za Rakesh zimesaidia kutufunua macho sana. Tatizo nchi hii hatupendi kufanya research-based decision making. Tunapendelea sana kuendeleza customs na dogmas.

Ukichukua mfano wa viboko mashuleni ni muhimu sana kufanya utafiti kutusaidia kufanya maamuzi. Tukumbuke suala hilo lilikuwa ndiyo practice kwa miaka sehemu nyingi sana duniani. Lakini matokeo ya utafiti yamekuja kuonyesha kwamba ule msemo wa kizamani wa spare the rod and spoil the child hauna scientific basis. Kwa hiyo trend katika nchi nyingi ni ama kudhibiti au kuondoa viboko na kutumia njia za kitaalamu kudhibiti nidhamu mashuleni.

Kwa vyovyote vile katika shule duni kama za uma za hapa nchini ni kujidanganya kutarajia viboko kusaidia katika elimu. By the way hata hapa nchini zipo shule hazitumii viboko na wanafunzi wake wanafanya vizuri tu. La msingi zaidi tufanye utafiti wa kutosha kujua kwa kina athari za viboko mashuleni na nini kifanyike kuboresha elimu.

Madai kwamba kupunguza viboko kumeongeza mimba mashuleni na kupunguza nidhamu hayana scientific basis.Je, muanzishaji wa thread hii anaweza kutupa reference kwenye quality journals za education na nyanja nyingine za hapa Tanzania na kwingineko kuonyesha kama viboko ndiyo adhabu bora ya kumkerebisha mtoto shuleni?
 
Watanzania wengi wanaona karibu sanaaa wakati mataifa makubwa yenye mpango wa kuwanyonya yanaona mbali kweli. Kaeni hivyo hivyo, vizazi vyenu vitapiga makaburi yenu kwa uwezo wenu mdongo wa kufikiri.

Lazima kuna reason behind katika haya na tena yanatoka kwenye msukumo wa mataifa makubwa ambako funds zinapatikana. Tunaomba pesa za maendeleo ya kujenga hospitali, shule, barabara lakini wanatupa pesa za kuaanzisha NGO. Upuuzi mkubwaaaaaaaaaaa.
 
Matokeo ya Utafiti wa G.R

Nimejaribu kusoma mara kadhaa 'matokeo' ya huu utafiti wako lakini bado naona unapwaya sana kuweza kusupport thesis yako kuhusu Rakesh. Kwa mfano unasema 'knowledge is no longer a power'......hii maana yake nini hasa (au unakusudia kusema nini hasa)?

Kuhusu maadili, wala haihitaji kufanya utafiti (casual observation is enough) kujua kuwa maadili katika jamii kwa ujumla wake yameporomoka sana na si kwa waliokuwa wanafunzi miaka ya 1992 na kuendelea bali hata wa kabla ya hapo....na kimsingi sioni ni vipi suala hili unaweza kulihusisha na Rakesh. Wakati mimi nipo shule (sekondari) nakumbuka kuna mwalimu alikuwa anatumia viboko kama vitisho ili kupata 'rushwa' ya ngono kutoka kwa wanafunzi wa kike (na huyo mwalimu ameshatangulia mbele ya haki kwa Ukimwi!). Kwenye suala la maadili unaweza pia kuangalia viongozi wetu (ambao wengi ni waliosoma kabla ya hiyo 1992, and some are even older than Rakesh).

Kinadharia ni kama unakubaliana na hoja licha ya kuwa umejizungusha kabla ya kudrive home a point
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sasa hii ya CDF hata mm sikubaliani nayo. Kwana inaondoa uhuru wa mbunge. wabuge wanatakiwa wawe watu wa kuhoji sio watendaji. Sasa ni wabunge wangapi umeona hata wametoa quarter report ya matumizi ya mifuko yako. Wabunge wangapi wanajua sheria na kaununi za finacial reporting.

Binafsi naona hili la CDF ilikuwa ni mtego kwa wabunge na wamenasa. With CDF wabunge hawana meno 32 tena.......... Na tusubiri CAG atakpoanza kukagua hayo matumizi hope haitakuwa 2015. Au na CDF ina kinga teh teh teh

kwa hiyo hizo Pesa za ujerumani nana hazikuw ana nia mbaya.

Hapana imeundiwa utaratibu wa returns sema tu ni kwa uadilifu kiasi gani ambapo mbunge hawezi kuweka na za mjomba ili wagawane baadaye
 
Pamoja na maelezo yako mazuri ambayo yanaushawishi mkubwa wa mtu kukubaliana na wewe lakini pia naomba kutofautiana na wewe. Sintaenda word by word kujibu hoja yako kwasababu ya ufinyu wa muda nilionao kwa sasa lakini kwa ujumla tu; sioni hapo tatizo la Rakesh na wafadhili bali tatizo la jamii kubwa ya watanzania ambao mara zote attitude yetu imekuwa zaidi tegemezi na kuwa watu tusiojimani kwamba tunaweza kufanya jambo la kutunufaisha kama taifa ama jamii.

Kama ulivyoeleza Rakesh amekuwa mwanzilishi wa hizo Projects/NGOs ukianza na za watoto wa mitaani; then HAKI ELIMU na baadaye TWAWEZA. Kwa haraka haraka utagundua kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuona tatizo nakulichukulia kuwa ni fursa ya yeye kuonyesha ni jinsi matatizo hayo yanaweza kutatuliwa. Sasa ukumbuke kuwa Rakesh si serikali wala si kiongozi katika serikali ambayo hasa ndiyo yenye dhamana ya kuyafanya hayo. Yeye kama raia wa Tanzania ameonyesha njia ili viongozi wa Taifa hili waweze kuona ni jinsi gani matatizo hayo yanaweza kuondolewa iwapo kutakuwa na mifumo na njia sahihi ya kuyaondoa. Sasa kama yeye ataendelea kufanya jambo hilo hilo moja kama vile yeye ndiyo serikali basi ujue hapa kunatatizo la msingi na pengine hatujui nini maana ya serikali na ni kwanini tunaipa kodi zetu za maendeleo.

Niishie tu kwakutoa pongezi nyingi sana kwa Rakeshi na wenzake kwa uzalendo wao na uwezo wao mkubwa wakuielimisha jamii nzima ya Tanzania katika kubadili mitizamo yao kwakutumia luga ya picha!

Ni wajibu wa serikali kuleta welfare kwa watu wake na kamwe raia mmoja anapoonyesha njia isichukuliwe kuwa sasa hiyo ndiye amechukua nafasi ya serikali iliyopo katika kutatua matatizo ya watu wake. Kama hizo concept/Ideas walizoziacha zimeshindwa kuchukuliwa ama na serikali au raia wengine hilo silo jukumu la Rakesh bali lahao waliobaki na maono ya Rakesh na ambao hata baada ya kupewa ideas wameshindwa kuzi sustain and actually wanaonyesha ni jinsi gani wasivyowabunifu na wenye ushawishi katika kutekeleza jambo. Nitatizo la watu wetu wengi kupenda tu kupokea cash bila kufikiria ni jinsi gani tunaweza kubadili matatizo yetu na kuwa fursa ama za kutuletea maendeleo au kuonyesha talent zetu katika jamii ili pia jamii itukumbuke tutakapokuwa kuondoka katika utumishi kwa kifo ama kwa kuzeeka.

Poverty is more of attitude than any thing!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kwa suala la maadili kushuka ndiyo nakubaliana na wewe (hii haikuwa 'hoja' yako) lakini hujaweza kunishawishi kwamba miradi ya Rakesh ndio imesababisha kushuka kwa maadili tunakokushuhudia.

Anasahau kuwa sio kila vinavyotokea kwa wakati mmoja vipo katika causal relation

Ice cream zinaliwa sana wakati wa majira ya joto

Malaria inaongezeka sana wakati wa joto

Ice cream ina sababisha malaria?
 
Watanzania wengi wanaona karibu sanaaa wakati mataifa makubwa yenye mpango wa kuwanyonya yanaona mbali kweli. Kaeni hivyo hivyo, vizazi vyenu vitapiga makaburi yenu kwa uwezo wenu mdongo wa kufikiri. Lazima kuna reason behind katika haya na tena yanatoka kwenye msukumo wa mataifa makubwa ambako funds zinapatikana. Tunaomba pesa za maendeleo ya kujenga hospitali, shule. barabara lakini wanatupa pesa za kuaanzisha NGO. Upuuzi mkubwaaaaaaaaaaa.

Hizo nchi unazozituhumu hizo hela za kujenga hospitali, shule na barabara walipewa na nani? Acha kuwa tegemezi wewe serikali yako ndiyo yenye jukumu ya kukupa wewe shule na barabara nzuri iwapo wewe unalipa kodi.

Kama wewe unategemea mojamba shangazi na hulipi kodi basi anza leo kufanya kazi ulipe kodi. Lakini kama wewe ni mkulima, mfanyakazi ama mfanya biashara basi na unalipa kodi yako ya maendeleo basi ni jukumu lako kuidai serikali iliyopo ikupatie hivyo vyote tena kwa quality nzuri maana wewe umetimiza wajibu wako wakulipa kodi na hivyo ni responsibility ya serikali kukupa wewe hivyo; kama haijakupa basi unahaki ya kuiwajibisha kwani imeshindwa kufanya kazi.
 
Anasahau kuwa sio kila vinavyotokea kwa wakati mmoja vipo katika causal relation

Ice cream zinaliwa sana wakati wa majira ya joto

Malaria inaongezeka sana wakati wa joto

Ice cream ina sababisha malaria?

Whether you like or not, topic hii inalengo la kuonyesha kwamba tulitakiwa kuwa na msingi yetu ya maisha yetu bila kuingiza misingi ya magharibi.

Suala la kutoa viboko ndo lilikotea madili mabaya kwa watoto hata huko ulaya na sasa wanalaumu. Mtoto anachelewa kurudi nyumbani, baba unamuuliza, anakujibu kwa dharau, unamnasa kibao, anapiga simu ploisi unachukuliwa na kufunguliwa mashaka ya kuharass mtoto wako. Inakuja hiyo? Huko ni kuharibu watoto na hiyo ndo ipo Marekani ambapo watoto sasa wanafanya wanalotaka.

Nasi tunaelekea huko kabla ya kufanya mafanikio ya hizo taratibu. Hayo na mengi tu hayajengi kabisa jamii
 
Pamoja na maelezo yako mazuri ambayo yanaushawishi mkubwa wa mtu kukubaliana na wewe lakini pia naomba kutofautiana na wewe. Sintaenda word by word kujibu hoja yako kwasababu ya ufinyu wa muda nilionao kwa sasa lakini kwa ujumla tu; sioni hapo tatizo la Rakesh na wafadhili bali tatizo la jamii kubwa ya watanzania ambao mara zote attitude yetu imekuwa zaidi tegemezi na kuwa watu tusiojimani kwamba tunaweza kufanya jambo la kutunufaisha kama taifa ama jamii.

Kama ulivyoeleza Rakesh amekuwa mwanzilishi wa hizo Projects/NGOs ukianza na za watoto wa mitaani; then HAKI ELIMU na baadaye TWAWEZA. Kwa haraka haraka utagundua kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuona tatizo nakulichukulia kuwa ni fursa ya yeye kuonyesha ni jinsi matatizo hayo yanaweza kutatuliwa. Sasa ukumbuke kuwa Rakesh si serikali wala si kiongozi katika serikali ambayo hasa ndiyo yenye dhamana ya kuyafanya hayo. Yeye kama raia wa Tanzania ameonyesha njia ili viongozi wa Taifa hili waweze kuona ni jinsi gani matatizo hayo yanaweza kuondolewa iwapo kutakuwa na mifumo na njia sahihi ya kuyaondoa. Sasa kama yeye ataendelea kufanya jambo hilo hilo moja kama vile yeye ndiyo serikali basi ujue hapa kunatatizo la msingi na pengine hatujui nini maana ya serikali na ni kwanini tunaipa kodi zetu za maendeleo.

Niishie tu kwakutoa pongezi nyingi sana kwa Rakeshi na wenzake kwa uzalendo wao na uwezo wao mkubwa wakuielimisha jamii nzima ya Tanzania katika kubadili mitizamo yao kwakutumia luga ya picha!

Ni wajibu wa serikali kuleta welfare kwa watu wake na kamwe raia mmoja anapoonyesha njia isichukuliwe kuwa sasa hiyo ndiye amechukua nafasi ya serikali iliyopo katika kutatua matatizo ya watu wake. Kama hizo concept/Ideas walizoziacha zimeshindwa kuchukuliwa ama na serikali au raia wengine hilo silo jukumu la Rakesh bali lahao waliobaki na maono ya Rakesh na ambao hata baada ya kupewa ideas wameshindwa kuzi sustain and actually wanaonyesha ni jinsi gani wasivyowabunifu na wenye ushawishi katika kutekeleza jambo. Nitatizo la watu wetu wengi kupenda tu kupokea cash bila kufikiria ni jinsi gani tunaweza kubadili matatizo yetu na kuwa fursa ama za kutuletea maendeleo au kuonyesha talent zetu katika jamii ili pia jamii itukumbuke tutakapokuwa kuondoka katika utumishi kwa kifo ama kwa kuzeeka.

Poverty is more of attitude than any thing!

Nice contribution, I wish ungekuwepo kwa muda kidogo tulijadili hili kwa mapana bahati mbaya ushaondoka. Kama umepata kusoma thread zilizokwishapita, Tatizo langu ni athari za miradi hii inayoanzishwa kwa nia njema, na amekuwa akiikacha baada ya kulipua bomu ni kama vile anakuwa katimiza lengo lake ambalo bado mie naamini litakuwa limefichika sana, na hapa ndio nataka tutadisi hilo
 
Anasahau kuwa sio kila vinavyotokea kwa wakati mmoja vipo katika causal relation

Ice cream zinaliwa sana wakati wa majira ya joto

Malaria inaongezeka sana wakati wa joto

Ice cream ina sababisha malaria?

Hoja hizi umenipita kwapani Mkuu sijajua zimejiungaje hapo
 
Kwa suala la maadili kushuka ndiyo nakubaliana na wewe (hii haikuwa 'hoja' yako) lakini hujaweza kunishawishi kwamba miradi ya Rakesh ndio imesababisha kushuka kwa maadili tunakokushuhudia.

Maadili yamezungumziwa katika hiyo thread Mkuu hukuisoma yote nini?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Whether you like or not, topic hii ina lengo la kuonyesha kwamba tulitakiwa kuwa na msingi yetu ya maisha yetu bila kuingiza misingi ya magharibi.

Suala la kutoa viboko ndo lilikotea madili mabaya kwa watoto hata huko ulaya na sasa wanalaumu. Mtoto anachelewa kurudi nyumbani, baba unamuuliza, anakujibu kwa dharau, unamnasa kibao, anapiga simu ploisi unachukuliwa na kufunguliwa mashaka ya kuharass mtoto wako. Inakuja hiyo? Huko ni kuharibu watoto na hiyo ndo ipo Marekani ambapo watoto sasa wanafanya wanalotaka.

Nasi tunaelekea huko kabla ya kufanya mafanikio ya hizo taratibu. Hayo na mengi tu hayajengi kabisa jamii

Viboko si ungeendelea navyo nyumbani! Na maadili mema ambayo yanatokana na Woga wa viboko si yangepatikana?
 
Kama Rakesh alipokuwa kuleana ilikuwa inajiendesha vizuri na kutimiza malengo yake vizuri anatakiwa kupongezwa kwa kuwa ni watoto wengi sana walisaidiwa ambao sisi wenyeji na wazawa wa mwanza tulishindwa kuwajali pamoja na kwamba tumewazaa wenyewe. Kama kuleana imekufa baada ya Rakesh kuondoka basi waulizwe hao waliokabidhiwa kituo wamefanya nini kuendeleza mafaniko ya Rakesh.

Kama Rakesh alipokuwa Hakielimu ilweza kujiendesha vizuri na kwa mafanikio yaliyotarajiwa basi anastahili kupongezwa kwani alitusaidia kufahamu upungufu uliokuwepo katika mfumo wetu wa elimu na hususan serikali inayowajibika kuwaelimisha watu wake na kuweka mazingira bora ya elimu kuanzia mishahara ya waalimu, vitendea kazi na miundombinu. Kama hakielimu imekuwa taabani baada ya Rakesh kuondoka basi waulizwe hao waliokabidhiwa wamefanya nini kuendeleza mafanikio yaliyokuwa yamekwisha fikiwa ama kuendeleza zaidi.

Kama Rakesh ameanzisha twaweza na inaonekana kufanya vizuri basi ni jambo la kushukuru na kumpongeza. Twaweza ni taasisi inayofanya kazi zake vizuri sana na kwa umakini mkubwa sana, ripoti zao za kila mara juu ya hali ya elimu ya tanzania na sasa wamepanua wigo kuelekea nchi za afrika mashariki zinaonyesha ni kwa kiasi gani wanatambua majukumu yao kwa nchi na kwa wananchi.

Kuja hapa kumshutumu ni kuonyesha jinsi baadhi ya watu wanavyokereka kuambiwa ukweli na bila shaka wanaokereka ni wale walioko serikalini ambao ndio wana wajibu wa kwanza kuhakikisha ustawi wa elkimu nchini Tanzania. Hatushangai kwa watu hao kumlalamikia Rakesh, kama kiongozi wao mkuu anaweza kutoa statement nyepesi tu kwamba wasichana wanaopata mimba wakiwa mashuleni ni kiherehere chao, sishangai kwa madai haya dhidi ya Rakesh kwani hapa ni kama kusisitiza kauli ya kiongozi wako mkuu kwamba Rakesh kawasababishia kiherehere hawa wasichana ndio maana mimba zimeongezeka!!

Yeke mbane

Hujasoma thread yote, maana maswali yako yote yana majibu pale juu katika hoja ya Msingi na mengine yamejibiwa na wachangiaji humu ndani. Hebu pitisha macho upya
 
Back
Top Bottom