Rakesh wa KULEANA – HAKI ELIMU na sasa TWAWEZA ni KIVULI cha nani?

LATEST INPUT 08 April 2013

Sasa Serikali inajadili kurudisha Adhabu za Viboko Mashuleni: Taratibu yaliyofichika tutayaona na Uzi huu utakamilika


ADIOS

Mkuu. ahasante sana kwa utafiti wako. humu jf mpo wachache sana ambao mnaandika kwa lengo la kulisaidia taifa. wengi hujadili udaku na siasa badala ya kuwasaidia wananchi kuepukana na matatizo yanayowakabili. wakati unapost uzi huu 2011, wengi walikubeza na wengine walidiriki kukuita ni mbaguzi. hayo yalikuwa ni mawazo yao lakini wewe ulitimiza wajibu wako kama mzalendo na matokeo yako sasa tunayaona
 
Hupaswi kubaki Mdomo wazi unapaswa kutafakari Hoja na soma maliza thread. Tatizo letu ni kupenda kusoma yanayotufurahisha. Kuna tatizo hapa la msingi.

Ongezeko la Mimba kama eneo moja ulilolitaja linatokana na utovu wa Nidhamu na kushuka kwa Maadili. Katika maandiko matakatifu Biblia na Kuran tumeelekezwa kutoa mapigo kidogo yasiyodhuru kwa mtoto kwa lengo la kumrudi kimaadili.

Kama tumeiga umagaharibi ambapo kwao wao abortion ni kama kwenda kupima maralia uansemaje hapa hakuna tatizo. Huwezi kuawa serious soma tena thread hii vema na wewe tafiti kwa muda wako

Kwa hiyo kwa akili yako Rakesh ndio amesababisha,au ni serikali yenu inayoendekeza kuomba misaada nchi za magharibi na kupewa masharti hata ya kukubaliana na ushoga?Umetumwa kuja kuitetea serikali kwa wanafunzi kufeli?Je shule za kata zina walimu wa kutosha?Je Rakeshi ndiye anayepaswa kulipa waalimu haki yao?
Serikali ina lawama kubwa sana kwenye hili.Rakesh Hawezi kuwa na akili kubwa kuliko serikali.
 
Rakesh wa KULEANA – HAKI ELIMU na sasa TWAWEZA ni KIVULI cha nani?

Kwa siku Miezi kadhaa sasa nimejikita katika kusaka dondoo Muhimu sana zinazowahusu Ndugu Rakesh Rajani na Mustafa Kudrat waanzilishi wa Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha KULEANA mwaka 1992 kilichopo huko Mwanza.

Safari ya Rakesh Rajan ilianzia huko akiwa na lengo mahususi na ambalo lilionekana muhimu sana na la kipekee kwa Taifa kutokana na kushamiri kwa ongezeko la watoto wa Mitaani ambao baadye waliamua kulibadili jina hili kwa madai kuwa Mtaa hauwezi kuzaa Mtoto na hivyo kupewa jina rasmi watoto wanaishi katika mazingira magumu kama vile ilivyobadilishwa kwa Albino na kuwa wenye ulemavu wa Ngozi.

Katika miaka hiyo ya 1992 – 1999 kuleana walifanya kazi kubwa na kuwa kituo ambacho kwa kiwango kikubwa kilisaidia kupunguza tatizo la watoto wanaosishi katika mazingira magumu na kuvutia watanzania wengine kuanzisha vituo kama hicho katika maeneo kwingineko Nchini ambapo tatizo hili lilinukuliwa kama moja ya matatizo ya msingi.

Nimetathmini mafanikio ya Miradi aliyoianzisha Rakesh Rajani na Athari kwa umma wa Watanzania nimegundua Athari ni nyingi kuliko faida za miradi hii na hivyo nasukumwa zaidi kuandika katika upande huo nikiamini kama yupo mdau anayeweza kulinganisha mazuri hayo achukue jukumu ili kwa pamoja tusaidiane kubaini kama malengo ya Rajani na wafuasi wake ni kwa masilahi ya Taifa au Ni kivuli cha Mr. NO BODY??

Mara zote ambapo amekuwa akiianzisha miradi hii na kuuhama amekuwa akifanikiwa pia kuwahamisha wafadhili wote ambao wamekuwa wakihisani miradi hii na kuhamia katika mradi huo mpya aliounzisha, kwa sasa kuleana ipo ICU, Huku haki elimu ipo maternity ward inasubiri mimba ya kifo iliyoachwa hapo na Rajani wajifungue na wao wakaungane na KULEANA kule ICU.


Anguko la KULEANA

Mwaka 1999 Rakesh Rajani kwa kushirikiana na Mustafa Kudrat walitoa kijitabu kilichojulikana kwa jina la THE STATE OF EDUCATION IN TANZANIA – Crisis and Opportunities. Moja ya eneo lilokaziwa zaidi katika Kitabu hiki lilikuwa to abolish corporal punishment in schools (Kukomesha adhabu za ukatili/viboko kwa wanafunzi)

Katika Hoja hii ambayo kimsingi ndio ilikuwa hatima ya Rajani KULEANA kama ilivyo kule HAKI ELIMU amekuwa na kawaida ya kuwasha moto na akishafanikiwa anahama mradi na kukimbilia katika Mradi mwingine.

Hakika katika uwanja wa siasa za Tanzania amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama malengo yake ndio haya ambayo tunayashuhudia leo hii. Tuanze kuangalia hadidu za rejea katika mpango huu wa kumaliza Adabu za viboko mashuleni.
Matatizo ya Adhabu za Viboko.

Utafiti wa Rajani na Timu yake walijiridhisha kuwa:
  • Adhabu ya viboko imejikita kwenye kuadhibu kuliko kumuelekeza anayeadhibiwa.
  • Inafundisha kuwa Ukatili ni jambo la kawaida katika Jamii.
  • Wakubwa kuwapiga wadogo ni kielelezo kuwa wenye Mamlaka wanaruhusiwa kuwakandamiza walio chini yao.
  • Na kwamba adhabu za viboko zinasababisha uoga na hasira kuliko kujenga Nidhamu.
  • Inavunja mahusiano muhimu sana ya Kijamii kati ya mtoa adhabu na muadhibiwa.
Mbadala baada ya kuondosha Adhabu za Viboko:

  • Watoto wapewe maonyo ya maandishi
  • Pia endapo watakosea jambo fulani kuliko kuadhibiwa wapewe nafasi ya kulirudia jambo hilo.
  • Wapewe makaripio ya mdomo
  • Wapewe nafasi ya kufanya shughuli za manufaa kama adhabu, mfano kusafisha darasa au kupalilia bustani ya shule.
Matokeo ya Utafiti wa G.R
  • Baada ya KULEANA ya Rajani kufanikisha Kam[peni hii ambayo pia ilipata Baraka za Bunge baada ya kulob kwa kutumia mashirika ya utetezi wa Hai za Mtoto kitaifa na Kimataifa, Hoja yao ya msingi ikapenya, matokeo yake sasa:
  • Tazama ongezeko la Mimba kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, sitaki kusema sekondari wanavyoziporomoa kila kukicha maana wao ni mazao ya awali ya azimio hili.
  • Leo ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi kufanya mapenzi na Mwalimu baada ya kuondoa ombwe la kinidhamu lililokuwepo kati ya Kada hizi mbili.
  • Maadili na Nidhamu kwa wanafunzi imeporomoka kupita maelezo ya kawaida.
  • Mbaya zaidi kutoakana na kushuka kwa Nidhamu na Maadili kiwango cha Elimu kimepromoka kwa karibu asilimia 60%
  • Knowledge is no longer a power


Safari ya Haki Elimu

Baada ya kufanikiwa katika hilo na kuacha maumivu haya makubwa kwa Taifa Rakesh Rajani na Timu yake wakatimukia HAKI ELIMU baada ya kwenda kujipumzisha marekani kwa Likizo ya Masomo ya Juu.
Haki Elimu wakaibuka na wito ‘’ TAFAKARI, CHUKUA HATUA’’

Mradi huu mara kadhaa ulitoa takwimu nyingi ambazo ziliibana serikali kutokana na uozo wake katika kushughulikia Elimu licha ya kuwa wakati mwingine walizidisha chumvi na kusababisha baadhi ya matangazo yao kupitia Kamisheni ya Utangazaji Nchini kusimamishwa hadi yatakapofanyiwa marekebisho ili kuendana na Uhalisia wa mabo na si ushabiki na kuchochea uongo.

Huu ndio ulikuwa mwisho wa Rajani Haki Elimu na kuamua kuanzisha Mradi mwingine wa TWAWEZA.


Udhaifu wa Haki Elimu

Fedha nyingi sana ilitumiak kutengeneza machapisho na kugharamia matangazo katika vyombo vya ahabari endapo kama ingeelekezwa katika kusaidia jamii moja kwa moja leo tungekuwa walau kwa kiwango fulani mikoa miwili mitatu ya mradi wananafuu katika matatizo haya ambayo Haki Elimu waliamua kutuaminisha kuwa ni Jukumu la Serikali tu na wananchi tunapaswa kulishwa kwa ncha ya Kijiko.

Kenya wamefanikiwa sana kwa kuchangia katika Elimu kutokana na Nguvu za WANANCHI, Nilidhani juhudi za Haki Elimu zingelenga kuwaelekeza watanzania kuhusika moja kwa moja katika kuchangia na kushiriki shuguli za maendeleo maana tumekuwa maarufu wa kuchangia Harusi kuliko kutujaza ujinga kuwa kila kitu itafanya serikali.

Wakatulazimisha kuamini kuwa serikali lazima itekeleze Majukumu hayo na sisi kazi yetu ni kutafakari na kuchukua hatua za kuibana serikali, hizi ni mbinu chafu zilizofanikiwa kuteka mawazo ya Watanzania.


Twaweza

Walau sasa anaonyesha kuwa social accountability ni muhimu katika chachu ya maendelo, licha ya kuwa kiitiko cha twaweza WANANCHI TWAWEZA NI SISI, Kina reflection kubwa na sina shaka kimebeba dhamira nyingine mbovu kama ilivyokuwa HAKI Elimu, Ninaendelea kuutathimini na mradi huu maana sijui akitoka hapa yeye na Timu yake wanaelekea wapi tena.


My Take:


  • Hivi kweli huyu Jamaa ametathimini madhara aliyotuachia kufuatia Kampeni za KULEANA na HAKI ELIMU?
  • Yupo kwa masilahi ya Taifa au ni Kivuli cha nani hiki kinachowatesa Watanzania kwa sasa?
  • Usalama wa Taifa wanazitambua mbinu chafu za miradi kama Hii?
  • Tutaendelea kukumbatia miradi ya Aina hii mpaka lini?


LATEST INPUT: 26th February 2013

Wakati naandika Uzi huu wachache sana walielewa, hata leo tunapoendelea kupiga dandana za matokeo ya kidato cha nne ni bahati mbaya sana hakuna anayetaka kwenda kwenye botom course zaidi ya kushughulika na matokeo.

Matokeo haya ya wadogo zetu leo hayajaja kama mvua za Vuli ambazo hazina dalili wala wakati maalumu, hapa tunamkuta mdau mwingine aliyekiingiza kizazi cha watanzania katika umagharibi ambao hatukuwa na uwezo nao na matokeo yake leo ZOMBI wamechorwa kwenye karatasi za mitihani.

Tuendelee kujadili, pengine hizi Tume viini macho zikaja na majibu ya kina, Ila ukweli huwa mchungu sana daima.


LATEST INPUT 08 April 2013

Sasa Serikali inajadili kurudisha Adhabu za Viboko Mashuleni: Taratibu yaliyofichika tutayaona na Uzi huu utakamilika.



ADIOS

Mkuu, nimesoma maandiko yako tena na tena, na nihitimishe kwa kusema sikubaliani na wewe kabisa.
Yaani katika matatizo yote tuliyonayo unakosa AIBU kabisa kwa kumsingizia Rakesh kuwa ndio chanzo?
You cant be serious!

Angalau ungefanya uchambuzi wa mchango na hasara ya Rakesh, kidogo nigekuelewa lakini sio ku- divert attention ya watu wanaohoji uvundo wa usimamizi wa elimu nchini kwa kumsingizia mtu mmoja tena asiye na uhusiano wa moja kwa moja na mfumo wa elimu.
 
Yaan anakubaliana na wewe Mkuu hata hukom katika madrasa kuna wataoto wanagwaya kwenda kwa kuhofia bakora ambazo hazina malengo na unapiga mtoto kama unaua Nyoka, Hiyo hapana hata mie siungi mkono

Adhabu ya viboko hata mimi siiungi mkono. Sema tu watanzania hatuna adhabu mbadala. Laiti tungeweza kuaply hizo mbadala nadhani ina manufaa kuliko viboko. Ila kulingana na Idadi kubwa ya wanafunzi, Walimu wanaona viboko ndo adhabu ya haraka kuliko mbadala kwani hizo zinahitaji usimamizi.
 
Back
Top Bottom