Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,627
Naomba mlifikishe hili suala kwa raisi kwani wasaidizi wake wapo kupiga dili tu. Tangu mwaka jana niliamua kufuata bidhaa Kampala hasa nguo na vipodozi.
Tangu nimeanza hii biashara ndugu zangu nimejifunza kuwa hii inchi kamwe tusitegemee kuwa inchi ya maendeleo ama kutoka hapa tulipo na kusonga mbele.
Ukifika Kampala bidhaa karibu zote ukiongea na wafanyabiashara watakwambia zinapitia bandari ya Dar es salaam lakini bei zake ni ndogo sana tofauti na bidhaa zilizoko nchini mwetu huku bidhaa za Waganda zikiwa nzuri sana.
Mwanzo nilidhani kwa vile niko Mwanza huenda ukaribu na Uganda umenifanya nichukue bidhaa Kampala,lakini nikajikuta nakutana na wafanyabiashara kutoka Dar es salaam kwa wingi wakifuata bidhaa hizi hizi Kampala.
Rais wangu mimi kama Mtanzania ninayeamini nchi yetu inastahili kuwa na maendeleo kama Afrika Kusini,inaniuma sana pesa zangu/zetu kuziacha Uganda kwa vile tu Wafanyabiashara wakubwa nchini mwetu serikali yako inawatoza ushuru mkubwa kiasi kwamba inawabidi wapandishe bei kwa sisi wenye mitaji midogo.
Rais wangu hebu fikri kama bidhaa tunazochukua Uganda zinakuwa nafuu na huku wakitumia Bandari yetu ya Dar! Tutendeeni haki sie Watanzania tusio na ndoto za kuwa wanasiasa ambao wanatumia siasa kujitajirisha huku wakituwekea masharti magumu katika biashara tofauti na nchi zingine ikiwemo Uganda ambayo kibiashara iko juu sana mheshimiwa.