Rais Kikwete na safari za nje

Mwenzenu naombeni mnisaidie: huyu mwenzetu Lunyungu ana miguu mingapi, maana yeye hupatikana katika matukio yote: Ikitokea Chacha Wangwe yuko Tarime atakwambia nipo Tarime, ikiwa Kikwete yupo Uholanzi anasema yupo huko naye anasubiri kumbana maswali, haya leo ametusalimia akiwa uwanjwa wa ndege wa Eldoret Kenya! Sasa huyu ndugu yuko wapi na ana miguu mingapi au yeye ni popo bawa?
 
Hehee,
Hivi watu hawajui waholanzi wana-share katika kampuni letu liitwalo Tanzania? Ohooo. Ile Kingdom ina tu-mizizi Tanzania. WaTanzania mnauzwa hamjijui eeeh? Msiniulize, ila ni tu-fununu tu.
 
sO FAR UNCONFIRMED REPORTS zinasema kuwa MUUNGWANA au MZEE WA PAMBA atakuwa na tribu za kwenda:

1 HOLLAND

2 GERMANY

sina hakika kuna nini anachokifuata huko lakini mnayo ratiba zake hebu tuwekeni sawa hapa
 
Napenda kukutoa wasi wasi na kukushauri uwe unasoma vyema na kuelewa maandiko ya Lunyungu.

Kuwako katika maeneo kama ya Chacha Wangwe si shida na kutoka Tarime kwenda Kenya si mbali . Majuzi nilikuwa Moshi kwa Bus nikaenda Musoma na nilikuwa niko Mwanza naelekea Bukoba katika kazi zangu Ujasiriamali ndipo yakazuka haya ya Kenya .Nikageuza nikaenda Kenya .

Now habari ya Holland a JK kasome tena . Nimesema nina nyeti za Mkuu wa Kaya kuwa Ulaya na atafika Holland . Nimeomba maswali niyapenyeze kwa vijana wangu wakamuulize Mzee . Nimerudia mara 2 kusema hili .

Ukiwa unakerwa na posting za Lunyungu usiwe unasoma na ukiamua kusoma tuliza akili . Niko Kenya na siko Ulaya .

Salaam toka Kenya .
 
Pia kuna fununu kabla ya mwezi Januari kukatika atatinga tena ndani ya USA.
 
HAKUNA HAJA YA KUTUMA SWALI HILI SIRINI NA KAMA YEYOTE ANASOMA HAPA NA YUKO KARIBU NA PREZO AU MAMBO YA NDANI AU UBALOZI (UBELGIJI) NAWASOGEZEA SWALI HILI AMBALO NDUGU ZANGU WA HUKO WANAULIZA KILA SIKU, LIULIZWE AU LISIULIZWE RAIS AJIANDAE KUWA NA MAJIBU AU MAELEZO YA SWALI LIFUATALO:

KWA NINI MSAIDIZI WA BALOZI (KONSULA) WA HUKO NETHERLANDS NI MDACHI BADALA YA KUWA MTANZANIA???? NA NI NANI ALIYEMTEUA NA ANAWAJIBIKA KWA NANI MAANA UBALOZI WA UBELGIJI HAUKO JUU YAKE.



Mliokuwa mnatafuta ma skendo ya Balozi zetu huko nje

MZUNGU AMBAYE SI RAIA WA KUZALIWA WALA WA KUPEWA ana pata ACCESS ZA SIRI ZA SERIKALI YETU UBALOZINI PALE HOLLAND huku FOREIGN IKIWA IMEJAA JESHI LA MA GRADUATES AMBAO HAYA NAFASI YA KWENDA RWANDA HAWAJAPEWA


Hivi wapinzani kazi yao ni nini jamani?
 
Mwanakijiji umeua kabisa hapo wale wa KIRARACHA huko moshi kilimanjaro atakwenda lini jamani???
 
JK sasa hatafika Holland na safari yake huko Itatangazwa baadaye . Badala yake JK atakuwa Ujerumani na baadaye kuelekea Finland . Habari za Kibalozi zinasema JK anaweza kuwa Holland kuanzia mwezi March ila watasema wakiwa tayari .
 
Mimi ni Mjasiriamali tu na kupata habari na kuwapa JF ndiyo maisha yenyewe sasa tutafanyeje .Usiogope na access
 
He he he hili wazo Membe kalichukua hapa hapa ukumbini...:) Kweli hii forum ni bab kubwa.


Membe afafanua safari za JK

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema ataandaa orodha ya safari za marais wa nchi za Afrika na gharama zao ili Watanzania waweze kulinganisha na safari zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete.
Kauli hiyo ya Membe inatokana na wadau mbalimbali kudai Rais Jakaya Kikwete amekuwa akifanya ziara nyingi nje ya nchi pamoja na kuongozana na ujumbe mkubwa unaogharimu taifa fedha nyingi.

Akizungumza juzi Dar es Salaam katika kipindi cha 'Hamza Kassongo Hour', kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten, alisema safari za Rais Kikwete ni chache na zenye tija kiuchumi ikilinganishwa na viongozi wengine wa nchi za Afrika.

Alisema si sahihi kulinganisha safari zinazofanywa na Rais Kikwete na marais waliotangulia kwa sababu dunia hivi sasa imebadilika na Tanzania inapaswa itafute wawekezaji kwa lengo la kukuza uchumi.

"Huwezi kulinganisha safari za marais waliotangulia na rais wa sasa, kwani dunia hivi sasa imeendelea na inahitaji rais mwenye kutafuta wawekezaji kukuza uchumi wa nchi yake," alisema Membe.

Alisema iwapo Rais Kikwete hatofanya safari hizo, maisha ya Watanzania na uchumi wa nchi utakuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo hivi sasa na nchi itakuwa tegemezi kwa kila kitu.

"Nchi kama Afrika Kusini na Uganda ambazo uchumi wao unakua vizuri kila kukicha viongozi wao wapo safarini kutafuta wawekezaji, sasa iweje sisi wenye uchumi mdogo Rais wetu asiwe na safari nyingi za kutafuta wawekezaji?" alihoji Membe.

Kuhusu ukubwa wa baraza la mawaziri alisema si hoja bali subira ya Watanzania inahitajika zaidi ili matunda ya kazi zinazofanywa na mawaziri hao zionekane baada ya miaka mitano.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Kikwete miaka miwili iliyopita kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu kuwa Rais amekuwa akifanya safari nyingi zisizokuwa na tija kwa taifa sanjari na kusafiri na ujumbe mkubwa.




 
Watanzania hatuoni matunda yoyote ya safari za Muungwana nje ya nchi. Kama kuna manufaa yoyote ya safari hizo basi yaorodheshwe ili tuyachambue kama kweli yalikuwa ni manufaa au usanii tu na UVDG.
 
Inasemekana wafanyakazi wa foreign wamedevelop a dangerous obsession na JF kama ilivyokuwa ikulu na sasa mpaka waziri wao naye kaamua kukujibuni indirect kufuatia ile thread yetu ya ITINERARY YA JK ya 2008. Kwa hili i wish to disagree na MEMBE kwenye kila kona ya hoja yake na one would have thought JOHN HOPKINS graduate kama yeye angeweza kuja na jibu la maana kuliko hili jibu lilijaa politics

Admin unaweza ukaimerge baada ya muda hii thread na ile nyingine:


Membe afafanua safari za Kikwete..


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema ataandaa orodha ya safari za marais wa nchi za Afrika na gharama zao ili Watanzania waweze kulinganisha na safari zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete.

Kauli hiyo ya Membe inatokana na wadau mbalimbali kudai Rais Jakaya Kikwete amekuwa akifanya ziara nyingi nje ya nchi pamoja na kuongozana na ujumbe mkubwa unaogharimu taifa fedha nyingi.

Akizungumza juzi Dar es Salaam katika kipindi cha 'Hamza Kassongo Hour', kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten, alisema safari za Rais Kikwete ni chache na zenye tija kiuchumi ikilinganishwa na viongozi wengine wa nchi za Afrika.

Alisema si sahihi kulinganisha safari zinazofanywa na Rais Kikwete na marais waliotangulia kwa sababu dunia hivi sasa imebadilika na Tanzania inapaswa itafute wawekezaji kwa lengo la kukuza uchumi.

"Huwezi kulinganisha safari za marais waliotangulia na rais wa sasa, kwani dunia hivi sasa imeendelea na inahitaji rais mwenye kutafuta wawekezaji kukuza uchumi wa nchi yake," alisema Membe.

Alisema iwapo Rais Kikwete hatofanya safari hizo, maisha ya Watanzania na uchumi wa nchi utakuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo hivi sasa na nchi itakuwa tegemezi kwa kila kitu.

"Nchi kama Afrika Kusini na Uganda ambazo uchumi wao unakua vizuri kila kukicha viongozi wao wapo safarini kutafuta wawekezaji, sasa iweje sisi wenye uchumi mdogo Rais wetu asiwe na safari nyingi za kutafuta wawekezaji?" alihoji Membe.

Kuhusu ukubwa wa baraza la mawaziri alisema si hoja bali subira ya Watanzania inahitajika zaidi ili matunda ya kazi zinazofanywa na mawaziri hao zionekane baada ya miaka mitano.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Kikwete miaka miwili iliyopita kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu kuwa Rais amekuwa akifanya safari nyingi zisizokuwa na tija kwa taifa sanjari na kusafiri na ujumbe mkubwa.Habari hii na Salehe Mohamed, picha na Chacha. DC
 
Hivi Membe ana akili kweli? Uganda na S.A wanaenda kutafuta wawekezaji kwa maana wameshaweka miundombinu sawasawa. Sasa mmungwana mambo ya muhimu kama barabara, maji na umeme yahajakaa vizuri anakimbia kutafuta wawekezaji wa nini? Nani alimwambia kuwa tunahitaji kwenda kuomba wamachinga waje Tanzania? Nenda Kariakoo ndio utajua hakuna wawekezaji kuna wamachinga wa kichina wengi tuu. Muungwana anatakiwa akae kwanza nchini aweke mambo sawa kabla hajaenda kutafuta hao wawekezaji. Hivi hata kwenye madini kuna haja ya kwenda kuwapigia watu magoti?
 
Nadhani tangu aingie madarakani, raisi atakuwa ameshajaza pasipoti kama mbili ama tatu hivi kwa uchache, kwa sababu pasipoti zetu zina leaf kama 48 na yeye kasafiri mara kadhaa sana (just kidding).

GT,
Unajua Membe anashangaza na kusikitisha sana kwa utetezi wake wa safari za raisi wetu ambazo tunazipigia kelele. Hivi yeye anafikiri anaongea na 'laymen' sio? Unapoamua kuwaita wawekezaji ujue kuna kitu kinakosekana mahali fulani nyumbani kwako ambacho hakiwavutii. Wawekezaji makini sio watu wa kusubiri kuitwa na kubembelezwa kuwekeza mahali, wao wana mikakati na taratibu zao za kusaka masoko na sehemu za kuwekeza mitaji yao, kiasi kwamba kama mahali fulani pana biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza mtaji wake basi wao hufika hata kabla ya kufuatwa na kubembelezwa. Mfano, Afrika Kusini wao wana madini ya aina mbali mbali, hawana haja ya kwenda Ulaya na kuwambia wazungu kwamba wana dhahabu! Ila wazungu ndio wanaifuata dhahabu ya Afrika kusini. Uwekezaji wote wanaopigia kelele akina Membe na wenzake ni katika madini tu, mbona hatuoni viwanda vikubwa vinavyoajiri maelfu ya watu vikianzishwa Tanzania? Mbona hatuoni wawekezaji wa kuaminika katika kilimo? Mazingira ya uwekezaji Tanzania hayavutii na sio tambarare kama viongozi wanavyotaka kutuaminisha kwa sababu:-

1. Miundombinu Mibovu
Barabara nyingi za Tanzania hazipitiki wakati wa masika. Na hii ni tabia sugu ya barabara zetu ambazo zimesahauliwa na sirikali. Unapomuita mwekezaji ili awekeze katika mbuga zetu, ambazo barabara zake si za kuaminika, sidhani kama ataitikia kwa moyo wote. Hakuna haja ya mtu wa Bukoba kupitia Kenya na Uganda anapotaka kwenda mkoani kwake, kama anasafiri kwa basi! Mbona wanaokwenda Ruvuma na Mbeya hawapitii Msumbiji ama Zambia wanapokwenda mikoani kwao? Hali kadhalika, viwanja vidogo vya ndege (airstrips)vingi vimesahaulika, hii nayo inakatisha sana tamaa wawekezaji. Hatuna reli za kuaminika. Bandari zetu ndio sina hata la kusema, zinafanya kazi pole pole sana na kazi zinazofanyika ni chini ya kiwango. Wateja wazikimbia, wanapitishia mizigo nchi jirani. Mwekezaji gani makini atakayepoteza muda bandarini na kupigwa faini na wateja wake kwa kuwacheleweshea biashara zao? Hatuko makini na kile tunachotaka kukifanya.

2. Urasimu
Kuna urasimu sana katika serikali na taasisi zake. Huduma nyingi zinapatikana kwa kuwalamba watu miguu ama kutoa rushwa, sasa kwa wawekezaji makini ambao wanataka kuwekeza mitaji yao mikubwa na yenye maana hawawezi kukubali urasimu huu na mizunguko isiyoisha, ya njoo kesho, kwa sababu muda ni mali.

3. Nishati
Tanzania tuna matatizo makubwa sana ya nishati, hapa namaanisha mafuta na umeme, ambavyo ni nyenzo muhimu sana kwa maendeleo yoyote yale. Umeme wetu ni wa kuazima, kwa maana ya kwamba si wa uhakika/kuaminika. Umeme unakatika bila taarifa, ukija unakuwa pungufu na kadhalika. Mtu anakuwa hana uhakika kama masaa machache baadaye atakuwa na umeme ama la! Sasa kwa mtu ambaye anafukuzana na oda za wateja lazima apate umeme wa uhakika ili azalishe kile wateja wake wanachokihitaji kwa muda huo. Umeme wetu hutegemea maji kwa asilimia 90 ili uzalishwe! Mvua zikigoma na umeme hakuna! Nani mwehu wa kuwekeza katika mazingira ya namna hii? Tunacheza! Bei za mafuta haziaminiki! Leo hivi, kesho vile. Miaka ya nyuma enzi za TIPER (RIP), angalau bei zilikuwa hazibadiliki kila mara kama sasa.

4. Hatuna Utashi wa Kisiasa
Viongozi wetu wengi hawana utashi wa kisiasa wa kuwavutia wawekezaji, sijajua shida iko wapi. Kila nikiangalia televisheni za nchi za nje, nawaonea sana wivu wenzetu wanavyotangaza biashara zao, hasa utalii. Nchi kama Malaysia, Trinidad na Tobago na India zimejaza matangazo ya utalii wa nchi zao katika runinga hizi, sisi kinatushinda nini? Hatuna pesa za kulipia matangazo haya? Hatutaki kujitangaza? Hatuwezi kujitangaza? Shida ni nini? Nani atutangaze? Nani awajibike kwa hili?

Nahitimisha kwa kusema kwamba, kama tunataka wawekezaji wa maana, ni lazima tufagie nyumbani kwetu pawe pasafi ili hao wanaoingia kuwekeza wakute hakuna uchafu. Hapo watakuja hata bila kuitwa, kwa sababu "CHEMA CHAJIUZA".
Ni Mtazamo tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom