Raisi kikwete asahau waliyotarajia watanzania.

curiosity

Member
Apr 4, 2012
10
1
Nimejaribu kuangalia kwa makini mtiririko wa utendaji wa Raisi wetu.. nashawishika kusema Raisi amesahau kabisa nini watanzania walitarajia kutoka kwake. Kwanza:
1. Huduma nzuri za afya
2.Huduma za elimu
3.Huduma za usafiri
4.Huduma za Biashara
5.Huduma za Bidhaa(za vyakula)
6.Kilimo kuwa cha kisasa.

Sisemi kuwa angetimiza yote hapo juu. ila angechagua maalum adili nayo huku mengine yakienda taratibu ili ajaye nae achague yalirobaki mpaka nchi iwe safi.

Cha kusangaza, Raisi hajashuhulikia suala hata moja likapata mtiririko wa kustawi, badala yake Raisi ametawanya na kudhoofisha kabisa baadhi ya mihimili ya uchumi ikiwemo, kilimo, viwanda, biashara za nje.

Siri moja ya uzembe wa kiongozi wetu ni kutotimiza maneno makali ya adhabu anazotaja. Huishia mdomoni hatimaye walanguzi wanaendelea kupeta, wafuja mali, na watumiaji vibaya wa madaraka.

Ushauri wangu kwa Raisi, atavunja baraza la mawaziri hii ni nzuri isipokuwa ili baraza liwe limevunjwa ni vema atateua mawaziri wenye uwezo na tena ambao ni watekelezaji.

Karibuni tumshauri Raisi
 
Back
Top Bottom