Rais Zuma Adendeka na Winnie Mandela

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409

Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari ya Kimataifa
Picha za rais wa Afrika Kusini mwenye ndoa tano mpaka sasa, Jacob Zuma, zinazomuonesha ‘akidendeka' na mtalaka wa rais Mstaafu, Mzee Nelson Mandela, Winnie Mandela, zimesambaa katika mitandao mbalimbali, Ijumaa limegundua.
Winnie na Zuma walinaswa na mapaparazi wakiwa wamekumbatiana huku midomo yao ikiwa imegusana kitendo kilichotafsiriwa kwamba, walikuwa ‘wakidendeka'.

Tukio hilo la ajabu kwa baadhi ya mila, desturi na tamaduni za Kiafrika, lilijiri wakati wa sherehe za kumpongeza ‘mnene' huyo wa nchi kuingia madarakani miaka miwili iliyopita.
Licha ya picha hizo kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali bila kuwahusisha wawili hao na mdudu wa mapenzi, wachangiaji wengi wa maoni wamekuwa wakitatizwa na denda hilo.
RAISZUMA.jpg "Nothing to hide" (hakuna cha kuficha) alisema mchangiaji mmoja alipotoa maoni yake katika moja ya mtandao ulioweka picha hizo.
"Kifupi picha hizi ni za kimahaba zaidi na kwa maadili ya kiongozi wa kiafrika si nzuri, inawezekana kwao kufanya vile si vibaya, lakini kwetu na nchi nyingi za kiafrika zinaashiria kitu kibaya," alisema mmoja wa wasomaji wa mitandao.

Habari zaidi zinasema kwamba, wakati wa kampeni za kuwania uongozi wa nchi hiyo, Winnie, mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo, alikuwa kambi ya Chama cha African National Congress (ANC) ambayo ilimuweka Zuma kuwa mgombea urais.
Rais Zuma amewahi kulaumiwa na baadhi ya watu wa nchi yake kutokana na tabia yake ya kupenda mahaba hasa baada ya ile skendo mbaya ya kudaiwa ‘kujirusha' na mdada mmoja ambaye anatajwa kuwa ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mara baada ya kuisawazisha skendo hiyo kisheria, Zuma alijikuta akitengeneza vichwa vingi vya habari pale alipofunga ndoa na kimwana mmoja, hivyo kuongeza idadi ya wake alionao, kutoka wanne hadi watano, licha ya mmoja kufa kwa kujinyonga na mwingine kutengana naye.
Hata hivyo, licha ya kiongozi huyo mwenye makeke mengi kuwa na wake wengi, bado ni kipenzi cha raia wake ambao wengi wanachukulia ndoa hizo kuwa ni kitu cha kawaida kikisimamiwa na mwongozo wa utamaduni wa kabila lake.
Hivi karibuni, kiongozi huyo wa taifa kubwa barani Afrika alikwenda kwenye kituo kimoja cha afya na kupima ‘ngoma' lakini majibu yalitoka ‘HANA' hali iliyomfurahisha sana ambapo hakusita kuonesha furaha yake.

Kwa upande wake, Mama Winnie Mandela naye aliwahi kupata skendo ya kudaiwa kutembea na kijana mmoja wakati mumewe (wakati huo) Mzee Nelson Madiba Mandela akiwa jela.
Kashfa hiyo ndiyo ilisababisha aachike na kiongozi huyo mstaafu mara baada ya mambo kuwa hadharani.
Zuma1.jpg
 
kama kawaida ya wachangiaji wazushi, hiyo picha inakushitua nini inamaana hata matumiza ya neno la kiswahili Denda huyajui?kama waandishi walikuambia ni makanjama hao uzushi tu
 
Wote wakwale na wanasifa zinazofanana za kupenda na kufanya mapenzi na wajukuu wao
 
Mwandishi amechemsha, hilo siyo denda (tongue/french kiss), ni busu la kwenye midomo (lips). Pamoja na hayo, watu wanaobusiana midomo huwa wana ukaribu sana, sina uhakika na kiwango cha ukaribu. Sidhani kama mtu yeyote unaweza kubusu midomo yake. Busu ambazo hazina matatizo wala question marks ni za mwenye mikono na mashavuni ambazo yeyote yule anaweza kugawiwa popote na wakati wowote bila maswali.

Ukiangalia hizo picha ni kwenye matukio mawili 2, maana kwenye kila picha wamevaa nguo tofauti, na hivyo ina ashiria huwa wanafanya hivyo kwenye matukio mbali mbali mbele ya kadamnasi. Swali ni kwamba kwanini wanabusiana midomo na siyo mashavu kama inavyoanywa na wengi? Ni swala la kawaida kwa wasauzi kubusiana midomo?

Zuma alishaujulisha ulimwengu kwamba yeye swala linaitwa ngono lina top priority, na hivyo anaweza kufanya chochote. Madikizela Winnie anaweza kuwa kwenye mission ya kulipa kisasi kwa mumewe ambacho sidhani kama kinaweza kuwa na maana yoyote. Tangu Mandela aachie ngazi, Winnie amekuwa mstari wa mbele ku-criticize policy za Mandela na baadaye za Mbeki. Tangu Zuma ameingia madarakani sijamsikia Winnie akim-criticize Zuma.

Labda kitu cha kujiuliza hizo picha ni za hao wahusika? Au zimerekebishwa kiaina? Maana hata kama ni busu la kawaida, namna wanavyokumbatiana inatia shaka.
 
Sijui watoto na vijana wetu wanajifunza nini kwa wazito kama hawa! Jamani!
 
watu weusi tumetegwa katika mahusiano, yani kama tungekuwa na kwenye uchumi tumechangamka kama kule basi wazungu wangetukoma
 
Back
Top Bottom