Rais wetu na safari mfululizo

Jamani tuache kumshtumu Muungwana maana hauwezijua kama moyo anapenda kusafiri au anasafiri bila kupenda maana huyu ni mkuu wa nchi anawajibu wa kufanya kila lililojema kwasababu hata alivyo ishiwa nguvu alikuwa katoka safari na ilibidi asikwepe jukumu la kwenda mwanza maana ilikuwa kazi yake.
Lamsingi ni kuwa wavumilivu tu! He is the PRESIDENT.
 
Pia leo anaingia new york na atakuwa hapo kwa situ tatu mpaka tarehe 5 december. Hii ni safari binafsi na sijui kama wataitangaza.
 
Ndugu Zangu
Nami wiki iliyopita nilkuwa Zambia katika safari ya kiutafiti gazeti la Sunday Post lilionyesha jinsi Raisi wao Rupiah Banda anavyosafiri na kutanua kwa kutumia pesa za umma hakuna tofauti hata kidogo na Raisi wetu. Ni kwamba siku hizi uraisi na ukubwa ni uwanja wa kutapanya pesa zetu na kama alivyowahi kusema kuwa kukaa Tanzania ni kugawana umaskini. Ukichukulia kuwa msafara wa Raisi una watu wasiopungua 30 na kila mtu analipwa si chini ya dola 500 kwa siku na kwa kuwa Mkulu wetu anakaa nje ya nchi si chini ya siku 15 kwa mwezi unaweza kujua jinsi gani ulaji wa pesa za nchi unavyoendelezwa na serikali yake. Kama nilivyokwisha kusema kama Mkulu wetu angafuta safari hizo kila hospitali na vituo vya afya nchini vingeweza kuwa na wodi za kutosha za akina mama wajawazito na kuondoa aibu ya akina mama watatu kuchangia kitanda kimoja. Nadhani watu wa usalama wa taifa mnaosoma mtungo huu mtamweleza mkulu wetu kwani hii ni aibu kubwa sana ikiwa ni pamoja na kubembea. Mwambieni tunaweza kumwekea bembea nzuri pale Ikulu na kwa kweli hakuna bembea nzuri zaidi ya kutatua matatizo ya wananchi wako.
 
kwani yanawahusu nini.....mwacheni atese amepata urais kwa mbinde sana.......mwacheni ale asivyo lima


Lakini Watanzania hawakumchagua ili 'atese', walimpa kura zao ili awatumikie. He is a complete flop!
 
Hizo hela zinazotumika kusafiri yeye na wapambe angeziweka kwenye zana za kilimo kwanza wananchi wangefaidika zaidi
 
Back
Top Bottom