Rais wetu Asaidiwe kuandaa Hotuba

Dar Es Salaam, Mbona unakwepa kutusaidia kufahamu tatizo la Rais wetu na badala yake unaanza ku-edit messages za watu? hapa kuna koma, pale kuna el hapa pawe hivi na unamaliza kwa mtindo wa jinsia ya aina fulani, kwamba ukizozwa wewe unaishia kuzomea.. Hiloooo! Oooo! yebaaa!

JF tunataka Uandike maoni yako kwa mada iliyoko mbele yetu. Hatujasema haleti maendeleo. Hatujasema hajafanya kitu, nk. Tatizo letu ni hotuba na aina ya maneno anayotumia ktk hotuba. Hata kama atatuletea kocha wa mpira kila mkoa kama kitendo cha maendeleo, bado hiyo siyo sababu ya kufurahia hotuba zilizopinda-pinda kwa uzembe wakati uwezekanao wa kuzionyoosha unaonekana.

Hotuba zake ni swaaafi sana hazina dosari, zinatoka moyoni sio kwenye karatasi za kuandikiwa, lipi zaidi ya hilo? au mmezowea kudanganywa-danganywa?
 
Haswa, taswira ya JK ni ukweli na uwazi na anaongea, kwenye hotuba zake ukweli mtupu, chuki binafsi zinawafanya mumchukie, kawakosa nini? Rais aliyewajengea mashule mengi kuliko Rais yeyote aliyepita! Rais aliyewafichua mafisadi wa toka enzi za Nyerere! Rais aliye ahidi na kuanzisha chuo kikuu kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki, katika muda usiofikia miaka miwili toka aahidi, Rais anaemalizia mabarabara yaliyowashinda ma Rais wote waliopita, mpaka sasa unaona raha ukienda Mwanza kutokea Dar, huna haja tena ya kupitia Kenya labda uwe na sababu zako za kupita huko, lakini si kuwa barabara ni mbovu. Rais alieweza kwa mara ya kwanza katika Historia kumuweka na kumfadhili Rais wa Merekani kwa siku nne katika Afrika, Looh, bado tu hajui kutoa hotuba? ooopssss, Rais wa kwanza wa Tanzania kuwa Mkulu wa AU,, Rais wa kwanza katika Tanzania alieweza kushusha bei ya mafuta yanayotumika kwenye magari na viwanda, haijawahi kutokea, bado hajui kutoa hotuba tuu? tafuteni jengine sio hili. Looohhh.

.......no wonder Tanzania ndivyo ilivyo today........kwi kwi kwi kwi
 
hivi mnataka aeleze nini.msaidieni au mundikieni kwenye web site yake kumueleza mnayopenda kusikiliza.pengine mumezoea porojo

Raisi wetu alimteua mwandika hotuba sio kwa uwezo wake wakuandika hotuba, nikimaanisha uzoefu na upeo. Yeye alikuwa analipa fadhila za mzee wake wa chama kwa kumsaidia kupata urais ndio sasa tunaona jinsi gani huyo jamaa anavyochemsha. Hiyo kazi inaitaji mtu mwenye uwezo wakuwa msikivu na ndio kuwa mwandishi au mwongeaji mzuri. Wewe kama unajifanya "much know" na ujichanganyi na watu ambao ni wananchi wakawaida, huwezi kujua shida na taabu zao za kila siku. Yote unayomsaidi mheshimiwa kuandika na maneno ya kutaka kuonekana ni mmoja wao kumbe na matusi na nje ya matarajio ya wananchi. Kuna watu wengi wenye uwezo wakuandaa excellent speech, ni bwana mheshimiwa kutumia human resource dept yake kuwapata.
 
Haswa, taswira ya JK ni ukweli na uwazi na anaongea, kwenye hotuba zake ukweli mtupu, chuki binafsi zinawafanya mumchukie, kawakosa nini? Rais aliyewajengea mashule mengi kuliko Rais yeyote aliyepita! Rais aliyewafichua mafisadi wa toka enzi za Nyerere! Rais aliye ahidi na kuanzisha chuo kikuu kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki, katika muda usiofikia miaka miwili toka aahidi, Rais anaemalizia mabarabara yaliyowashinda ma Rais wote waliopita, mpaka sasa unaona raha ukienda Mwanza kutokea Dar, huna haja tena ya kupitia Kenya labda uwe na sababu zako za kupita huko, lakini si kuwa barabara ni mbovu. Rais alieweza kwa mara ya kwanza katika Historia kumuweka na kumfadhili Rais wa Merekani kwa siku nne katika Afrika, Looh, bado tu hajui kutoa hotuba? ooopssss, Rais wa kwanza wa Tanzania kuwa Mkulu wa AU,, Rais wa kwanza katika Tanzania alieweza kushusha bei ya mafuta yanayotumika kwenye magari na viwanda, haijawahi kutokea, bado hajui kutoa hotuba tuu? tafuteni jengine sio hili. Looohhh.

Dar,

Kama unalipwa kwa kazi hiyo basi unastahili kupata malipo hayo. Hata hivyo Watanzania hawali orodha ya mafanikio!
 
Last edited:
Wewe ulishaona wapi Rais akachaguliwa mwandishi wake na mwandika hotuba zake na watu wengine.

Kama kashindwa kusoma magazeti na kuona au kuwasoma watu wanaojua kupanga hoja zikapangika ni makosa yake mwenyewe. Na bado makosa mengi tu yanakuja akiendelea kuwa na watu ambao hata kusoma kwao kwenye shule za uandishi wa habari kulikuwa kwa kuwaegemea watu wengine. Kama kweli waliusomea uandishi kwa kina kiasi hicho wanachojidai kwa sifa walizonazo. Uandishi kwa ajili ya rais sio sawa na kuandika makala. Unamtaka mtu anayeweza kuandikiwa spichi na watu sio chini ya wanne. Halafu yeye akaketi na kuzisuka zote kutoa kitu kimoja bomba ile mbaya na ambapo haionekani kama rais au waziri mkuu karopoka kama mhuni wa mitaani!
 
Dar,

Kama unalipwa kwa kazi hiyo basi unastahili kupata malipo hayo. Hata hivyo Watanzania hawali orodha ya mafanikio!

Dark City, mwenzetu huyu Dar ni die hard fan wa JK, na ni haki yake lakini kama anafanya kazi kubwa hivyo ya kumtetea ni vyema akihakikisha analipwa ipasavyo.
Alafu mi nahisi huyu Dar asije akawa ndo speechwriter wake na issue inamgusa moja kwa moja.... kwikwikwii...
 
Dar,

Kama unalipwa kwa kazi hiyo basi unastahili kupata malipo hayo. Hata hivyo Watanzania hawali orodha ya mafanikio!

Wewe unataka ulishwe na KIKWETE, akaa, una nini wewe unategemea kulishwa?
 
Dark City, mwenzetu huyu Dar ni die hard fan wa JK, na ni haki yake lakini kama anafanya kazi kubwa hivyo ya kumtetea ni vyema akihakikisha analipwa ipasavyo.
Alafu mi nahisi huyu Dar asije akawa ndo speechwriter wake na issue inamgusa moja kwa moja.... kwikwikwii...

Hahahaha, hoja zingine zina-chekesha, hivi na nyinyi huwalipa nani kwa kumponda Jakaya? au ndio zile agenda za siri?
 
I think three things motivates speeches za kiongozi wa nchi
1. Who am I - Yeye anajionaje, anajitambuaje, ana-self perception gani - and ni kwa kiasi gani ana-identify with hiyo perception! Especially what does it take to identify correctly with this self perception! (This is not the same as saying nyinyi mnamuona yeye ni nani!)
2. What is his mission - nini anataka ku-achieve, ana-believe in it kwa kiasi gani, ana commitment ya kuki-achieve kiasi gani, legacy gani anataka kuacha etc.
3. Anazungumza na nani - Usually kiongozi akiwa anazungumza anatakiwa kuwa na social-cross section ya audience anayoilenga! So, usually the speech reflects the audience in the view of the leader, for instance nimelenga peasants, waume wenza, wapinzani, etc.

Perhaps itasaidia wanao-kerwa na speeches kujua hayo matatu; labda wao si walengwa, labda wanataswira tofauti na taswira aliyonayo mzungumzaji; labda mission yake sio mission wanayotaka wao etc.

Poleni sana waungwana - Life can be a b***** sometimes!
 
Tuliuliza na tumekuwa tukiuliza bila majibu kwa miaka mingi sasa.

Kwa nini vichwa hivi havifuzu? Hotuba gani hizi?
 
Kwa kweli hotuba zake hazikidhi haja na hupoteza air time ya tv bure tu. Hivi kutuambia mvua hazinyeshi, bei za vyakula zimepanda, mabomu yamelipuka, Chadema wameandamna , kina cha maji mtera kimeshuka blah,blah, blah anaona sisi watanzania hatujui hali halisi ya maisha tunayoishi mpaka atutangazie yeye?

Tutazidi kuandamana hadi kieleweke
 
Huyu Rais jamani na hizi hotuba zake! Ni kama Tz hatuna wataalamu wa hotuba kiasi kwamba Rais hajapata mtu wa kumuandikia hotuba za ki-Rais.

Zile za kila mwisho wa mwezi ni kama summary ya matukio. Yeye akaziita hotuba.

Akatoa ile ya half term ikawa imejaa matusi pale alipojidai kutoa michapo. Eti lazima uliwe ndo ule. Tena kwa kurudia-rudia na kucheka. Rais huyo!

Kuna ile nyingine ya siku ya UKIMWI hiyo ndo alitoa mpya. UKIMWI ni wa kujitakia. Mbele ya wananchi wake, wenye ukimwi na wasio na ukimwi. Wakubwa na watoto. Akaendelea na matusi mengine.

Huko Pemba tena ndo kaja na hayo anayodhani ni ushujaa wa kisiasa kwa kutumia maneno kama ya taarabu.

Rais yabidi ashauliwe apate mwandishi wa maana. Aaambiwe asome hotuba na siyo kutoa yake kichwani maana yaonekana uwezo huo hana. Najua ugumu utakuwa ktk kujibu maswali lakini kwa Rais wa Africa ni rahisi kukwepa mahojiano. Tahadhari yaficha aibu.

Hapo kwenye red nimekubali. Inaonekana anajitahidi sana kumwiga "Mzee" Nyerere anadhani Mwalimu alikuwa wa mchezo; jembe lile (RIP). Akina Mkapa wamejaribu wameshindwa ndio itakuwa Kikwete hata maprofesa wengi hawawezi hiyo na uprofesa wao; ni Baba wa Taifa peke yake alikuwa na uwezo huo; kwa kiasi fulani Dr. Slaa ndiye aneyeonekana angalau kuweza kulegeza gidamu za viatu vya Mwalimu.

Hao wengine saizi yao ni madesa tu na u-Dr. wa kujipachika kana kwamba kuwa Dr. ni sifa! Sifa ni jinsi gani ulivyoweza kulivusha taifa lako salama na sio blaa blaa za kijinga.
 
"Taarifa kamili" iambatane na CV ya mtajwa itakayojumuisha kiwango chake cha elimu.

Hapo kwenye red. Kiwango cha elimu si kigezo pekee. Laiti ungejua baadhi wasomi wa nchi hii walio karibu na au kwenye utawala walivyochangia matatizo makubwa tuliyonayo leo hii. Kuna vitu vinahitajika zaidi, kiwango cha elimu ni sehemu tu na kwa bahati mbaya ma-CV mengi yamejaza madudu hayo - heri hata karatasi la chooni kuliko hiyo mi-CV.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom