Rais wetu anapokuwa hapatikani kutoa maamuzi

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,570
187
Wadau nataka kufahamu hii imekaaje jana PM. Mizengo Pinda anatangazia umma kuwa ameshindwa kuwasiliana na Rais kwa sababu yuko angani hapa inatia shaka inakuwaje Rais anaporuka kwenye Gulfstream 55 anakuwa hana hot line ya kuzungumza na wateule wake aliowaachia kuongoza nchi? Nijuavyo mtu kama Abrahamivic wa Chelsea anapatikana kwa wapambe wake muda wote anapokuwa angani naye anatumia Gulfstream 55 kama ya JK sasa hapa kuna mgogoro. Tujadili usalama wa nchi kuwa haina mawasiliano na Rais anapokuwa angani. karibuni
 
Hiyo aliyoisema Pinda ni lugha ya kisiasa tu, na haina ukweli wowote. Mimi nadhani JK alifahamu ugumu wa bajeti ya wizara ya Nishati, akishiriki kuandaa deal ya kuwaweka sawa wabunge, kisha akaondoka. Sasa huku nyuma mambo yame backfire, ni lazima alindwe kwa lugha nzuri. Hata hivyo hana ujanja ni lazima arudi tu nyumbani na kuikuta ngoma bado mbichiiiiii!!!!!!!!!!.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA, ALINUSURIKA KWENYE DOWANS, HAPA NAPO NGOJA TUONE.
 
Hayuko concerned na mambo/mustakabali wa nchi. Hajali/hana haja kufahamu chochote kinachoendelea nyuma yake.
 
Wadau nataka kufahamu hii imekaaje jana PM. Mizengo Pinda anatangazia umma kuwa ameshindwa kuwasiliana na Rais kwa sababu yuko angani hapa inatia shaka inakuwaje Rais anaporuka kwenye Gulfstream 55 anakuwa hana hot line ya kuzungumza na wateule wake aliowaachia kuongoza nchi? Nijuavyo mtu kama Abrahamivic wa Chelsea anapatikana kwa wapambe wake muda wote anapokuwa angani naye anatumia Gulfstream 55 kama ya JK sasa hapa kuna mgogoro. Tujadili usalama wa nchi kuwa haina mawasiliano na Rais anapokuwa angani. karibuni
Nani kakwambia abrmo anamiliki gulfstream? Ye ana boing na pia sasaiv ameagiza airbus A380 hawez tembelea ndege za kimasikini yule
 
Tusubiri tuone atasema nini? kama hili ni dili la ccm basi kuna uwezekano akalipiga chenga kiaina, utaskia ooh tusubiri uchunguzi ufanyike, ooh tuachie mamlaka husika... porojo nyingi za kisiasa..! hapa lazima watu waingie mitaani, nadhani kila sikio la mtanzania ameshasikia yaliojiri na wanasubiri kauli ya JK
 
Naona pinda alitaka kutupotezea eti raisi yuko safarini kama yangekuwa yametokea mapinduzi angesema hayo?
 
Yeye, wanawe, kakazake ,marafiki zake wote wana majenereta na yanalipiwa na serikali mafuta kwa hiyo hapati adha hii
 
Back
Top Bottom