Rais wangu, wananchi wako hatujakutuma kwenda kufanya kazi hizi!

Billion 5.2 kutumika mpaka atakaporudi kwa kuzitembelea USA na CANADA tu.

Halafu nae waziri wa ardhi Tibaijuka anapandisha kodi za viwanja kiholela ili mkuu wao apate hela za kwenda nazo kutalii huku sisi walala hoi tunaumia!!
 
Raisi wangu mpendwa,wakati unazunguka kutafuta kura yangu/zetu katika kampeni za uraisi ulijipambanua kwa kutoa ahadi kedekede kwa kutuhakikishia maisha bora kwa kila mtanzania.
Katika sera zako sikuona sehemu uliyokua unaomba upewe nafasi ili uwe mtembezi wala ombaomba.
Safari za kiongozi wangu za kwenda nje zimekua nying kuliko za kuja huku matombo,ulanga, nanguruwe na kwingineko hapa nchini.
Vijana wamekosa matumaini kiasi kwamba imebaki liwalo na liwe,imefikia point watu sasa wanatafuta sababu ya kufa kwa mfano hebu tazama watu hawaogopi tena polisi na silaha zao tena,nachelea kusema tuendako ni pagumu sana my president please safeguard the situation.
Kuna kazi nyingine ambazo mabalozi wanaweza kuzifanya sio mpaka kila mwaliko lazma uende wewe.
Nakutakia safari njema huku marekani na canada.

kipindi cha pika bomu cha star tv wamemtungia nyimbo .msafiri
 
Siyo laana mkuu. Hajui afanye nini hapa nyumbani. Kuna siku alisema akiwa London, na ninamnukuu....."Wanasema ninasafiri safiri sana. Kah! sasa wanataka nikae nao tu, tule nao mihogo?" ....Mwisho wa kumnukuu

Hebu tujiulize mihogo ina shida gani? Mimi naipenda kuliko mkate na chips!! Ushauri tupende vyakula vyetu vya asili na mwiko kuvibeza hata tukiukaa uongozi uliotukuka/umaarufu kwa kiwango gani!!!
 
Siyo laana mkuu. Hajui afanye nini hapa nyumbani. Kuna siku alisema akiwa London, na ninamnukuu....."Wanasema ninasafiri safiri sana. Kah! sasa wanataka nikae nao tu, tule nao mihogo?" ....Mwisho wa kumnukuu

Mimi nadhani hizi safari sio bure ipo siku ukweli utajulikana,yani kila siku marekani au uingereza,why not japani,india,korea,ujerumani,africa ya kusini nk? Kwa nini iwe ni rais wa tanzania tu anayesafiri mara nyingi hivi? Je rais wetu anaweza kupitisha zaidi ya mwezi bila kusafiri? Watanzania tunajifunza nini kuwa na aina hii ya viongozi?
 
Siamini kama haya niyasomayo ni maneno ya watanzania wazalendo, huwezi kuwa na rais asiye tembea nchi nyingine. Hata atakayeingia ikulu 2015 atafanya hivyo. Tanzania sio kisiwa.
Lakini pia najiuliza kama ni kweli rais hajawahi kutembea maeneo ya vijijini kama wachangiaji wanavyojaribu kutujuza hapa, haki haipatikani kwa mambo ya kuzusha, inatufanya tu tulio nje ya box tufikiri zaidi.
 
kwenye kampen alzunguka nch nzma na mzk juu,tena wasanii we2 wakatoa rmx za kumcfia,mbna hujarudia kuizunguka tz kuangalia kama zile ahad zmetimia?!
 
anataka kuvunja record ya kuwa rais wa kwanza afrika aliyesafiri sana na kupanda ndege nyingi, kula sana na wazungu.
 
Watanzania wenzangu Tuombeni Mungu sana kuhusu mustakabali mzima wa nchi yetu..hili vuguvugu lisije tupeleka tusipo pataka wala kupazoea,kwa kuwa najua kuna wasiotaka kusikia amani wala maendeleo Tanzania.
 
Back
Top Bottom