Rais wangu Kikwete, siwezi kununua hata dagaa sasa!

Wewe kijana unaweza kunipiga mkwala mbuzi mimi? Tatizo nyie vijana wa kizazi cha sasa ni wavivu mno.

Hivi unataka ushinde vijiweni na kwenye vilabu vya mbege bila kufanya kazi halafu unalalamikia serikali ikupe pesa!

Hata kodi ya nyumba unataka serikali ukulipie? Hiyo itakuwa serikali au upo peponi? Kama upo tayari njoo nikupe ajira..

Kila mwezi takupa 400,000 kama upo tayari ni-PM
Nafurahi kama ujumbe umekufikia barabara.Unasema vijana wa sasa ni wavivu na hawataki kufanya kazi,umewapa kazi wakakataa kufanya?Unatambua kua tatizo kubwa kwa sasa Tz ni ajira,halafu wewe unasema hawataki kufanya kazi,WHAT NONE SENSE!Kama unaona ni mkwala Mbuzi jitokeze hadharani na uongee hizo PUMBA zako uone kitakachojiri kwako.
 
Subiri 2015 kura yako i-expire, ndio utie akili
Kwa sasa endelea tu kukumbuka zile pilau na kama vipi pika tshirt na kanga ule
 
m'k'were wewe ni kiboko! Kanyaga twende ukija kutoka madarakani rate ya dollar iwe 2500, mi nshshtuka mda mrefu nina tumia dollar a/c, hayo mashilingi inflation yake sipati picture!
 
Rais Kikwete, miezi 2 iliyopita dagaa kilo moja ilikuwa tsh 3000, leo hii dagaa tsh6200.

Nina watoto 3 wanaosoma, siwezi kuwalisha. Nyama siwezi kununua, na hata dagaa siwei kununua kwa mshahara wa laki 250,000.

Nadhani umeshindwa kuongoza nchi kilichobaki ni sisi kuingia mitaani kukuondoa kama hautaki kuondoka mwenyewe. Siwezi kuendelea kuvumilia, kwa maana kama dagaa chakula cha masikini siwezi kukinunua ni nini sasa nitakachoweza kununua kuwalisha wanangu?

Niwalishe wanangu nini? Nilikupigia kura nikiamini kwamba ungeleta mabadiliko uliyoyaahidi...... baba ondoka, kwa maana umekiua chama chetu cha CCM, vinginevyo tunakwenda Chadema wamama wote
Wakati JK anawapa salamu wafanyakazi walifikiri anatania.
View attachment 42832
 
JK ongeza kasi zaidi, usilegeze mpaka tutakapokataa kupokea kofia na vitenge na skafu n.k, ndiyo uanze kulegeza kwa sasa twende kazi mzee!!!!!!!!!!!
 
Umeongea vizuri ila nilipofika kwenye RED ndio umenichosha kabisa, sasa unamlalamikia Kikwete kwa lipi wakati wewe unapigiwa mdundiko na ukiwepo tshirt na kanga ulikuwa unajisikia raha? na bado mtauza mpaka miili yenu mwaka huu.

JK oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, kanyaga twende baba mpaka wapate akili hawa Wadanganyika.

Ni kama kuoa mke kwa uzuri wake wa sura.Mtajibeba mpaka kaburini kudadeki.
 
Sasa ni wakati wa kutathmini ni vipi utasurvive uibe wakuue wakufunge au uende ikulu na bakuli la kuombea mboga(dagaa)
 
huyo faidha foxy anayetetea ccm mimi namfaham ni mtu wa usalama wa taifa na yupo ikulu.so hawezi ku feel pinch ya maisha huku mtaani.
 
Rais Kikwete, miezi 2 iliyopita dagaa kilo moja ilikuwa tsh 3000, leo hii dagaa tsh6200.

Nina watoto 3 wanaosoma, siwezi kuwalisha. Nyama siwezi kununua, na hata dagaa siwei kununua kwa mshahara wa laki 250,000.

Nadhani umeshindwa kuongoza nchi kilichobaki ni sisi kuingia mitaani kukuondoa kama hautaki kuondoka mwenyewe. Siwezi kuendelea kuvumilia, kwa maana kama dagaa chakula cha masikini siwezi kukinunua ni nini sasa nitakachoweza kununua kuwalisha wanangu?

Niwalishe wanangu nini? Nilikupigia kura nikiamini kwamba ungeleta mabadiliko uliyoyaahidi...... baba ondoka, kwa maana umekiua chama chetu cha CCM, vinginevyo tunakwenda Chadema wamama wote

Yes JichoD this is what I meant. Maisha bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na kutokula vitu vya ajabu ajabu kama dagaa. Nadhani sasa mnanielewa vizuri. J K
 
halafu kumbe ni mwanamke. Ndio hawahawa walisema wanataka rais handsome. Kuleni sura yake sasaaaa!!!!!!!
 
Njaa tulikuwa nayo wakati wa Nyerere. Tunapanga foleni ya unga wa msaada (wa njano) kwa kaya kwa wiki kilo moja. Dagaa ilikuwa anasa.

Leo mwenye njaa ni ama mvivu kupita kiasi au hana akili timamu. Au ni katika wale wanaongojea kupewa na wanashindwa hata kujituma. Leo tunaona mpaka wageni kutoka Ulaya, Asia na nchi zingine za Kiafrika wakikimbilia hapa kuja kuchuma, fursa wanaziona zimejaa kedekede, halafu mtu analalamika tuna njaa. Mie nasema hamna macho lakini si njaa.

yani wewe mama nitapata ban nyingine kwa ajili yako! This vulture infested region you call it WHAT??!!
 
Sijui unaposema masikini unamaanisha nini? lakini nachojua mimi dagaa sio chakula cha masikini,
labda kama wewe sio masikini wa Tanzania.

Pili unayetaka atoke madarakani ni ccm au Jakaya, sababu nimeona unatishia kwenda chadema.

Tatu, hata mimi hapo mwanzo nilikuwa na mawazo kama yako, nilifikia hatua kidooogo nianzishe
harakati za kumuondoa rais madarakani bila kujijua kwamba nilikuwa nafuata mkumbo wa nchi za
kiarabu ambao mpaka sasa umethibitika ni njia ovu kabisa ya kufanya mabadiliko ya kiuongozi.

Katika nchi zote zilizowaondoa marais wao madarakani kwa kujazana barabarani na kufanya fujo,
hakuna hata moja iliyopata faraja sanasana ni fedheha na dhiki kubwa imewazukia.

Ni lazima watanzania tukubaliane na hali halisi, kwamba Jakaya Mrisho Kikwete ndio Rais wetu na
kama sio Mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuruhusu Uhai umtoke kabla ya Muda wake Kumalizika basi
ni Lazima amalize muda wake.
 
Inflation ni jambo la kawaida. Soon ita recovery!
Sawa sawa, Nadhani tatizo ni kwamba hatukuwahi kuexperience haya mambo, na hili
litatuchanganya sana, sababu huwa najiuliza mbona wazee hawalalamiki? kumbe sababu
ni kwamba wakati wa Ujana wao walipigwa na inflation ya ukweli kiasi kwamba hii wanaona
ni cha mtoto na ndio maana hata Jakaya akiwaita kuongea nae wanaenda kwa furaha
na kijani kipichi zao.

I hope tutapita salama
 
yani wewe mama nitapata ban nyingine kwa ajili yako! This vulture infested region you call it WHAT??!!

Huupendi ukweli? Njaa tulikuwanayo wakati wa Nyerere, tukipanga foleni kuanzia saa 9 za usiki kungoja kilo moja ya unga wa manjano kwa wiki kwa kaya. Hiyo ndio njaa, ulikuwepo wewe? uliza tuliokuwepo.

Leo mtu anakaa kwenye mtandao na laptop ya millioni anakwambia anashindwa kununua dagaa. Wacha maskhara weye.
 
huyo faidha foxy anayetetea ccm mimi namfaham ni mtu wa usalama wa taifa na yupo ikulu.so hawezi ku feel pinch ya maisha huku mtaani.

Mimi nnakuambia kama uko mitaani na unashindwa kujikimu basi wewe ni mvivu wa kutupa. Mikazi iliyojaa mpaka wanakuja wachina, wanyasa, wahindi, wewe huzioni tu?
 
Huupendi ukweli? Njaa tulikuwanayo wakati wa Nyerere, tukipanga foleni kuanzia saa 9 za usiki kungoja kilo moja ya unga wa manjano kwa wiki kwa kaya. Hiyo ndio njaa, ulikuwepo wewe? uliza tuliokuwepo.

Leo mtu anakaa kwenye mtandao na laptop ya millioni anakwambia anashindwa kununua dagaa. Wacha maskhara weye.

usiki = usiku
 
Back
Top Bottom