Subirini njaa itakapoingia. Sasa kila kitu kipo na hali ndio hiyo.
dah!!! wakati mwingine kweli tupu.pengine yafaa tuishi kufutana na nyakati maana sasa sio kama ya zamani.Dagaa huwezi kununua lakini fedha ya kuingia mtandaoni unayo, au unaiba mtandao wa ofisini?
Wapi hapo nikanunue mie juz nimenunua 30000 hao dagaa kwa kilo.mweehNadhani hao ni wale dagaa wa Ziwa Victoria na may be dagaa wa Baharini... Kimbembe ni kwa sisi tuliozoea dagaa wa KIGOMA-ziwa tanganyika hapo ndio balaa maana kwasasa bei ni 22,000 kwa Kilo. Maisha bora kwa kila mtaanzania.
:A S embarassed:
miakaya 83 kunawadudu fulani hivi walitokea nakuanza kushambulia mimea mashambani walikuwa wengi balaa!!! tulikuwa tunawafahamu kwa jina la mbilizi. yaani usiombe wajaa mashambani hata kutembea tulikuwa tuna tembea kwa timing kukwepa kuwa kanyaga.mwaka uliofuata njaa njaa yake ilibidi serikali ilete chakula mfano wa ngano kilikuwa sijui kinaitwa buluga na mafuta ya usa.nilishuhudia baadhi ya watu wanashindia kula mboga mboga za polini.Njaa tulikuwa nayo wakati wa Nyerere. Tunapanga foleni ya unga wa msaada (wa njano) kwa kaya kwa wiki kilo moja. Dagaa ilikuwa anasa.
Leo mwenye njaa ni ama mvivu kupita kiasi au hana akili timamu. Au ni katika wale wanaongojea kupewa na wanashindwa hata kujituma. Leo tunaona mpaka wageni kutoka Ulaya, Asia na nchi zingine za Kiafrika wakikimbilia hapa kuja kuchuma, fursa wanaziona zimejaa kedekede, halafu mtu analalamika tuna njaa. Mie nasema hamna macho lakini si njaa.
kwanini asijinyonge kwa kamba kuliko kufedheka na hilo gonjwa la ukimwi.acha ujinga wewe uza mwili'unamlalamikia kikwete akuletee hela nyumbani''komaa upate elfu22 nyingii hili ununue kilo nyingi za dagaa'hii ndio africa bana nyie vpi'komaaa wewe.'kila cku kikwete kikweteee fanya kazi rais haezi kuwa na roho mbaya kiasi hiki'timu yake ndio inamfanyia hujuma'pumbavu nyie CHADEMA.
Wakati anaondoka madarakani $1 ilikuwa sawa na 17/- . Njaa ilitokana na Oil embargo, ukame katika EA pamoja na hila za wamagharibi kuzuia ujamaa. Hata hivyo tulikuwa na Gold reserve yetu (benki na ardhini) na vijana walisoma bure.Njaa tulikuwa nayo wakati wa Nyerere.
miakaya 83 kunawadudu fulani hivi walitokea nakuanza kushambulia mimea mashambani walikuwa wengi balaa!!! tulikuwa tunawafahamu kwa jina la mbilizi. yaani usiombe wajaa mashambani hata kutembea tulikuwa tuna tembea kwa timing kukwepa kuwa kanyaga.mwaka uliofuata njaa njaa yake ilibidi serikali ilete chakula mfano wa ngano kilikuwa sijui kinaitwa buluga na mafuta ya usa.nilishuhudia baadhi ya watu wanashindia kula mboga mboga za polini.
tuombe mungu njaa kali kama hizo za mwaka 74 na 84 zisijirudie.
Wakati anaondoka madarakani $1 ilikuwa sawa na 17/- . Njaa ilitokana na Oil embargo, ukame katika EA pamoja na hila za wamagharibi kuzuia ujamaa. Hata hivyo tulikuwa na Gold reserve yetu (benki na ardhini) na vijana walisoma bure.
hii picha ndio hali halisi ya mtanzania huyu mtoto amekata tamaa na maisha. kweli inatia uchungu sana sasa hivi dar sukari kili shs 2200-2500, maharage hayashikiki sembe ndio inakimbia tuende wapi sisi walalahoi..... JK inchi imekushinda kubali kungatuka
Nilikupigia kura nikiamini kwamba ungeleta mabadiliko uliyoyaahidi......
Sioni sababu ya kulalamika kama ulimpigia kura, na kura yako itadumu kwa miaka mitano, so miaka mitano haijaisha vumilia tu dada subiri 2015