Rais wa Zanzibar akutana na mkurugenzi wa Benki ya Dunia

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130




1463-564x272.jpg

Salma Said,
BENKI ya Dunia imepongeza uendelezaji wa miradi ya maendeleo hapa Zanzibar na kueleza lengo lake la kuunga mkono ili kuhakikisha wajasiriamali wadogo wadogo wanawekewa mazingira mazuri ya kuwawezesha kujiajiri.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. John Murray McIntire wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.
Amesema kuwa Benki ya Dunia imeridhiridhishwa na hatua za uendelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopo Zanzibar kiasi cha kupelekea Benki hiyo kuendelea kuiunga mkono katika shughuli zake hizo ili wananchi wake waweze kujiimarisha na kupambana na umasikini.
Akielezea mafankio yaliyopatikana ni pamoja na ukamilishaji wa ukarabati wa barabara ya kutulia na kurukia ndege katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Zanzibar na kusema kuwa Benki hiyo inaangalia uwezekano wa kugharamia utanuzi zaidi na uendelezaji wa uwanja huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja ya kupandia na kurukia ndege pamoja na barabara za kuegesha ndege.
Sambamba na hilo pia Bw. McIntire amemueleza Dk Shein kuwa Benki ya Dunia itaendelea kuiunga mkono sekta ya elimu kwa ukamilishaji wa shule kumi za Sekondari za kila Wilaya za Zanzibar ambazo ujenzi wake unaendelea kwa Unguja na Pemba.
Bw. McIntire ambaye amefuatana na Bw. Jamal Saghir kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Sekta, Idara ya Maendeleo endelevu Afrika pamoja na Maafisa kutoka Makao Makuu ya Dar-es-Salaam msimamizi wa Mradi wa MACEMP ambao wote kwa pamoja wameeleza haja ya kuendeleza miradi inayosimamiwa na Benki hiyo hapa Zanzibar.
Nae. Dkt. Shein amesema kuwa Benki ya Dunia imekuwa na uhusiano na ushirikiano na Tanzania ikiwemo Zanzibar tokea miaka ya 1960, ambapo hadi hii leo imeweza kutoa mashirikiano mazuri na kuiunga mkono kikamilifu Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo.
Aidha, Dk. Shein amesema kuwa azma ya Benki ya Dunia kuunga mkono sekta ya uvuvi ni hatua nzuri kufikia lengo lililowekwa na serikali la kuimarisha sekta hiyo katika bahari kuu.

Katika mazungumzo hayo pia Dk. Shein, ametoa shukurani zake kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kutokana na pongezi za kufanikisha uchaguzi mkuu uliopita zilizotolewa na uongozi huo kwake na kwa wananci wa Zanzibar.
#gallery-1 { margin: auto; } #gallery-1 .gallery-item { float: left; margin-top: 10px; text-align: center; width: 33%; } #gallery-1 img { border: 2px solid #cfcfcf; } #gallery-1 .gallery-caption { margin-left: 0; } Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia,kwa nchi za Tanzania,Uganda na Burundi, John Murray Mclntire,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,(katikati)Mkurugenzi Jamal Saghir. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia,kwa nchi za Tanzania,Uganda na Burundi, John Murray Mclntire,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia,kwa nchi za Tanzania,Uganda na Burundi, John Murray Mclntire,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana,baada ya mazungumzo yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom