Rais wa UTPC ashindwa kuwashawishi waandishi wa mkoa wa Iringa

Mlyafinono

Senior Member
Apr 6, 2012
177
47
Rais wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania UTPC Keny Simbaya ameshindwa kuwashawishi waandishi wa habari wa mkoa wa iringa kuandika habari za wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani iringa.


Hatua ya waandishi wa habari kugomea kuandika habari za polisi inafuatia tukio la kikatili la kuuawa kwa mwandishi wa chanel ten Daudi Mwangosi lililofanywa na jeshi la polisi septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo wilayani mufindi mkoani Iringa.

Waandishi wamesema kwasasa bado wanaomboleza msiba mkubwa uliomkumba mwandishi mwenzao,na kuwataka wanaoandaa sherehe hizo kuchukua waandishi kutoka dar au mikoa mingine ya jirani.

Daudi Mwangosi aliuawa kikatili kwa kupigwa na bomu mbele ya kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda
 
Bila kujitambua hauwezi kujua nini unachokifanya. Kila mtu atasimamia msimamo anaouona yeye ni thabiti.
 
huyo naye huenda keshakula bahasha ya khaki..haiwezekani watu walitangaza waziwazi kuwa hawatashirikiana na polisi halafu eti anaenda kuwashawishi..it doesn't bring sense!
 
Hivi kweli waandishi wa Iringa wanaamini bila wao kuandika shughuli ya usalama wa barabarani itakwama!
Hata ikikwama, kweli wanaamini polisi ndio wanaoathirika na kukosekana usalama barabarani?!
Hwa waandishi inaonyesha hawajui nini madhumuni ya kazi yao...
 
Back
Top Bottom