Anaona raha Kila siku Kuongelea Umasikini kama ni kitu cha kujivunia.
Mara 1000 ningeona rais anafanya jambo la maana kwa kuitisha mkutano wa kitaifa unaojumuisha watu mbalimbali wa matabaka mbalimbali na kujadili namna ya kuondoa umaskini. Ifike mahali sasa kama taifa tuwaambie viongozi wetu waache kutuabisha na kutafuta majawabu kwa wanyonyaji.
Watanzania ndio wanaokumbana na adha ya umaskini, lakini kwa hakika ni watanzania hawa hawa maskini ndio wenye majawabu juu ya namna ya kutokomeza umaskini. Tatizo tulilo nalo ni kasumba mbaya kwa viongozi wetu kujadili with the wrong people.
Hii campaign ya nutrition imeletwa na Marekani. It is not coming from us, na kwa mtu mwenye akili timamu Marekani wamebuni hii campaign kama njia mojawapo ya kupambana na influence ya China Africa. Wanajua watu wengi bado hawana chakula cha kutosha, na mchina yeye haongei mambo ya chakula, sasa wanacheza na akili za viongozi wetu. Na campaign inaongozwa na shirika lao USAID. kila anapokwenda Kikwete anakumbana na mkurugenzi wa USAID! Inakuwaje? Mbona hao USAID hawawagandi wakenya? Au Tanzania wana shida ya chakula kuliko Kenya?
yaani huyu mzee jamani...yaani anajiona jabali kujisifia nchi masikini wakati ina kila kitu cha kuifanya iwe tajiri....daaaah
Tatizo la viongozi wetu ni waoga sana linapokuja swala la hao weupe. Hata kama huna tatizo mweupe wa ulaya akituambia tuna tatizo huwa tunawakubalia. Hapo ndipo mwanzo wa matatizo kwa vile, ni kama mganga wa kienyeji, chochote akitakacho tunawapa ili mradi atuhakikishie kuwa atatuondolea tatizo letu ambazo sisi wenyewe hatulijui ila yeye.
hongera sana kikwete
wewe ni malalamikaji tu,hebu jiulize wewe umefanya nini kuondoa umaskini wa watanzania zaid ya kubeza wanayofanya wengine.
Kaonge vizuri sana. Congrats Mr. President.
Naona hamuielewi lugha ndio maana hamjui mnachokiongea humu.
Bono hapo anamsifu Kikwete kwa kuonesha mfano bora na anasema huyu si kiongozi wa Tanzania tu bali ni wa Kontinenti zima, ambalo kwa mazuri na mabadiliko aliyoyafanya kwa muda mchache inabidi wengi wajifunze kutoka kwake.
Mtakufa navyo vijiba vya roho!
Nakubaliana na wewe kabisa. Viongozi wetu wanatoa ajenga nje ya nchi. Ni nani hasa ameanza hii ajenda ya Nutrition? Ni Tanzania? Yaani barani Afrika hizo nchi nne ndio zina tatizo la nutrition and food security?
Pamoja na kwamba tunalima kwa kutumia jembe la mkono, Tanzania hakuna shida ya chakula. Tatizo ni distribution. Mikoa ya kusini mahindi yanaozea ndani kwa sababu (a) hakuna soko au/na (b) wakulima wanakatazwa kuuza mazao yao kwa jinsi wanavyotaka. Pili, ni vigumu sana kutoa mazao toka upande mmoja wa nchi kwenda upande mwingine kwa sababu ya miundo mbinu e.g barabara na reli.
Na pengine tujiulize, kama wakulima wanatumia hizi zana za ujima lakini wanavuna na kupata ziada, ingekuwaje kama wangepewa zana za kisasa? Ni lini serikali imeshirikiana kwa karibu na wakulima kwa kuwapa zana bora i.e matreka, mbolea na mbegu bora (sio fake) halafu watu wakashindwa kulima?
Sasa ninapoona rais anakazana kwenye uzalishaji wakati mazao yanozea ndani unashindwa kuelewa nani kampa hiyo ajenda? Hao wakulima wakubwa wakija watasafirisha mazao kwa kutumia migongo yao?
Naona hamuielewi lugha ndio maana hamjui mnachokiongea humu.
Bono hapo anamsifu Kikwete kwa kuonesha mfano bora na anasema huyu si kiongozi wa Tanzania tu bali ni wa Kontinenti zima, ambalo kwa mazuri na mabadiliko aliyoyafanya kwa muda mchache inabidi wengi wajifunze kutoka kwake.
Mtakufa navyo vijiba vya roho!
Naona hamuielewi lugha ndio maana hamjui mnachokiongea humu.
Bono hapo anamsifu Kikwete kwa kuonesha mfano bora na anasema huyu si kiongozi wa Tanzania tu bali ni wa Kontinenti zima, ambalo kwa mazuri na mabadiliko aliyoyafanya kwa muda mchache inabidi wengi wajifunze kutoka kwake.
Mtakufa navyo vijiba vya roho!
Teh tehMhh, nilifikiri ni JPM atakayefanya mahojiano kumbe ni JK