Rais wa mpito aomba utulivu Tunisia

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
TUNIS, Tunusia
RAIS wa serikali ya mpito nchini Tunisia Foued Mebazaa , ameapishwa na amemuomba waziri mkuu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, ikijumuisha wajumbe kutoka vyama vya upinzani.

Kwa mujibu wa taarifa Rais Mebazaa ambaye ni spika wa zamani wa nchi hiyo, alisema hayo baada ya kuapishwa kuchukua wadhifa wa rais wa mpito kufuatia Rais Zine al Abidine Ben Ali kukimbilia nchini Saudi Arabia . Rais Ben Ali alilazimika kuikimbia nchi baada ya ghasia zilizodumu kwa takriban mwezi mzima, zilizosababisha mauaji na uharibifu wa mali za watu na serikali, wakidai ajira na hali bora ya maisha. Baraza la Katiba la Tunisia limesema kuwa uchaguzi mpya utafanyika katika muda wa siku 60, licha ya kuwa viongozi wa upinzani wanasema muda zaidi unahitajika.
Katika hatua nyingine serikali ya Qatar imesema itaheshimu uamuzi wa wananchi wa Tunisia, kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Ben Ali kwa njia ya maandamano ya umma.

Taarifa iliyotolewa juzi na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, ilisema Qatar itaendeleza ushirikiano wake na watu wa Tunisia kwa maslahi ya pande zote mbili, huku ikiahidi kuwa serikali inafuatilia kwa makini mambo yanavyoendelea nchini Tunisia. Kauli kama hii pia ilitolewa leo na Umoja wa nchi za Kiarabu, Arab League, ambayo iliwataka wananchi wa Tunisia kuwa watulivu na wenye umoja, huku taasisi husika za nchi hiyo zikiandaa taratibu za kuumaliza mgogoro uliopo kwa njia za amani. Rais Nicolas Sarkozy juzi aliitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri, kujadili hali ilivyo Tunusia. Juzi nchi hiyo ilimkataa Rais Ben Ali alipokuwa akielekea mjini Paris kwa ajili ya kujihifadhi, Ufaransa ilihofu kuwakera raia wa Tunisia wanaoishi Ufaransa.
 
Back
Top Bottom