Rais wa Maurtania apinduliwa.

Mhhh.. taratibu bandugu hamkawii kuitwa wachochezi mnao tishia amani ya nchi!

Hapa si Amani ya nchi ni amani ya MAFISADI nchi itapata amani ya kweli mpaka pale watu watakakuwa wanalala milango wazi, hawaweki walinzi, hawaweki magrili milangoni, Laptop zikiachwa kwenye gari vioo havivunjwi na kuibiwa, Watu wanatembea usiku bila woga, Watu wanakula wanachokitaka, wanadrive magari wanayoyapenda. Hii ndio Amani ya kweli ambayo haipaswi kutishiwa kama itapatikana.

Je Amani hii itapatikana vipi?, Ni pale tutakapowatoa mafisadi na kuhakikisha nchi yetu inatumia rasilimali zetu kwa manufaa ya wananchi wote badala ya kikundi cha watu wachache, Ili kukuza uchumi wetu, watu wapatiwe ajira zinazolipa vizuri, Hakutakuwa na mtu mwenye mawazo ya kuvizia cha mtu kwani tayari ana ajira yake halali. Tukifika hapa yeyote atakeye sema tutumie jeshi kuwaondoa viongozi itabidi adhibitiwe kwa laana zote za wananchi
 
Naona hawa jamaa wa Mauritania wana ka-uzoefu wa haya mambo ya kondoa serikali kila zinapochemsha.

Haka kamtindo kalisaidia sana nchi za Afrika siku za nyuma hadi viongozi wetu walipogundua ujanja wa kulindana.
 
Ushauri wa bure; anayetaka kuitisha mapinduzi ya kijeshi Tanzania jamani atafute kijiwe kingine; ya kwetu ni mapinduzi ya fikra kwani ukileta mapinduzi ya kijeshi na watu wana fikra zile zile matokeo yake ni kuwa kuna wengine nao watataka kuwapindua wengine na wao kuna mtu atataka kuwapindua!

Watu wameshindwa kusupport mapinduzi ya fikra, mnatumaini watasupport mapinduzi ya kijeshi? labda njozini.

Hao wanajeshi Mauritania wamepindua nchi kwa sababu wamekatiwa ulaji, wamefukuzwa kazi.

Go figure!
 
Sishabikii mapinduzi ya kijeshi; lakini kwa nchi iliyo usingizini kama Tanzania, it is unthinkable eti jeshi limgeuke JK na serikali yake. Tutaendelea kuimba sifa kwa serikali hadi kiama, huku umasikini ukiongezeka.

Wajeshi walishawahi kuingia Magogoni, tena dhidi ya Kidume mwenyewe, acha hawa lightweights wa siku hizi, kwa hiyo sijui kama kweli ni unthinkable.

By the way, hivi Kanali yuko popular kiasi gani Jeshini ?

Maana alianza kulipiza visasi dhidi ya Majenerali ambao hawakujiunga na mtandao kwa kuwa fire Uwaziri, kama vile Brig Gen. Hassan Athumani Ngwilizi. Yeah, ile idea ya Mtandao ilikuwa nzuri unapojaribu kujenga coalition ya kukusaidia kuchaguliwa, lakini baada ya kuwa Rais, huwezi kuendelea kuwa maindi watu ambao walitumia demokrasia yao kukataa kuku support.

(Sishabikii kum depose Kanali ila tunatathmini uwezekano wa haya mambo tu.)
 
jeshi halina madaraka ya kuongoza nchi, ni viongozi wa kiraia na jeshi letu liko chini ya Raia. Kama tuna viongozi wa kiraia ambao tumewachagua na ambao wanavuruga tumaini letu ni sanduku la kura 2010! Jeshi lazima litii mamlaka ya Kiraia na hakuna mahali popote ambapo wanapewa madaraka ya kuchukua madaraka ya kiraia au hata kuangalia halisia. Wanajukumu ambalo liko very clear na nje ya hapo ni kwenda nje ya wajibu wao.

Hata hivyo siko naive kiasi cha kutoelewa ulazima wa Jeshi kuingilia kati utawala wa kiraia. Nina amini kuna mazingira ya nadra sana na ya lazima sana ambapo Jeshi la Wananchi linapotakiwa kuingilia utawala wa kisiasa. Na mazingira hayo kwa sasa Tanzania hayapo.

a. Wakati mtawala wa Kiraia anapohabaribu mchakato na matokeo ya kura na hivyo kulazimisha kuendelea kukaa madarakani. Jeshi linawajibika kuirudisha nchi kwa utawala halali wa kiraia. Mfano, Comoro.

b. Utawala wa kiraia unapoanza kuandika na kutekeleza sheria za kibaguzi ambazo zinawafanya wananchi au baadhi ya wananchi kuwa wakimbizi au kukosa haki za msingi ambazo ni za binadamu (kwa mujibu wa Azimio la UM) au zilizoko katika Katiba. Utawala wa kiraia unapoanza kufanya hivyo na hauko tayari kubadili mwelekeo Jeshi lina haki ya kurudi na kuirudisha Katiba mikononi mwa wananchi.

c. Wakati mtawala/utawala wa kiraia unapoanza kampeni ya mauaji, mateso na unyama dhidi ya Raia kwa kutumia vyombo mbalimbali, basi Jeshi lina wajibu wa kuingilia kati na kumsimamisha mtawala huyo.

Hata hivyo, siamini kuwa jeshi lina haki ya kuingilia utawala wa kiraia ati kwa sababu:

a. Sera za chama tawala ni mbovu au utendaji wa serikali ni mbaya. As long as ubovu/ubaya huo unatokana na usimamizi mbaya wa majukumu, uzembe, n.k basi mchakato wa kawaida wa nidhamu na sheria unatakiwa kufuatwa na kama wananchi wameichoka serikali hiyo wanapewa muda wa kuiondoa madarakani kwa kutumia uamuzi wao wenyewe yaani kura.

b. Wananchi wanapopewa nafasi ya kupiga kura na wao katika uchaguzi huru wanaamua kurudisha serikali ile ile mbovu madarakani, wasitarajie jeshi kuwaokoa.

c. Kama kuna kitu ambacho wananchi hawakipendi dhidi ya viongozi wao au serikali yao ni wajibu wao kuelimishana, kufanya kampeni dhidi ya uongozi/kiongozi huyo na kwa hakika kutafuta chaguo jingine kwa njia za kidemokrasia.

You can call this "Mwanakijiji's Principle".
 
Ni kweli tunahitaji mapinduzi lakini si ya kuanza na wanajeshi. Kwanza si ya wanajeshi kwa sababu wao wanaweza kusababisha kumwagika kwa damu-jambo hilo hatulitaki. Pili, wameshindwa kuyfanya mapinbduzi-hata kwa style wanayoijua wao.
Hivyo, sasa tunahitaji mapinduzi kutoka kwa kundi jingine-wananchi wa kawaida ambao kimsingi ndio mabosi wa viongozi. tatizo moja kwetu ni kuwa tuliowachagua wawe viongozi, wamejigeuza kuwa watawala. Tufanye mapinduzi kwa kuchochea fikra za wapiga kura ili wasichague tena viongozi ambao wana dalili ya kujiegeuza watawala.
Tukifanikiwa kuwachochea wananchi wawe na mwamko na kuwa makini wanapofanya maamuzi yao ya nani awaongoze, tunaweza kuleta mabadiliko. Kinachofaa ni jinsi ya kuwaonyesha wananchi hao kuwa upande wa kanga na bakuli la pombe ni vitu vya kupita kwa muda mfupi tu, lakini mustakabali wa Tanzania ni wa muda mrefu

Ewaaa..tuko pamoja kwa hili.Tunatakiwa kwanza kuwaamsha wananchi kabla ya kufanya mapinduzi yoyote yale. Tunatakiwa kuwafumbua akili na utashi wao kuwa umasikini Tanzania haujaletwa na Mungu bali unaletwa na uongozi mbovu,kulindana,rushwa na ufisadi.Tukishaweza hilo japo kwa asilimia chache then ni rahisi kufanya mapinduzi yoyote yale,yawe ya amani au ya damu.
Ni lazima viongozi wetu waelewe kuwa kamwe hatupendi kusikia nchi yetu inawekwa kwenye orodha ya nchi masikini duniani huku hali tunazo rasilimali na utajiri mwingi.Wakati umefika ndugu zangu kuamka na kusema hapana kwa serikali zetu zisizokuwa na huruma kwa wananchi.
Mapinduzi ni lazima,mapinduzi yanawezekana! ni suala la muda tu.

Wembemkali.
 
jeshi halina madaraka ya kuongoza nchi, ni viongozi wa kiraia na jeshi letu liko chini ya Raia. Kama tuna viongozi wa kiraia ambao tumewachagua na ambao wanavuruga tumaini letu ni sanduku la kura 2010! Jeshi lazima litii mamlaka ya Kiraia na hakuna mahali popote ambapo wanapewa madaraka ya kuchukua madaraka ya kiraia au hata kuangalia halisia. Wanajukumu ambalo liko very clear na nje ya hapo ni kwenda nje ya wajibu wao.

Hata hivyo siko naive kiasi cha kutoelewa ulazima wa Jeshi kuingilia kati utawala wa kiraia. Nina amini kuna mazingira ya nadra sana na ya lazima sana ambapo Jeshi la Wananchi linapotakiwa kuingilia utawala wa kisiasa. Na mazingira hayo kwa sasa Tanzania hayapo.

a. Wakati mtawala wa Kiraia anapohabaribu mchakato na matokeo ya kura na hivyo kulazimisha kuendelea kukaa madarakani. Jeshi linawajibika kuirudisha nchi kwa utawala halali wa kiraia. Mfano, Comoro.

b. Utawala wa kiraia unapoanza kuandika na kutekeleza sheria za kibaguzi ambazo zinawafanya wananchi au baadhi ya wananchi kuwa wakimbizi au kukosa haki za msingi ambazo ni za binadamu (kwa mujibu wa Azimio la UM) au zilizoko katika Katiba. Utawala wa kiraia unapoanza kufanya hivyo na hauko tayari kubadili mwelekeo Jeshi lina haki ya kurudi na kuirudisha Katiba mikononi mwa wananchi.

c. Wakati mtawala/utawala wa kiraia unapoanza kampeni ya mauaji, mateso na unyama dhidi ya Raia kwa kutumia vyombo mbalimbali, basi Jeshi lina wajibu wa kuingilia kati na kumsimamisha mtawala huyo.

Hata hivyo, siamini kuwa jeshi lina haki ya kuingilia utawala wa kiraia ati kwa sababu:

a. Sera za chama tawala ni mbovu au utendaji wa serikali ni mbaya. As long as ubovu/ubaya huo unatokana na usimamizi mbaya wa majukumu, uzembe, n.k basi mchakato wa kawaida wa nidhamu na sheria unatakiwa kufuatwa na kama wananchi wameichoka serikali hiyo wanapewa muda wa kuiondoa madarakani kwa kutumia uamuzi wao wenyewe yaani kura.

b. Wananchi wanapopewa nafasi ya kupiga kura na wao katika uchaguzi huru wanaamua kurudisha serikali ile ile mbovu madarakani, wasitarajie jeshi kuwaokoa.

c. Kama kuna kitu ambacho wananchi hawakipendi dhidi ya viongozi wao au serikali yao ni wajibu wao kuelimishana, kufanya kampeni dhidi ya uongozi/kiongozi huyo na kwa hakika kutafuta chaguo jingine kwa njia za kidemokrasia.

You can call this "Mwanakijiji's Principle".

d. Kama wananchi hawaridhiki, wawatumuie wawakilishi wao bungeni, KUPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA SERIKALI, Rais anang'olewa na uchaguzi mpya unaitishwa
 
You can call this "Mwanakijiji's Principle".

"Mwanakijiji's Principle" imeacha wazi kabisa uhalali wa mapinduzi ya kijeshi katika mazingira fulani fulani. Tena imeyaainisha kwa vipengele.

Sasa, wale ambao wanataka kujadili na kujiuliza kama mazingira yapasayo ya Mwanakijiji's Principle yamefika au hajafika, na pia wale ambao tayari wamesha jishawishi kwamba mazingira hayo yapasayo sasa yamefika, je, na hao "[w]akatafute kijiwe kingine" cha kuyatathmini na kuyasema hayo au wanapoisoma Kanuni hiyo kwenye kijiwe hiki wakubaliane nayo bila majibu na wasubiri aliyeandika Kanuni atangaze kwamba mazingira hayo sasa yamefika ?

Na kama kijiwe hiki sio cha kujadili au kudai kwamba mazingira ya Mwanakijiji's Principle sasa yamefika, je huoni kwamba wakienda "[ku]tafuta kijiwe kingine" kuyatathmini hayo, hudhani unaweza kukuta wameshaharakisha na wameshafika Magogoni wakati mazingira hayajafika, na watu kama nyinyi ambao hamhudhurii kwenye "kijiwe kingine" hamjapata nafasi ya kuwasihi kwamba, kwa sasa, watumie "mapinduzi ya fikra" ?

Ningekuwa mimi nimetangaza Kanuni ya kusihi au kushawishi watu mazingira sawia ya kufanya jambo nisingefukuza ninaotaka waitumie kanuni hiyo hiyo kutoka kwenye kijiwe hicho hicho.

Isipokuwa kama ni Kanuni kwa waliokubali misingi ya Kanuni kabla hata Kanuni haijaandikwa.
 
Mimi hili suala la kijeshi siliungi mkono kwa asilimia 100 lakini pia naliunga mkono si kwa kiwango cha asilimia 100.

Kwa sababu kama milango bado iko wazi kuleta mapinduzi ya kifikra na kukomboa fikra za watanzania basi let us pursue it otherwise kama utawala unaunyima njia ya kuwakilisha fikra mbadala au njia stahiki za ku-impart revolutionary ideas in a peacefully were,then let us pursue millitary action as the last resort because our government doesnt allow us to impart revolutionary ideas in a peacefully way.

Kwa hiyosiwezi kukataa kabisa kwa asilimia mia moja matumizi ya kijeshi ikiwa tunazidi kukandamizwa na wale tuliowapitisha kwa kura na kutuzuia kuelimisha raia wenzetu,eti kwa sababu wao hawataki kutoa hiyo elimu ya uraia ili tusiwapindue kwa kutumia sanduku la kura.
 
Movie kama hii inahitajika Tanzania ,yaani naona kama hawa wajeshi wamewaamsha wenzao,yaani kule ni chuki ya kufukuzwa ukubwa,sasa hapa kuna haja ya kuwashitukizia mafisadi na kuwaweka chini ya ulinzi mpaka wataje ilikuwajekuwaje wakasaini mikataba usiku ,tena nje za ofisi za ubalozi,tena na mikataba mingine wamegaiwa vijisenti ,wangine wana feza kuishinda serikali wamiziweka mabenki ya nje,na wangine wamekwenda Ikulu kufanya biasharaza za utapeli,yaani majeshi wetu wanayo kila sababu ya kufanya zoezi hili.Au mpaka wafukuzwe kazi ndio wataona uchungu wa rohoni.
 
Kupindua serikali haimaanishi nchi itakuwa na maendeleo...sana sana wanaopindua wote wanakuwa na uroho na tamaa ya madaraka tuu...Niambieni dikteta gani aliyepindua aliondoka madarakani kwa hiari....
Be careful of what you wish for!!!

Hii video inanikumbusha wale wanajeshi wa Chad
http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/7545352.stm
 
"Mwanakijiji's Principle" imeacha wazi kabisa uhalali wa mapinduzi ya kijeshi katika mazingira fulani fulani. Tena imeyaainisha kwa vipengele.

Sasa, wale ambao wanataka kujadili na kujiuliza kama mazingira yapasayo ya Mwanakijiji's Principle yamefika au hajafika, na pia wale ambao tayari wamesha jishawishi kwamba mazingira hayo yapasayo sasa yamefika, je, na hao "[w]akatafute kijiwe kingine" cha kuyatathmini na kuyasema hayo au wanapoisoma Kanuni hiyo kwenye kijiwe hiki wakubaliane nayo bila majibu na wasubiri aliyeandika Kanuni atangaze kwamba mazingira hayo sasa yamefika ?

Na kama kijiwe hiki sio cha kujadili au kudai kwamba mazingira ya Mwanakijiji's Principle sasa yamefika, je huoni kwamba wakienda "[ku]tafuta kijiwe kingine" kuyatathmini hayo, hudhani unaweza kukuta wameshaharakisha na wameshafika Magogoni wakati mazingira hayajafika, na watu kama nyinyi ambao hamhudhurii kwenye "kijiwe kingine" hamjapata nafasi ya kuwasihi kwamba, kwa sasa, watumie "mapinduzi ya fikra" ?

Ningekuwa mimi nimetangaza Kanuni ya kusihi au kushawishi watu mazingira sawia ya kufanya jambo nisingefukuza ninaotaka waitumie kanuni hiyo hiyo kutoka kwenye kijiwe hicho hicho.

Isipokuwa kama ni Kanuni kwa waliokubali misingi ya Kanuni kabla hata Kanuni haijaandikwa.

Kuhani Bravo...

Hii hoja yako ndio inatwa "kufikiri nje ya kiboksi."
 
"Mwanakijiji's Principle" imeacha wazi kabisa uhalali wa mapinduzi ya kijeshi katika mazingira fulani fulani. Tena imeyaainisha kwa vipengele.

Sasa, wale ambao wanataka kujadili na kujiuliza kama mazingira yapasayo ya Mwanakijiji's Principle yamefika au hajafika, na pia wale ambao tayari wamesha jishawishi kwamba mazingira hayo yapasayo sasa yamefika, je, na hao "[w]akatafute kijiwe kingine" cha kuyatathmini na kuyasema hayo au wanapoisoma Kanuni hiyo kwenye kijiwe hiki wakubaliane nayo bila majibu na wasubiri aliyeandika Kanuni atangaze kwamba mazingira hayo sasa yamefika ?

good question!

Na kama kijiwe hiki sio cha kujadili au kudai kwamba mazingira ya Mwanakijiji's Principle sasa yamefika,

I never said that! because if I did then by default my own discussion of mazingira here at JF would be breaking that principle.

je huoni kwamba wakienda "[ku]tafuta kijiwe kingine" kuyatathmini hayo, hudhani unaweza kukuta wameshaharakisha na wameshafika Magogoni wakati mazingira hayajafika, na watu kama nyinyi ambao hamhudhurii kwenye "kijiwe kingine" hamjapata nafasi ya kuwasihi kwamba, kwa sasa, watumie "mapinduzi ya fikra" ?

wakianzisha hicho kijiwe... we will cross that bridge

[/quote]
Ningekuwa mimi nimetangaza Kanuni ya kusihi au kushawishi watu mazingira sawia ya kufanya jambo nisingefukuza ninaotaka waitumie kanuni hiyo hiyo kutoka kwenye kijiwe hicho hicho.

Isipokuwa kama ni Kanuni kwa waliokubali misingi ya Kanuni kabla hata Kanuni haijaandikwa.[/QUOTE]

This is what I said:

Ushauri wa bure; anayetaka kuitisha mapinduzi ya kijeshi Tanzania jamani atafute kijiwe kingine; ya kwetu ni mapinduzi ya fikra kwani ukileta mapinduzi ya kijeshi na watu wana fikra zile zile matokeo yake ni kuwa kuna wengine nao watataka kuwapindua wengine na wao kuna mtu atataka kuwapindua!

Watu wameshindwa kusupport mapinduzi ya fikra, mnatumaini watasupport mapinduzi ya kijeshi? labda njozini.

Is this so hard to decipher what I actually said?
 
Back
Top Bottom