Rais wa Maurtania apinduliwa.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,944
703
Rais wa Maurtania Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi amepinduliwa. Kwa mujibu wa habari za kuaminika ni kwamba kikosi maalumu wa kumlinda Rais (Presidental Security Batallion) kilifika nyumbani kwa Rais huyo na kumuweka chini ya ulinzi kisha kuondoka naye. Habari hizo zilithibitishwa na binti wa Rais huyo aitwaye Amal Mint Cheikh Abdallahi.

Mapinduzi haya ya kijeshi yametokea baada ya Rais kumfukuza Mkuu wa Majeshi General Mohamed Ould Cheikh Mohamed Ahmed Ghazouani na Mkuu wa kikosi maalumu cha kumlinda Rais, Mohamed Ould Abdelaziz.

Habari hizo vilevile zimedai kuwa wengine ambao wako chini ya ulinzi ni Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo. Mapinduzi hayo yametokea bila umwagaji damu.

Rais JK ana shughuli nzito akiwa kama Mwenyekiti wa AU. Sasa sijui kama litatumwa jeshi huko kama Comoro au watatumia Demokrasia.
 
Kaazi kweli kweli. This is another test for african leaders, tuone kama watafanya kama walivyofanya Comoro. Wameshindwa kwenda Zimbabwe kwa sababu ulifanyika 'uchaguzi wa kidemokrasia,' tuone na huko sasa
 
Rais wa Maurtania Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi amepinduliwa. Kwa mujibu wa habari za kuaminika ni kwamba kikosi maalumu wa kumlinda Rais (Presidental Security Batallion) kilifika nyumbani kwa Rais huyo na kumuweka chini ya ulinzi kisha kuondoka naye. Habari hizo zilithibitishwa na binti wa Rais huyo aitwaye Amal Mint Cheikh Abdallahi.

Mapinduzi haya ya kijeshi yametokea baada ya Rais kumfukuza Mkuu wa Majeshi General Mohamed Ould Cheikh Mohamed Ahmed Ghazouani na Mkuu wa kikosi maalumu cha kumlinda Rais, Mohamed Ould Abdelaziz.

Habari hizo vilevile zimedai kuwa wengine ambao wako chini ya ulinzi ni Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo. Mapinduzi hayo yametokea bila umwagaji damu.

Rais JK ana shughuli nzito akiwa kama Mwenyekiti wa AU. Sasa sijui kama litatumwa jeshi huko kama Comoro au watatumia Demokrasia.

Sasa jamaa anafukuza mpaka mkuu wa kikosi cha kumlinda anategemea nini......i hope damu haitamwagwa kama AU waki deal na hili suala mapema .
 
Imeandikwa' Siku yaja ambapo wana hawa wataamka. Hivyo tuvute subira tu, hata sisi wafagizi, ipo siku tutaamka na kuwaonyesha hao wanajeshi kile walichopaswa kukifanya
 
Haya mbona hayatokei Tanzania?
Pamoja na kulipwa mishahara midogo, maisha duni na kuteswa kote huku ndugu zenu tukiendela kutesekana na mafisadi kuiba pesa kila kukicha, ila nyie wanajeshi mnakaa kimya tuuuuuu
Fanyeni kama wanavyofanya wengine wenye uchungu na nchi zao, acheni kulinda maslahi ya wachache na kuipeleka nchi yetu kwenye matatizo kila kukicha, lindeni maslahi ya walio wengi na kuifanya Tanzania, Tanzania kweli kutokana na mali zetu tulizonazo.

Ushauri wa bure!!!!!

Hata mie nilikuwa nafikiria hivyo. Jeshi linatakiwa kuhakikisha pesa zote za EPA pamoja na nyinginezo zikiwemo MEREMETA zirudishwe kwa nguvu kama JK hataki kuwashughulikia FISADIZ. Chukuwa FISADIZ wote sweka ndani, wakishasafisha huo uchafu wa FISADIZ kisha warudishe madaraka kwa Rais mchaguliwa. Maana JK hataki kuwashughulikia FISADIZ.
 
Haya mbona hayatokei Tanzania?
Pamoja na kulipwa mishahara midogo, maisha duni na kuteswa kote huku ndugu zenu tukiendela kutesekana na mafisadi kuiba pesa kila kukicha, ila nyie wanajeshi mnakaa kimya tuuuuuu
Fanyeni kama wanavyofanya wengine wenye uchungu na nchi zao, acheni kulinda maslahi ya wachache na kuipeleka nchi yetu kwenye matatizo kila kukicha, lindeni maslahi ya walio wengi na kuifanya Tanzania, Tanzania kweli kutokana na mali zetu tulizonazo.

Ushauri wa bure!!!!!

hata mimi inanitia kichefuchefu. unajua sisi hapa hatuna jeshi. na kila ninapokutana nao hapa bongo, huwa ninadharau akili zao. si waliapa kulinda nchi yao kwa maisha yao yote sasa inakuwaje inchi inaenda kombo. itakuwa aibu siku raia wakawaida, tena wasiokuwa na mafunzo wataingia barabarani kutaka maelezo toka kwa viongozi wao huku wanajeshi wakitazama tu.
 
Duh, hivi bado mapinduzi yapo hadi leo Afrika? Ndo maana Zanzibar wanasema Mapinduzi daima!
 
Haya mbona hayatokei Tanzania?
Pamoja na kulipwa mishahara midogo, maisha duni na kuteswa kote huku ndugu zenu tukiendela kutesekana na mafisadi kuiba pesa kila kukicha, ila nyie wanajeshi mnakaa kimya tuuuuuu
Fanyeni kama wanavyofanya wengine wenye uchungu na nchi zao, acheni kulinda maslahi ya wachache na kuipeleka nchi yetu kwenye matatizo kila kukicha, lindeni maslahi ya walio wengi na kuifanya Tanzania, Tanzania kweli kutokana na mali zetu tulizonazo.

Ushauri wa bure!!!!!

Mhhh.. taratibu bandugu hamkawii kuitwa wachochezi mnao tishia amani ya nchi!
 
Huu sio uchochezi hata kidogo
Habari hiyo inajaribu kutafakari kiapo walichokula ndugu zetu na hali halisi ya sasa hivi nchini kwetu pamoja na wajibu wao wa kufanya kazi

Ni kweli tunahitaji mapinduzi lakini si ya kuanza na wanajeshi. Kwanza si ya wanajeshi kwa sababu wao wanaweza kusababisha kumwagika kwa damu-jambo hilo hatulitaki. Pili, wameshindwa kuyfanya mapinbduzi-hata kwa style wanayoijua wao.
Hivyo, sasa tunahitaji mapinduzi kutoka kwa kundi jingine-wananchi wa kawaida ambao kimsingi ndio mabosi wa viongozi. tatizo moja kwetu ni kuwa tuliowachagua wawe viongozi, wamejigeuza kuwa watawala. Tufanye mapinduzi kwa kuchochea fikra za wapiga kura ili wasichague tena viongozi ambao wana dalili ya kujiegeuza watawala.
Tukifanikiwa kuwachochea wananchi wawe na mwamko na kuwa makini wanapofanya maamuzi yao ya nani awaongoze, tunaweza kuleta mabadiliko. Kinachofaa ni jinsi ya kuwaonyesha wananchi hao kuwa upande wa kanga na bakuli la pombe ni vitu vya kupita kwa muda mfupi tu, lakini mustakabali wa Tanzania ni wa muda mrefu
 
Wanajeshi wa Tanzania fanyeni kweli basi!Tunawasikilizia and you have our support!
 
We uliona wapi Mwanajeshi aliyefuzu na kuiva anavaa shati la kijani kama Combat?

Hii ipo Tanzania, au wewe hujaona?
Hili la wanajeshi inakuwa kama watu wa Jamhuri ya Prof. J(Kumbuka wimbo wake - Ndio Mzee) i.e. jeshi la ndio mzee, hata kama mishahara yao haiwafikishi mwisho wa mwezi au hauleti tija ya maendeleo katika maisha. Wakati huo watu wanaowalinda wanazindi tumbukia katika dimbwi la umasikini kila siku na kuhatarisha maisha yao.
 
Huu sio uchochezi hata kidogo
Habari hiyo inajaribu kutafakari kiapo walichokula ndugu zetu na hali halisi ya sasa hivi nchini kwetu pamoja na wajibu wao wa kufanya kazi

Mzee wa matuzi....MKJJ aliporuhusu tupige simu na kutowa maoni yetu mara baada ya kuwahoji marehemu Wangwe,mama Killango na wabunge wengine...Nillitowa hoja hii ya jeshi...Sikumbuki iliishia wapi lakini MKJJ aliipinga akisema tusubiri uchaguzi wa 2010.
 
Sishabikii mapinduzi ya kijeshi; lakini kwa nchi iliyo usingizini kama Tanzania, it is unthinkable eti jeshi limgeuke JK na serikali yake. Tutaendelea kuimba sifa kwa serikali hadi kiama, huku umasikini ukiongezeka.
 
Haya mbona hayatokei Tanzania?
Pamoja na kulipwa mishahara midogo, maisha duni na kuteswa kote huku ndugu zenu tukiendela kutesekana na mafisadi kuiba pesa kila kukicha, ila nyie wanajeshi mnakaa kimya tuuuuuu
Fanyeni kama wanavyofanya wengine wenye uchungu na nchi zao, acheni kulinda maslahi ya wachache na kuipeleka nchi yetu kwenye matatizo kila kukicha, lindeni maslahi ya walio wengi na kuifanya Tanzania, Tanzania kweli kutokana na mali zetu tulizonazo.

Ushauri wa bure!!!!!

BABAH nakuunga mkono. Hivi hawa wenzetu wenye nyenzo hawaoni watanzania wanavyonyanyaswa na mafisadi? kwa nini wasitukomboe? nataka niwaambie watanzania kwa jinsi Chama cha Mafisadi kilivyoweka mizizi, ni mtutu tu wa bunduku unaoweza kuwang'oa. Naomba kila kukicha atokee kichaa mmoja amwondoe JK pale kwenye Ikulu yetu takatifu ili asiendelee kuinajisi na ufisadi wake.
 
jamani jeshi na polisi hawajwa WETU...Mandela siku ya uhusru wa afrika kusini alipochukua nchi alimwambia askari mzungu...LEO UMEKUWA ASKARI WETU. jamaa alilia sana kwani aligundua watu waliowatesa sana wamechukua utawala.

iko siku nao hawa MABAKA MABAKA WATAKUWA WETUUU...TUSUBIRI...
 
Ushauri wa bure; anayetaka kuitisha mapinduzi ya kijeshi Tanzania jamani atafute kijiwe kingine; ya kwetu ni mapinduzi ya fikra kwani ukileta mapinduzi ya kijeshi na watu wana fikra zile zile matokeo yake ni kuwa kuna wengine nao watataka kuwapindua wengine na wao kuna mtu atataka kuwapindua!

Watu wameshindwa kusupport mapinduzi ya fikra, mnatumaini watasupport mapinduzi ya kijeshi? labda njozini.
 
MKJJ mijadala iko mingi sana hapa jf na sidhani kama ni kweli inamuhamasisha mtu yeyote..Kwani if that was the case basi hata serikali yenyewe ingeshawajibika!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom