Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 8,637
- 7,919
Kwanza kabisa,siyo jambo la kujisifu ikiwa unazalisha umeme kwa kutumia non-renewable sources,kwa sababu naona kama unazifagilia generators zinazotumia mafuta.Ulioleta hii mada unam quote Rais out of context, mbona huongei na laivyosema kuwa kwa awamu zote zilizopita umeme uliwekezwa ni 600MW tu na nyingi zinategemea vyanzo vya maji. Na katika kipindi chake kifupi 145MW tayari (si za kutegemea maji) na mitambo mingine ipo njiani ambayp imeagizwa kuanzia June mwaka jana, mipya kabisa. Na uwekezaji mwingine kwenye makaa ya mawe na njia zingine mbadala, mbona yote hayo huyasemi? Au ulitaka mitambo ikiagizwa leo kesho ifanye kazi? Unanshangaza! Kakosea nini hapo na ndivyo vyanzo vya umeme alivyovikuta na mvua zimegoma kujaza mabwawa, hayo ndio baadhi ya matatizo aliyokuta kawachiwa na awamu zilizopita nae anafanya kila njia kuhakikisha anayatatua na mfano mzuri kuwa mitambo imeagizwa na mikataba imesainiwa na jitihada zinafanywa sio kama hazifanywi ulitaka nini zaidi ya hicho?
Pili ukosefu wa mvua sio sababu ya kukosekana kwa umeme,but let's say ndiyo sababu,mvua hailetwi na mungu bali binadamu.Tumechukua hatua gani kuhakikisha rufiji river basin inapata mvua?
Tatu,uwekezaji wa kwenye makaa ya mawe ni hadithi tulizozisikia muda mrefu,mungu jalia tukipata megawati kadhaa kutoka kiwira(200 and above),nitampa pongezi zake.
Mwisho,ni aibu kwa nchi yenye natural gas,water,sunshine,coal na matakataka mengi barabarani kuagiza mitambo inayotumia disel(nyakato).