rais siyo kupiga maneno

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
"Being president is not about telling stories." Haya ndiyo maneno Mitt Romney kamwambia rais Obama, na hatihati Obama sasa anaelekea kuzamisha jahazi lake. Nani atamfunga paka kengere hapa kwetu kumwambia JK kuwa urais siyo maneno ni kuonyesha kwamba unatimiza malengo uliyoweka na kuwaletea maendeleo wananchi wako?

Rais wetu JK hakuweka malengo yeye aliota kuingia ikulu tu na aliporudi 2010 akaishia kuwapatia ahadi hewa wapiga kura kumrudisha...sasa karudi hana jipya tena zaidi ya kuendelea kupiga soga Msoga huku wananchi wake wakielemewa na maisha.....oooh tuna migodi ya madini....umetoza kodi kiasi gani?.....oooohh tutachimba gas baharini...geologist gani ulimtuma chini ya bahari kutafuta gas?....ooohh kila kitu watanzania mtapata. Japo watanzania walishindwa kumtosa 2010 haya ni machungu kwa chama chake CCM kutoswa 2015...labda watapata akili na kurudia maadili waliyoyakataa.

Wafanyakazi watafanya kazi gani ambayo huwatumi mr president? utaishia kulalamika hawafanyi kazi wanakalia maandamano na kupiga soga maeneo ya kazi.
 
Back
Top Bottom