Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,260
- 33,857
Kuna mambo yanatokea kuuzunguka Urais wa Magufuli, ni lazima kama Raia wenye wajibu wa kikatiba wa kulinda hadhi ya taasisi hiyo kubwa sana na yenye heshima ya hali ya juu katika nchi yetu,tuchukue hatua kuilinda.
Kwa mfano shindano linaloitwa la kumpata mtu maarufu (Siyo kiongozi maarufu) Afrika kumshirikisha Rais wetu, kama watanzania tungepigana kuliondoa jina la Rais wetu kwenye shindano hilo. Hivi inaeleweka kwamba huwezi kushindanishwa na wale usio nao kwenye daraja moja? Yaani hadhi ya Rais wetu kweli inaweza kufanana na ya Mfanyabiashara Dewji?
Yaani tuona ni sawa tu kwa Rais wetu kushindanishwa na watu ambao hata kwenye nchi zao hawafahamiki kiasi cha kulingana sifa na Rais wetu? Badala ya Rais wetu kushindanishwa na marais wenzake wa Afrika anashindanishwa na wafanyabiashra na viongozi wa taasisi zisizo za serikali? Kweli ni jambo la kujivunia hili?
Wasadizi wa Rais ambao wengi ni wateule wa Rasi wanaposema ama kufanya vitendo vya kijinga si wanamdhalilisha Rais mwenyewe? Waziri anaposema kuna viwanda 52,000 bila ya kunyumbulisha viwango vya viwanda hivyo si anamdhalilisha aliyemteua?
Hata kama hatumkubali Magufuli kama binadamu lakini ni lazima tukumbuke kwamba yeye ni Rais wetu na ni lazima taasisi ya Rais anayoiongoza iheshimiwe. Ni lazima Rais aheshimiwe na wale wanaoshusha hadhi ya ofisi anayoingoza wajifunze kujiheshimu.