Rais na takukuru wameshindwa kazi.

tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,511
500
Takukuru haina uwezo wa kufuatilia na kuwafikisha mahakamani mafisadi walioficha mabilioni ya fedha katika benki hizo za Uswisi. Kama asasi hiyo ingekuwa na uwezo huo, pengine ingekuwa tayari imefikia mwisho mwema katika suala lile la kashfa ya ufisadi wa rada ambalo limefikia hata hatua ya kuandikiwa kitabu na mchunguzi mmoja wa kimataifa! ........ Takukuru husikika zaidi pale tu skandali kubwa zinapoibuliwa na wengine na si yenyewe kuwa ya kwanza kuziibua skandali hizo.

Source:– Raia mwema

Ndugu zangu msitegemee rais Kikwete afanye kitu....ameshindwa EPA, ameshindwa kashfa ya RADAR, ameshindwa kila kitu....naona miaka mitatu (3) iliyobaki aondoke madarakani ni kama miaka 20. Hatuna rais ila mbabaishaji, hilo halina ubishi.....hakuna anachofanya.

Source:– Raia mwemaRais

Jakaya Kikwete .....hatujamsikia kwa muda mrefu akifungua kinywa chake kukemea ufisadi huu mkubwa au hata kuchukua hatua zozote kubwa (maamuzi magumu) kupambana na hawa tunaowaita mafisadi papa.Hatukumsikia Kikwete akifungua kinywa chake hata pale ripoti ya benki kuu ya Uswisi ilipoitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi ambayo viongozi wake wameficha mabilioni ya fedha kwenye akaunti za benki za nchi hiyo.Hitimisho: Ndugu zangu, nyumba yetu (Tanzania) ni chafu, na inahitaji kufagiliwa.

Source: Maoni ya Wasomaji – Raia mwema, mtandaoni.
 
Hadi hii leo bado wanaficha list ya corrupt government officials waliokutwa na $200 million kwenye bank accounts zao kule Switzerland.
 
matanzania tuyafananishe na uchafu wa sokoni maana hawana cha kufanya bali malalamiko ukila chakula unashiba una jamaba ndiyo watanzania walivyo huyu raisi ma mtusi kila siku kwa ajili ya nini?? nchi haibadilishwi na raisi bali mwana nchi
 
Takukuru haina uwezo wa kufuatilia na kuwafikisha mahakamani mafisadi walioficha mabilioni ya fedha katika benki hizo za Uswisi. Kama asasi hiyo ingekuwa na uwezo huo, pengine ingekuwa tayari imefikia mwisho mwema katika suala lile la kashfa ya ufisadi wa rada ambalo limefikia hata hatua ya kuandikiwa kitabu na mchunguzi mmoja wa kimataifa! ........ Takukuru husikika zaidi pale tu skandali kubwa zinapoibuliwa na wengine na si yenyewe kuwa ya kwanza kuziibua skandali hizo. Source:– Raia mwemaNdugu zangu msitegemee rais Kikwete afanye kitu....ameshindwa EPA, ameshindwa kashfa ya RADAR, ameshindwa kila kitu....naona miaka mitatu (3) iliyobaki aondoke madarakani ni kama miaka 20. Hatuna rais ila mbabaishaji, hilo halina ubishi.....hakuna anachofanya.Source:– Raia mwemaRais Jakaya Kikwete .....hatujamsikia kwa muda mrefu akifungua kinywa chake kukemea ufisadi huu mkubwa au hata kuchukua hatua zozote kubwa (maamuzi magumu) kupambana na hawa tunaowaita mafisadi papa.Hatukumsikia Kikwete akifungua kinywa chake hata pale ripoti ya benki kuu ya Uswisi ilipoitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi ambayo viongozi wake wameficha mabilioni ya fedha kwenye akaunti za benki za nchi hiyo.Hitimisho: Ndugu zangu, nyumba yetu (Tanzania) ni chafu, na inahitaji kufagiliwa.Source: Maoni ya Wasomaji – Raia mwema, mtandaoni.

ndugu tatizo siyo Takukuru au nani? tatizo ni mfumo mzima wa uongozi, hao viongozi wote waliochaguliwa na mkuu
wa kaya hawana madaraka kamili wanakuwa controlled na mhusika mwenyewe in other words anaodhi hayo madaraka yote kwahiyo wahusika hao ni powerless unless mkuu wa kaya atake mwenyewe. kwahiyo tunachotakiwa kudai ni mabadiliko ya ki mfumo .
 
Eti lowasa apewe urais ili awakamate mafisadi na kuwafilisi!....je, ataweza kuanza na yeye mwenyewe kwanza akiwa fisadi mkuu wa mafisadi?
 
Ingelikuwa mimi ndio Kaka Mkubwa ningekimbia nchi. Yaani kila kona hatari tupu.
 
Aiseeee baba yangu hao mafisadi ndio walio mweka jei kei madarakani,,wananguvu kuliko mahakama,wakitaka kutembea na mama rizi 1 dakika 2 wanampata

ngoja na mimi niuze mbege nikaweke pesa crdb au m pesa
 
Jana nilimsikia na kumuona Mbunge wa Kisesa CCM Luhanga Mpina akisema kwamba atamkabidhi SPIKA wa bunge la JMT report inayoonesha kwamba Tanzania ni nchi ya 13 kwa kuficha pesa nje ya nchi, na Watanzania hao wameficha takribani Tshs. 11 trilioni! Nimetafuta hiyo habari katika magazeti ya leo lakini siioni?

Je magazeti yanaogopa kuandika hiyo habari yasije yakakutwa na kilichomkuta MWANAHALISI?!
 
Back
Top Bottom