Rais Mteule Barack H. Obama!

Mkjj kumfananisha Obama na JK sijui ulifikiria kwa hoja zipi.

JK kama angekua na shahada kama za Obama na akaambiwa akafanye wall street ingekua ni mara moja tu JK angekwenda wall street.

Kinyume na hapo Obama aliacha hizo post nzuri nakwenda kufanya kazi ya kujitolea Chicago.
Niambie ni lini JK aliacha kazi zinazoleta mapesa au kuacha deals za ufisadi akaenda kufanya kazi za kujitolea.
 
Kupanda kwa bei ya mafuta kuna uhusiano na vita vya Iraq. Wingi wa mafuta yalitokuwa yanatumika katika vita vya Iraq kwa siku ulikuwa ni mkubwa ukilinganisha na wingi wa mafuta yaliyokuwa yanatumika ndani ya Marekani kwa siku na hapo ukitilia maanani kwamba US ndiye consumers mkubwa wa mafuta duniani. Hivyo ongezeko hilo kubwa liliongeza demand ya mafuta kuwa kubwa mno na hatimaye kusababisha bei ya mafuta katika soko la dunia kuongezeka kwa haraka sana. Of course Kichaka hakutaka Wamreakni wajue kwamba ongezeko la bei ya mafuta duniani limechangiwa sana na uvamizi wa Iraq.

unajua ni kiasi gani cha mafuta kinatumika China na India kwa siku na ni ongezeko la kiasi gani katika miaka nane iliyopita? Unajua nchi za kiafrika na sehemu nyingine ambazo uchumi wao unakuwa zinachukua mafuta kiasi gani kwa siku? Unaweza kuelezea ni ongezeko gani la mafuta toka Angola, Venezuela, Urusi na Niger na Nigeria limetokea katika miaka hii nane iliyopita? Unataka kusema kuwa hakukuwa na ongezeko la uzalishaji mafuta duniani to offset consumption ya Marekani Iraq?
 
Mkjj kumfananisha Obama na JK sijui ulifikiria kwa hoja zipi.

JK kama angekua na shahada kama za Obama na akaambiwa akafanye wall street ingekua ni mara moja tu JK angekwenda wall street.

Kinyume na hapo Obama aliacha hizo post nzuri nakwenda kufanya kazi ya kujitolea Chicago.
Niambie ni lini JK aliacha kazi zinazoleta mapesa au kuacha deals za ufisadi akaenda kufanya kazi za kujitolea.

sasa ukitafuta kulinganisha watu wawili hadi vitanda vyao na wapi walikula then unachotafuta ni carbon copy ya mtu; haipo.
 
Wabongo siku hizi kweli mnakosa time na kupoteza mda bure,sasa mkishangilia uchaguzi wa obama kwanza mnafanikiwa nini zaidi???Hou mda kwa nini usiende kariakoo ukaangali kitu cha maana cha kufanya???Jamani sasa hivi watu wanacheza na time sio days tena.Kwa hiyo tujaribu kuwa serious kwa kila dunia ya sasa inakwenda vibaya
 
Hivi kumbe Israel hawamuungi mkono messiah!! Ajabu kweli. Umejuaje lakini na wewe?

Acheni utani wa kumlinganisha Obama na Nyerere jamani. Mtu hata kazi hajaanza, mnaanza kumlinganisha na magwiji. Naamini hata yeye hatakuwa tayari kukubali kulinganishwa na Nyerere. Ni aibu. Acheni basi afanye kazi ndio tuanza kufanya hizo comparisons.

Kwa upande wa Afrika nakubaliana na MKJJ kuwa wengi inawezekana wanamuunga mkono kwa sababu ya rangi yake; hakuna ushahidi hata hivyo wa kuthibitisha hili. Lakini sio wote, wengine sisi tumekuwa loyalists wa Democrats kwa miaka mingi. Mbona wakati wa mchakato wengine tulikuwa upande wa Fighter Hillary? I think Obama alishavuka level ya kuungwa mkono kwa sababu ya rangi yake.

BBC walionyesha kwenye Web site yao wakati huo China nao walikuwa hawamuungi mkono lakni bado kibao kikageuka China na sasa ana support kubwa sana. Hata Hillary angekuwa ndiye mgombea wa Democrats bado Watanzania wengi tungemuunga mkono na hali kadhalika sehemu kubwa ya dunia kama siyo dunia yote. Nitatafuta niangalie kama kibao kimegeuka huko Israel kuhusiana support ya Obama. Info zote ziko kwenye mtandao ukizitafuta utazipata hakuna haja ya kwenda kwa Sheikh Yahya ili akufanyie utabiri ni nchi gani duniani inamsupport Obama.

Weusi wengi Marekani pia walikuwa kwa Hillary kwa sababu hakuna aliyetegemea Obama kuwa hapa alipo leo hii. Hata pundits walidai kwamba primaries kwa democrats ni formalities tu kwani hakuna ambaye angeweza kushindana na excellent organisation ya akina Clintons na pia uwezo wao mkubwa wa kuchangisha pesa na pia ukitilia maanani wakti huo opinion polls zilikuwa zinaonyesha Obama akiwa nyuma ya Hillary kwa point 25. Kibao kilipoanza kugeuka African Americans wengi wakaanza kuikimbia kambi ya Hillary na support kubwa aliyokuwa nayo Obama kwa wazungu ikamfikisha hapa alipo leo hii.
 
Ndugu zangu wote kuna kila dalili za huyu mwenzetu kuwa anatimiza ndoto za Martin Luther King Jr kuwa ipo siku Mwafrika ataiongoza America na kutokomeza wimbi la ubaguzi. Hadi sasa kuna kijimbo kinaitwa DIXVILLE NOTCH, New Hampshire: Obama ameshinda kura 15 kati ya 21 na mpinzani wake amepata kura 6 tu. Kijimbo hiki kina historia ya kutopendelea wagombea kupitia Democratic, hivyo kuwasusa tangu mwaka 1968 ambapo waliacha kumpigia mgombea yeyote kupitia tiketi ya Democratic. Lakini kwa kuwa na imani na Chama cha Democratic safari hii wameamua kufanya kweli. Inasemekana kuwa kati ya waliojiandikisha asilimia 100 yote imepiga kura leo na kuleta mabadiliko hayo. Mengi zaidi fuata link hii

Dixville Notch has spoken: It's Obama in a landslide - CNN.com

mazee hebu cheki hizo data zako again. hii prophesy ya kuwa someday a blackman will come to rule united states ilisemwa na robert kennedy sio martin luther.
 
Obama siyo mwafrika ila ni nani?

(a) mmarekani mweusi mwenye asili ya afrika
(b) mzungu
(c) mwafrika wa marakeni

lipi jibu sahihi hapo?

Jibu ni A. he is an afrikan amerikan and not white or half-cast (chotara). marekani mtu akliwa na 1/8 ya black blood basi he is classified as black negroid. and if this was in the 60s he could be classified as a "nigga" or "negro". lastly, therz nothing like "amerikan afrikan" (mwafrika wa marekani)
 
Counting chickens before they hatch, huh? Pullleeeeaaaaasssee!!!!

I am not convinced until the fat lady sings her butt off! Mpaka watangaze matokeo ndio ntaweza kuungana na watu wengi duniani kuamini mtu mweusi raisi wa dunia.....ooopppssss, raisi wa marekani

we waache watu hawakawii kumwaga pilau zao za kusheherekea. has history taught people anything!!!!!!!!!!!
 
Jibu ni A. he is an afrikan amerikan and not white or half-cast (chotara). marekani mtu akliwa na 1/8 ya black blood basi he is classified as black negroid. and if this was in the 60s he could be classified as a "nigga" or "negro". lastly, therz nothing like "amerikan afrikan" (mwafrika wa marekani)

Social classification doesn't deny scientific accuracy. It is scientifically innacurate to call someone who is mixed, black.
 
sasa ukitafuta kulinganisha watu wawili hadi vitanda vyao na wapi walikula then unachotafuta ni carbon copy ya mtu; haipo.
Basi turudi kwenye post yako

Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".

Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!

Halafu unajijua kwamba uko kama kinyonga?

Mwaka 2005 ulikua wewe pia ndio mpiga debe mkubwa wa JK kule DHB. picha za mikutano yake nk

Mkjj bado hatujafa bado tupo hapa hapa tunakuona na kigeugeu chako.
 
Basi turudi kwenye post yako



Halafu unajijua kwamba uko kama kinyonga?

Mwaka 2005 ulikua wewe pia ndio mpiga debe mkubwa wa JK kule DHB. picha za mikutano yake nk

Mkjj bado hatujafa bado tupo hapa hapa tunakuona na kigeugeu chako.

Ouuch....wewe kweli mchokozi......
 
Basi turudi kwenye post yako



Halafu unajijua kwamba uko kama kinyonga?

Mwaka 2005 ulikua wewe pia ndio mpiga debe mkubwa wa JK kule DHB. picha za mikutano yake nk

Mkjj bado hatujafa bado tupo hapa hapa tunakuona na kigeugeu chako.

well.. ad hominem..
 
Obama is an American full stop na hili hakuna la sisi Waafrika kujivuna kwamba ni mwafrika wala nini .Trust me weusi wa US baada ya Uchaguzi na miaka 4 uijayo watakula kisago sana kama ilivyo sasa Tanganyika moto wake baada ya JK .Mimi yangu macho na naweka nguvu zaidi katika siasa za hapa nyumbani .
 
Nitatafuta niangalie kama kibao kimegeuka huko Israel kuhusiana support ya Obama. Info zote ziko kwenye mtandao ukizitafuta utazipata hakuna haja ya kwenda kwa Sheikh Yahya ili akufanyie utabiri ni nchi gani duniani inamsupport Obama.


Israel votes till now 739 Barack Obama 64.7%


John Mc Cain 35.3%
 
unajua ni kiasi gani cha mafuta kinatumika China na India kwa siku na ni ongezeko la kiasi gani katika miaka nane iliyopita? Unajua nchi za kiafrika na sehemu nyingine ambazo uchumi wao unakuwa zinachukua mafuta kiasi gani kwa siku? Unaweza kuelezea ni ongezeko gani la mafuta toka Angola, Venezuela, Urusi na Niger na Nigeria limetokea katika miaka hii nane iliyopita? Unataka kusema kuwa hakukuwa na ongezeko la uzalishaji mafuta duniani to offset consumption ya Marekani Iraq?

Of course nchi za OPEC ziliongeza uzalishaji ili kutake advantage ya bei kubwa ya mafuta. Marekani ndiyo nchi inayotumia mafuta kwa wingi kuliko nchi nyingine duniani. Katika kipindi cha Money Matters cha CNN ambacho kina watangazaji mbali mbali akiwemo Ali Velshi kinachoonyeshwa kila jumamosi 1.00pm ET na kurudiwa 3.00pm ET j'pili. Huyo Ali Velshi alitamka kwamba data za US katika matumizi ya mafuta zilionyesha kwamba kama jeshi la marekani lingetengwa kama nchi basi consumption yake ya mafuta kwa siku ilikuwa ni kubwa kuliko nchi ya Marekani. Sasa huwezi kutegemea ongezeko kubwa la matumizi ya mafuta ya jeshi la Marekani yasiongeze bei ya mafuta katika soko la dunia.
 
Social classification doesn't deny scientific accuracy. It is scientifically innacurate to call someone who is mixed, black.

well u can call it scientifically innaccurate but in ameriKKKa a "ONE DROP RULE" is always applied on classification of people. the rule says that "a person with any trace of African ancestry is considered black unless having an alternative non-white ancestry which he or she can claim, such as Native American, Asian, Arab, or Australian aboriginal". this rule is also applied in several south amerikan countries too. marekani hamna cha chotara wala nini.
 
well u can call it scientifically innaccurate but if yu have heard bout the "ONE DROP RULE" which says that "a person with any trace of African ancestry is considered black unless having an alternative non-white ancestry which he or she can claim, such as Native American, Asian, Arab, or Australian aboriginal". this rule is also applied in several south amerikan countries too. marekani hamna cha chotara wala nini.


meaning Africans' genes are dominant over those from other races?
 
Kuna mamilioni ya watu katika bara letu ambalo wanasubiri kwa hamu ushindi unaotarajiwa wa Obama kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huko Marekani. Kuna tafrija na sherehe zilizoandaliiwa sehemu mbalimbali ambapo watu weusi watasimama kufurahia ushindi wa Obama.

Sitoshangaa wengi wanaosubiri huo ushindi wa Obama wanafanya hivyo si kwa sababu wanakubaliana na sera zake zote (kuongeza kodi, kugawanya utajiri n.k) au misimamo yake ya kijamii (kuunga mkono utoaji mimba au haki za mashoga n.k) bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".

Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".

Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!

hapa najikumbusha maneno ya Mwalimu "Sisi bwana hatutukuzi rangi, tunatukuza mtu bwana"!

Yawezekana ulimwengu ukakosea katika ushabiki wake wa Obama kama Watanzania asilimia 80 ya wapiga kura walivyokosea walipomshabikia Kikwete. Kweli Obama ataweza kutimiza ahadi yake ya "kuibadili Marekani, na kuibadili dunia"?

Yawezekana kiongozi ambaye watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu zilipaswa kumshabikia ni McCain na siyo Obama kama wangeamua tu kuweka rangi pembeni? Well, masaa 24 yajayo will give us a clue.

Nimeshangazwa na tabia hii ya Waafrika wengi .Sijamsikia akiitaja Afika katika kampeni zake kabisa kabisa bali America American sasa watu wanacho komaa nacho ni kitu gani ? JK ndani ya USA wacha mtaona .
 
Hebu tuangalie kidogo hoja zilizotolewa na niweza kuona uzito wake:

a. Watu wanamshabikia Obama kwa sababu ya chuki yao dhidi ya sera za Rais Bush.

Hili linashangaza. Sera za Bush kuhusu nchi gani? Hakuna Rais wa Marekani aliyefanya mengi kwa Tanzania na Afrika kuliko Rais Bush. Kwa kila hali. Siyo Carter wala siyo Clinton ambao wameipa Afrika nafasi ya kufanikiwa kuliko alivyofanya Rais Bush.
Kweli tunaweza kumpongeza Bush kwa mengi aliyoifanyia Tanzania na Afrika.Lakini je mengi hayo hayana ajenda nyingine zaidi ya UPENDO WA BUSH kwa Afrika?Na kama ni upendo,why uwe katika dakika za mwisho za urais wake?Au ndio kuua soo la kuwa unpopular home lakini shujaa nje ya nchi?Hivi si kweli kwamba charity begins at home?Twende mbali kidogo.Hivi Bush angetupenda kweli Watanzania asingemkomalia JK kuhusu ufisadi?Hizo fedha za Milenia zitawanufaisha walengwa au mafisadi?
Tukiwauliza mashabiki wa Obama wa Tanzania kwamba ni kitu gani ambacho Bush amekifanya kwa Tanzania ambacho kinawafanya wamchukie Bush na wampende Obama?
Na tukiwauliza mashabiki haohao wa Tanzania kitu gani MCCAIN amewafanyia ili wampende yeye badala ya Obama watasemaje?By the way,how come kumpenda Obama kutafsiriwe kuwa ni kumchukia Bush?
Ndio maana kati ya majibu mazuri ambayo JK amewahi kutoa ni pale alipoulizwa na media wakati Bush amekuja nyumbani kuwa ni mgombea gani Tanzania ingempendelea ashinde huko Marekani. Yeye alijibu na kusema "yeyote yule kwa kadiri ya kwamba atakuwa kwetu Afrika kama alivyokuwa Rais Bush". Huu ni ukweli.
Hivi kwa upeo wako kuhusu JK ulitegemea jibu gani la busara kutoka kwake?Na hata angekuwa na upeo wa hali ya juu,would you expect him to disappoint Bush kwa kusema Watanzania wangependa Obama ashinde?

Hatujauliza hivi Obama ana sera gani kuhusu Afrika? Mwenye jibu aseme lakini sera ya Bush inajulikana na imeonekana. Sioni dalili yoyote kuwa Obama atakuwa zaidi ya Bush kwa Afrika. So hii chuki ya Bush ni wazi haihusiani na sera za Bush kwa bara letu kwani sera zake zimetupa nafasi ya kufanikiwa, nafasi ya kupiga hatua katika mambo mbalimbali. Leo hii Tanzania inapokewa watalii wengi zaidi kutoka Marekani kuliko wakati mwingine wowote, vijana wetu wengi wamepata nafasi ya kuja Marekani kwa urahisi zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa mahusiano ya Tanzania na Marekani. Leo hii kuna miradi kadhaa ya hali ya juu ambayo imefadhiliwa na USAID.
Je tumejiuliza MCCAIN ana sera gani kuhusu Afrika?Angalau tunaweza kupata excuse ya JINI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA kwa Obama.Mara ya mwisho kwa Mccain kuja Afrika ni lini (kama ameshawahi kuja)? Again,unakosea ku-equate ushabiki kwa Obama na chuki dhidi ya Bush.Sijui hiyo connection inatoka wapi!
Nadhani na mapema mno kudai kwamba "sioni dalili yoyote ya Obama kuwa zaidi ya Bush kwa Afrika" kabla hata Obama hajashinda uchaguzi huo.Did you happen to know kwamba Bush angeipenda Afrika kabla hajaingia Ikulu?
Je kuna uthibitisho wowote kwamba Obama akishinda watalii kutoka Marekani watapungua?Na tunaweza kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza ujio huo wa watalii kutoka Marekani unamnufaishaje mwananchi wa kawaida huko nyumbani.


Nina bahati ya kupata daily press releases kutoka Ubalozi wa Marekani Dar na ninajua kwa hakika ni mambo mangapi yanafanywa na Marekani kuipa Tanzania nafasi. Hii haikuwa hivyo wakati wa Clinton (a Democrat) na nathubutu kusema haitakuwa hivyo chini ya Obama.
Ni kweli misaada kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla inaweza kupungua,na hiyo si kwa Obama pekee bali hata Mccain,au hata Bush angeendelea na urais.Sababu ni matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Marekani.Lakini kinachonitatiza hapa ni huo UHAKIKA kuwa Obama hawezi kumpiku Bush.Any empirical (TESTED) evidence on that?Kwaninu tusisubiri daily press releases a year from now kabla ya kufanya conclusions hizo sasa?
b. Angalia mataifa mengine yanavyomshabikia Obama, haiwezekani kuwa ni kwa sababu ya rangi, uliona umati wa watu kule Ujerumani?

Hii inashangaza. Haitakuwa mara ya kwanza kwa watu weupe kujitokeza kumshangaa mtu mweusi ambaye anaonekana kutofit "the stereotype".
Mbona hatukuyaona hayo kwa Collin Powel au Condoleeza Rice?
Lakini hapa kuna kitu kingine pia. Ni kweli kuna wale ambao wanamshabikia Obama kwa sababu ya mlengo wake wa kushoto wa kiliberali. Obama anaendana na mwelekeo huo wa kiliberali ambao leo hii unaonekana katika misingi ifuatayo:

a. Kupunguza nguvu ya Jeshi la Marekani duniani
b. Kusababisha redistribution of wealth to the so called middle class (a.k.a the workers)
c. Mwelekeo wa kisoshalist mambo leo (neo-socialism) ambapo hawafuati ukomunisti wa kina Max, Juche au Lenin bali wanafuata ile "njia ya kati" kama ilivyo katika nchi za Uskandinavia, Hispania, na Australia. Hii wenyewe wanaiita "social capitalism".
d. Kueneza wazo la "haki" za mtu mmoja mmoja katika masuala ya ndoa za ushoga, utoaji mimba, n.k
e. Kuongeza nguvu za mamlaka ya serikali katika sekta binafsi na hivyo kutaka kutoza kodi kubwa kwa matajiri na kodi ndogo au kutotoza kodi kwa watu wa kipato cha chini na hivyo kuadhibu matajiri na watu waliofanya kazi kujenga maisha yao.
f. Kupunguza clout (ujiko) wa Marekani katika nguvu za uchumi na hivyo kuufanya ulimwengu uwe sawa. Kimsingi kujaribu (kama alivyosema bi. Albright) kupunguza the Super Power status of America. Kwamba kuwa na Super Power mmoja duniani si vizuri.
n.k n.k
Sasa baadhi ya hawa wanaomshabikia Obama ni kwa sababu ya mwelekeo huo.
Ahaa,kumbe inawezekana hata Watanzania wanavutiwa na uliberali wake zaidi kuliko RANGI yake!

c. Obama atabadilisha sera za Bush hususan katika nchi za mapigano za Iraq na Afghanistan na hivyo kufanya America ipendwe.

Mojawapo ya vitu ambavyo yawezekana watu wengi hawajavipata vizuri ni kuwa historia haiwatendei haki watu walio so liberal kama Obama. Bahati nzuri tuna mfano mzuri wa dovish president wa Marekani Bw. Jimmy Carter ambaye chini ya uongozi wake na nia yake ya kuifanya Marekani kuwa "kama nchi nyingine tu" na kushinda kuchukuua maamuzi magumu wakati wa Mgogoro wa Irani (1979) kumefanya watu waone ulinganifu kati yake na Obama.

Lakini itakuwa makosa makubwa kwa watu kudhania kuwa Obama akiwa Rais basi mwangaza mpya wa amani utatokea duniani. Obama atakula kiapo kile kile alichokula Bush na jukumu lake la kwanza na la pekee ni kwa nchi ya Marekani.

Rais Obama hatosita kutumia nguvu zote za Taifa hili kukabiliana na tishio lolote lile. Kama Iran, Syria, North Korea au nchi yeyote inafikiri itaweza kumpiga mkwara Obama na kuwa Obama atakaa chini na maghaidi kuzungumza nchi hiyo itafanya makosa. Obama hatosita kutumia the fully military mighty of the States na sitakuwa wa kwanza kushangaa nikiona na yeye picha yake na mfano wake (effigy) ikichomwa moto na kumuita yeye "Shetani Mkuu"!

Anayefikiri kuwa utawala wa Marekani chini ya Obama linapokuja suala la kimataifa itakuwa ni tofauti sana na ya Bush mtu huyo haelewi sentiments za Wamarekani kuhusu Taifa lao.

Hivyo, kudhania kuwa Obama akiwa Rais vita Iraq na Afghanistan zitakoma na ya kuwa Marekani itasita kutumia majeshi au vikosi vyake sehemu yoyote duniani ni naivette of the first class.
Marekani,kama Taifa lolote lile, ina haki ya kujilinda.Hata hivyo kama kujilinda huko kutamaanisha kuzalisha maadui zaidi kuliko marafiki nadhani wewe na mimi tunajua mwisho wake ni nini.Nadhani sera za Obama kuhusu Irak na Afgahnistan ziko wazi.Bush na neocons wenzie walifanya kosa kubwa sana kukimbilia Irak wakati adui yao mkubwa-Osama-yuko hai kwenye mapango ya Afghanistan.
Matarajio ya wengi ni kwamba priorities za usalama wa Marekani ziendane na hali halisi.Na hapa tunaweza kugusia tena point yako ya UPENDO wa Bush KWA AFRIKA.Kama ambavyo umeeleza,SENTIMENTS za Wamarekani ndio zinazomsukuma Rais kufanya hili au lile,and for that matter inaelekea hata Bush alifanya aliyofanya kutokana na SENTIMENTS hizo.
Back to foreign policy,Obama has made it clear kwamba hatasita kuivamia Pakistan iwapo itathibitika Osama kajificha huko na Pakistan haitoi ushirikiano wa kutosha.Sasa sijui hao wanaodaiwa kudhani kwamba Obama atamaliza vita ya Afghanistan ni akina nani kwani inajulikana kabisa kwanini vita hiyo ilianzishwa in the first place.Na Obama ameeleza bayana intention yake ya kuondoa majeshi ya Marekani huko Irak (na kuongeza nguvu zaidi Afghanistan) kwa vile huko ndiko chanzo za 9/11.

d. Huu ni uchaguzi wa kihistoria na ndio maana watu wengi wanafuatilia.

Hili ni kweli kabisa na binafsi sisemi ni vibaya kwani nami ni shabiki wa historia. Ninaona fahari kuishi wakati huu kuweza kuona tunachokiona. Macho yetu bila ya shaka hayatakaa kuona nafasi kama hii tena (hasa kama Obama atashinda) kwani kutokuangalia rangi kwenye uchaguzi huu ni kutokuwa wa kweli.

Yawekana kabisa kwamba ushabiki wa Watanzania,na kwingineko duniani nako kunatokana na uchaguzi huu kuwa wa kihistoria.Na katika hilo,inawezekana kabisa kwamba wale Wajerumani waliojazana siku ile kumshangilia Obama walikuwa wakishuhudia history in the making and not kushangaa mtu mweusi asiye steriotypical!

Obama angekuwa mtu mweupe wala asingefika hapa alipofikia. Kama angekuwa mtu mweupe mahusiano yake na kina Ayers, Rev. Wright yasingempa hata nafasi. Ile siku ambapo video ya Wright ilipotoka na kuoneshwa kuwa huyo ndiye alikuwa mchungaji wake na ya kuwa alionekana naye kwa hakika siyo tu angejitenga naye angetakiwa kudrop. Lakini kwa vile ni mweusi na yule mchungaji ni mweusi watu waliliweka pembeni maana kulipigia kelele ingeonekana kuwa ni "racist".

Mwanakijiji,hivi Wamarekani lukuki,regardless ya rangi zao,wanaomsapoti Obama ni wapumbavu kiasi hicho cha kumhukumu mtu kwa association yake pekee na sio uwezo wake?Mbona hata mume wa Sarah Palin alikuwa supporter wa successionist party huko Alaska?Kwanini hawakumwambia a-drop?

Na hivi better case ya racism ni kumsapoti mtu mweusi au kumsapoti mtu mweupe?Hizo cases za akina Rev Wright si zingeweza kabisa kutumiwa na racists kama excuse yao dhidi ya Obama,badala ya kumsapoti?

Obama angekuwa mweupe kauli zake kadhaa huko nyuma na kutokuwa na rekodi ya kuonesha utendaji zisingempa nafasi yoyote ile. Hata Sen. Clinton alisema kwa haki kuwa "McCain bring experience, but Obama speech". Ndiyo watu wanachoshangilia kuhusu Obama ni maneno matamu kama ya kiongozi mwingine tunayemjua.
Na kwanini unadhani Democrats walimpuuza Hillary na kumchagua Obama?Weusi wa Obama au Weupe wa Hillary?
Watu wanachofurahia ni jinsi gani anaweza kuungurama kama mkombozi akiahidi kuleta mabadiliko katika maisha ya wanadamu. Ndio anasimama katika maelfu ya watu akiahidi mbingu hapa hapa duniani na ninakumbuka wakati ule wa kampeni hadi watu wanazimia na anaharakisha kama malaika "hebu msaidieni huyo, kuna glasi ya maji karibu".. ?
Unaweza kuwa sahihi kama ambavyo yule anayeamini kuwa Obama ni wakala wa mabadiliko.Sitaki kabisa kuamini kwamba Wamarekani (hasa weupe) ni wapumbavu kiasi hicho cha kudanganywa na mtu mmoja mweusi kwa maneno yake matamu tu ya kuwaahidi mbingu hapa duniani.Na mie nisiyeamini hivyo niko nje ya Marekani.
Ndio tufurahie kuwa kwa Taifa lenye watu wengi weupe, taifa ambalo limewanyanyasa watu weusi, Taifa lililonufaika na utumwa na ambalo lina alama za kitumwa hadi leo hii, kwa taifa hilo hata kumpa nafasi ya kugombea tu ni jambo ambalo lazima litutie moyo.
Kumbe basi inawezekana kabisa furaha na ushabiki wa Watanzania ni sehemu ya furaha na ushabiki wa weusi wengi kuona angalau kumbukumbu za unyama dhidi ya weusi zinaanza kufutika taratibu.
Lakini pia tukumbuke jambo moja, kuna uwezekano mkubwa kuwa kama Obama angekuwa ni mtu mweusi ambaye wazazi wake wote ni weusi waliozaliwa kutoka katika uzao wa watumwa, yawezekana kabisa asingepewa nafasi hiyo kwani kabla yake wapo viongozi wengi weusi wenye uwezo wa lugha (Alan Keyes mmojawapo) na maneno (Revs. Jackson, Sharpton n.k) ambao kwa hakika wanajisikia resentment ya aina fulani kwa kuona kijana huyo ambaye hakulipa gharama ya haki za watu weusi. Lakini wote leo wanakubaliana bila ya shaka (na mimi naungana nao) kuwa Obama amekuja wakati muafaka, na ujumbe muafaka, katika kipindi na wakati kama huu kwa Marekani. Na hicho ndicho naamini kinaweza kumpatia ushindi.
Hivi Obama AMEPEWA NAFASI HIYO au AMESHINDA KWENYE KINYANG'ANYIRO KILICHOJUMUISHA WAGOMBEA WENZIE KADHAA (WEUPE)?

Na hakuna kitu kingine kinachompa ujiko huo kama siku hii ya leo ambapo Bibi yake (mtu mweupe) amefariki dunia on the eve of such an historic moment. Tukumbuke kuwa nao weupe wanamclaim Obama kuwa ni wa kwao, and rightly so, kwa sababu ya rangi yake.
Naamini hii ingekuwa na uzito zaidi laiti kifo cha bibi yake kingetokea siku Obama alipombwaga Hillary kupata nomination ndani ya Democrat party.Na kama multi-ethnicity ya Obama ndio kigezo,then kwanini WEUPE WOTE WASINGE-RALY BEHIND MCCAIN?

Bottom line is,Wamarekani wamechoshwa na failed policies za Republicans zilizoathiriwa zaidi na failed presidency ya Bush.Naamini kwamba laiti Obama angekuwa mgombea mweupe kutoka Democrats basi uchaguzi ungeshamalizika mapema.Dems wana kila sababu ya kufanya vizuri katika uchaguzi huu kwa vile Republicans wame-mess up big time.
 
meaning Africans' genes are dominant over those from other races?

Yap! thatz true indeed. if an afrikan gene gets into any other race most definetely the baby will come out w/ black features i.e. big head, large nose, thick lips, curly hair, volumptuous body n ass (girls) etc.
 
Back
Top Bottom