Rais Mteule Barack H. Obama!

Ningekuwa Marekani nigempigia kura Obama. Bila kujali policies zake. Kisa, ana damu ya Kiafrika (hasa Afrika mashariki). Nukta.

Good for you....

Sitashangaa ulimpigia kura Kikwete kwa kudhani ana sura nzuri pia
 
Obama siyo mwafrika ila ni nani?

(a) mmarekani mweusi mwenye asili ya afrika
(b) mzungu
(c) mwafrika wa marakeni

lipi jibu sahihi hapo?

Obama ni Mmarekani chotara. Baba yake ni Mkenya (mweusi mwafrika) na mama yake ni mmarekani mzungu. Kwa hiyo Obama ni nusu mzungu na nusu mwafrika mweusi
 
Mzee,

Mbona unataka kupandisha watu pressure bure. Maoni yako unatuwekea hapa kama breaking news as if it has been reported to be happening right now. Au ulitaka uwe na thread yako??????

Of course there is such a possibility ambayo watu kama akina Nyani McCain wanaiombea itokee...........!!!!!!!!!!


Mr. Zero, hii ni inevitable thinking hasa ukijua kuwa siyo simba na yanga effect hapa ila ni serious matter ya national interests, nationalism, the great world policy, world economy and the world peace ultimately from US to US citizens and US to the rest of the world citizens and their countries. You and me need to think outside the box as well!!
 
Good for you....

Sitashangaa ulimpigia kura Kikwete kwa kudhani ana sura nzuri pia

Hivi mpaka leo kuna watu wanamuona JK ana sura nzuri.

Sioni uzuri wa Kikwete labda tu aseme ni mweupe kidogo.

Mzuri kwa sura na sera ni Anna Kilango Malecela
 
Kuna mamilioni ya watu katika bara letu ambalo wanasubiri kwa hamu ushindi unaotarajiwa wa Obama kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huko Marekani. Kuna tafrija na sherehe zilizoandaliiwa sehemu mbalimbali ambapo watu weusi watasimama kufurahia ushindi wa Obama.

Sitoshangaa wengi wanaosubiri huo ushindi wa Obama wanafanya hivyo si kwa sababu wanakubaliana na sera zake zote (kuongeza kodi, kugawanya utajiri n.k) au misimamo yake ya kijamii (kuunga mkono utoaji mimba au haki za mashoga n.k) bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".

Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".

Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!

hapa najikumbusha maneno ya Mwalimu "Sisi bwana hatutukuzi rangi, tunatukuza mtu bwana"!

Yawezekana ulimwengu ukakosea katika ushabiki wake wa Obama kama Watanzania asilimia 80 ya wapiga kura walivyokosea walipomshabikia Kikwete. Kweli Obama ataweza kutimiza ahadi yake ya "kuibadili Marekani, na kuibadili dunia"?

Yawezekana kiongozi ambaye watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu zilipaswa kumshabikia ni McCain na siyo Obama kama wangeamua tu kuweka rangi pembeni? Well, masaa 24 yajayo will give us a clue.

Kwanza,kumshabikia Obama kutokana na rangi yake sio dhambi.Wengine watatafsiri kuwa ni ubaguzi wa Kiafrika,wengine wataita brotherly love.Je hiyo Obamania hapo Marekani nayo ni sababu ya rangi pia?Hivi Obama akishinda leo,sababu kuu itakuwa rangi yake au imani waliyonayo wapiga kura wengi kwake?

Historia imeonyesha mara kadhaa kwamba kuwa na rekodi hakumaanishi UFANISI.Mbona Kingunge ana rekodi na uzoefu kwenye siasa na bado UFANISI WAKE NI KARIBU NA ZERO?Mbona Bush alikuwa na uzoefu wa miaka minne,lakini akshindwa kuutumia kipindi cha pili na hivyo kuwafikisha hapo mlipofika?

By the way,hakuna fool-proof method ya kumpata kiongozi ambaye wanaomshabikia wanaamini atakuwa mkombozi lakini akaishia kuwa tofauti na matarajio yake.Kama uzoefu ungekuwa ni kigezo basi ni dhahiri,Mccain asingekuwa hapo alipo muda huu (angeshakuwa defacto president).

Yawezekana TZ tunashangilia RANGI,Kenya wanashangilia asili,Japan wanashangilia kwa ajili ya perfecture ya Obama,Indonesia kwa sababu Obama aliwahi kuishi hapo.Lakini vipi kuhusu OBAMANIA sehemu mbalimbali duniani?Obama alitapisha watu hapo Ujerumani (na hawa wanasifika kwa ubaguzi),alijaza watu hapo London,na anashabikiwa na wengi Ulaya (na sihitaji kusisitiza kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa Ulaya ni weupe).WaTZ wanaweza kuwa wanamshangilia Obama kwa ajili ya rangi yake,na hilo sio kosa,lakini kuhitimisha kuwa hiyo ndio sababu pekee ya Wa-TZ wengi kufanya hivyo ni sawa na kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.Hebu angalia article hii kutoka Gallup ya Oct 28,2008


October 28, 2008

World Citizens Prefer Obama to McCain by More Than 3-to-1
Latest: Most Chinese Have No Opinion in U.S. Election

Editor's update: Gallup Polls just completed in China, Armenia, and Bolivia have now been added to this report, and overall findings have been adjusted to reflect the results. The global survey now represents nearly three-quarters of the world's population, with China's high percentage of "don't know" responses slightly reducing the margin by which world citizens prefer Barack Obama to John McCain.

Gallup Polls conducted in 73 countries from May to October 2008 reveal widespread international support for Democratic Sen. Barack Obama over Republican Sen. John McCain in the U.S. presidential election. Among these nations, representing nearly three-quarters of the world's population, 24% of citizens say they would personally rather see Obama elected president of the United States, compared with just 7% who say the same about McCain. At the same time, 69% of world citizens surveyed did not have an opinion.

World citizens are more divided over whether the outcome of the U.S. election makes a difference to their country, with 26% saying it does and 22% saying it does not. Moreover, 52% of those surveyed did not have an opinion.

Overall, citizens in Europe are the most likely to state a preference for the next president of the United States and to think the election makes a difference to their country. Citizens in Asia are the least likely to state a preference for the next president of the United States and to think the election makes a difference to their country. In individual countries, only Georgia and the Philippines prefer McCain to Obama by a statistically significant margin.

Gallup Polls conducted in 70 countries from May to September 2008 reveal widespread international support for Democratic Sen. Barack Obama over Republican Sen. John McCain in the U.S. presidential election. Among these nations, representing nearly half of the world's population, 30% of citizens say they would personally rather see Obama elected president of the United States, compared with just 8% who say the same about McCain. At the same time, 62% of world citizens surveyed did not have an opinion.

KWA DATA ZAIDI CLICK HAPA
 
Mwanakijiji unachanganya mambo sasa!
Do not undermine the significance of things, e.g the step this nation, US, has made through the years. That's why you hear many women voting for McCain just because of Sarah Palin. Let them! They feel like their time has come.
People vote for numerous reasons, race included, not because it's cool to be of one race or the other; but upholding the history, and recognizing great contributions made by great people in the past. People like Abraham Lincoln, Rosa Parker, Martin Luther King Jr etc who fought for what people are going to celebrate after Obama's victory. However, skin color alone is not enough for such an imporant job. We've witnessed at least a few black people attempting to run for US presidency in the past, but could not get far. What is different this time? Is a black person with leadership qualities.
If you think Obama is not fit for presidency just because he is not a Washington insider, you either are completely ignorant of history or have chosen to ignore its facts. It's as if you're suggesting that only people like Dick Cheney should be elected presidents. People do not qualify to be presidents for longevity in poitics but leadership qualities, of which Obama potray more than the desparate McCain.
Comparing Obama na JK is serious misunderstanding. I'm not going to discuss it here.
 
Ni hatari sana kwa Africa Obama asiposhinda uchaguzi huu, maana mirais ya nchi za kiafrika itahalalisha kuiba na kubadilisha matokeo katika chaguzi zijazo.
 
Ni hatari sana kwa Africa Obama asiposhinda uchaguzi huu, maana mirais ya nchi za kiafrika itahalalisha kuiba na kubadilisha matokeo katika chaguzi zijazo.

Kwani asiposhinda ina maana uchaguzi utakuwa umeibiwa? Wewe vipi bana...mbona una mentality ya kichadema chadema....yaani nyinyi uchaguzi ni wa huru na haki tu pale mnaposhinda? mkishindwa mnalalama mmeibiwa kura.....Obama atashindwa kihalali kabisa. Subiri uone
 
Hebu tuangalie kidogo hoja zilizotolewa na niweza kuona uzito wake:

a. Watu wanamshabikia Obama kwa sababu ya chuki yao dhidi ya sera za Rais Bush.

Hili linashangaza. Sera za Bush kuhusu nchi gani? Hakuna Rais wa Marekani aliyefanya mengi kwa Tanzania na Afrika kuliko Rais Bush. Kwa kila hali. Siyo Carter wala siyo Clinton ambao wameipa Afrika nafasi ya kufanikiwa kuliko alivyofanya Rais Bush.

Tukiwauliza mashabiki wa Obama wa Tanzania kwamba ni kitu gani ambacho Bush amekifanya kwa Tanzania ambacho kinawafanya wamchukie Bush na wampende Obama?

Ndio maana kati ya majibu mazuri ambayo JK amewahi kutoa ni pale alipoulizwa na media wakati Bush amekuja nyumbani kuwa ni mgombea gani Tanzania ingempendelea ashinde huko Marekani. Yeye alijibu na kusema "yeyote yule kwa kadiri ya kwamba atakuwa kwetu Afrika kama alivyokuwa Rais Bush". Huu ni ukweli.

Hatujauliza hivi Obama ana sera gani kuhusu Afrika? Mwenye jibu aseme lakini sera ya Bush inajulikana na imeonekana. Sioni dalili yoyote kuwa Obama atakuwa zaidi ya Bush kwa Afrika. So hii chuki ya Bush ni wazi haihusiani na sera za Bush kwa bara letu kwani sera zake zimetupa nafasi ya kufanikiwa, nafasi ya kupiga hatua katika mambo mbalimbali. Leo hii Tanzania inapokewa watalii wengi zaidi kutoka Marekani kuliko wakati mwingine wowote, vijana wetu wengi wamepata nafasi ya kuja Marekani kwa urahisi zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa mahusiano ya Tanzania na Marekani. Leo hii kuna miradi kadhaa ya hali ya juu ambayo imefadhiliwa na USAID.

Nina bahati ya kupata daily press releases kutoka Ubalozi wa Marekani Dar na ninajua kwa hakika ni mambo mangapi yanafanywa na Marekani kuipa Tanzania nafasi. Hii haikuwa hivyo wakati wa Clinton (a Democrat) na nathubutu kusema haitakuwa hivyo chini ya Obama.

b. Angalia mataifa mengine yanavyomshabikia Obama, haiwezekani kuwa ni kwa sababu ya rangi, uliona umati wa watu kule Ujerumani?

Hii inashangaza. Haitakuwa mara ya kwanza kwa watu weupe kujitokeza kumshangaa mtu mweusi ambaye anaonekana kutofit "the stereotype". Lakini hapa kuna kitu kingine pia. Ni kweli kuna wale ambao wanamshabikia Obama kwa sababu ya mlengo wake wa kushoto wa kiliberali. Obama anaendana na mwelekeo huo wa kiliberali ambao leo hii unaonekana katika misingi ifuatayo:

a. Kupunguza nguvu ya Jeshi la Marekani duniani
b. Kusababisha redistribution of wealth to the so called middle class (a.k.a the workers)
c. Mwelekeo wa kisoshalist mambo leo (neo-socialism) ambapo hawafuati ukomunisti wa kina Max, Juche au Lenin bali wanafuata ile "njia ya kati" kama ilivyo katika nchi za Uskandinavia, Hispania, na Australia. Hii wenyewe wanaiita "social capitalism".
d. Kueneza wazo la "haki" za mtu mmoja mmoja katika masuala ya ndoa za ushoga, utoaji mimba, n.k
e. Kuongeza nguvu za mamlaka ya serikali katika sekta binafsi na hivyo kutaka kutoza kodi kubwa kwa matajiri na kodi ndogo au kutotoza kodi kwa watu wa kipato cha chini na hivyo kuadhibu matajiri na watu waliofanya kazi kujenga maisha yao.
f. Kupunguza clout (ujiko) wa Marekani katika nguvu za uchumi na hivyo kuufanya ulimwengu uwe sawa. Kimsingi kujaribu (kama alivyosema bi. Albright) kupunguza the Super Power status of America. Kwamba kuwa na Super Power mmoja duniani si vizuri.
n.k n.k

Sasa baadhi ya hawa wanaomshabikia Obama ni kwa sababu ya mwelekeo huo.

c. Obama atabadilisha sera za Bush hususan katika nchi za mapigano za Iraq na Afghanistan na hivyo kufanya America ipendwe.

Mojawapo ya vitu ambavyo yawezekana watu wengi hawajavipata vizuri ni kuwa historia haiwatendei haki watu walio so liberal kama Obama. Bahati nzuri tuna mfano mzuri wa dovish president wa Marekani Bw. Jimmy Carter ambaye chini ya uongozi wake na nia yake ya kuifanya Marekani kuwa "kama nchi nyingine tu" na kushinda kuchukuua maamuzi magumu wakati wa Mgogoro wa Irani (1979) kumefanya watu waone ulinganifu kati yake na Obama.

Lakini itakuwa makosa makubwa kwa watu kudhania kuwa Obama akiwa Rais basi mwangaza mpya wa amani utatokea duniani. Obama atakula kiapo kile kile alichokula Bush na jukumu lake la kwanza na la pekee ni kwa nchi ya Marekani.

Rais Obama hatosita kutumia nguvu zote za Taifa hili kukabiliana na tishio lolote lile. Kama Iran, Syria, North Korea au nchi yeyote inafikiri itaweza kumpiga mkwara Obama na kuwa Obama atakaa chini na maghaidi kuzungumza nchi hiyo itafanya makosa. Obama hatosita kutumia the fully military mighty of the States na sitakuwa wa kwanza kushangaa nikiona na yeye picha yake na mfano wake (effigy) ikichomwa moto na kumuita yeye "Shetani Mkuu"!

Anayefikiri kuwa utawala wa Marekani chini ya Obama linapokuja suala la kimataifa itakuwa ni tofauti sana na ya Bush mtu huyo haelewi sentiments za Wamarekani kuhusu Taifa lao.

Hivyo, kudhania kuwa Obama akiwa Rais vita Iraq na Afghanistan zitakoma na ya kuwa Marekani itasita kutumia majeshi au vikosi vyake sehemu yoyote duniani ni naivette of the first class.

d. Huu ni uchaguzi wa kihistoria na ndio maana watu wengi wanafuatilia.

Hili ni kweli kabisa na binafsi sisemi ni vibaya kwani nami ni shabiki wa historia. Ninaona fahari kuishi wakati huu kuweza kuona tunachokiona. Macho yetu bila ya shaka hayatakaa kuona nafasi kama hii tena (hasa kama Obama atashinda) kwani kutokuangalia rangi kwenye uchaguzi huu ni kutokuwa wa kweli.

Obama angekuwa mtu mweupe wala asingefika hapa alipofikia. Kama angekuwa mtu mweupe mahusiano yake na kina Ayers, Rev. Wright yasingempa hata nafasi. Ile siku ambapo video ya Wright ilipotoka na kuoneshwa kuwa huyo ndiye alikuwa mchungaji wake na ya kuwa alionekana naye kwa hakika siyo tu angejitenga naye angetakiwa kudrop. Lakini kwa vile ni mweusi na yule mchungaji ni mweusi watu waliliweka pembeni maana kulipigia kelele ingeonekana kuwa ni "racist".

Obama angekuwa mweupe kauli zake kadhaa huko nyuma na kutokuwa na rekodi ya kuonesha utendaji zisingempa nafasi yoyote ile. Hata Sen. Clinton alisema kwa haki kuwa "McCain bring experience, but Obama speech". Ndiyo watu wanachoshangilia kuhusu Obama ni maneno matamu kama ya kiongozi mwingine tunayemjua.

Watu wanachofurahia ni jinsi gani anaweza kuungurama kama mkombozi akiahidi kuleta mabadiliko katika maisha ya wanadamu. Ndio anasimama katika maelfu ya watu akiahidi mbingu hapa hapa duniani na ninakumbuka wakati ule wa kampeni hadi watu wanazimia na anaharakisha kama malaika "hebu msaidieni huyo, kuna glasi ya maji karibu".. ?

Ndio tufurahie kuwa kwa Taifa lenye watu wengi weupe, taifa ambalo limewanyanyasa watu weusi, Taifa lililonufaika na utumwa na ambalo lina alama za kitumwa hadi leo hii, kwa taifa hilo hata kumpa nafasi ya kugombea tu ni jambo ambalo lazima litutie moyo.

Lakini pia tukumbuke jambo moja, kuna uwezekano mkubwa kuwa kama Obama angekuwa ni mtu mweusi ambaye wazazi wake wote ni weusi waliozaliwa kutoka katika uzao wa watumwa, yawezekana kabisa asingepewa nafasi hiyo kwani kabla yake wapo viongozi wengi weusi wenye uwezo wa lugha (Alan Keyes mmojawapo) na maneno (Revs. Jackson, Sharpton n.k) ambao kwa hakika wanajisikia resentment ya aina fulani kwa kuona kijana huyo ambaye hakulipa gharama ya haki za watu weusi. Lakini wote leo wanakubaliana bila ya shaka (na mimi naungana nao) kuwa Obama amekuja wakati muafaka, na ujumbe muafaka, katika kipindi na wakati kama huu kwa Marekani. Na hicho ndicho naamini kinaweza kumpatia ushindi.

Na hakuna kitu kingine kinachompa ujiko huo kama siku hii ya leo ambapo Bibi yake (mtu mweupe) amefariki dunia on the eve of such an historic moment. Tukumbuke kuwa nao weupe wanamclaim Obama kuwa ni wa kwao, and rightly so, kwa sababu ya rangi yake.
 
Counting chickens before they hatch, huh? Pullleeeeaaaaasssee!!!!

I am not convinced until the fat lady sings her butt off! Mpaka watangaze matokeo ndio ntaweza kuungana na watu wengi duniani kuamini mtu mweusi raisi wa dunia.....ooopppssss, raisi wa marekani
 
Tukiwauliza mashabiki wa Obama wa Tanzania kwamba ni kitu gani ambacho Bush amekifanya kwa Tanzania ambacho kinawafanya wamchukie Bush na wampende Obama?

Bila kutaka kuonekana shabiki wa Obama, kitu kikubwa kinachotuumiza wengi Tanzania na nchi nyingine za Afrika leo ni bei kubwa ya mafuta (Kikwete shahidi yetu namba 1). Tunaamini kuwa moja ya sababu kubwa zilizosababisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani ni vita vilivyoongozwa na marekani dhidi ya kile inachokiita ugaidi. Tunaamini kwamba Bush angeweza kupambana na ugaidi bila kupigana vita kwa aina iliyotokea.
Ndio maana leo hii, katika kile tunachoweza kukitafsiri kuwa jirani yako muombee njaa, watu wamefurahia (hata kisirisiri) kuyumba kwa mfumo wa fedha duniani kwani tumekuwa tukishuhudia bei ya mafuta ikishuka kwa kasi tusiyoitarajia (ingawa bado hajatunufaisha sana huku kwetu).
watu wasingependa kuona mtu ambaye yupo chama kimo ja Bush akiendeleza madhila haya na ndio maana wengi wanashabikia Obama
 
Denial State

denial for what? has the winner been declared? this thing is a toss up and will go down to the wire.....McCain angekuwa keshashinda halafu wewe unakataa matokeo ingekuwa denial. Pre election polls don't decide the election and that's what seems to be the problem with you people...going by the opinion polls.....the real poll is underway right now and no one has won it yet!!!
 
Bila kutaka kuonekana shabiki wa Obama, kitu kikubwa kinachotuumiza wengi Tanzania na nchi nyingine za Afrika leo ni bei kubwa ya mafuta (Kikwete shahidi yetu namba 1). Tunaamini kuwa moja ya sababu kubwa zilizosababisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani ni vita vilivyoongozwa na marekani dhidi ya kile inachokiita ugaidi. Tunaamini kwamba Bush angeweza kupambana na ugaidi bila kupigana vita kwa aina iliyotokea.
Ndio maana leo hii, katika kile tunachoweza kukitafsiri kuwa jirani yako muombee njaa, watu wamefurahia (hata kisirisiri) kuyumba kwa mfumo wa fedha duniani kwani tumekuwa tukishuhudia bei ya mafuta ikishuka kwa kasi tusiyoitarajia (ingawa bado hajatunufaisha sana huku kwetu).
watu wasingependa kuona mtu ambaye yupo chama kimo ja Bush akiendeleza madhila haya na ndio maana wengi wanashabikia Obama

Kupanda kwa bei ya mafuta hakuna uhusiano wa moja kwa moja na vita vya Iraq kwani Iraq kabla ya vita ilikuwa kwenye embargo na mafuta yake yalikuwa monitored. Hata baada ya vita leo Iraq inazalisha mafuta zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Ongezeko la bei ya mafuta limetokana na sababu nyingi sana za kiuchumi ambazo nitawaachia wachumi kuzichambua. Ndio maana leo hii wakati vita bado inaendelea Iraq na Afghanistani bei imeshukua chini kwa kasi ya ajabu.

Sera za Marekani kuhusu mambo ya nchi za nje hazitobadilika sana chini ya Obama kama watu wanavyotarajia. Na usishangae kuwa kama Obama atakuwa Rais utaona anavyoanza kurudi mrengo wa kati na kuanza kusema "kuhusu Iraq tutaangalia hali halisi ardhini na kuwasikiliza majenerali kuhusu hatua za kufanya" na hatopigia tena debe la "kuyaondoa majeshi yetu Iraq kwa kufuata timebtable".. it is all abt politics.
 
Will it be a Bradley effect again?
Nashindwa kabisa ku-anticipate what will happen to US politics should Obama not be elected a next US president earliest today.

1. Kwa professionals pls fikirieni halafu mfikirie what will be the political situation within US and the world at large.
2. What will be the implications for not choosing Obama
3. What should be done to overcome the Bradley effect
4. AOB

There is a possibility of B effeft, but I doubt it because Obama has inspired many Americans from all races.
 
Kupanda kwa bei ya mafuta hakuna uhusiano wa moja kwa moja na vita vya Iraq kwani Iraq kabla ya vita ilikuwa kwenye embargo na mafuta yake yalikuwa monitored. Hata baada ya vita leo Iraq inazalisha mafuta zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Ongezeko la bei ya mafuta limetokana na sababu nyingi sana za kiuchumi ambazo nitawaachia wachumi kuzichambua. Ndio maana leo hii wakati vita bado inaendelea Iraq na Afghanistani bei imeshukua chini kwa kasi ya ajabu.

Sera za Marekani kuhusu mambo ya nchi za nje hazitobadilika sana chini ya Obama kama watu wanavyotarajia. Na usishangae kuwa kama Obama atakuwa Rais utaona anavyoanza kurudi mrengo wa kati na kuanza kusema "kuhusu Iraq tutaangalia hali halisi ardhini na kuwasikiliza majenerali kuhusu hatua za kufanya" na hatopigia tena debe la "kuyaondoa majeshi yetu Iraq kwa kufuata timebtable".. it is all abt politics.

Kupanda kwa bei ya mafuta kuna uhusiano na vita vya Iraq. Wingi wa mafuta yalitokuwa yanatumika katika vita vya Iraq kwa siku ulikuwa ni mkubwa ukilinganisha na wingi wa mafuta yaliyokuwa yanatumika ndani ya Marekani kwa siku na hapo ukitilia maanani kwamba US ndiye consumers mkubwa wa mafuta duniani. Hivyo ongezeko hilo kubwa liliongeza demand ya mafuta kuwa kubwa mno na hatimaye kusababisha bei ya mafuta katika soko la dunia kuongezeka kwa haraka sana. Of course Kichaka hakutaka Wamreakni wajue kwamba ongezeko la bei ya mafuta duniani limechangiwa sana na uvamizi wa Iraq.
 
Oyaaa...taratibu nyie watu.....mshaanza kuongea kama vile kashinda.... Obama bado hajashinda na sidhani kama atashinda uchaguzi huu.

Ha ha ha Today you're Nyani tumbili ngedere McOld and tomorrow you can go back to your new name leanBack :)
10360627.gif

Remember that we still have enough space in our tent, feel free to join us
later today to celebrate Obama's landslide victory. You don't need to feel lonely
 
Back
Top Bottom