Rais Magufuli: Sijazuia shughuli za siasa kwa watu waliochaguliwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Rais Magufuli amesema hajazua shughuli za siasa, atatenda haki kwa watu wote, Nchi kwanza vyama baadae.

Magufuli: 12,500 Idadi ya wafanya kazi hewa, wote tumewaondoa, na kuokoa mabilioni ya fedha za serikali


Rais Magufuli: Mlinichagua bure, nimeamua kuwatumikia bure. Naomba Mungu anisaidie na endeleeni kuniombea

Rais Magufuli: Tumeamua kujenga Serikali kwa misingi ya maadili ya Baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere

Rais Magufuli: Ni lazima tutengeneze Tanzania mpya

Rais Magufuli: Nchi ni mbili, Tanzania na Kenya, ambako baada ya uchaguzi maandamano yanaendelea, inasikitisha.

Rais Magufuli: Sijazuia shughuli za siasa kwa watu waliochaguliwa

Rais Magufuli: Mimi sijaribiwi. Wasije kunijaribu. Siasa nzuri ni wananchi wapate maisha mazuri

Rais Magufuli: Nataka nchi yenye nidhamu

Rais Magufuli: Sitawabagua Watanzania. Maslahi ya nchi kwanza, vyama baadae.

Rais Magufuli: Nawaomba vijana wajue vya bure vimekwisha. Kila moja afanye kazi. Dhamira yetu ni maisha mazuri kwa watanzania


Rais Magufuli : Serikali yote inahamia Dodoma.

Rais Magufuli: Nikihamia Dodoma mimi, majengo yote ya Serikali yaliyoko DAR nitayapiga mnada

Rais Magufuli: Maamuzi ya miaka 50 kuhamia Dodoma lazima. Walizoea kubembelezwa.

Rais Magufuli: Niliwahi kukaa Libya wiki mbili, ilikuwa nchi nzuri, wakachonganishwa na waliotaka mafuta yao.

Rais Magufuli: Iraq, Syria, Somalia wanauana kwa makundi yaliyotengenezwa. Watu wamekuwa wakimbizi.


Rais Magufuli: Mabeberu wanamezea mate raslimali za Tanzania. Naomba msimame imara. Amani hii tuilinde na tutafika kwa ajili yaTanzania mpya

Rais Magufuli: Tumeongeza mapato toka billion 850 hadi 1.2 trilioni kwa mwezi.

index.jpeg

 
Magufuli: Hakuna siasa mpaka 2020 - Mtanzania
4.jpg

*Asema ni wakati wa kazi, atamani kuongoza awamu moja

* Wapinzani, wadauwampinga wadai anataka kuua demokrasia

Elizabeth Hombo na Johanes Respichius, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amepiga marufuku vyama kufanya ushindani wa siasa mpaka baada ya miaka mitano ili wananchi wahoji wanasiasa kama wametekeleza yale waliyoyaahidi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Alitoa kauli hiyo Ikulu Dar es Salaam jana baada ya kukabidhiwa ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva.

“Niwaombe wanasiasa wenzangu wafanye siasa za ushindani kwa nguvu zote baada ya miaka mitano ili wananchi watuhoji tuliyoyaahidi kama tumeyatekeleza au hatujayetekeleza.

“Kila nchi hata zile zilizobobea kwenye demokrasia unapokwisha uchaguzi unakuwa ni wakati wa kazi.
“Haiwezekani mkawa kila siku ni siasa watu watalima saa ngapi? Kila siku ni siasa, ni vema tukatimiza wajibu wetu tuliopewa na wananchi na watatupima kwenye hilo.

“Ni matumaini yangu kuwa Watanzania tunaowaongoza wanataka maendeleo. Iwe kwa bahati nzuri au mbaya Serikali inayoongoza ni ya Chama Cha Mapinduzi.

“Yapo tuliyoyaahidi kuyatekeleza kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitano, nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kutekeleza hayo niliyoahidi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema Rais Magufuli.

Alisema ushindani wa sasa ambao unatakiwa ufanywe kwa nguvu ni kwa wale wawakilishi waliopewa mamlaka na wananchi kupeleka hoja zao kwenye maeneo yao.

“Kama ni madiwani wakapeleke hoja kwa nguvu zote kwenye maeneo yao, kama ni wabunge wakazungumze kwa nguvu sana bungeni lakini hata kuziba midomo nayo ni demokrasia, hiyo ni demokrasia ya mwelekeo wa ya aina yake,”alisema.

Alisema ingawa watu mbalimbali walijitokeza kugombea katika uchaguzi wa mwaka jana, uchaguzi huo haukuwa na mshindi wala mshindwa na kwamba Watanzania wote ni washindi.
“Uchaguzi umekwisha, wakati wa uchaguzi watu mbalimbali walijitokeza kugombea wengine wakaibuka washindi lakini naomba niwaambie kwamba uchaguzi huu haukuwa na mshindi wala mshindwa, sisi Watanzania wote kwa umoja wetu ni washindi,”alisema.

Alisema Serikali yake imeamua kufanya kazi kwa kushirikiana na vyama vyote vya siasa lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi na atalisimamia hilo kwa nguvu zote kwa kuwa ni wajibu wake.

Rais aliahidi kushirikiana na wanasiasa katika changamoto zote zenye kujenga taifa na ushauri na maombi ya vyama hivyo vya siasa atavipokea kwa mikono yake miwili.
 
Hiyo ya kutufanyia kazi bure sio kweli. Analipwa Mshahara na gharama zote analipiwa na kodi za wananchi.
Hiyo ya bure sio kweli.

Hiyo ya kusema hajazuia Shughuli za siasa kwa waliochaguliwa ni kujichanganya kama M wanafunzi wa Primary, kwa sababu tamko lilikuwa dhahiri kabisa kwamba hakuna siasa hadi 2020. Iweje leo yeye afanye siasa waziwazi na kujitetea? Huu ni Udikteta.
 
Kwahiyo mikutano ya hadhara imeruhusiwa kwa vyama vyote? Si amesema hajazuia siasa au ni mimi ndo nimemwelewa vibaya? Watanzania wanataka atoe ufafanuzi kuhusu zuio la mikutano ya hadhara na si kufanya siasa.
 
Back
Top Bottom