Rais Magufuli: Natamani Malaika ashuke na aifungie mitandao ya kijamii

Huo ndio uongozi uvumilie tu kama wenzake. Asitegemee sifa tu kutoka kwa kila mtu. Afanye maendeleo kama amekusudia hivyo akimaliza muda wake atasifiwa na aliowafurahisha. Tupo kwenye karne nyengine asiombe kuturudisha nyuma kwaajili ya kutaka kusifiwa tu. Ubinafsi hauna nafasi kwenye karne hizi.
 
Kumkosoa kiongozi wa nchi pale anapokosea hata siku moja haiwezi kuwa uchochezi. Huyu mungu wa Ikulu hataki kukosolewa pamoja na madudu chungu nzima ambayo ameyafanya kwa muda mfupi kama vile kuwa one man show government, kuwaogopa mafisadi akina Lugumi, Escrow, IPTL, MV ufisadi, kutoiheshimu katiba ya nchi, kuongeza deni la Taifa kwa 55.8% kwa miezi 11 tu ya kuwepo madarakani toka Trillioni 43 hadi kufikia Trillioni 67. Ni lazima akosolewe kwani nchi ikienda mrama Watanzania wote tunaisoma namba bila kujali kama ni wa kutoka ukoo wa panya au la. Yeye mwenyewe ni mpiga dili mzuri sana kwa kukwapua nyumba, kujenga barabara za chini ya viwango kwa gharama kubwa, kulifanganya bunge kuhusu mabilioni chungu nzima yaliyopotea ujenzi na kununua boto bovu kwa bilioni 8 ambalo sasa liko juu ya mawe. Haya yote ndiyo yanamsababisha huyu mtukufu wa Ikulu atake kuwaita mashetani ili wafunge mitandao yote nchini.

Hapana humu mnachonga saaana....badala ya kupongeza mnaponda kinoma....mnaleta uchochezi
 
"Mtu anayekwazwa na meseji za Twitter, Facebook au Whatsapp (social media) hapaswi kupewa mamlaka ya kuongoza nchi"....Bi. Hilary Clinton, Sept. 26, 2016)
 
Kuna vimwandishi uchwara kwenye mitandao ya kijamii kazi yao kutukana maendeleo yanayofanywa na serikali

Sasa kama hivyo 'vimwandishi ni uchwara', why bother? Na kama wanachoandika si kweli au hakina maana, ya nini kukosa usingizi kiasi cha kutamani malaika wawanyamazishe?
 
Mzee hatak social media wakati yy ana account ya tweeter fb

Sidhani kama hataki social media. Asichopenda ni kukosolewa. Kama watu wanaotumia social networks wangekuwa wanafanya kazi ya kumsifia tu (kama anavyojisifia kwa kupitia account zake za Twitter na Facebook), hangekuwa na shida na mitandao ya kijamii. Elewa: akisema anachukia social media, anachomaanisha ni kwamba anachukia kukosoloewa. Na kauli kama 'no research no right to speak' zinathibitisha hilo.
 
maendeleo gani ? Huyu ngosha mshamba sana hutwo tudaladala Twa angani tuwili majigambo kibao, hat mchezaji kama christian Ronaldo anazo, yeye alikimbilia kujenga uwanja chato akasahau hakuna ndege ndo maana ameshindwa kununu madawa Hosp. anakimbilia kununa ndege. chato oyeee!!
Sasa hivi ukiumia kuipata huduma ya tetanus inj kwenye zahanati zetu ni sawa na kukutana na tembo posta na ukibahatika kuifuma hosp binafsi dose moja inaanzia elfu nane mpaka elfu kumi sijui kuna nini aisee
 
IMG_1475220348.603304.jpg

Wahi kabla hajashuka....ban inakuja
 
Sidhani kama hataki social media. Asichopenda ni kukosolewa. Kama watu wanaotumia social networks wangekuwa wanafanya kazi ya kumsifia tu (kama anavyojisifia kwa kupitia account zake za Twitter na Facebook), hangekuwa na shida na mitandao ya kijamii. Elewa: akisema anachukia social media, anachomaanisha ni kwamba anachukia kukosoloewa. Na kauli kama 'no research no right to speak' zinathibitisha hilo.
No research no right to speak.. Wakati watu wanasubir ajira, mishahara haitaki, kupandisha, no Increments sasa kwa haya machache Research ya nn yy apige kaz kama slogan yake invosema aache tumkosoe anapokosea
 
Kiongozi ni lazima awe na kiwango fulani cha kuvumilia mawazo yanayotofautiana na yake kutoka kwa anaowaongoza, vinginevyo ataishia katika kuminya uhuru wao wa kutoa mawazo kwa kiwango cha kuwafanya wasiwe na uwezo wa kufikiri.
 
Hawa Twaweza ni wazushi tu wanawekwa MUJINI na ruzuku toka MACCM ili kufanya tafiti zao za kipumba.vu ambazo hazina mantiki yoyote na haziingii akilini.

Wakija kustuka miaka 5 hakuna kitu tumeishia na Q400 tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sheria ya matimizi ya mtandao ipo wazo Boss, Ulichoandika wewe ni kukumbusha tu.
Ninasema na nitarudia kusema Mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri kuleta Changamoto na ushauri kwa viongozi wetu tutafika mbali.

Mfano mzuri ni kwenye forum hii ya Jamii ambapo tuna vichwa exceptional, Great thinkers ambao michango yao inaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha ngambo

Tatizo letu kubwa ni kushindwa kuvumiliana.Utakuta mtu anatoa hoja nzuri anaishia kutukanwa,hapo ndipo tuliposhindwa kutumia Mitandao
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo letu kubwa ni kushindwa kuvumiliana.Utakuta mtu anatoa hoja nzuri anaishia kutukanwa,hapo ndipo tuliposhindwa kutumia Mitandao

Tetty nafikiri Unaifahamu vizuri sana Jamii forum pamoja na Ktuoa Michango mizuri ya kimaendelea kuna members huku wametumwa kutetea vyama vyao tu. Kuna watu wana ajira za kudumu humu ili kutetea Chama fulani. Hii inaharibu sana lengo halisi la Jamii forum kuwa home of Great thinkers.

All in all Naweza kusema hapa kwangu ni kama shule. I have learnt alot from Jeifu
 
Nakuelewa ni wakati sasa wamiliki watupie macho kwenye hili,JF iwe kama zamani darasa la kujifunza.

Kuna wengine tulianza kuwa members lakini kazi yetu kubwa ilikuwa kusoma tu,mpaka tulivyapata uelewa ndipo tulianza na siye kutumbukiza hoja zetu.

Lakini leo mtu anaingia tu na kutoa matusi badala ya kujibu hoja kwa hoja
 
Back
Top Bottom