Rais Magufuli: Natamani Malaika ashuke na aifungie mitandao ya kijamii

Mlizima bunge live............

Mkazinunua Taasisi Huru.......

Mnazifungia Radio Huru........

Mnategemea wananchi watolee wapi hisia zao?...........
 
piga kazi kwa moyo mmoja kama unadhani ya mwaka mmoja unaweza kufanya kila kitu fanya mengi mazuri ndani ya huo mwaka ututhibitishie wale twenye jakamoyo usikimbizane na upepo maana upepo hauwelewiki unaweza kurudi kule unakotoka
 
Mlizima bunge live............

Mkazinunua Taasisi Huru.......

Mnazifungia Radio Huru........

Mnategemea wananchi watolee wapi hisia zao?...........
nilipoona avatar yako nikajua comrade kumbe...wale wale...wasioitakia nchi mema.
 
Sheria ya matimizi ya mtandao ipo wazo Boss, Ulichoandika wewe ni kukumbusha tu.
Ninasema na nitarudia kusema Mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri kuleta Changamoto na ushauri kwa viongozi wetu tutafika mbali.

Mfano mzuri ni kwenye forum hii ya Jamii ambapo tuna vichwa exceptional, Great thinkers ambao michango yao inaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha ngambo
 
Mhe Rais watanzania wengi tunakuunga mkono kwa kazi zako nzuri unazolifanyia taifa letu fanya kazi baba achana na mitandao ya jamii kwanza mitandao ya jamii ni sehemu ndogo sana na si mawazo ya watanzania wengi.

Wengi wa watanzania kazi zako tunaziunga mkono kwani unapigania watanzania masikini, na kwa kweli tungekuwa na rais kama wewe tokea tupate uhuru ,tanzania tungekuwa tunapaa katika nchi za Afrika.

Tunakutakia maisha marefu na hata Mungu anakuunga mkono Mzee.
 
Hao wa mitandaoni siyo Watanzania? Nadhani neno sahihi lingekuwa "Raisi jifunze kubeza maneno yasiyo ya msingi" Hao masikini anaowatetea ndiyo watumiaji wa kubwa wa mitandao kwa hiyo sioni mantiki ya kutaka kusema raisi usihangaike na mitandao.
 
Kama watu mmeshindwa kumuelewa na kutafsi alikuwa na maana gani basi kazi tunayo

Nakumbuka wale wanaosema Ewe Mwana Kondooo,hembu fuata mambo mungu alioamrisha.
Sasa wasioelewa moja kwa moja wanajiuliza ehhh kondoo vipi tena anapewa amri.

Tujifunze kuelewa na kuchambua
 
Tuwe makini jamani na baadhi ya maneno tunayoyaandika mtandaoni. Hii sheria ya Mtandao itatukamata.
 
Kama Magufuli alimaanisha serikali kununua ndege 2 za abiria ni "kupiga hatua kubwa kimaendeleo" basi ana matatizo ya uelewa wa dhana ya maendeleo. Hii ni sawa kabisa na Kikwete aliposema hajui kwanini Tanzania ni maskini mwaka 2006. Kwani mbona mwishoni mwa miaka ya 70 ATC ilikuwa na ndege 10 na shirika lenyewe halikuendelea bali liliishia kulisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi? Hakuna mantiki yoyote kwa serikali kutumia fedha ya walipa kodi kununua hizo ndege alhali inaweza kuweka mazingira mazuri kwa mashirika kama Precision Plc kupanua huduma zake nchini. Kwa mfumo wa uendeshaji wa ATC, shirika litaendelea milele kuwa mzigo kwa walipa kodi. Mfumo wa uendeshaji ATC ni ule uliowekwa chini ya sera za Ujamaa ambazo hazikuzingatia ufanisi na tija kama misingi ya kanuni za uendeshaji; na faida kama lengo la shirika.
 
Back
Top Bottom