Rais Magufuli mteue Dr. Dalali Kafumu kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara

Kwa hili la Dangote limedhihirisha uwezo mdogo wa waziri wa viwanda na limedhihirisha ni mpiga sound tupu na hana uwezo wa kutuletea Tanzania ya viwanda. Napendekeza JPM mteue Dr Dalali Kafumu kuwa waziri wa viwanda wasukume hili gurudumu wakisaidia na Prof Muhongo.

Mwijage mpeleke wizara ya michezo huko ndio kuna wapiga sound wanaomfaa.
Ni mmewe? au kakuongo uje kumpigia debe
 
Ni mawazo yako sikulaumu ila kuliko kupiga hizi porojo ungejikita kueleza uwezo wa huyo Kafumu ukiambatanisha na sifa alizonazo.

Kwanza kwa nini huyo Kafumu na sio wengine?..tuanzie hapo.
Sahihi kabisa, atupe majibu
 
Hivi ni yupi alisema huyu dangote anataka vitu vya bure?? Sijui ni gas au makaa ya mawe!

Ni nani??
 
Kafumu alizarauliwa na JK itakua JPM.. Huyu juz Kafumu sio ndio alikua na meseji anasambaza kua tulihaidi kumpa gesi bure Dangote aende zake huko.. Ni watu walioingia katika siasa kwa bahati mbaya
 
Kwa hili la Dangote limedhihirisha uwezo mdogo wa waziri wa viwanda na limedhihirisha ni mpiga sound tupu na hana uwezo wa kutuletea Tanzania ya viwanda. Napendekeza JPM mteue Dr Dalali Kafumu kuwa waziri wa viwanda wasukume hili gurudumu wakisaidia na Prof Muhongo.

Mwijage mpeleke wizara ya michezo huko ndio kuna wapiga sound wanaomfaa.
Madalali na wapiga dili mnahangaika sana
Huyo Dalali si ndie alikua anatoa leseni za madini kama hana akili vile
 
Viongozi waandamizi wanapaswa kuweka akiba ya maneno,hoja zao,kauri zao,misimamo yao..Nazidi kumwomba Mungu azidi kuwajalia afya njema,hekima kuu,Upendo wa kifalme na ukali wa haki wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kimsingi.

Viongozi simameni ktk unyenyekevu,ufahamu mkubwa,Usikivu,Ibada,Haki,Kweli,Utakatifu...

Mungu mwenyezi akiwa Upande wa Viongozi wakuu,Ni nani ataweza kuwa kinyume nao na akashinda???
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
Mkuu wa nchi ndo tatizo katika nchi hii, rejea yaliyompata mafuru, kumbwa hataki kukosolewa na wataalam. hivyo hata huyo Kamfumu akipewa kazi chini ya Magufuli sidhani kama ataweza
 
mbona kafumu mwenyewe hatak kabisa kusikia hiyo kitu inaitwa teuz ya Magu kwan kwenye ishu ya madini inamlipa zaid ya huo uwaziri
 
Kafumu alizarauliwa na JK itakua JPM.. Huyu juz Kafumu sio ndio alikua na meseji anasambaza kua tulihaidi kumpa gesi bure Dangote aende zake huko.. Ni watu walioingia katika siasa kwa bahati mbaya
Alihaidi - Aliahidi
Hivi watu kuweka ha badala a ni athari ya lugha zetu za asili au ni tatizo la mtu bila kujali athari ya lugha za makabila yetu?

Mara kadhaa ninashuhudia matatizo ya matumizi ya ha badala ya a, na kuna wakati a badala ya ha, za badala ya dha, r badala ya l au l badala ya r.

Ni makosa ambayo hutegemei kuyaona hata kwa mtu aliyemaliza vizuri elimu ya msingi lakini wengi wanaofanya makosa haya wana elimu ya sekondari. Tatizo ni nini hasa?
 
Kafumu? Chadema tunakumbukumbu nzuri? Kuna spinning zingine unahitaji kurukwa na akili kidogo ....
 
Alihaidi - Aliahidi
Hivi watu kuweka ha badala a ni athari ya lugha zetu za asili au ni tatizo la mtu bila kujali athari ya lugha za makabila yetu?

Mara kadhaa ninashuhudia matatizo ya matumizi ya ha badala ya a, na kuna wakati a badala ya ha, za badala ya dha, r badala ya l au l badala ya r.

Ni makosa ambayo hutegemei kuyaona hata kwa mtu aliyemaliza vizuri elimu ya msingi lakini wengi wanaofanya makosa haya wana elimu ya sekondari. Tatizo ni nini hasa?
Facebook generation
 
huyo dalali hafai hata kidogo, mtu hata jimboni kwake hana nyumba yupoyupo hajielewi.
 
Kwa hili la Dangote limedhihirisha uwezo mdogo wa waziri wa viwanda na limedhihirisha ni mpiga sound tupu na hana uwezo wa kutuletea Tanzania ya viwanda. Napendekeza JPM mteue Dr Dalali Kafumu kuwa waziri wa viwanda wasukume hili gurudumu wakisaidia na Prof Muhongo.

Mwijage mpeleke wizara ya michezo huko ndio kuna wapiga sound wanaomfaa.
Kabla hajapewa wadhifa wowote, hebu atupe ukweli kuhusu lile sakata la kuuziwa mlima wa makaa ya mawe KABULO uliokuwa ni mali ya mradi wa kiwira.

Jee si ndiye aliemlazimisha Mwanasheria wa wizara ya madini kuwahalalishia ile kampuni ya kina Yona kuweza kuwauzia huo mlima wa AUSTRALIA matapeli, na akamshauri Ngeleja alikubali hilo ili wapige deal. Hapo ndipo alipopata mchango wake wa kwenda kugombea ubunge .

Huyu ndugu anamadudu mengi sana
 
Why Dalali?
anajua nini kuhusu viwanda?
kwa nini asipelekwe nishati...?

Dalali alikuwepo wakati Dangote anaongea na Magufuli?

Kuna nukuu ya dalali ililetwa hapa jukwaani kutoka Facebook/Twitter nadhani akimtetea Dangote na kui criticize serikali kwamba in fact ilimuahidi Dangote hizo gas za bure kipindi cha Kikwete na kwamba serikali iache siasa kwa hili la Dangote na uwekezaji kwa ujumla. Kwa nukuu hiyo, kama ilikuwa ya kweli, nadhani Magufuli hawezi kumteua Dalali kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, labda awe hakuisoma hiyo nukuu ya Dalali. Halafu kama umemsikiliza vizuri Dangote akiongea pale Ikulu utagundua alicheza siasa kwa kukana tuhuma ambazo huenda zilikuwa ni za kweli. Inaonekana kama aliamua kucheza na akili ya Magufuli; kupata "favor" ya Magufuli; ambayo inaweza kuwa haitofautiani sana na ile aliyokuwa ameipata hapo awali kutoka kwa Membe/Kikwete.
 
Kwa hili la Dangote limedhihirisha uwezo mdogo wa waziri wa viwanda na limedhihirisha ni mpiga sound tupu na hana uwezo wa kutuletea Tanzania ya viwanda. Napendekeza JPM mteue Dr Dalali Kafumu kuwa waziri wa viwanda wasukume hili gurudumu wakisaidia na Prof Muhongo.

Mwijage mpeleke wizara ya michezo huko ndio kuna wapiga sound wanaomfaa.
Kwa kipi?
 
Back
Top Bottom