Wapiga "dili" wazidi kubanwa. Heko Magufuli na Serikali yako!

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,983
6,237
Ilikuwa ni kawaida kukuta vijana mjini kazi yake kupiga dili za kukwepa kodi na utapeli unaofanana na huo kwa connections kule TRA, TPA, BRELA, TBS, TFDA sasa hivi awamu mpya hakuna dili tena lazima utafute kazi halali.

Na kama ndo na shule hata ya NGUMBARU ilikukosa basi jiandae kulia machozi tu.

Heko Awamu hii kwa kuleta heshima ya kazi na shule pamoja na UBUNIFU
 
Hao ndo wanaolia sasa hivi pesa hakuna. Lakini walio na kazi na mishahara yao halali heshima pale pale. Pole pole tutajifunza kwamba wizi na ujanja ujanja kamwe havijawahi kuendeleza taifa lolote. Kufanya kazi kwa JUHUDI NA MAARIFA na KUBANA MATUMIZI ndivyo vinavyoleta maendeleo ya taifa; go east or west!
 
wapiga dili waende huko CONGO DR sis hapa ni kazi tu. Jitu limeishia darasa la 2 halijui hata kusoma unalikuta linazungukia dili za mamilioni kwa mwamvuli wa UDALALI. Waziri wa Biashara peleka muswada bungeni MADALALI WASAJILIWE na wawe na Elimu angalau SHAHADA ya KWANZA ya CHUO KIKUU kinachotambuliwa na serikali.
 
Kwan imekuaje mkuu si inaendelea ama? Ukitaka kitu.huko lazima uwaone usipoenda nao unazunguka week 3
 
Ilikuwa ni kawaida kukuta vijana mjini kazi yake kupiga dili za kukwepa kodi na utapeli unaofanana na huo kwa connections kule TRA, TPA, BRELA, TBS, TFDA sasa hivi awamu mpya hakuna dili tena lazima utafute kazi halali. Na kama ndo na shule hata ya NGUMBARU ilikukosa basi jiandae kulia machozi tu. Heko Awamu hii kwa kuleta heshima ya kazi na shule pamoja na UBUNIFU
Mm siwezi kuwalaumu hao mnaowaita majizi maana walitengenezwa na serikali zilizotangulia.
Hatuna budi kujua namna ya kuwasaidia ili wasije kujiingiza kwenye magenge ya ujangiri na ujambazi.

Si vyema kushangilia matatizo ya wengine alafu ukajiita mzalendo
 
Nabado
Mbona tutaheshimiana mjini
Labda mnazungumzia wapiga dili wa solo la Tandale na madalali wa nyumba mjini.
Wapiga dili kama Singh wao wanaendelea kutuchapa Mil 400 kila siku sie tunaimba hapa kazi tuu!
Kinachotokea sasa hivi ni mdororo wa uchumi uliosababisha mzunguko wa fedha kukatika kama kule Zimbabwe pale awali.
Hivi Mugabe akisimama na kutamba amedhibiti kupiga dili ndio maana hali iko vile sii ataonwa mpuuzi?
Ndiko tuendako hao mnaowadanganya watakapozinduka na kujielewa.
 
Ilikuwa ni kawaida kukuta vijana mjini kazi yake kupiga dili za kukwepa kodi na utapeli unaofanana na huo kwa connections kule TRA, TPA, BRELA, TBS, TFDA sasa hivi awamu mpya hakuna dili tena lazima utafute kazi halali. Na kama ndo na shule hata ya NGUMBARU ilikukosa basi jiandae kulia machozi tu. Heko Awamu hii kwa kuleta heshima ya kazi na shule pamoja na UBUNIFU
Kama wewe kunguru utakufa na njaa ila dili bado zinapigwa kama kawaida sema mtindo wa dili umebadilika kumbuka mjini hakuna mashamba mjini kinachoitajika ni akili kama wewe uko kwenu simiyu usije mjini kabisa utakufa na njaa uncle anapigwa za macho kama kawa kama dawa
 
Nimeona kipofu akiwaongoza wazima.
 
Kama wewe kunguru utakufa na njaa ila dili bado zinapigwa kama kawaida sema mtindo wa dili umebadilika kumbuka mjini hakuna mashamba mjini kinachoitajika ni akili kama wewe uko kwenu simiyu usije mjini kabisa utakufa na njaa uncle anapigwa za macho kama kawa kama dawa
Kwahiyo wewe kupiga deal ndio unaona ufahari kabisa!!! Hamnazo kweli wewe! Mwanaume wa kweli haishi kwa kupiga deal anaishi kwa deal halali!!
 
Kumzuia m bongo kupiga dili ni km kuusimamisha mkufu kwa supu ya pweza,dili bado zinapigwa sema kimya kimya hamjui tu msijidanganye wapiga dili wana akili nyingi kuliko nyie mnaojiita mmesoma..
 
Labda mnazungumzia wapiga dili wa solo la Tandale na madalali wa nyumba mjini.
Wapiga dili kama Singh wao wanaendelea kutuchapa Mil 400 kila siku sie tunaimba hapa kazi tuu!
Kinachotokea sasa hivi ni mdororo wa uchumi uliosababisha mzunguko wa fedha kukatika kama kule Zimbabwe pale awali.
Hivi Mugabe akisimama na kutamba amedhibiti kupiga dili ndio maana hali iko vile sii ataonwa mpuuzi?
Ndiko tuendako hao mnaowadanganya watakapozinduka na kujielewa.
Hivi Mugabe hakuwekewa vikwazo na wale washika dau huko ughaibuni?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwahiyo wewe kupiga deal ndio unaona ufahari kabisa!!! Hamnazo kweli wewe! Mwanaume wa kweli haishi kwa kupiga deal anaishi kwa deal halali!!
Dili halali.? trump asingekuwepo pale alipo mkuu
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
Inawezekana hata maana ya kupiga dili hamjui.dili si lazima ziwe za magumashi,na hata hizo za magumashi bado zinapigwa kama kawa.
 
Back
Top Bottom