Rais Magufuli aongoza Baraza la Mawaziri Ikulu Jijini Dar es Salaam leo

MIONGONI MWA WALIYOFIKIA KWENYE KIKAO YAPO HAPO CHINI SOMA

SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo (tarehe 29 Septemba, 2016) Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.

Mradi huom kubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2.
 
View attachment 409144
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea mara baada ya kumalizika kwa

View attachment 409146 View attachment 409147 Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016

View attachment 409145
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kabla ya kuanza kwa Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016

View attachment 409146
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongoza
Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016
Hili sio baraza la mawaziri nadhani ni Seminar elekezi maana baraza la mawaziri kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977 wajumbe wake ni mawaziri,Rais wa Zanzibar anaingia kama mjumbe wa baraza la mawaziri,makamu wa Rais na Katibu Mkuu Kiongozi pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaingia kwa Vyeo vyao,haruhusiwi Naibu Waziri wala Gavana kwenye Kikao icho maana ni kikao cha maamuzi ya nchi,Katiba inawabada kuingia kwenye kikao icho.
 
Kuhusu ajira za vijana wanyonge wasioijua kesho yao ktk maisha yao
 
MIONGONI MWA WALIYOFIKIA KWENYE KIKAO YAPO HAPO CHINI SOMA

SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo (tarehe 29 Septemba, 2016) Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.

Mradi huom kubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2.

Sasa kuna vijana wa Ufipa humu yaani hawajielekezi katika substantive issues bali kuangalia nani yupo wamekula nini, na trivialities nyingine.
 
Kuna haja ya kuwa na ukumbi wa mikutano wenye nafasi, kwa mbanano huo inaweza kuwa shida kukimbia in case kunatokea dharura
 
Hili sio baraza la mawaziri nadhani ni Seminar elekezi maana baraza la mawaziri kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977 wajumbe wake ni mawaziri,Rais wa Zanzibar anaingia kama mjumbe wa baraza la mawaziri,makamu wa Rais na Katibu Mkuu Kiongozi pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaingia kwa Vyeo vyao,haruhusiwi Naibu Waziri wala Gavana kwenye Kikao icho maana ni kikao cha maamuzi ya nchi,Katiba inawabada kuingia kwenye kikao icho.
Mkuu, hilo ni Baraza la mawazi. Umesahau kuwa kuna kitu kinaitwa "Changamoto za muungano?"
 
Hadi nawaonea huruma hawa wateuliwa.....wamepooza maskini.....hakuna cha "Fyokofyoko" wala kukenua meno!!!!!
Hahahaa,kweli namba inasomwa...
Eti we January,si ujiuzulu tu...Hahahaaa!
 
Hivi nao wanapata sitting allowance(posho ya makalio) kama wabunge?
 
Jaman kuhusu ajira hawajazungumzia!?
Tukiwaajiri zile mbili za kwenda mbali na hapa kuwabeba washangaaji tutazipata wapi? Vumilieni kama vipi suseni kabisa kuajiriwa ili tupate nyingi tu za kujenga bomba la mafuta. Natania tu, ajira ni mpaka nanihi agraduate ili tuajiri kwa mkupuo. Mpo?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom