Rais Magufuli: Angalia sana suala la Dodoma litakuwa kete ya wapinzani 2020

Umenena sawa!
Wahame kwa phase!
Mfano waziri Mkuu ameshasema anaenda so wizara zilizochini yake ziingie phase 1 ya safari ya Dodoma!
Hawa watamsaidia kupima gharama, lkn pia kwa kuwa wako na boss wao, then issues za coordination na mambo mengine ya kiutawala yatakuwa hayana huitaji wa kusafiri kwani wote watakuwa pamoja!
Bado wizara zifuatane kwa hatua ili tusiwe na confusion! Wakienda wizara Athen, waanze na waziri hadi wakurugenzi, then idara zao kuu zinakuja hadi wizara kàmili inatimia! Tathmini yao itaenda kwa wizara zinazofuata hadi safari itimie
Sio sifa kupeleka wizara hata kama zitafeli! Ila ni heshima kuwa na mchakato makini hata kama utachukua miaka 20 lkn uliofanyika kwa uhakika! Wakijipanga two ministry per year, hadi 2020 atakuwa kahamisha wizara 8, akifanikiwa second term anamalizia zilizobaki! Labda na speed tayari itakuwa juu vya kutosha hata kuruhusu wizara 4 hadi 5 kwa mwaka!
Malawi , Brazil , Nigeria walihamia miji mipya pasipo kujali changamoto Leo hii maisha yanaendelea na baadhi ya wizara na ofisi za balozi zipo miji ya zamani mitandao inafanya kazi , magufuli anajua kuwa CDA na wajanja wengi wamekula Pesa nyingi za kuijenga Dodoma lakini Kwa kuwa uhamiaji ulikuwa wa kusua sua ikawa vigumu kuwadhibiti . Sasa serikali ya Korea , China, ulaya na America wametoa Pesa hata waarabu wa Dubai nap wanakuja kuwekeza Dodoma kutakuwa na maendeleo ya kasi hakuna mfano.
 
Hii ni kama safari ya wana wa Israel kutoka Misri kwenda kaanani. Hakuna kumtanguliZa mtu kama chambo.

Mguu pande mguu sawa nyuma geuka mbele tembea. Kwa maringo mpaka Dom.
Mataifa mengi yameahidi kugharamia ujenzi wa Dodoma .
 
Mh. Rais,
Nakusupport asilimia 100 serikali kuhamia Dom. Lakini nataka nikupe tu angalizo 'kuwa makini na nenda polepole' la sivyo litakuumiza 2020.

Hebu fikiria kwa nini Mwalimu aliamua kuhamishia serikali Dodoma na alishindwa? na mwinyi je, Hata basi Mkapa mfuasi mkubwa wa Mwalimu alishindwa.

Kikwete nae! Suala hili siyo dogo unavyofikiria lazima lina changamoto ambazo huwezi kuziona sasa kwa macho.

Lakin huko mbele litakughalimu. Watu watakusifu sasa lkn hao ndo watakuwa wa kwanza kukulaumu.

Mfano,utatumia sasa fedha nyingi kughalimia uhamisho kiasi kwamba mambo muhimu ya maendeleo ukaweka kando.

Bado, watumishi hawa watafika DOM na kukuta issue nyingi wanatakiwa kuja kufuatilia tena dsm hivyo kila siku wanagongana kuja dsm na perdiems kibao.

Je, ukiona ni mzigo kuendesha serikali toka dodoma utageuza tena kusema urudishe serikali Dsm?

Nashauri, pata ushauri kwanza kwa hawa marais wastaafu kuhusu ugumu wa serikali kuwa Dom ndipo utekeleze la sivyo mapungufu yatakayo jitokeza kwenye hili suala yatakuwa ndo agenda kuu ya upinzani na kushindilia kuwa ulikurupuka.

Tafadhali linganisha hili na issue ya nyumba za serikali inavyokusumbua.
kwanza marais waliopita wengi hasa kuanzia mwinyi,'Mkapa na jk walikuwa busy na madili Yao Pesa iliyopotea Kwa ufisadi kwenye tawala zao Leo hii Dodoma ingekuwa Kama Dubai Kama wangetaka iwe hivyo hawakushindwa kuhamia Bali waliamua kujilimbikizia mbali binafsi, Nigeria na Malawi walikuja Dodoma kujifunza jinsi ya kuhamia miji mipya Leo hii wao tayari wamehamia huko lakini Tanzania bado ipo usingizini ambapo magufuli kazinduka sasa.
 
TCU, NACTE, HESLB pamoja na idara ndogo ndogo za elimu na vyuo vikuu mama viko dar! Hizi taasisi zinafanya kazi karibu zaidi na Wizara ya Elimu. Kwa hiyo ni sahihi kabisa kwa ile budget ya kukarabati ofisi za wizara dar kwa sababu hawataondoka kwa sasa!

Huo ni mtazamo wangu tuuu

Sijasema kukarabati jengo la Dar ni makosa ni vzr ukanisoma vzr. Aina ya ukarabati mkubwa ulioanishwa na gharama zake ni ngumu kwa wizara kutenga pia pesa za ujenzi wa jengo jipya Dodoma kwani wao hata jengo huko hawana. Na kama mpango wa kuhamia Dodoma very soon ungekuwepo awali, im sure wangetenga pesa kwenye budget hii japo za maandalizi ya awali ili kuhamia huko lakini hawakufanya hivyo kuonenesha kuwa huenda huu ni mkurupuko kama ile mikurupuko mingine tulioishuhudia so far.
 
Usishangae rais ajaye nae akaamua kurudi mdo mdo dar
Wala si uwongo. Tena ikiwa upinzani watashindwa kuitumia kete hii 2020, basi 2025 wagombaniaji wa ticket ya ccm atakayeshinda ahadi yake kubwa itakuwa ni kurudisha serikali dsm. Amin usiamin.
 
Malawi , Brazil , Nigeria walihamia miji mipya pasipo kujali changamoto Leo hii maisha yanaendelea na baadhi ya wizara na ofisi za balozi zipo miji ya zamani mitandao inafanya kazi , magufuli anajua kuwa CDA na wajanja wengi wamekula Pesa nyingi za kuijenga Dodoma lakini Kwa kuwa uhamiaji ulikuwa wa kusua sua ikawa vigumu kuwadhibiti . Sasa serikali ya Korea , China, ulaya na America wametoa Pesa hata waarabu wa Dubai nap wanakuja kuwekeza Dodoma kutakuwa na maendeleo ya kasi hakuna mfano.
Naanza kupata mashaka na nchi kuwa na maendeleo kupitia ccm!
Kweli vijana wao ndio vila. za hivi?
Hebu fikiria kama makao makuu ingekuwa inahamia Arusha nani angejadili?
Dodoma si mji unaweza kuhimili influx ya watumishi wa juu karibu 7000-10,000 kwa speed kubwa hivyo! Kuhama sio majengo, ni huduma, kwa watendaji na wafuata huduma! Just imagine bunge lenye watendaji wasiofika 1000 likianza huduma zinasimama kwa kuzidiwa na watu!
Mwanza na Arusha zinaweza kumudu ongezeko hata la watu 100,000 kwa mwezi, au Unguja hata Tanga na Kilimanjaro zisingekuwa na tatizo kwa influx ya watu 10,000 - 20,000 kwa Mara moja!
Dodoma bado! Na busara zisipotumika tutakuja kuona!
Usitaje taje majina ya nchi tu ili utoe mifano bila ya kufanya ulinganifu wa shughuli! Katika kuhama kuna vitu vingi vya kuzingatia kabla ya kufikia uamuzi!
So kabla ya kusema nchi Fulani ilihamisha makao kutoka mji A kwenda B bado mlipaswa kuangalia factors nyingi zaidi ya kuhama mji tu!
 
Wewe upo Dar na inawezekana una biashara zako hapo sasa unawaza utakosa wateja maana hoja yako nyepesi sana
Hivi unafikiri kakurupuka tu hajafanya utafiti na kupata ushauri wa kutosha? tatizo watu wengi hawapendi mabadiliko..kama marais waliotangulia hawakufanikiwa hicho ndio kigezo cha kila Rais ajeye ashindwe kufanya hivyo. Everyone is unique
Hivi suala la Sukari liliishia wapi vile?
 
Tanzania ina matatizo mengi sana angeshughulika na makubwa kwanza sahizi nchi haijatulia kabisa watu wanapanga kuhama,loh,hilo fungu la uhamisho linachotwa wapi labda?watu wanakunywa maji machafu huko vjjn,mweeh! Acha tuone!!
Ngoja tuone kama watajilipa hela ya uwamisho, maana na sheria zipo wazi?
 
e _ government bado mnatumia mtandao wa vodacom, TTCL mmeiua usalama na usiri wa doc zenu utakuwake??
Kama huna data subiri 'ukuta' tarehe moja sio kukurupuka....Rais yupo makini na tunamsuport..what the hellis is dar es salaam
 
wangesubiri bajeti ya mwakani wakatenga mfano hata Bil 500 za kuhamisha wizara kumi na mwaka unaofuata tena Bil 500 wanaondoka na wengine.
Hadi inapofika 2020 wanakuwa wamemaliza bila kuumiza maeneo mengine. Sasa hizi sifa za kina wenzangu za kushindana kutangulia Dodoma ndio nn sasa?
Isome serikali ya mnyanma(Kama nimepatia jina) utaona shida wanayopata mpaka sasa kuhamisha makao makuu ya nchi yao pamoja na miundombinu kuwa tayari.
 
Hakuna hoja hapa sana sana wewe utakuwa mtumishi usiyetaka kwenda Dodoma.

Hivi issue ya katiba mpya imetumia kiasi gani na imeishia wapi? Sababu hili nalo tuliambiwa litaizika CCM 2015.
 
Comments nyingi za vijana wa ccm au wale wanaoipenda serikali ya Magufuli zinatupa ishara kuwa awamu hii haiwezi kubadilika!
Tunachokiita kukurupuka kumbe ndicho kinachopendwa na wafuasi watiifu wa ccm na wapiga kura wa Magufuli!
So tuliowapigia ccm au Magufuli na sasa haturidhishwi na wale ambao hawakumchagua Magu, tusitegemee kuona ndoto zetu zikitimia, na kwa kuwa Demokrasia inapima mizani na kuruhusu waliowengi wasikilizwe kwanza, tuheshimu tu maamuzi ya wengi!
Watanzania waliomchagua waliyataka haya tunayyoyaona leo, so there is no need kulia au kulalamika! Maamuzi ya wengi acha yaheshimiwe!
 
Hakuna hoja hapa sana sana wewe utakuwa mtumishi usiyetaka kwenda Dodoma.

Hivi issue ya katiba mpya imetumia kiasi gani na imeishia wapi? Sababu hili nalo tuliambiwa litaizika CCM 2015.
Hicho ndicho kinachoitwa misuse of resources! Sometimes ni mbaya kuliko hata huo ufisadi!
Serikali haiwezi kujisifia kufanya mambo bila ya kuwa na umakini matokeo yake ni nchi kupata hasara!
Mlifail ktk katiba, so huna hofu kufail kwa uhamiaji wa serikali Dodoma kwa kuwa failure ni second name kwa ccm, right?
 
Kenya mpaka leo wameshindwa kuhamia isiolo walipopendekeza kuwa makao makuu. Tz tutaweza jameni? haya yetu macho..Tuogope historia itakuja kutuhukumu
 
daah hii kweli ni ushu ya ukurupukaji,,,mam,bo ya nchi hayawezi kwenda kwa maamuzi ya mtu mmoja huku utekelezaji ni wa wengi akikosea wote mmekosea...hii haikwepo kwenye ilani yake nakumbuka hivyo, pia kwenye bajeti na mpango wa maendeleo pia halikwepo....hela zinatoka wapi kuweka miundombinu muhimu ya serikali dodoma+gharama za uamisho...sote wapenda maendeleo ila hili halieweki labda tupate uchambuzi toka serikalini juu ya chanzo cha fedha kugharamia hili swala...
 
Serikali iende Dodoma. Ili Dar isimame kama kitovu na jiji la kibiashara. Kama ilivyo Abuja na Lagos au New York na Washington DC. Foleni zipungue kiana. Kwani wizara zote zikihamia huko na idara muhimu walau watumishi wa Umma na wategemezi wao kama laki moja hivi wataondoka. Ingawaje ukweli wa mambo wakubwa wengi kila wikiendi watakuja kula raha jijini Dsm.
Na Ukawa ibaki ktk utawala wa miaka yote ktk jiji la Dsm, CCM watakuwa hawana chao tena Dsm.
 
Mh. Rais,
Nakusupport asilimia 100 serikali kuhamia Dom. Lakini nataka nikupe tu angalizo 'kuwa makini na nenda polepole' la sivyo litakuumiza 2020.

Hebu fikiria kwa nini Mwalimu aliamua kuhamishia serikali Dodoma na alishindwa? na mwinyi je, Hata basi Mkapa mfuasi mkubwa wa Mwalimu alishindwa.

Kikwete nae! Suala hili siyo dogo unavyofikiria lazima lina changamoto ambazo huwezi kuziona sasa kwa macho.

Lakin huko mbele litakughalimu. Watu watakusifu sasa lkn hao ndo watakuwa wa kwanza kukulaumu.

Mfano,utatumia sasa fedha nyingi kughalimia uhamisho kiasi kwamba mambo muhimu ya maendeleo ukaweka kando.

Bado, watumishi hawa watafika DOM na kukuta issue nyingi wanatakiwa kuja kufuatilia tena dsm hivyo kila siku wanagongana kuja dsm na perdiems kibao.

Je, ukiona ni mzigo kuendesha serikali toka dodoma utageuza tena kusema urudishe serikali Dsm?

Nashauri, pata ushauri kwanza kwa hawa marais wastaafu kuhusu ugumu wa serikali kuwa Dom ndipo utekeleze la sivyo mapungufu yatakayo jitokeza kwenye hili suala yatakuwa ndo agenda kuu ya upinzani na kushindilia kuwa ulikurupuka.

Tafadhali linganisha hili na issue ya nyumba za serikali inavyokusumbua.

ana miaka 4 na miezi 4 kutekeleza hayo
 
Back
Top Bottom