Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

JF inafurahisha!

Raisi anasafiri na mapipi kwenye gari, mabaki anagawia watoto ambao anajua kabisa kama kiongozi wa nchi wanahitaji zaidi ya pipi....tunatofautiana sana katika kufikiri. Wanaosupport eti kama mzazi well, mimi namwona Kikwete ni zaidi ya hapo kama head wa state.....anamajukumu mengi....sidhani kama Obama anaweza fanya hilo, ama Sarkozy na other serious leaders!

We are too cheap! Nilitegemea JF watu wanafikiria zaidi ya wale walevi wa kangala na wanzuki usukumani kumbe sivyo!

Ndugu inaonyesha hata hufahamu faida ya kusafiri na vitu hivyo, kama ni mfanya kazi wa ofisini ,utatambua umuhimu wa pipi au kama ni msafiri wa masafa marefu basi hukosi kuelewa faida zake na zaidi ikiwa utakuwa unahitajika kuzungumza na watu ,sikupeleki kwenye habari za madenda maana hapa si pahala pake,
Hivyo ukifikiria utaona umuhimu wa Raisi na si yeye tu hata wale wapambe wake hawakosi kuwa nazo kwenye makoti.

Na kuanguka kwa baadhi ya pipi hakumfanyi kuwa Raisi alimtupia au alimrushia ,inaonekana kuwa Raisi yumo ndani ya gari na ipo juu ukilinganisha na kimo cha mtoto pia ufahamu kuwa hapo yupo kwenye seat belt hivyo amejipinda kwa kiasi fulani probability ya kuanguka kwa pipi itakuwepo kwa hesabu zozote zile utakazozipanga.
Sidhani kama alimgaia mabaki nionavyo alimtolea kiasi tu cha kumfurahisha mtoto ,Obama anawagaia watoto matoys tu au wakibahatika huwaonyesha meno na wengine huwatolea mikono tu bila ya kuwapa kitu.
 
Are you serious kwamba viongozi uwatajao (serious leader by your definition) hawawezi kuwapa watoto pipi wakiwa kwenye ziara ya kuwatembelea wananchi? Naamini kweli tunatofautiana sana katika kufikiri!!! si mchezo.. ila tu kunakitu kinaitwa public relation.. maybe we have to think that way before we say G8 leaders can't do that

Yaani wewe acha tu hizi logic zingine hizi...
 
Breach of executive security and safety protocol.

...mkuki kwa nguruwe (?)

Black_Kid_on_Bike_Surrounded_by_Aus.jpg
 
Pointi bado ni ile ile. Ubaya uko wapi hapo ku take time na kujumika na wananchi? Iwe familia yako au wananchi wengine? Kwani alivyomgawia dogo hizo pipi ilichukua muda gani, siku nzima? Na nini kilichoenda mrama kwa sababu ya yeye kumgawia dogo pipi?

Halafy "baracade" ndio nini?

I meant Presidential motorcade
Huoni kuna kasoro alichofanya?
 
Sio wajibu wa rais kuwawezesha watu. Kujitafutia kipato ni chaguo lako (period). Rais anachoweza kufanya ni kukuhamasisha tu au ku-regulate sheria ambazo zitafanya uongeze kipato chako au ujitume zaidi.

Vilevile JK alizaliwa kama binadamu wengine. Hivyo yeye kuwa rais, hakufanyi aache yale ubinadamu wake na kuwa super-binadamu.

Mkuu Zakumi,
Naona unajikanyaga au unaanguka mwenyewe. Mie nimesema Rais awawezeshe watu. Wewe umesema Hapana ila kila mtu ajitafutie kipato chake mwenyewe. Haya ya KIPATO umeyaleta mwenyewe na UYANYWE MWENYEWE.

Kikwete ni binadamu, ni kweli kabisa. Hizo Pipi akawagawie wanae akina Riddhy na wajukuu zake. Hapo hakuna atakayesema kitu maana hata mie ntamshukia. Akigawa pipi kwa watoto wake/watoto wa nduguze jamaa na marafiki na tena isiwe safari ya kiserikali, hamna neno. Ila kugawa Pipi kwenye safari ya kiserikali, kwa kweli INANIPA UTATA.

Wajibu wa Rais si KUHAMASISHA tu. Rais na serikali yake lazima wajenge mazingira mazuri ili KUWAWEZESHA Watanzania wataokuwa wakichakalika kuwa na mafanikio katika maisha yao. Sasa kama UNALIPA KODI na Rostam Azziz anakuja na kuzila badala ya hizo pesa zijenge Reli/barabara itakayopitisha bidhaa zako mwakani, unafikiri next year utauza hizo Kahawa zako?
Serikali ni watu waliosoma, wanatembea na kuona vingi. Kuna muda inabidi hata KIBOKO kitembee ili muradi tu watu wasife njaa, watoto wasome, wasilale nje, wapate huduma muhimu nk.
Ndiyo maana wanapoomba KURA wanasema "NITAKULETEENI PIPI, umeme, Maji, Barabara, Meli nk nk".
 
'security breached'! huh,...acheni kuiangalia picha kiuoga uoga... msafara huo ulikuwa hata kuondoka bado.

Hamuwezi hata kuangalia reflection kwenye gari? Red Carpet, security staff,... Mungu wangu, are we serious hatuwezi kuangalia 'nje ya box' kiasi hiki?
 
I meant Presidential motorcade
Huoni kuna kasoro alichofanya?

Kwenye hiyo picha naona gari moja tu. Sioni magari mengine kwa hiyo siwezi kusema sana juu ya hilo. Kama wewe unazo picha zinazoonyesha hiyo "Presidential motorcade" yake imesababisha kila kitu kusimama ziweke hapa mimi na wengine tuzione halafu tulijadili hilo
 
'security breached'! huh,...acheni kuiangalia picha kiuoga uoga... msafara huo ulikuwa hata kuondoka bado.

Hamuwezi hata kuangalia reflection kwenye gari? Red Carpet, security staff,... Mungu wangu, are we serious hatuwezi kuangalia 'nje ya box' kiasi hiki?

Umeshaambiwa hapo Kikwete alisimamisha "Presidential motorcade" yake....mimi sijui maana sikuwepo. Sasa labda wengine walikuwepo...I dunno
 
Hivi watu mlitegemea huyo mtoto akatae hizo peremende? Kuna vitu na vitu vya kukosoa lakini hili kwa kweli mnachemka. Eti mnakosoa Kikwete kumpa pipi dogo? Hehehe akili ya wasomi wa Kiafrika inashangaza sana

Hebu tujenge scenario hapa inayomake sense. Raisi anafanya ziara akiwa ndani ya moja ya mashangingi yake. Njiani anakutana na katoto ambako kwa dalili zote na za wazi kabisa kanareflect hali za watoto wengi vijijini. Kitu anachofanya Raisi ni kungiza mkono mfukoni au ndani ya boksi la pipi analotembea nalo kwenye gari na kukapa katoto haka pipi.

Katoto kanatoka mbio kwa furaha hadi kwa wazazi wake ambao kwa wakati huo labda hawajui hata mlo wa siku hiyo utapatikanaje. Wazazi wanamwuliza mtoto hizo pipi katoa wapi na mtoto anasema kapewa na Raisi ! Ghafla mzazi anakumbuka kwa mbali kuwa mwaka 2005 walipewa kanga, fulana na kofia wakati wa kampeni ili wampe kura mgombea Uraisi !

Baba anamgeukia mkewe huku macho yakilengalenga machozi na kwa huzuni anatikisa kichwa - anakumbuka jinsi maisha tangu siku hiyo yalivyozidi kuwa ya dhiki siku hadi siku !
Raisi aliyewaahidi maisha bora leo, miaka mitano baadaye, anapita akigawa pipi kwa watoto !
 
"Scenario" yako inafaa sana kuwa moja ya talking points za opposition wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu. Get with Zitto on that one. Ila kwa kinachozungumziwa hapa sioni relevance yake.
 
Mkuu Zakumi,
Naona unajikanyaga au unaanguka mwenyewe. Mie nimesema Rais awawezeshe watu. Wewe umesema Hapana ila kila mtu ajitafutie kipato chake mwenyewe. Haya ya KIPATO umeyaleta mwenyewe na UYANYWE MWENYEWE.

Kikwete ni binadamu, ni kweli kabisa. Hizo Pipi akawagawie wanae akina Riddhy na wajukuu zake. Hapo hakuna atakayesema kitu maana hata mie ntamshukia. Akigawa pipi kwa watoto wake/watoto wa nduguze jamaa na marafiki na tena isiwe safari ya kiserikali, hamna neno. Ila kugawa Pipi kwenye safari ya kiserikali, kwa kweli INANIPA UTATA.

Wajibu wa Rais si KUHAMASISHA tu. Rais na serikali yake lazima wajenge mazingira mazuri ili KUWAWEZESHA Watanzania wataokuwa wakichakalika kuwa na mafanikio katika maisha yao. Sasa kama UNALIPA KODI na Rostam Azziz anakuja na kuzila badala ya hizo pesa zijenge Reli/barabara itakayopitisha bidhaa zako mwakani, unafikiri next year utauza hizo Kahawa zako?
Serikali ni watu waliosoma, wanatembea na kuona vingi. Kuna muda inabidi hata KIBOKO kitembee ili muradi tu watu wasife njaa, watoto wasome, wasilale nje, wapate huduma muhimu nk.
Ndiyo maana wanapoomba KURA wanasema "NITAKULETEENI PIPI, umeme, Maji, Barabara, Meli nk nk".[/QUOTE]

Kuna misemo miwili ilinipa taabu sana kuingia kichwani mwangu. Miafrika ndivyo ilivyo na Mitanzania mivivu ya kufikiri.

Kwa kutumia picha hiyo ningetemea angalau mtoe hoja ya kulinganisha nyumba iliyopo mbele ya magari na thamani ya magari. Kwani nyumba hiyo inaweza kuwa chochote kile, shule, zahanati au ofisi ya katibu kata.

Lakini kwa uzembe mnaangalia insignificants.
 
Ngoja na mie NISUBIRI PIPI yangu mwakani.

Ila sema Washamba hawa siku zote huwa wanagawa Yollow T-Shirt za Njano na Green Vest za Kijani au mchanganyiko. Mie zamani nilikuwa SIMBA SC. Kwa hiyo hiyo Rangi huwa siipendi sana. Labda wakinipa nguo ntaomba wanipatie tu Khanga kwa ajili ya Mke wangu Nyanso.
Watoto wa Kizungu kila mwaka wana Baba Krismas. Ila sisi Tanzania tuna BABA CCM ambaye huja kila baada ya miaka 5. Ukibahatika sana labda mbunge wenu afe hapo watapita wakigawa tena upya. Mwisho hubaki mara moja moja VX zikiingia kijijini, watu hufungua madirisha na kurusha sasa Pipi kwa watoto.

Waambieni watoto wenu wasiwe na tabia ya kupokea vitu ovyo ovyo kwa watu wasiowafahamu. Vitakuja kuwatokea PUANI na tupate akina Maumba wengine.
 
Hebu tujenge scenario hapa inayomake sense. Raisi anafanya ziara akiwa ndani ya moja ya mashangingi yake. Njiani anakutana na katoto ambako kwa dalili zote na za wazi kabisa kanareflect hali za watoto wengi vijijini. Kitu anachofanya Raisi ni kungiza mkono mfukoni au ndani ya boksi la pipi analotembea nalo kwenye gari na kukapa katoto haka pipi.

Katoto kanatoka mbio kwa furaha hadi kwa wazazi wake ambao kwa wakati huo labda hawajui hata mlo wa siku hiyo utapatikanaje. Wazazi wanamwuliza mtoto hizo pipi katoa wapi na mtoto anasema kapewa na Raisi ! Ghafla mzazi anakumbuka kwa mbali kuwa mwaka 2005 walipewa kanga, fulana na kofia wakati wa kampeni ili wampe kura mgombea Uraisi !

Baba anamgeukia mkewe huku macho yakilengalenga machozi na kwa huzuni anatikisa kichwa - anakumbuka jinsi maisha tangu siku hiyo yalivyozidi kuwa ya dhiki siku hadi siku !

Raisi aliyewaahidi maisha bora leo, miaka mitano baadaye, anapita akigawa pipi kwa watoto !

Tuendelee kujenga scenario. Wakati rais anampa mtoto pipi, rais akamwambia mtoto kazana na masomo. Mimi nilikuwa hivyohivyo kama wewe.

Mtoto akarudi nyumbani na kuanza kufanya bidii shuleni. Miaka ishirini inayokuja mtoto ni top Tanzanian nuklia sayantisti.
 
Dah! Hii scenario yako Companero akiiona lazima akununulie bia....si unamjua alivyo?
 
Hebu tujenge scenario hapa inayomake sense. Raisi anafanya ziara akiwa ndani ya moja ya mashangingi yake. Njiani anakutana na katoto ambako kwa dalili zote na za wazi kabisa kanareflect hali za watoto wengi vijijini. Kitu anachofanya Raisi ni kungiza mkono mfukoni au ndani ya boksi la pipi analotembea nalo kwenye gari na kukapa katoto haka pipi.

Katoto kanatoka mbio kwa furaha hadi kwa wazazi wake ambao kwa wakati huo labda hawajui hata mlo wa siku hiyo utapatikanaje. Wazazi wanamwuliza mtoto hizo pipi katoa wapi na mtoto anasema kapewa na Raisi ! Ghafla mzazi anakumbuka kwa mbali kuwa mwaka 2005 walipewa kanga, fulana na kofia wakati wa kampeni ili wampe kura mgombea Uraisi !

Baba anamgeukia mkewe huku macho yakilengalenga machozi na kwa huzuni anatikisa kichwa - anakumbuka jinsi maisha tangu siku hiyo yalivyozidi kuwa ya dhiki siku hadi siku !
Raisi aliyewaahidi maisha bora leo, miaka mitano baadaye, anapita akigawa pipi kwa watoto !

Ewaa.. mkuu hapa tupo ukurasa mmoja..hii ndo tunaita 'kufikiria nje ya kiboksi'!
 
Back
Top Bottom