Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Nyani,
Huoni kuwa mtoto yule alikuwa kaandaliwa? Siwezi amini kuwa hii ilitokea kibahati. Labda mtu aje aseme kuwa Mkuu huwa anakula Pipi na muda wote huwa anazo na aliamua kumgawia hizo Pipi huyo mtoto.

Vinginevyo kama alitoka Dar na hayo Mapipi aliyonunua au aliletewa kutoka Uarabuni na kuamua kuja KUYAGAWA MWENYEWE, hapo mie naona kuna kitu kinamiss. Kama alipewa mengi basi angeliwapatia hata wafanyakazi wake wapite na kuwagawia watoto au angezipeleka kwa watoto yatima.

Kama mtoto hata mie ningelipenda saaana nipewe hizo PIPI. Ila kwa RAIS kutoka na MAPIPI Dar hadi sijui Lindi na kuanza kuzigawa kwa watoto............ Yaani katika majukumu yake yoote, hili pia akalipa kipaumbele....... ngoja nikagawe Pipi Lindi?

Nilishaona Michael Jackson alipotembelea watoto yatima, akawa hana zawadi ya kuwapelekea kama ukumbusho wa yeye alikuwa hapo. Akaenda dukani na kununua CD zake na kuwapelekea hao watoto pamoja na zawadi nyingine nyingi. Kama Mwanamuziki, kila kitu kinakubalika. Ila kama Rais, kitu gani angeliwapelekea watoto ili kwa miaka mingi waje wamkumbuke? Hao watoto wakibaki kuwa WALALAHOI, milele watabaki wakimsifu. Ila kama Dogo akisoma na aje ajisifu kuwa alipewa Pipi na Kikwete, basi huyo FORM ONE itabidi akimbie shule kwa kuchekwa.

NB: Hivi alimpa au ALIM-MWAGIAGA mapipi?
 
kwa kuwa tunazungumzia hisia tu na wote hatujui kilichotokea,mi nafikiri inawezakana pipi alizotoa kikwete zilikuwa zinahitimisha zawadi zingine zilizotangulia au ulikuwa utangulizi wa zawadi zingine ambazo zilifuata na ambazo sisi hatuzijui.Naamini Rais mzima hawezi kugawa pipi na kutokomea.Ila nae rais mambo yake bwana!Anatembea na pipi za nini? Ndugu tunayo kazi...........
 
angemwambia "sidanganyiki"
Tehe heheh!

Watu wengine mahepe ,sasa mtoto ana safura au minyoo ,yeye imemuhusu nini ? Maana kwa hivyo mnavyofikiria ,sijui mtoto hajashiba au ananjaa sioni hoja hiyo kunhusisha na Raisi mpita njia tu !!

Zipo hoja za kuhoji lakini si hali ya mtoto ambayo inahitaji daktari kujua yote hayo.

Tatizo WaTanganyika hamtosheki ,hivi mlitaka agawe gari moshi?

Hapana, tulitaka agawe bastola, ili keshokutwa huyu mtoto aende kujitafutia chochote pale benki ya NMB!
 
hhehehe msianze tena siasa za kimapinduzi hapa

huyo mtoto anatuwakilisha wengi ambao tumeridhika na the status quo kwa kupewa 'pipi' zetu in form of ahadi tamu tamu ambazo utekelezaji wake ni mgumu

inabidi tufike mahali kila mmoja awepo kwenye gari lake, hata kama sio at the same level, lakini kwa hili tofauti ni kubwa mno....sisemi kuwa JK kakosea ila picha inanifanya nifikiri zaidi...na ingekuwa mimi ndo JK ningeshuka kabisa chini walau nikagua hayo malenge lenge kichwani kisha niwawajibishe wahusika kuanzia wizara ya afya....na wizara ya elimu kwa kushindwa ktekeleza sera na mipango ya maendeleo...au hii ni utopia tu?

Oooh please..your so called "metaphor" ni mbofu! Hukuweka hilo wazi, na pili umesema "in fact". Kama watu kama wewe ambao somehow mko "sophisticated" but yet fail to string together even a coherent sentence...it just makes me go hmmmmm....

Still, ubaya uko wapi kwa Kikwete kumpa huyo mtoto peremende? Orodhesha huo ubaya hapa...

Sasa mkuu wakati unasema metaphor ni 'mbofu' mbona hujaonesha ulipo ubofu wake? Mi nilidhani liko wazi na ndio maana walioelewa walielewa ijapokuwa sitegemi kila mmoja kumweliewa mwenzie jinsi ambavyo angependa

Hilo la 'coherence' as you put it...naliacha kama lilivyo.

Pili, tangu mwanzo nilishasema kuwa simaanishi kuwa JK kafanya vibaya,

Hapa ni muhimu kuelewa pia kuwa tusizoee tu kuona vitu jinsi vilivyo na kuvikubali jinsi vilivyo...tuende mbali zaidi ya hiyo picha na nadhani ndilo lilikuwa lengo la mtoa hii mada/picha.
 
Kweli TZ kuna Pumba... sasa hapa kosa la JK kumpa mtoto uyo pipi ni lipi? at least give him credit he is kind enough to get close to local people na kuinteract nao kama JK not president. Nyie mnataka president awe ni mtu wa matawi ya juu tu? Dah na wengine wanamponda mtoto lol.. jamaani mwacheni mtoto awe mtoto na inawezekana ata huyo mtoto aonja pipi kwa miezi sasa kwanini aikatae? acheni pumba
 
Watu kweli wapo irrational hapa. Kibaya zaidi kuna wengine wanajidai wana advanced degrees lakini ukisoma comments zao ubakaki kusema 'hmmmm' hivi huyu kweli kamaliza hata sekondari...yaani pumba juu pumba.

Ni kweli watu wengi wanazo advance degree. Lakini mfumo wa elimu umehimiza sana watu kutumia mitulinga na sio kuwa creative au rational.
 
Binafsi nikikutana/nikiwa na mtoto awe wa ndugu, jamaa au rafiki nafikiria kumpa zawadi kama hizo pipi,lawalawa n.k. viendanavyo.
JK ana mapungufu yake lakini kwa hili hajakosea na simlaumu!..
 
Baada ya kumbana anadai eti kamtumia mtoto kama "metaphor"....Lol

Where is The Truth when you need him?

Mkuu nadhani hapa hatupo 'kubanana'.....hapa nimetoa ufafanuzi baada ya wewe kushindwa kunielewa nilikuwa namaanisha nini, napia kwa upande mwingine kuona kuwa kuna maelezo ya aina moja tu kuhusu iyo picha..kwamba ni tukio la JK kupma mtoto pipi, na ni jambo jema...SAWA. Lakini upande mwingine je? hapa JK kama baba hakuna mwenye tatizo na hilo na nimekuwa clear na hilo!
 
Nyani,
Huoni kuwa mtoto yule alikuwa kaandaliwa?

Hapana sijaona popote pale panapoonyesha mtoto yule kuwa aliandaliwa kwenda kupokea hizo pipi. Kama wewe una compelling evidence niwekee hapa na mimi nione labda nitabadili mtazamo wangu

Siwezi amini kuwa hii ilitokea kibahati. Labda mtu aje aseme kuwa Mkuu huwa anakula Pipi na muda wote huwa anazo na aliamua kumgawia hizo Pipi huyo mtoto.

Imani yako ni imani yako na mimi siwezi kuikataa. Ukija na facts na kuonyesha maandalizi hapo ndipo nitakubali au kukataa. Imani yako/zako nakuachia mwenyewe.

Vinginevyo kama alitoka Dar na hayo Mapipi aliyonunua au aliletewa kutoka Uarabuni na kuamua kuja KUYAGAWA MWENYEWE, hapo mie naona kuna kitu kinamiss. Kama alipewa mengi basi angeliwapatia hata wafanyakazi wake wapite na kuwagawia watoto au angezipeleka kwa watoto yatima.

More conjecture!

Kama mtoto hata mie ningelipenda saaana nipewe hizo PIPI. Ila kwa RAIS kutoka na MAPIPI Dar hadi sijui Lindi na kuanza kuzigawa kwa watoto............ Yaani katika majukumu yake yoote, hili pia akalipa kipaumbele....... ngoja nikagawe Pipi Lindi?

Hiyo ni statement of fact. So which is which? Unaamini au unajua?

Nilishaona Michael Jackson alipotembelea watoto yatima, akawa hana zawadi ya kuwapelekea kama ukumbusho wa yeye alikuwa hapo. Akaenda dukani na kununua CD zake na kuwapelekea hao watoto pamoja na zawadi nyingine nyingi. Kama Mwanamuziki, kila kitu kinakubalika. Ila kama Rais, kitu gani angeliwapelekea watoto ili kwa miaka mingi waje wamkumbuke? Hao watoto wakibaki kuwa WALALAHOI, milele watabaki wakimsifu. Ila kama Dogo akisoma na aje ajisifu kuwa alipewa Pipi na Kikwete, basi huyo FORM ONE itabidi akimbie shule kwa kuchekwa.

Hapa sijui hata unazungumzia nini. You are just rambling.
 
Nyie mnataka president awe ni mtu wa matawi ya juu tu? Dah na wengine wanamponda mtoto lol.. jamaani mwacheni mtoto awe mtoto na inawezekana ata huyo mtoto aonja pipi kwa miezi sasa kwanini aikatae? acheni pumba

Mkuu hatusemi Rais awe matawi. Ila pia asitudanganye kuwa yeye ni kama sisi wakati hata vumbi hakanyagi. Mtoto na awe mtoto. Na aendelee kula pipi zake na keki na vitu vingine kibao. Ila wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi na ikibidi hata huko mashuleni ili hawa watoto wawe wanapata Pipi mara kwa mara na si kusubiri hadi Kikwete ajaze Mapipi kwenye VX lake na kuja kuzigawa Lindi. Asipofika, kijiji hicho milele hawatakula PIPI?

Binafsi nikikutana/nikiwa na mtoto awe wa ndugu, jamaa au rafiki nafikiria kumpa zawadi kama hizo pipi,lawalawa n.k. viendanavyo.
JK ana mapungufu yake lakini kwa hili hajakosea na simlaumu!..

BelindaJ.
Huo ndiyo wajibu wa wazazi. Wazazi muwe na uwezo wa kuwanunulia watoto Pipi. Wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi/Wajomba/shangazi kuwa na mapesa ya kununua hizo pipi na si Rais kuja kuwagawia watoto pipi na hadi nyingine zinamwagika mkononi. Wee kono la Muungwana limejaza pipi kibao na tumikono twa dogo, nyingine ziliishia CHINI. Sasa hapo Dogo akaanza kuokota kama Mbwa. Kimila za Kinyamwezi hapo NINAKUZILIA.
 
Mkuu hatusemi Rais awe matawi. Ila pia asitudanganye kuwa yeye ni kama sisi wakati hata vumbi hakanyagi. Mtoto na awe mtoto. Na aendelee kula pipi zake na keki na vitu vingine kibao. Ila wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi na ikibidi hata huko mashuleni ili hawa watoto wawe wanapata Pipi mara kwa mara na si kusubiri hadi Kikwete ajaze Mapipi kwenye VX lake na kuja kuzigawa Lindi. Asipofika, kijiji hicho milele hawatakula PIPI?

Wajibu ni wa kwetu sote kuanzia pale tunapochagua viongozi na kuhakikisha tunapowachagua wanafanya kazi kama walivyoahidi watafanya. Sasa kama mnamwona raisi hafanyi kazi yake kama alivyoahidi na kama anavyopaswa basi alaumiwe na hizo lawama ziendane na makosa yake. Lakini kwa yeye kumpa pipi dogo na nyinyi mnamshikia bango kama vile kalisababishia taifa hasara kubwa sana is beneath contempt!

Na wajibu wa kuleta maendeleo sio wa raisi peke yake bali taifa zima.
 
Huyo mtoto alitakiwa awepo darasani anasoma; na si kupokea pipi. Hiyo picha inaonesha INEQUALITIES ni tatizo linalokuwa kwa kasi sana ndani ya TZ. Rais yupo kwenye gari la kifahari + msafara wa wapambe; halafu huyo mtoto hata viatu hana. Sasa hivi kuna tofauti kubwa sana kati ya maskini (mlalahoi) na mtu wa middle class ndani ya TZ.

hana viatu?mbona picha haijamuonyesha mpaka chini na tukaona hiyo miguu kama hajavaa viatu.
 
Hapana sijaona popote pale panapoonyesha mtoto yule kuwa aliandaliwa kwenda kupokea hizo pipi. Kama wewe una compelling evidence niwekee hapa na mimi nione labda nitabadili mtazamo wangu

Imani yako ni imani yako na mimi siwezi kuikataa. Ukija na facts na kuonyesha maandalizi hapo ndipo nitakubali au kukataa. Imani yako/zako nakuachia mwenyewe.

Hiyo ni statement of fact. So which is which? Unaamini au unajua?

Hapa sijui hata unazungumzia nini. You are just rambling.

Tutabishana sana ila ukweli unabaki kuwa:

1. Huyo mtoto alichaguliwa na Walinzi wake na kuletwa pale karibu na gari la Rais. Tungeliona kundi la watoto wamezunguka gari tungeliamini kuwa ilikuwa imetokea kibahati. Mwenyewe umesema kuwa kuna mkono wa mtu kavaa Kaunda suti. Kwa hiyo utake usitake, huyu mtoto alichaguliwa (kuandaliwa) na kupelekwa pale kwa Kikwete.
2. Kikwete alikuja na hizo Pipi kutoka huko alikotoka. Hizo pipi hazikuanguka kutoka mbinguni kama Mana. Alifahamu kabisa kuwa nabeba Pipi na ntaenda kuzigawa kwa kitoto chenye bahati.

3. Alipofika pale akaagiza wamletee huyo mwenye bahati na kijana akaletwa huku wengine wakiambiwa kaeni mbali maana hatuwaoni. Labda mkuu napo hapa utakuja na madai nilete ushahidi. Ushahidi sina na kwa niseme kuwa "wenyewe walijipanga na wakakaa mbali". Dogo akaja na bila kujua kinafanyika nini, Dogo akaona mkono unatoka na MAPIPI kibaooo. "Salaleee, Mungu anipe nini?" Dogo ni kufungua mikono na kumwagiwa mipipi. Hakumuuliza hata kama wazazi wanamruhusu ale Pipi maana anaweza kuwa na kisukari.

Kama hayo maelezo nayo unataka ushahidi, basi na mimi ntaomba ushahidi kama kweli ni wewe leo unaandika au ni nduguyo.
 
BelindaJ.
Huo ndiyo wajibu wa wazazi. Wazazi muwe na uwezo wa kuwanunulia watoto Pipi. Wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi/Wajomba/shangazi kuwa na mapesa ya kununua hizo pipi na si Rais kuja kuwagawia watoto pipi na hadi nyingine zinamwagika mkononi. Wee kono la Muungwana limejaza pipi kibao na tumikono twa dogo, nyingine ziliishia CHINI. Sasa hapo Dogo akaanza kuokota kama Mbwa. Kimila za Kinyamwezi hapo NINAKUZILIA.

Sikonge
Inawezekana ni uwingi wa pipi mkononi mwa JK anavyompa huyo mtoto ndo umejiuliza maswali mengi au?Mana kama ulivyosema zingine zitadondoka na kama mtoto ataziokota .
Yaani tukae tutegemee ipo siku JK atawawezesha hao wazazi kununua pipi. Itafika lini hiyo?..Ndo mana wengine tunasubiri ahadi za wabunge wao zitimie kumbe ni siasa tu!
Pengine kwa hiyo picha watu tumepata tafsiri na mawazo mbalimbali. Bado naona ni sawa tu kwa hili mkuu..Ila pia sipingani na mawazo yako..
 
Mkuu hatusemi Rais awe matawi. Ila pia asitudanganye kuwa yeye ni kama sisi wakati hata vumbi hakanyagi. Mtoto na awe mtoto. Na aendelee kula pipi zake na keki na vitu vingine kibao. Ila wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi na ikibidi hata huko mashuleni ili hawa watoto wawe wanapata Pipi mara kwa mara na si kusubiri hadi Kikwete ajaze Mapipi kwenye VX lake na kuja kuzigawa Lindi. Asipofika, kijiji hicho milele hawatakula PIPI?

BelindaJ.
Huo ndiyo wajibu wa wazazi. Wazazi muwe na uwezo wa kuwanunulia watoto Pipi. Wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi/Wajomba/shangazi kuwa na mapesa ya kununua hizo pipi na si Rais kuja kuwagawia watoto pipi na hadi nyingine zinamwagika mkononi. Wee kono la Muungwana limejaza pipi kibao na tumikono twa dogo, nyingine ziliishia CHINI. Sasa hapo Dogo akaanza kuokota kama Mbwa. Kimila za Kinyamwezi hapo NINAKUZILIA.

Sio wajibu wa rais kuwawezesha watu. Kujitafutia kipato ni chaguo lako (period). Rais anachoweza kufanya ni kukuhamasisha tu au ku-regulate sheria ambazo zitafanya uongeze kipato chako au ujitume zaidi.

Vilevile JK alizaliwa kama binadamu wengine. Hivyo yeye kuwa rais, hakufanyi aache yale ubinadamu wake na kuwa super-binadamu.
 
Mkuu hatusemi Rais awe matawi. Ila pia asitudanganye kuwa yeye ni kama sisi wakati hata vumbi hakanyagi. Mtoto na awe mtoto. Na aendelee kula pipi zake na keki na vitu vingine kibao. Ila wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi na ikibidi hata huko mashuleni ili hawa watoto wawe wanapata Pipi mara kwa mara na si kusubiri hadi Kikwete ajaze Mapipi kwenye VX lake na kuja kuzigawa Lindi. Asipofika, kijiji hicho milele hawatakula PIPI?

BelindaJ.
Huo ndiyo wajibu wa wazazi. Wazazi muwe na uwezo wa kuwanunulia watoto Pipi. Wajibu wa Rais ni kuwawezesha wazazi/Wajomba/shangazi kuwa na mapesa ya kununua hizo pipi na si Rais kuja kuwagawia watoto pipi na hadi nyingine zinamwagika mkononi. Wee kono la Muungwana limejaza pipi kibao na tumikono twa dogo, nyingine ziliishia CHINI. Sasa hapo Dogo akaanza kuokota kama Mbwa. Kimila za Kinyamwezi hapo NINAKUZILIA.

lol mhh sikujua wanyamwezi wanapenda kuzila hivyo lol. Sikonge, Naelewa ukisemacho, ila my argument hapa ni kwamba watu tunakuwa tunamjudge sana JK. Na hatuwezi mmjudge na picha maana we dont know alisema nini au aliongea nini na wakazi wa lindi. Pia kumbuka there are is a limit to what government/president can do regarding motivating each individual person/citizen in a country. That means sisi wenyewe wananchi inabidi tujimotivate. Mfano mzuri watu wangapi vijijini ata mijini wanapractice polygamy na wanaendelea kuoa dispate not having enough money to support one wife and kids? sasa kwenye kama ii issue JK unataka afanye nini? asambaratishe families? na watanzania ukiandia kuhusu polygamy wanakwambia ni culture yetu!!! Mi naona tuache tabia ya kublame other people so much na tuanze kutake our own blames and learn from our own as well as other peoples mistakes. Tukianza kujifunza hivi then as a country tutaanza kuupiga chini umasikini.. maana kila mtu ataanza kuwa responsible on his/her own individual life. N.B Inawezekana ata kam JK angempa huyo mtoto tution fee wazazi wake wangeila au baba yake angeenda kuolewa mke wa kumi! So ni hivi vitu ambavyo vinaangusha maendeleo ya jamii.
 
JF inafurahisha!

Raisi anasafiri na mapipi kwenye gari, mabaki anagawia watoto ambao anajua kabisa kama kiongozi wa nchi wanahitaji zaidi ya pipi....tunatofautiana sana katika kufikiri. Wanaosupport eti kama mzazi well, mimi namwona Kikwete ni zaidi ya hapo kama head wa state.....anamajukumu mengi....sidhani kama Obama anaweza fanya hilo, ama Sarkozy na other serious leaders!

We are too cheap! Nilitegemea JF watu wanafikiria zaidi ya wale walevi wa kangala na wanzuki usukumani kumbe sivyo!
 
Nilipojiunga na Jamii Forums nilikuwa nafikiri naingia kwenye network ya big ideas on how we can improve the life of mwanakijiji wa Tanzania ... not this rubbish! wewe ndugu una watoto, nieces au nephews?
 
Back
Top Bottom