Rais kubadilisha mawazo sio unyonge na sio ushindi wa CHADEMA

Watanzania wenzangu mabadiliko ya kweli ya taifa hili hayataletwa na vyama vya siasa tunaona njia ileile CUF waliyopita CHADEMA wanaifuata. Kweli viongozi wote wa siasa bongo ni sawa na wachojali ni maslahi binafsi. Real Changes italetwa na watanzania watakapoamu kufanya hivyo na siyo vyama vya siasa. Kwa hili la Katiba CHADEMA tumeona mmepotoka mnakurupuka blia strategies. Kwani mmeshindwa kutumia kanuni ya 86. Pili mnakula matapishi yenu kwa kuwalalamikia CUF kumbe nanyi lenu ni hilo hilo.
 
Kweli, inaweza kuwa inatokana na busara za Kiwete kuamua kutosaini muswada huo kwa ajili ya faida ya Taifa; hata vivyo hiyo pia itasaidia kuonyesha kuwa wabunge wazomeaji wa CCM pamoja na spika wao hawana busara za kuona mambo yenye tija kwa Taifa kwa kiasi ambacho wanapitisha muswada bila kuutafakali kwa kina hadi pale Rais Kikwete mwenyewe atumie busara zake kuona madudu hayo.
 
Binafsi ninakubaliana nawe. Kuna mambo ambayo CDM inatakiwa iwe inawaelimisha vema mashabiki wake na hili la wapi pa kushangilia na jinsi ya kushangilia ushindi ni mojawapo. Amasivyo watakuwa wanajiwekea magogo mbele ya safari ya usuhishi wa kidiplomasia katika mambo ya Kitaifa. Kutaka kujionyesha mwamba au mshindi ndiko kumepelekea baadhi ya nchi au vyama Tawala kugeuka Madikteta.
CDM watakuwa na haki ya kushangilia kwa kufanya kazi yao vema kama chama makini cha siasa, Kikwete atakuwa na haki ya kupongezwa kwa mara ya kwanza atakuwa amefanya jambo gumu kama rais wa nchi na wananchi tutawashangilia pande zote mbili.
Win win win, no looser!
 
Nimewaza kuwa ni muhimu na kwa haraka tukaweka bayana kuwa endapo rais Mh. Dr. Jakaya Kikwete ataamua kutokutia saini muswada wa katiba. Basi ijulikane sio unyonge bali ni busara, hekima na heshima kwake. Kwa upande wa CDM ni muhimu nao wakatae kulitumia hilo au watu watakaolitumia hilo kama ushindi. Haya mambo yaonekana kama madogo lakini yasipowekwa sawa yanazuia ufanisi huko mbele.

Chadema wakatae kupokea sifa katika hili na wao waseme kwa nguvu kuwa ni busara ya Rais na utashi wake. Naye rais ni muhimu akasisitiza kuwa ameheshimu mawazo chanya yaliyopelekwa kwake na kama baba ameamua kuwasikiliza watoto wote.

Hongera Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa busara zako na usikivu wako. Hongereni viongozi wa CHADEMA.

Hongereni wananchi wa Tanzania kwa umoja na mshikamano wenu.


Unajua rais wako ni kigeugeu ndo mana unamtetea in advance.




Il Gambino.
 
Ninachosema.....kama kweli rais kakubaliana na CDM kimsingi, basi kapata busara ya juu ya kupongezwa kwa kuwasuta waziwazi wabunge wake kwa kuwa na ushabiki usio na tija. Atakuwa amewapa somo wabunge wake kujali utaifa zaidi ya ushabiki wa ki...
 
Jk toka umekuwa rais umenikuna maana umeachana na ushabiki. Kumbuka jk dhamana ya amani ya nchi utaulizwa wewe. Bora uwe na urafiki wa nje ya ccm maana ndani ya ccm ni unafiki mtupu. Kukubaliana na cdm kutaitoa ccm kwa ushindani basi hivyo hutalaumiwa wewe. Ccm wakishindwa kwa sababu ya kulazimisha utalaumiwa wote. Hapa tulipofika angalia tuendako usisikilize wanaotaka urais ili mradi wewe ulishapata wako na hurudii.
 
JK anapaswa kuelewa hii phrase "God, grant me the serenity to accept the things I cannot change, the courage to change the things I can, and the wisdom to know the difference." ya Neibur......itamsaidia
 
kweli kabisa.... kukubali kuweka katiba mpya isiyo na unafiki itamsaidia mheshimiwa raisi kumaliza kipindi chake kwa amani na pia itamsaidia kuchuna GAMBA LILILOBAKI kule ccm bila kutumia msuli!
 
Ni kama mswada upi ambao rais alishawahi kukataa kuusaini katika miaka hii 50 ya uhuru?
 
Wana JF ni mapema sana kuanza kumpongeza mtu au upande fulani,maana sidhani hata kila kitu kilichozungumzwa wakati wa kikao cha viongozi wa Chadema na Rais na timu yake kama kuna mtu amekipata kwa ukweli wake na mapana yake,na suala la kuusaini huo mswaada bado liko mafichoni,hakuna anaejua nini kitafanyika,nadhani pia hata JK atakuwa na muda zaidi wa kutafakari kwa kina.nashauri tusitoe pongezy kwa Rais tuwe na subira ili tukija kuanza kujadili tutakuwa na kitu cha uhakika.Nawasilisha
 
Watanzania wenzangu mabadiliko ya kweli ya taifa hili hayataletwa na vyama vya siasa tunaona njia ileile CUF waliyopita CHADEMA wanaifuata. Kweli viongozi wote wa siasa bongo ni sawa na wachojali ni maslahi binafsi. Real Changes italetwa na watanzania watakapoamu kufanya hivyo na siyo vyama vya siasa. Kwa hili la Katiba CHADEMA tumeona mmepotoka mnakurupuka blia strategies. Kwani mmeshindwa kutumia kanuni ya 86. Pili mnakula matapishi yenu kwa kuwalalamikia CUF kumbe nanyi lenu ni hilo hilo.

Kutumia kanuni au sheria kunawezekana tu pale ambapo wasimamizi wa kanuni au sheria hizo wana busara nia ya kuzitumia.
Watanzania walishuhudia pale spika alivyojifanya haoni tatizo na kuharakisha mjadala badala ya kuuliza tatizo ni nini ili atoe ufafanuzi.
Hata kama mtu hajui au hakufuata kanuni, siyo busara kumpuuza bali ni muhimu kumuelewesha kwa ufafanuzi ulio wazi kwa faida yake na wengine pia.
Uwepo wa sheria na kanuni ni kitu kingine tofauti na matumizi ya sheria na kanuni hizo yanayotegemea zaidi utashi na uadilifu wa wa wasimamizi.
 
Nitazungumzia zaidi Rais kama mtu badala ya Rais kama taasisi.

Kama mtu, JK kafanya jambo zuri KUJIRUDI baada ya kusema aliyoyasema mbele ya wazee Dar es Salaam. Alitumia neno "kelele" za wapinzani. Kwa heshima ya kawaida, neno hilo lilikuwa baya kutumiwa na Rais eti kwa sababu wengine wana mtazamo tofauti na wamepinga hata kwa kususia vikao vya Bunge kuhusu Muswada. Kusema atasaini bila kujali chochote halafu kisha akakutana nao na kuzungumza na kukubaliana kuboresha huo muswada, ni kushindwa kuhimili shinikizo. Na kamwe isikuchukuliwe kuwa ni utashi wake!! Utashi wake aliuonesha mbele ya wazee.

Rais kama taasisi inapaswa kuwaunganisha watu badala ya kuwagawa. Kama mkuu wa nchi alipaswa kuangalia na kujiridhisha kuwa taasisi yake ni kweli ilikusudia kuwasilisha muswada ule Bungeni. Hii ni pamoja na kupenda kujua wengine wanafikiria nn kwanza. Pili, baada ya kujua madai ya Kambi ya Upinzani, Jukwaa la katiba na wanaharakati wengine - angechukua hatua hata ya kusimamisha muswada na kuwasilikiza wengine kupitia ushawishi wake Bungeni. Hakufanya hivo. Kitendo anachofanya sasa cha kujaribu kurekebisha muswada si cha taasisi ya Urais!!! Na hakina nguvu kisheria!! Ni wajibu wa BUNGE!! Na wengine wanaposema Rais asiwe na madaraka makubwa hivi - hili ni eneo moja linalothibitisha nguvu nyingi za taasisi hii.

Ameaibisha taasisi ya Urais mara kadhaa sasa. Kwanza kwa kuzungumza na wazee kuhusiana na maswala ya wafanyakazi na pili kuhusiana na uchumi badala ya wawekezaji/waajiri/wenye viwanda/mabenki/wafanyakazi na siasa badala ya wananchi ambao ndio hutoa nguvu ya kisiasa si kwa wabunge na viongozi wengine tu, bali hata taasisi ya Urais.

Kwa namna yoyote, CDM ameshinda katika hali - hata kama kutakuwa na badiliko moja ktk miuswada uliopita!! na taasisi ya urais imedhoofishwa na tabia na hulka za raisi katika kushughulikia mambo mengi, si hili na Katiba tu.
 
Mtaka haki, nakupongeza kwa busara za zilizomo kwenye ujumbe wako huo juu. Kama inawezekana, watumie wajumbe wa CDM kila mmoja ujumbe huu ausome. Ni ujumbe muhimu sana kwa mtu mwenye nia njema. Bahati mbaya sina contacts za wajumbe wa CDM. Huu ni ujumbe muhimu sana kwao kuufahamu na kuufuata kama wanataka kusonga mbele na nia yao nzuri.

Hapa hatushindani kutafuta mwenye nia njema kwa TZ kwa maana ni wazi wote CCM na CDM wana nia njema. Tunachopingana ni kujua nani anaweza kudeliver ili nchi iendelee haraka zaidi.
Busara za hivi kama livyotoa Mtakahaki ni busara zina mapungufu. Ni busara yenye ujumbe usioleta nguvu ya mageuzi yeyote katika jamii iliyolala kama TZ. Raisi akiona ya CDM ni bora na akakubali mwenyewe na akasaini sioni kwa nini CDM wasishangilie kwa vifijo kwa ushindi wa hatua ya kwanza. Naamini raisi anaweza akakubali kusaini lakini akatoa sababu tofauti - lakini bado CDM wana haki ya kufurahia wazo lao kukubalika. Lazima tujenge mila ya ushindani ambapo kukubali, kuheshimu na kumzawadia mshindi iwe lazima.
Bunge letu si la CHAMA KIMOJA eti CDM wasitambe, eti wawaheshimu CCM na fikra sahihi zao : nO - kushindana kwa HOJA kwa namna yeyote ile ni muhimu sana. Utaheshimiana vipi na wanakuletea njaa, ....umaskini!
Kama raisi atasaini, basi CDM ni haki yao ku-intimidate CCM wapendavyo kwa hoja - kama CCM wamaubavu si JK asaini basi maana kwa kufanya hivyo atakua amewapa CDM nguvu zaidi na mwanya mzuri zaidi wa UPINZANI.
 
Kweli, inaweza kuwa inatokana na busara za Kiwete kuamua kutosaini muswada huo kwa ajili ya faida ya Taifa; hata vivyo hiyo pia itasaidia kuonyesha kuwa wabunge wazomeaji wa CCM pamoja na spika wao hawana busara za kuona mambo yenye tija kwa Taifa kwa kiasi ambacho wanapitisha muswada bila kuutafakali kwa kina hadi pale Rais Kikwete mwenyewe atumie busara zake kuona madudu hayo.

Hao hao si ndio walimbambikia tena kusaini madodoso yao ambayo yalikuwa kinyume na yaliyopitishwa na bunge? Kama angekuwa muoga asingeunda kamati ya kuchunguza ni vipengele gani vimeongezwa. Ni nadhani Raisi akiwa na msimamo kwa upande wa umma ataliboresha bunge na wabunge wa CCM watajua kinachowapeleka bungeni sio kusengenyana au kutafuta ni nani maarufu au tumkomoe nani bali ni kuwatetea wananchi na tanzania yetu wote. Tanzania itajiimarisha na itakuwa na maendeleo kutokana na wananchi kujitungia sheria wenyewe kutokana na sehemu walipo. Mfano: Wamachinga wasingekuwa wasumbufu kama wangeshirikishwa kutunga sheria za mji au wilaya kwa sababu anaposhirikishwa ndio hapo somo la uraia linapoanzia.
 
Mtaka haki thanks great thinker, wewe ni Mzalendo kati ya wazalendo! Na mie naongeza kwamba; Rais wetu aandae maandamano rasmi, huku wameshikana mikono na kina, Slaa, Lipumba, Mtikila, Mkama, Lowasa, Nape..... Kuionyesha Dunia kwamba tZ Imewezekana.

Waswahili wana msemo kuwa; "Yaliyo pita si ndwele tugange yajayo"
 
JK hana cha kufanya bali kutokusaini na kuirudisha bungeni, wenye nchi washamwambia ataiingiza nchi ktk vurugu iwapo atasaini.
 
Nimewaza kuwa ni muhimu na kwa haraka tukaweka bayana kuwa endapo rais Mh. Dr. Jakaya Kikwete ataamua kutokutia saini muswada wa katiba. Basi ijulikane sio unyonge bali ni busara, hekima na heshima kwake. Kwa upande wa CDM ni muhimu nao wakatae kulitumia hilo au watu watakaolitumia hilo kama ushindi. Haya mambo yaonekana kama madogo lakini yasipowekwa sawa yanazuia ufanisi huko mbele.

Chadema wakatae kupokea sifa katika hili na wao waseme kwa nguvu kuwa ni busara ya Rais na utashi wake. Naye rais ni muhimu akasisitiza kuwa ameheshimu mawazo chanya yaliyopelekwa kwake na kama baba ameamua kuwasikiliza watoto wote.

Hongera Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa busara zako na usikivu wako. Hongereni viongozi wa CHADEMA.

Hongereni wananchi wa Tanzania kwa umoja na mshikamano wenu.

Mkuu swali hapa ni kwanini unatetea udhaifu. Rais anaonekana wazi kuwa hajui mswada huu wa katiba una maana gani kwa Tanzania, kwa sasa mawazo chanya ndani ya CCM yanakandamizwa, yaliyomengi ni hasi hadi Rais analazimika kupokea mawazo chanya kutoka nje. Post yako inakiri udhaifu wa rais.
 
Back
Top Bottom