Rais Kikwete; Watanzania tukukumbuke kwa lipi ulilotufanyia?

1474746057331.jpg
 
Wana jamii
Salaam.

Mh Jakaya Kikwete, mstaafu wetu umebarikiwa kipaji cha kutabasamu sana hata ukichukia ni ngumu kufahamu hayo yote ni kipaji cha MUNGU Baba.

Ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu ulipoamua kikatiba na kisheria kupumzika kwa hiari baada ya kazi kubwa ulioifanya ya kuiongoza nchi ya Tanzania, Baba Mh Jakaya Mrisho Kikwete ninakukumbuka sana hasa katika ucheshi wako, nakutakia afya njema Mh Rais mstaafu JK MUNGU akupe nguvu na afya tele.
 
Ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu ulipoamua kikatiba na kisheria kupumzika kwa hiari baada ya kazi kubwa ulioifanyia nchi yetu Tanzania, Baba Mh JK ninakukumbuka sana hasa katika ucheshi wako, nakutakia afya njema Mh Rais mstaafu JK mungu akupe nguvu na afya tele.

Unamkumbuka kwa lipi?huyu ndo chanzo cha kutuletea hili janga lilipo sahizi.asingekuwa yeye leo tusingefika hapa.lakini ni jambo jema naye anasomeshwa namba japo namba yake haisomi kama yetu lakini anaiyonja joto ya jiwe.nimemuona juzi yuko na kuku wengi nikasema angalia asije akapata naye kideri.acha maneno wekaaa mziki bambataaaa...
 
angalau umesema 'mungu' amtie nguvu na sio MUNGU, kama Magubike ni "potelea mbali" basi Chekacheka ni "potelea pote!" yani hapo mmoja dumu mwingine mfuniko.
 
Rais msitaafu ninayemiss ni Mwinyi tu wengine tatizo waligeuza ikulu pango la walanguzi
 
Ipo siku hata Magu mtamkumbuka tu kwa uchapaji kazi wake....
IMG_20161201_135050.png

Hao ndio Watanganyika welevu sana wa kusahau na wepesi sana kukumbuka si mlikuwa mkimkebehi kwa kila aina ya meneno!..
Sisi wenye nasaba nar.tunamuombea dua Mwenyezi Mungu ampe afya.njema na uhai mrefu...Amiin
 
Tumewazoea kwa kumbukumbu zenu; mnamkumbuka nyerere, mwinyi, mkapa , kikwete, pia hata naye magu mtamkumbuka tu, wazee wa kumbukumbu!
 
Unashindwa kuwakumbuka babu na wazazi wako walojitahidi kukuandalia misingi imara ya kujituma katika utafutaji , wewe unamkumbuka mtu asojua ata chimbuko lako!


Chimbuko lake ni nchi ya Tanzania, Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo kijiji cha Msoga, Ni mwana diplomasia mbobezi, mchumi pia,
 
Unamkumbuka kwa lipi?huyu ndo chanzo cha kutuletea hili janga lilipo sahizi.asingekuwa yeye leo tusingefika hapa.lakini ni jambo jema naye anasomeshwa namba japo namba yake haisomi kama yetu lakini anaiyonja joto ya jiwe.nimemuona juzi yuko na kuku wengi nikasema angalia asije akapata naye kideri.acha maneno wekaaa mziki bambataaaa...
Kakwambia anamkumbuka kwa tabasamu lake mkuu
 
Binafsi kuna mengi mazuri nayatambua aliyofanya Kikwete. Lakini, pamoja na mazuri yake, kitendo cha kuchangia kwa kiasi kikubwa kumleta Magu, kumetia doa mazuri yake yote. Mbaya zaidi, kitendo cha Kikwete kuuacha mchakato wa "Katiba ya wananchi" njiani, ndio kumeleta janga kubwaaa. Na kwa hayo, mimi sitomsahau kwa mateso tunayoendelea kuyapata Watanzania.
 
Watu wengine mnachanganyikiwa tu
hivi Obama kumleta Trump hakukupi mateso ????
 
Back
Top Bottom