Rais kikwete tukueleweje?

hittler

Member
Jul 18, 2011
55
10
Hii tabia ya rais kukaa kimya wakati wananchi wanahitaji kusikia tamko la mkuu wa nchi linanikanganya sana. Hivi kweli kwa ali ilivyo Tanzania, ili tatizo la umeme ni lakufumbia macho? Umeme umekuwa kero kwa wafanyabiashara, wananchi wa kawaida na ata kwa hao wanaoitwa investors. TRA wanashindwa kukusanya mapato kama ilivyotakiwa, wanafunzi wanashindwa kusoma, viwanda havizalishi alafu rais anaenda kutafuta wawekezaji. Naogopa sana muda si mrefu umeme utazimika Tanzania nzima. Mbona baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Nyerere alikuwa anasema wazi kama ni kipindi cha mavuno au kujifunga mkanda? Rais Kikwete tukueleweje?
 
Kwani uliwahi kumuelewa anayoyaeleza? Wengi tumemsikia akiongelea umeme, mpaka BBC wamem interview na hiyo interview imewekwa humuhumu JF. Mpaka waziri mkuu kaomba wapewe wiki tatu kuja na kitu kinachoeleweka kuhusu wizara hiyo na hususan suala la umeme, unataka Rais akueleweshe vipi ndio umuelewe? na Jee, utamuelewa?
 
kazi ipi unayosema wewe? Niambie wamefanya nini!?


Umeme wa Mvua Bado kuja! Tamko!
tamko ni hili hapa
-mitambo uya umemem sio kama koti unaloweza kwenda tu dukani na kulichukua
-yeye sio mawingu aende akanyeshe mtera ili mabwaya yajae
..................mnataka matamko gani mengine?
huyu Rais alikuwa ni waziri wa nishati na madini kakaa pae maisha yake yote sasa mnataka nini tena??? anajua A mpaka B
 
Kama wameshindwa kuwa na mipango madhubuti ya kuwa na vyanzo mbadala vya umeme kwa vipindi vyote vya uongozi vilivyopita, iweje waweze kuwa na jibu la mgao wa umeme ndani ya wiki tatu?
Nasema tusubiri uongo mwingine tena baada ya hizo wiki tatu kuisha.
Naomba kuwasilisha.
 
Kama wameshindwa kuwa na mipango madhubuti ya kuwa na vyanzo mbadala vya umeme kwa vipindi vyote vya uongozi vilivyopita, iweje waweze kuwa na jibu la mgao wa umeme ndani ya wiki tatu?
Nasema tusubiri uongo mwingine tena baada ya hizo wiki tatu kuisha.
Naomba kuwasilisha.

Umeongea maneno mazuri sana ambayo yanastahili kila sifa.

Nnaamini kabisa kwa utendaji wa kikwete, jibu lipo na mambo ni mazuri kabisa. Achana na awamu zilizopita ambapo hata kuuliza au kusema kama kuna matatizo ilikuwa shida. Tumeona masuala magumu kabisa Kikwete akiyatatua kiulaini. Nna imani sana na Kikwete na nna imani sana na utendaji wake. Na nna uhakika umeme ni kipindi cha mpito tu na Kikwete kisha weka mikakati ya kutatua "once and for all".
 
huyu jamaa sijui anataka tmko gani zaidi ya yanayotolewa.
Ndo walewale wakulalamika na kuchombeza.
 
Unataka tamko gani zaidi ya hili, "mzee ruksa alikaa miaka 10 hakuyamalza, mzee Nkapa alikaa miaka 10 hakuyamalza, mie (jk) miaka 5 hayajaisha na mingne 5 hayatakwisha"
 
Mkuu anaskilizia kwanza, ana pima upepo..bora tu akae kimya manake akiongea duuh..!
 
Mimi ndo Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete a.k.a Boyz2Men,wengi hupenda kuniita SailorMan,mzee wa kujirusha,watanzania wanafiki wananiita brazamen na nikiwa majuu najulikana kama Superbegger japo binafsi napenda kuitwa Vasco da Gam wa karne ya 21 ama mzee wa Ahadi.....mtanielewa tu taratibu jamani!
 
Back
Top Bottom