Rais Kikwete safarini Ghana

Status
Not open for further replies.
Ni jambo la uungwana kwa Rais aliyepo madarakani kuhudhuria mazishi ya ya Rais mwenzake ambaye amefariki akiwa madarakani. Aidha, tangu lini tumekuwa na tabia ya kuamua nani akamzike nani? Kwa mujibu wa miongozo ya kidini na kimaadili kuwazika wenzio ni jambo la sudi hivyo Kidiplomasia, kimaadili, kidini Mhe. Rais hajakosea kwenda Ghana.
 
naomba muongozo,kwa nini mazishi ya J.Atta Mills yamechukua muda hivi,is there something behind?wale wana usalama,,,,,naomba muongozo...kuna utata hapo.
 
Mimi namuomba akirudi aje na KATIBA YA GHANA nasikia is one of the best constitution. Itatusaidia wakati wa kutengeneza katiba yetu. Tena aje nazo copy nyingi.
 
Ni haki yake kuhudhuria mazishi ya kiongozi mwenzake! Mbona sisi tunahudhuria za ndugu zetu hatuulizana!
 
binadamu hatuna jema, binasfi sioni ubaya wa yeye kwenda msibani. kwa nini atume muwakilishi na wakati ratiba yake imeruhusu?
 
Leader like kikwete who has just paralysed the health sector is now happy to die abroad UNLIKE John Atta Mills who died peaceful on his own land.It's not the matter of attending funeral only,at least he should learn something from the deceased
 
sasa jamani sio kwamba kila safari ya raisi tunaikosoa!! Nyingine zinamantiki.
Inajenga mahusiano mazuri na nchi husika wakijua kuwa tanzania tupo nao pamoja katika kipindi kugumu walichonacho.
Unakumbuka hayati mwl jk alinyofariki!? Ilikuwa inafariji kuona maraisi na viongozi maarufu waliohudhuria msiba ule.
Unachotaka watu wakufanyie, na wewe wafanyie hicho hicho!




ameungana na akina hillary clinton?......ila kaa ukijua waingereza wana maslahi yao kwenda huko ghana....so nasita kukuunga mkono kuwa rais ameenda kuzika huko ghana ili na sisi watz tukipata msiba waje kutuzika!!!!.......tunachosema rais kikwete atulie ikulu atafakari namna ya kutusaidia wananchi wake maana tunakufa na maisha magumu huku yeye na watu wake wakiendelea kuneemeka na kuenjoy safari zisizo za lazima........anatumalizia hela zetu huyu jamani.
 
Lazima aende kwa vile naye siku akifa watakuja watu kama hao , siyo kama wewe hata Mshenga wako mwenyewe ataona kama hakuna umuhimu kwa vile ulishawachosha uswazi kwenu kwa majungu.
Teh teh ama hakika thatha unafurahisha mi sijakosoa yeye kwenda msibani hii ni utamaduni wetu, tatizo ni kuwa hii kwake huwa ni golden chance maana hatulii huyu bwana...Sina maana hiyo unayoifikiria ndugu
For ur information maiti haina issue mi hata wasipokuja watu msibani siyo deal maana maiti haisemi, lakini sijajiandaa kihivyo maana ninaishi na watu wa aina zote, sina majungu kama unavyodhania... May be we ndo mtu wa majungu maana hunijui sikujui ila neno ulilonichagulia ni MAJUNGU..Kisaikolojia naweza sema ume-project tatizo lako kwangu ili upate relief ya mzigo wa majungu uliyonayo moyoni na rohoni na inawezekana kabisa kuwa wewe ni mtu wa majungu tena sana..
Anyway asante maana hata kipimo cha mtu ni kauli zake yaweza kuwa kwa nilichoandika basi umenipima na kuniweka katika kundi hilon kwa kauli zangu..nashukuru kwa tathmini.
Wakatabahu,,
Back to re-build the Nation corrupted by CCM
 
RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA RAIS JOHN ATTA MILLS WA GHANA JIJINI ACCRA LEO



http://www.youtube.com/watch?v=AffWIbzPBWg&feature=player_detailpage



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo wakati shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Ghana Marehemu Profesa John Evans Atta Mills katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra leo.







Shughuli mbalimbali za mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie baada ya shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana jijini Accra leo.

Jukwaa kuu katika uwanja wa Independende Square wakati wa Shughuli mbalimbali za mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo.
PICHA NA IKULU.

 
Aiseee baba yangu mi ninachoomba asife mtu mwingine maharufu manake jei kei lazima aende tena cha kushangaza akitutoka yeye watakuja wawakilishi 2 kumuaga mimi sinipo huku rombo mtaniambia tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom