Rais Kikwete ndiye anayefaa kuongoza – Dk. Mwakyembe

Katika watu wasiokuwa na akili ya kuishi na kudumu kama mwanasiasa sijaona kama huyu Mwakyembe!

Katika mtazamo wake siku zote alikuwa anakandamiza serikali ya Jk akiwa kama frontliner.Leo kunani hata aseme JK ni kiongozi safi si unafiki tu.

Mimi naamini kuwa Jk ni safi sana...na anajua ku calculate trends za kisiasa zinavyoelekea,na sioni kama ana matatizo kama ya Mkapa.Mwakyembe angefaa kwenda Chadema mapema mno.Kwenye CCM kishaharibu,hata akisema nini!
 
"Mimi kwangu namuona Rais anafaa kuongoza…bali tunapaswa tumuondolee baadhi ya watu wanaomchafua," alisema Dk. Mwakyembe huku akiwataka watu wasimfikirie vibaya anapotoa hoja zake kuwa ni mbwembe bali anajiamini kutokana na elimu aliyonayo na hivyo anajivuna. ''


Anafaa kuongoza genge la wahuni.
 
2010 hiyoooooooo inakaribia. Watu presha juu, kuuma na kupuliza. Nakwambia Dr. Makyembe, hata kama umsifu Rais kiasi gani, fahamu kuwa katika list ya watu ambao anajua wanamziba asisonge na wewe upo. Yeye anapenda mafisadi rafiki zake wapete, wewe unawaziba halafu unafikiri anakupenda? Usijidanganye kabisa ndugu yangu.

Umewekewa visasi na maswahiba wake, naye anawapenda kuliko wewe!!!! Uwe tu na mipango yako mathubuti kuhusu uchaguzi 2010. Sasa hivi hujagundua tu wanataka wakutafutie kesi halafu itavutwa weee hadi wakati wa kupitisha wagombea na kwa kuwa una kesi basi jina lako litakuwa kapuni. Pole sana!!

Otherwise, you are a hero!!! Na huogopi!!! Ila sasa naona kama umeanza kwa na hofu!!! Za nini hizo?? Kuwa ngangari tu baba. Pigana kiume.
 
Dr. Mwakyembe katoa maoni yake kuhusu JK, nawe unayo yako. Kumkebehi Dr huyu ni ufinyu wa mawazo. Ni kweli JK ni rais bora ukilinganisha na tutusa la awamu ya tatu, ambalo limetukisha kutemewa mate na "miungu' wake. Ni kweli JK baadhi ya wasaidizi ni mafirauni, na tumeona anavyo waondoa taratibu na kwa style isiyoleta uchafuzi wa hali ya hewa kisiasa. After 2010 wengi wachafu hawatakuwepo.
Mwakyembe kalifanyia kazi nzuri taifa, wote tunajua. Kelele za JF hazimnyimi usingizi shujaa huyu.

Dr. aluta continua...............
 
Dr. Mwakyembe katoa maoni yake kuhusu JK, nawe unayo yako. Kumkebehi Dr huyu ni ufinyu wa mawazo. Ni kweli JK ni rais bora ukilinganisha na tutusa la awamu ya tatu, ambalo limetukisha kutemewa mate na "miungu' wake. Ni kweli JK baadhi ya wasaidizi ni mafirauni, na tumeona anavyo waondoa taratibu na kwa style isiyoleta uchafuzi wa hali ya hewa kisiasa. After 2010 wengi wachafu hawatakuwepo.
Mwakyembe kalifanyia kazi nzuri taifa, wote tunajua. Kelele za JF hazimnyimi usingizi shujaa huyu.

Dr. aluta continua...............

Hivi wewe tupe ushujaa mmoja alioufanya Mwakyembe???? Kama ya Richmond???
Kwanza report ya richmond imejaa mapungufu kwasababu most of their facts ni allegation without a physical evidence.

Mikataba inayotuhumiwa ni legal contract ambazo hazionyeshi uvunjaji wa sheria wowote labda jinsi tenda zilivyotolewa ndio unaweza kutia shaka.

Tuje mwakyembe mwenyewe kama kweli angelikuwa shujaa angelideclare basi kama ana likiwanda la umeme (windfarm) mbeya badala yake anasubiri hadi JF ije kumuumbua. Mwenyewe ameita press conference kuelezea kuwa hakuwa na ulazima wa disclose but amesahau kuwa unapofanya investigation kama trustee unatakiwa kudisclose any interest katika kampuni au ishu mnayochunguza ili kuprotect the integrity of the commitee tutajuaje kama hizo allegation amezipika au ametumia nguvu za ushawishi kimtazamo????

Mie kwakweli siko na wewe simuoni kama shujaa bali msanii tu wa kisiasa ambaye anataka popularity na kudanganya wananchi wamchague I stand to be corrected!!!!
 
Hivi huyu anaofia atafukuzwa kwenye chama au ile vita imemshinda mie sijamuelewa anachomaanisha na kama ni kweli siungani nae mkono now tanzania we need changes over everthing even our lifestyle
 
Jamani ile mishangingi yenye viyoyozi kama Alaska, pamoja na marupurupu yanayoenda nayo yanawatia wehu hawa wapiganaji wetu.

As if njia pekee ya kuhakikisha wanakula ni kutegemea largesse ya rais na administration yake.

Ingawa siamini dini, nakubali katika falsafa ya "njia ile ni nyembamba" na "wengi watasemwa, waipitayo kikweli ni wachache"
 
Jamani ile mishangingi yenye viyoyozi kama Alaska, pamoja na marupurupu yanayoenda nayo yanawatia wehu hawa wapiganaji wetu.

As if njia pekee ya kuhakikisha wanakula ni kutegemea largesse ya rais na administration yake.

Ingawa siamini dini, nakubali katika falsafa ya "njia ile ni nyembamba" na "wengi watasemwa, waipitayo kikweli ni wachache"

Sawasawa kaka waadilifu tanzania wapo lakini wanahesabika kwangu mie mmoja wao ni nyerere lakini wengine hawa naona wanakuwa na hidden ajenda zao nyuma but wanasahau Tanzania ya sasa si kama ile ya miaka ya zamani ya kila kitu ndio mzee!!!
 
Hapo Mwakyembe anaogopa kumwambia mfalme umekaa uchi,huyo jamaa ni muoga,anaogopa ku address the real problem,naamin kabisa mwakyembe anajua for sure Kikwete ndo tatizo kuu kabisa,ili vita ya ufisadi iweze kushinda,kikwete ndo anatkiwa atoswe wa kwanza kabisaa,mwakyembe analijua nhilo,ila sijui anaogopa nii kuliweka wazi hilo,binasfi namuona ni mnafik,anajua problem ni nin,ila anatuambia the source of the problem eti ndo anafaa kuongoza.
Wana CCM wote wanajua JK ndiye tatizo,ila no one with the balls to address that bila kigugumizi..
Duuu tunasafari ndefu sana bado
 
Kuna mwana JF mmoja huwa anajiita mkereketwa wa CCM, na yeye ni mpiganaji na Mwakyembe ni role model wake! at the same time huwa anampinga sana JK na kumuona garbage if not trash.

Leo hii kipenzi chakwa mwakyembendiye kinara wa kumsifia JK!

Pole FMES
 
Back
Top Bottom